GASTO LEE

GASTO LEE WANAUME NJOONI TUONGEE 💪🤝

+255673502502

Call/Whatsapp

I"m sorry Hutuliza Moyo sana...Ila usiambiwe na Doctor.
11/08/2024

I"m sorry Hutuliza Moyo sana...
Ila usiambiwe na Doctor.

FAHAMU AINA ZA U.T.I SUGUA)lower U.T.ILower U.T.I ni hatua ya ugonjwa kushambulia maeneo ya urethra nakibofu cha mkojo (...
26/04/2024

FAHAMU AINA ZA U.T.I SUGU

A)lower U.T.I

Lower U.T.I ni hatua ya ugonjwa kushambulia maeneo ya urethra na
kibofu cha mkojo (bladder). Katika hatua hizi, mgonjwa atasikia dalili
zifuatazo:
1. Maumivu wakati wa kukojoa
2. Kujisikia kukojoa mara kwa mara lakini kutoa mkojo kidogo tu
3. Damu katika mkojo
4. Mkojo wenye rangi ya chai
5. Mkojo wenye harufu kali
6. Maumivu ya kiuno kwa wanawake
7. Maumivu ya sehemu za nyuma kwa wanaume

*B) Upper U.T.I

Upper U.T.I ni maambukizi ya ndani ya figo. Hii ni hatua mbaya sana
endapo bacteria wataanza kuingia kwenye mkondo wa damu kutoka
kwenye figo – SEPSIS. Sepsis huweza kusababisha msukumo wa
damu kuwa mdogo sana (Low Blood Pressure), msh*tuko au kifo.

Dalili za upper UTI
1. Maumivu ya maeneo ya juu ya mgongo
2. Homa
3. Kusikia baridi
4. Kusikia kichefuchefu
5. Kutapika

Ukiipuuza U.T.I Unaweza kupata athali kubwa sana k**a zifuatazo
1.Figo kushindwa kufanya kazi (kidney failure) hii ni hatari sana ,hutokana na bacteria kushambulia figo
2.Kupatwa magonjwa ya kibofu ,k**a kibofu kuziba ,kushindwa kukojoa ,hii hupelekea MTU kukojoa kwa mirija
3 .maumivu ya mgongo, kiuno na NYONGA
4.kupoteza hamu ya tendo la ndoa.nk.
5.kuharibu homon(hormon inbalance)
6.mimba kuharibika
7.kishindwa kubeba mimba.
kwa kupata tibalishe isiyo na kemikali wala madhara

Wasiliana nasi call or whatsapp
0673 502 502

NI DINI TU❗{ MAMBO KUMI NA MOJA UNAYOJISAHAULISHA MWAFRIKA}1) .Ni dini inayowazuia Waafrika kujifikiria na kujifikirisha...
08/04/2024

NI DINI TU❗{ MAMBO KUMI NA MOJA UNAYOJISAHAULISHA MWAFRIKA}

1) .Ni dini inayowazuia Waafrika kujifikiria na kujifikirisha wenyewe:

2) .Dini ndiyo inayowafanya Waafrika wafikirie kuwa ni zawadi kutoka kwa mungu kuwa maskini na kuishi katika mifereji ya dunia.

3) .Ni udini unaowazuia Waafrika kupigana dhidi ya watesi wao.

4) .Dini ndiyo inayomfanya Mwafrika huyo kuwapa wageni ardhi yenye rutuba zaidi barani Afrika huku wakiishi kwenye miamba na dampo za takataka.

5) .Ni dini inayowafanya Waafrika wenzangu kuniita kafiri, & mpagani, na kumwita mtu wa kabila nyingine "ndugu yake."

6) .Ni dini inayowaambia Waafrika kukaa magotini, kufumba macho, na kushikana mikono ikiwa wanataka kutimiza malengo yao ya maisha; huku mbio zingine zikitoka na kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo yao peke yao.

7) .Ni dini inayowaambia Waafrika wapeleke watoto wao kanisani kuimba na kucheza ili kupata maarifa, huku watoto wengine wa dunia wapo shuleni wakisoma jinsi ya kuwatawala watoto wa kiafrika.

8) .Ni dini inayomwambia Mwafrika kwamba ni bora zaidi kwao kumpenda Myahudi aliyekufa au Mwarabu aliyekufa kuliko kuwapenda wazazi wao au watoto wao.

9) . Ni dini inayomwambia Mwafrika masikini kwamba wawape watoto wao karo ya shule kwa waombaji watakatifu kitaaluma ili wanunue ndege za kibinafsi, wakati watoto wao wenyewe hawawezi hata kuandika majina yao wenyewe ikiwa maisha yao yalitegemea.

10) .Ni dini inayowaambia Waafrika kusahau furaha katika maisha, wasubiri hadi baada ya kufa ili wawe na furaha: "Furaha yote katika dunia hii ni ya jamii nyingine zote isipokuwa Waafrika" inasema dini.

11) .Ninaweza kuendelea milele lakini kwa sasa unapata uhakika.

🕹AFRICA SASA KWA KUWA UNAJUA SABABU KUU YA MATATIZO YAKO, JE, UTAFANYA NINI KUHUSU HILO❓

Usiseme sijakwambia.."Mtoto mdogo alivyokuja Kwenye Dunia hii amekuja na Udogo wake lakini Ni kiumbe cha Kale" Na ndio m...
30/03/2024

Usiseme sijakwambia..

"Mtoto mdogo alivyokuja Kwenye Dunia hii amekuja na Udogo wake lakini Ni kiumbe cha Kale"

Na ndio maana nyie mnaongea na yeye anatafiri pamoja na udogo Wake.

Hivyo Kumbuka Kujua Vyema Ni Kujua Kutojua..

Usije Na Majibu Yako Mfukoni Haya Ni Maisha Tuu....!!!!😎😎

BAWASIRI/KIKUNDU (HAEMORHOIDS)BAWASIRI NI NINI?Ni mkusanyiko wa damu ndani ya njia ya haja kubwa (mkundu na puru) katika...
30/03/2024

BAWASIRI/KIKUNDU (HAEMORHOIDS)

BAWASIRI NI NINI?
Ni mkusanyiko wa damu ndani ya njia ya haja kubwa (mkundu na puru) katika sinusoid za ateri na vena za njia ya haja kubwa. Ikumbukwe kwamba mifumo hii ya damu ni ya kawaida na kila binadamu anazo. Mifumo hio ya damu ya ndani ya njia ya haja kubwa ikijaa damu ndipo inavimba na inakua bawasiri au vijivimbe laini ndani ya njia hiyo. Watu wengi sana wana bawasiri na kwa kua hazinaga dalili basi hata watu wengi hawajijui k**a wana hali hii.Bawasiri huwapata sana watu kuanzia miaka 30 hadi 65;chini ya miaka 20 au juu ya miaka 70 ni ngumu sana kupata bawasiri. Ikumbukwe kwamba bawasiri zipo sana na k**a hazikupi shida yeyote wala hazihitaji matibabu ya aina yeyote

AINA ZA BAWASIRI

👉BAWASIRI ZA NDANI(INTERNAL HAEMORHOIDS)

👉BAWASIRI ZA NJE(EXTERNAL HAEMORHOIDS)

👉BAWASIRI MCHANGANYIKO(MIXED HAEMORHOIDS)

WALIOPO KWENYE HATARI YA KUPATA BAWASIRI

👉Wanaoharisha sana(diarrhea)

👉Wajawazito( pregnancy)

👉Wanaopata choo kigumu kwa muda mrefu(chronic constipation)

👉Wanaokaa muda mrefu kwenye kiti( prolonged sitting)

👉Watu wenye kiribatumbo(obesity)

👉Wanaofanya mapenzi ya njia ya haja kubwa(a**l in*******se)

👉Wanaonyanyua vitu vizito(Regular heavy lifting)

👉Watu wenye maisha mazuri na wasomi(Higher socioeconomic status)

👉Waliofanyiwa operesheni ya aina yeyote ya mkunduni(Rectal surgery)

👉Wenye magonjwa ya ini(Hepatic disease)

👉Watu wenye saratani ya utumbo mpana(Colon malignancy)

👉Wenye presha ya puru(Elevated a**l resting pressure)

👉Wenye presha ya Ini(Portal hypertension

ATHARI ZA BAWASIRI
🔹Upungufu wa damu mwilini
🔹Kutokwa na kinyesi bila kijitambua
🔹kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
🔹kupungukia nguvu za kiume (kwa wanaume)
🔹kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu
🔹Kupata tatizo la kisaikolojia

NJIA ZA KUJIKINGA DHIDI YA BAWASIRI

🔹Kula mboga za majani na nafaka zisizo kobolewa kwa wingi
🔹kunywa maji mengi lita sita hadi kumi na mbili kwa siku
🔹Acha kufanya ngono kwa kutumia tundu la haja kubwa (kulawitiwa)
🔹Punguza kukaa chooni kwa muda mrefu, kunaweza kuongeza shinikizo katika njia ya haja kubwa.

MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA UGONJWA WA BAWASIRI
➡️matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri, mara nyingi wagonjwa wa bawasiri hupatiwa tiba ya kukatwa kinyama na kushauriwa kuendelea na tiba ya vyakula Lakini tiba huwa haina matokeo mazuri kwasababu baada ya Muda tatizo hujirudia kutokana na kwamba hawajatibu chanzo cha tatizo hivyo tiba nzuri ya bawasiri ni kutumia dawa itakayotibu chanzo cha tatizo huku ukiendelea na tiba ya chakula, MFANO MZURI WA DAWA NI *FAHARI BAWASILI* na *BAWASIR LIQUID* hizo zinatibu na kuondoa tatizo moja kwa moja kwa muda wa wiki mbili tu hata k**a ulishawahi kufanyiwa upasuaji hivyo ni vizuri kutumia dawa hizo ili kumaliza tatizo pamoja na hayo ni
vyema ukazingatia mambo yafuatayo ili KUEPUKANA na ugonjwa wa bawasiri

ZINGATIA KANUNI YA CHAKULA BORA KWA KUPENDELEA KULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA NA NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GLASI SITA HADI 12 KWA SIKU
EPUKA KUTUMIA MUDA MREFU CHOONI

MADHARA YA BAWASIRI
➡️Ugonjwa wa bawasiri una madhara makubwa iwapo hautapatiwa tiba ya uhakika haya ni baadhi ya madhara ya bawasiri

➡️KUPATA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

➡️KUPATA TATIZO LA KUSHINDWA KUHIMILI KINYESI

➡️HUPUNGUZA MORAL YA KUFANYA KAZI KUTOKANA NA MAUMIVU

➡️HUATHIRI KISAIKOLOJIA
MWANAMKE HUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA

➡️KUPATA KANSA YA YTUMBO
✍ hayo ni mambo ya msingi sana kuyajua kabla ya kujua tiba

+255 749 798 009 call 📞
+255 673 502 502 WhatsApp

TUPO DAR ES SALAAM , MBEZI MWISHO NA MBEYA BLOCK T.

NYOTE MNAKARIBISHWA.

Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea ni baada ya ...
30/03/2024

Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea ni baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus. Kemikali ambayo ni acidi inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, k**a ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine k**a kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito.

AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO

Kuna aina zipatazo mbili za Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers)

Vidonda vya tumbo kubwa (Gastric ulcers) – Hivi ni vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani kwenye tumbo kubwa
Gastric_Ulcer-1200x720

2. Vidonda vya utumbo mdogo (Duodenal ulcers) – Hivi ni vidonda ambavyo hutokea kwenye utumbo mdogo (hasa juu)
duodenal-ulcer

CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO

Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;

Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)
Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu k**a asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)
Kuwa na mawazo mengi
Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
Kunywa pombe na vinywaji vikali
Uvutaji wa sigara
Kuto kula mlo kwa mpangilio

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO

Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na endelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vinadalili k**a;

gastrita

Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa k**a ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula
Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo
Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa
Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu
Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu
Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
Kushindwa kupumua vizuri.

Dose ya Vidonda Vya Tumbo ni 120000/-

By; Dr Gasto Lee ✍🏾
+255 749 798 009/+255 673 502 502 📞

Figo zako ni kiungo muhimu sana katika mwili. Hufanya kazi ya kuondoa uchafu katika damu na kutengeneza mkojo.Pia figo h...
25/03/2024

Figo zako ni kiungo muhimu sana katika mwili. Hufanya kazi ya kuondoa uchafu katika damu na kutengeneza mkojo.

Pia figo husaidia kudhibiti shinikizo la damu na kudumisha uwiano wa kemikali. Vilevile, hutengeneza seli nyekundu za damu.

Lakini watu wengi hutekeseka kutokana na figo zao kushindwa kufanya kazi na kushambuliwa na magonjwa yasiyokuwa kuambukiza.

Wataalamu wa matibabu wanasema kiwango cha ugonjwa wa figo katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kinatisha. Watu hutumia pesa nyingi kwa ajili ya matibabu na kusafisha figo.

Gharama ya kila mwaka ya matibabu ya figo kwa wastani barani Afrika kwa mtu mmoja ni kati ya dola za kimarekani 13k - 25k.

Wagonjwa wamekuwa wakitegemea usafishwaji angalau mara mbili kwa wiki ili kuishi. Kwa kuondolewa uchafu na maji yaliyozidi katika figo kwani figo haiwezi tena kufanya hivyo. Miongoni mwa wazee na vijana, ugonjwa wa figo umekuwa ukiwamaliza.

Wakati ulimwengu unaadhimisha siku ya figo tarehe 14 Machi, wataalamu wanatufundisha jinsi tunavyoweza kulinda figo zetu.

👉Kunywa maji mengi kwa siku

Ukiwa na takriban vikombe 8 vya maji ya kawaida ya kunywa kwa siku, maji yatalinda figo, haswa kwa wagonjwa walio na hatarini k**a vile wagonjwa wa kisukari, shinikizo la damu, ugonjwa wa seli mundu.

👉Punguza pombe na acha sigara

Kupunguza au kuacha kabisa pombe na sigara ni muhimu ili mtu kuziweka figo zake katika afya. Pombe na sigara ni maadui wa figo.

👉Tumia dawa kwa usahihi

Unapaswa kumuuliza daktari wako kuhusu matumizi ya dawa. Baadhi ya dawa zinaweza kuharibu viungo vyako, hasa figo. Tafuta ushauri wa matibabu na usinunue dawa mtaani.

👉Fanya vipimo vya tumbo

Kitu kingine ambacho kila mtu anapaswa kufanya, ni vipimo vya tumbo angalau mara moja kila baada ya miaka miwili hadi mitano. Ili kuangalia afya ya figo na viungo vingine.

👉Fanya mazoezi ya mwili

Tumia dakika 30 au zaidi kwa siku kufanya mazoezi. Husaidia kurekebisha kalori zako na kubaki katika uzito mzuri.

Je wewe k**a wewe unatumia njia ipi kuilinda figo yako?

Dr Gasto Lee
0749798009

UKIAMKA!!!1. Kunywa Glass 1-2 za Maji Asubuhi hii, Fanya hivyo Kwa Ajili ya Vital organs zako !2. Pata Angalau dk 15-30 ...
22/03/2024

UKIAMKA!!!

1. Kunywa Glass 1-2 za Maji Asubuhi hii, Fanya hivyo Kwa Ajili ya Vital organs zako !

2. Pata Angalau dk 15-30 za Mazoezi ya Asubuhi, KEGEL ni MUHIMU zaidi Kwa Mwanaume!

3. Oga Maji Baridi (Zingatia mazingira na sehemu iliyopo).

4. "Kaa Mbalii" na Sukari Nyingi.

5. Kula Angalau yai 1 Leo Kwa Ajili ya Moyo na Ubongo

6. Pata Muda wa Kuyafurahia Maisha Yako na mafanikio uliyopata, hata k**a ni kidogo na Kwa kufanya Hivyo utailinda Afya yako ya Akili

7. Hakikisha unapata Mboga za Majani Kwa Ajili ya Kuimarisha Kinga Yako ya Mwili.

8. Usikae sehemu moja kwa Masaa au muda mrefu, inuka jinyooshe, tembea, Utauokoa uti wako wa mgongo!

9. Pata Muda wa Kupumzika, Ni nzuri Kwa Afya yako ya Akili.

10. Like & Repost ili iwafikie na Kuwasaidia Wengine

Welcome 0749798009K**a una Changamoto hizo..Mbeya Tz na Dar Es Salaam
22/03/2024

Welcome 0749798009

K**a una Changamoto hizo..

Mbeya Tz na Dar Es Salaam

Dawa ya Asili Ya Vidonda Vya TumboKatika makala hii nitakueleza kiundani juu ya dawa ya vidonda vya tumbo.Vidonda vya tu...
05/03/2024

Dawa ya Asili Ya Vidonda Vya Tumbo

Katika makala hii nitakueleza kiundani juu ya dawa ya vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo ni majeraha au vidonda ndani ya kuta za tumbo.

Vidonda vya tumbo husababishwa na nini?

Kwa kawaida vidonda vya tumbo husababishwa na bakteria aitwaye Helicobacter pylori au kwa kifupi H. pylori.

Watu wawili katika kila watu watatu hapa duniani wana huyu bakteria tumboni mwao.

Na ingawa wengi wa watu hawa wenye huyu bakteria hawaonyeshi dalili yoyote ya kuumwa vidonda vya tumbo bado baadhi yao wanatokewa kuumwa.

Karibu asilimia 2 mpaka 20 ya watu wenye H. pylori wanaugua vidonda vya tumbo.

Wakati hakuna uelewa wa moja kwa moja ni jinsi gani huyu bakteria anaingia tumboni, bado ni bakteria wa kawaida anayepatikana tumboni mwa watu wengi na anaweza kukuingia kupitia chakula na maji ya kunywa.

Tatizo la vidonda vya tumbo linalosababishwa na huyu bakteria ni kuwa anachelewa sana kukuonyesha dalili kwamba una vidonda vya tumbo.

Wakati unaweza kuishi na vidonda vya tumbo kwa muda fulani bila kukuletea shida kubwa, kuviacha kwa muda mrefu bila kupata matibabu kunaweza kukuletea madhara makubwa kiafya.

Tunatambuwa pia asidi inahusika pia na kutokea kwa vidonda vya tumbo.

Zaidi ya nusu ya watu wote wenye vidonda vya tumbo vidonda vyao ni matokeo ya asidi kuzidi mwilini na siyo H. pylori bakteria moja kwa moja.

Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH yaani potential hydrogen. Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.

Unaweza kukinunua kipimo cha PH na kupima Ph ya mate yako au ya mkojo wako kila mara ili kupata mwelekeo wa namna gani ufanye alkalini katika mwili wako ibaki kuwa ya 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako.

Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.

Unapokaribia kutaka kula chakula chochote, au ukiwaza kutaka kula au ukiuona tu msosi kwa macho, TUMBONI MWAKO HUZARISHWA haidrokloriki asidi ili kuuandaa na kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Kadri unavyoendelea kuishi haidrokloriki ASIDI HIYO HUENDA KUTOBOA KUTA ZA TUMBO na hatimaye taratibu baadaye hukusababishia VIDONDA VYA TUMBO.

Kila mtu anapaswa kula zaidi vyakula vyenye alkalini yaani matunda na mboga za majani na kunywa vinywaji vyenye asidi chache na ikibidi basi atumie vinywaji vyenye alkalini nyingi k**a juisi ya limau, juisi ya chungwa, ya zabibu na maji halisi.

Hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea kusikia maumivu yatokanayo na vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo pia vinaweza kukutokea k**a matokeo ya kutumia dawa za kupunguza maumivu kwa muda mrefu bila ushauri wa kitaalamu, kuvuta sana sigara au kunywa pombe kupita kiasi.

Jina langu naitwa Dr Gasto Lee ni Tabibu wa Tiba Asili Tanzania

Endelea kusoma ….

Dalili 17 za vidonda vya tumbo

Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni pamoja na:

1. Kuchoka choka sana bila sababu maalum

2. Kuumwa mgongo au kiuno

3. Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu na hamu ya tendo la ndoa.

4. Kizunguzungu

5. Kukosa usingizi

6. Maumivu makali sehemu ya mwili

7. Maumivu ya Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali

8. Kichefuchefu

9. Kiungulia

10. Tumbo kujaa gesi

11. Tumbo kuwaka moto

12. Miguu kuwaka moto na ganzi

13. Maumivu makali sehemu kilipo kidonda

14. Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika k**a cha mbuzi

15. Kukosa hamu ya kula

16. Kusahahu sahau na

17. Hasira za mara kwa mara

Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma k**a sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali.

Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.
Utambuzi wa vidonda vya tumbo

Utambuzi wa kubainisha vidonda vya tumbo hufanyika hospitalini kwa kutumia mionzi au X-Ray kwa lugha ya kikoloni.

Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana k**a ‘endoskopi’ au ‘biopsi’, ambayo huyakinisha hali halisi.

Matibabu ya vidonda vya tumbo

Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni au mwilini kwa ujumla.

Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.

Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4 mpaka 6 za matibabu.

Vidonda vya tumbo ni majeraha au vidonda ndani ya kuta za tumbo.

Majeraha au vidonda hivyo huleta maumivu yanayokera na hutokea mara nyingi tumboni na yanaweza kutibika lakini k**a hutachukuwa hatua mapema za kutibu yanaweza kukuletea majanga mengine mengi kiafya.

Tumbo na utumbo mdogo vina kuta maalumu yenye ute ute wa ulinzi ambao hulilinda tumbo lako dhidi ya maadui wanaoleta shida tumboni mwako yaani bakteria wabaya, virusi na vijidudu nyemelezi vingine.

Matokeo ya mashambulizi hayo ya huyu bakteria ni kutokea kwa vidonda kwenye kuta za tumbo na kuweka uwazi (vidonda) ambavyo hutumika k**a njia ya kupitia bakteria wengine wabaya na kuongeza gesi tumboni.

Wakati unaweza kuishi na vidonda vya tumbo kwa muda fulani bila kukuletea shida kubwa, kuviacha kwa muda mrefu bila kupata matibabu kunaweza kukuletea madhara yafuatayo;

Madhara 9 ya Vidonda vya tumbo mwilini

1. Kuvuja damu ndani ya mwili (Internal bleeding and serious blood loss)

2. Upungufu wa damu (Anemia)

3. Kutapika damu

4. Kupata kinyesi cheusi k**a cha mbuzi

5. Kuvurugika kwa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula (Obstructed digestion)

6. Shida katika kupumua

7. Saratani ya tumbo (Stomach cancer)

8. Msongo wa mawazo (stress)

9. Kupungua kwa nguvu za kiume

Ni mhimu kupata vipimo na uchunguzi zaidi wa daktari mapema tu unapohisi unaweza kuwa na vidonda vya tumbo ili kuzuia usipatwe na madhara haya yatokanayo na vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo huwa ni rahisi kutibika unapowahi kuanza matibabu kuliko ukisubiri mpaka viwe sugu

Jinsi ya kuimarisha mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula

Pia unaweza kuimarisha afya ya mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kwa kufanya yafuatayo

1. Kunywa maji glasi 2 (nusu lita) mara tu uamkapo kutoka kitandani kila siku. Kunywa tena kiasi hiki cha maji kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na cha jioni kila siku.

2. Kula chakula kichache milo mingi. Kula hata mara 5 kwa siku lakini chakula kidogo kidogo siyo kingi kwa wakati mmoja.

3. Kula pole pole ulapo chakula

4. Hakikisha unapokula chakula huna mawazo mawazo (stress) yoyote.

5. Kula zaidi vyakula vyenye nyuzi nyuzi

6. Kula vyakula vyenye bakteria wazuri (probiotics) k**a vile mtindi na uji wa unga wa ndizi

7. Punguza kukaa chini au kwenye kiti masaa mengi

Hata k**a utampata huyu bakteria (H. pylori) k**a unao bakteria wengine wazuri tumboni ni rahisi kwako kumdhibiti huyu anayeleta vidonda vya tumbo.

Kuimarisha afya ya mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula ni jambo zuri kiafya siyo kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo tu bali kwa mtu yoyote asiyependa kuugua mara kwa mara kwani tumboni ndiko kuliko na injini ya mwili wote kwa ujumla.

H. pylori ni bakteria anayesababisha vidonda vya tumbo kwa karibu ya zaidi ya nusu ya watu wote duniani hivyo uwezekano wa kumpata au kuugua ugonjwa huu ni mkubwa sana kwa mtu yoyote.

Dawa ya vidonda vya tumbo > stomach ulcers

Stomach ulcers ni dawa ya asili ya vidonda vya tumbo

Unapotaka kutibu vidonda vya tumbo ni mhimu kutambua kwanza nini kinaweza kuwa ndiyo chanzo hasa cha tatizo kwa upande wako.

Watu wengi wanaugua vidonda vya tumbo k**a matokeo ya kushuka kwa kinga zao za mwili jambo linalosababisha bakteria mbalimbali kushambulia na kutoboa tumbo.

Kadri hawa bakteria mbalimbali wanavyozidi kuongezeka tumboni wanaharibu mfumo wa kawaida wa uundwaji wa asidi mwilini na kupelekea asidi nyingi zaidi kuzalishwa zaidi ya inavyohitajika na mwili.

Asilimia 98 ya watu wengi wanaougua vidonda vya tumbo ni matokeo ya asidi nyingi kuzidi mwilini.

Stomach ulcers ni dawa nzuri ya asili ambayo;

*Inaongeza mara dufu kinga yako ya mwili
Inaua bakteria mbalimbali tumboni akiwemo bakteria wa vidonda vya tumbo H.Pyrol

*Inaweka sawa usawa wa asidi na alkalini mwilini Kwa kiasi chake

*Inarahisisha kutibu vidonda sehemu mbalimbali mwilini (ina vitamini C ya kutosha)

*Inaondoa gesi tumboni

*Inasafisha na kuondoa sumu mbalimbali mwilini

*Inaondoa msongo wa mawazo (stress)

*Inadhibiti virusi (anti-virus)

*Inauongezea nguvu na ufanisi mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

*Inaondoa uchovu sugu na kuongeza nguvu za mwili kwa ujumla

*Inatibu maumivu na matatizo karibu yote ya tumbo ikiwemo bawasiri

Ni dawa ya uhakika kwa kutibu vidonda vya tumbo.

Usitumie dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa Tabibu.

K**a unahitaji Chronic ulcers Dozi yake inagharimu (210,000) niachie tu ujumbe WhatsApp +255749798009

Na ikiwa utanunua dawa hii ya asili kwa ajili ya kutibu kabisa vidonda vya tumbo kutoka kwangu, nitakufundisha na vingine vifuatavyo kupitia WhatsApp BURE kabisa ;

1. Vyakula na vinywaji ambavyo mgonjwa anatakiwa kula kuanzia chakula cha asubuhi, cha mchana na cha jioni kwa siku 7 jtatu mpaka jpili.

2. Vyakula na vinywaji ambavyo havina asidi nyingi mwilini

3. Namna ya kuipunguza hydrokloriki asidi inayozarishwa tumboni wakati wa mmeng’enyo wa chakula isilete madhara ya kutoboa kuta za tumbo na kukuletea vidonda vya tumbo.

4. Mbinu nyingine nje ya vyakula na vinywaji za kupunguza asidi mwilini

5. Namna ya kumuua bakteria wa vidonda vya tumbo kwenye vyakula au vinywaji vya lazima unavyotumia kila siku.

6. Namna nzuri ya kudhibiti msongo wa mawazo (stress) kwenye maisha yako. Msongo wa mawazo ni moja ya sababu nyingine inayoongeza na kusababisha vidonda vya tumbo.

SHARE POST HII NA WENGINE UWAPENDAO.

Kwa Pamoja Tunajali Afya Yako.Dr Gasto Lee0749798009
05/03/2024

Kwa Pamoja Tunajali Afya Yako.

Dr Gasto Lee
0749798009

Kwa Pamoja Tunajali Afya Yako..Dr Gasto Lee0749798009
05/03/2024

Kwa Pamoja Tunajali Afya Yako..

Dr Gasto Lee
0749798009

Address

MAGUFULI TERMINAL
Dar Es Salaam
255

Opening Hours

Monday 06:00 - 20:00
Tuesday 06:00 - 20:00
Wednesday 06:00 - 20:00
Thursday 06:00 - 20:00
Friday 06:00 - 20:00
Saturday 06:00 - 20:00
Sunday 06:00 - 20:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when GASTO LEE posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to GASTO LEE:

Share

Category