
16/10/2024
Moja ya swali ninaloulizwa sana ni vipimo gani nifanye k**a sibebi mimba?
Dr Kihwaga
Wenzi wakijaribu Kutafuta MTOTO kwa MWAKA mzima au zaidi pasipo mafanikio,k**a mwanamke ana shida tunasema ni 'UGUMBA' infertility kitaalamu.
Anatakiwa kuchunguza ijulikane chanzo cha kutokupata MIMBA na ATIBIWE accordingly.
yafuatayo yanatakiwa Kufanyika.
1️⃣Kuchukuliwa history(maelezo,hapa maswali huwa ni Mengi sana sanaaa kuhusu Mzunguko,sex,pombe,kutoa mimba,matumizi njia za uzazi wa mpango,kutoka uchafu etc),lakin pia Dr atamchunguza(examination) hapa kuna kuchunguza ndevu,chunusi(inaweza kuwa ishara ya kuwa na homon nyingi za kiume mwilin,au ugonjwa unaitwa PCOS (vivimbe kwenye mfuko wa mayai na mvurugiko wa homon) na mengineyo.
2️⃣Mwanamke anaetafuta MIMBA lazima ijulikane BMI yake,k**a SIO mwembamba sana au sio MNENE sana maana huwa vinaathiri uwezo wa Kubeba Mimba,k**a unene umezidi kupunguza uzito ni MUHIMU ili apate MIMBA,na k**a ni mwembamba sana atashauriwa aongezeke uzito
3️⃣.PICHA/ULTRASOUND ni MUHIMU pia,na ni kipimo cha awali sana kwa mwanamke ambae hapati Mimba,hiki tunaangalia k**a mwanamke ana uvimbe kwenye kizazi,mirija au kwenye mfuko wa mayai,endometriosis,PID.
4️⃣HORMONAL PROFILE,kipimo cha homon Pia Muhimu sana,Hormones Sio KIPIMO KIMOJA,Ni hormones mbali mbali ZINAPIMWA k**a kuna iliyo/zilizo chini au zipo juu kuliko kawaida mwanamke anatibiwa
Hormones tunazopima huwa ni HIZI
Follicle stimulating hormones,lutenaizing hormone,oestrogen,
Progestrones,Prolaction hormone,testosterones,Na thyroid hormones huwa zinapimwa kwa dalili zake.
5️⃣HSG yaan Hysterosalpingography kipimo cha kuchunguza Kizazi pamoja na MIRIJA k**a Imeziba au ipo vizuri.
6️⃣LAPARASCOPY hii ni Kipimo cha Kuchunguza mji mzima wa uzazi,mirija kujua k**a mirija haijaziba k**a kwenye kizazi kuna shida yeyote k**a mikunjo,uvimbe etc......kipimo hiki hufanyika theatre kabisa.
Vipimo HIVI sio kwamba kila Mwanamke anafanyiwa VYOTE.
Kila mwanamke anafanyiwa kipimo fulan kutokana na Dr alivyochukua maelezo yake na dalili alizonazo.
Na siku zote tunaanza na vipimo virahisi kwanza kuelekea vipimo vya Juu zaidi,mfano utapiga ultrasound kwanza kabla ya laparascopy.
mama unaetafuta MTOTO,umefanyiwa vipimo gani mpaka SASA?
Kwa zaida jamii huamini moja kwa moja shida ya kutopata watoto ni kwa wanawake tu lakini tafiti zinaonyesha zipo sababu zinazotoka kwa mwanaume pia tunashauri wote wafanyiwe vipimo ili kupata suluhisho la kudumu wasiliana nasi leo upate ofa ya punguzo la gharama za vipimo hivi vya uzazi kwa asilimia hamsini YES ni ni 50% tu kwa vipimo vyote hivyo tupigie kwa waliopo dar es salaam na mikoani pia 0765320641 / 0692470564