Afya ni Utajiri

Afya ni Utajiri Karibu Sana Ukurasa wangu wa Afya ni Utajiri, hapa utaweza kujifunza mambo kadha wa kadha kuhusiana na afya ya mwili na mazingira

JE WAIJUA KARAFUU !? NA JE WAJUA FAIDA ZAKE MWILINI !?KARAFUU ni zao linalotokana na mkarafuu.Kwa hapa Tanzania na Afrik...
17/12/2021

JE WAIJUA KARAFUU !? NA JE WAJUA FAIDA ZAKE MWILINI !?

KARAFUU ni zao linalotokana na mkarafuu.Kwa hapa Tanzania na Afrika Mashariki hupatikana sana huko visiwani Zanzibar. Umaarufu wa zao hili ni kuwa halimo katika kundi la vyakula wala vinywaji lakini ni kiungo na dawa muhimu sana kwa maisha ya binadamu.Unajua ni kwanin !????

Zao hili lina matumizi mengi, ambapo hutumika k**a kiungo katika vyakula na vinywaji, pia ni dawa kwa maradhi ya tumbo, meno na misuli vile vile hutumika katika kuleta harufu nzuri ya kinywa, mwili na mazingira ya nyumbani.

Pia hutumika katika uzalishaji wa bidhaa nyingine ikiwamo sigara, mafuta ya karafuu ambayo hutumika kwa kuchulia misuli inayouma, kutengeneza dawa za meno na manukato.

Karafuu hutumika kwenye vyakula mbalimbali ikiwamo nyama, biriani, pilau, mchuzi wa masalo na vyakula vikavu k**a vile vileja, beskuti na donat na kwa upande wa vinywaji karafuu hutumika katika chai na maziwa.

wataalamu wanasema kuwa karafuu husaidia usagaji mzuri wa chakula tumboni na ni nzuri kwa matibabu ya maumivu ya tumbo, tumbo kujaa gesi na kiungulia. Hivyo, ni miongoni mwa kiungo muhimu katika vyakula kutokana na vinasaba vya aina ya eugnol vilivyomo ndani yake.

Aidha, hutumika katika utengenezaji wa mafuta ambayo husaidia kusafisha damu. Tafiti zinaonyesha kuwa vinasaba vilivyomo katika karafuu vinapunguza sumu katika damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu.

Pia karafuu hutumika katika viwanda kwa ajili ya kutengezea dawa za meno kwa ajili ya kutunza meno na kuondosha maumivu ya meno na fidhi, kung’arisha meno na kuleta harufu nzuri ya kinywa, harufu iliyomo katika karafuu husaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni.

Karafuu pia inatajwa kusadia kutibu vidonda vya mdomo na kuimarisha afya ya fizi pamoja na kuzuia meno kuoza.

Madaktari wa meno wamekuwa wakitumia mafuta ya karafuu kwa ajili ya kutibu matatizo ya meno, hii ni kwa sababu mafuta hayo yamekusanya vinasaba vya eugnol ambavyo ni vizuri kwa meno na fidhi.

Karafuu inatumika katika urembo… wanawake hupenda kusugulia mwili (scrub) kwa kuchanganya unga wa karafuu kavu iliyosagwa na mafuta ya n**i na liwa ambapo husuguliwa mwili mzima kwa ajili ya kuondoa uchafu na kuufanya mwili kuwa nyororo.

Sabuni zinazotengenezwa kwa karafuu huondoa harara, vipele na chunusi na hivyo kuifanya ngozi iwe nyororo na yenye kuvutia.

Matumizi ya karafuu na mafuta yake humfanya mtu kuwa mchangamfu… humwondolea uchovu kwa vile karafuu inaiweka akili katika hali nzuri nakufanya ubongo ufanye kazi vizuri. Pia husadia kuondoa matatizo ya kusinzia, kupoteza kumbukumbu na wasiwasi.

Mafuta ya karafuu yanapochanganywa na chumvi, husaidia kuondosha maumivu ya kichwa, matatizo katika mfumo wa upumuaji, kusafisha koo na hutibu kikohozi, mafua na pumu.

15/04/2019

HOMA YA DENGUE

Dalili za ugonjwa huu ni homa, kuumwa kichwa, maumivu ya viungo na uchovu Dalili hizi huanza kujitokeza kuanzia kati siku ya 3 na 14 tangu mtu alipoambukizwa kirusi cha homa ya dengue. Kwa wakati mwingine dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria, hivyo basi wananchi wanaombwa kuwa wakati wakipata homa kuhakikisha wanapima ili kugundua k**a wana vimelea vya malaria ua la ili hatua stahiki zichukuliwe.

Virusi vya homa ya dengue vinaenezwa kwa binadamu baada ya kuumwa na mbu aina ya �Aedes�. Mbu hawa hupendelea kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au hata ndani ya nyumba. Viluwiluwi vya mbu hawa huweza kuishi katika mazingara ya ndani ya nyumba mpaka wakawa mbu kamili na kuanza kusambaza ugonjwa huu kwa binadamu.

Mbu hawa huwa na tabia ya kuuma wakati wa mchana. Ugonjwa huu hauenezwi kutoka binadamu mmoja kwenda kwa mwingine. Homa ya dengue inaweza kutibika k**a mgonjwa atapelekwa hospitali mapema na kupatiwa matibabu ya haraka.

Hakuna tiba maalumu ya ugonjwa wala chanjo bali mgonjwa anatibiwa kutokana na dalili zitakazoambatana na ugonjwa huu k**a vile homa, kupungukiwa maji au damu. Endapo mgonjwa atachelewa kupatiwa matibabu, mgonjwa anaweza kupoteza maisha.

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya dengueo Kuangamiza mazalio ya mbu

*Fukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo

* Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu k**a vile, vifuu vya n**i, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.

* Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
Hakikisha maua yandayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama.

* Funika mashimo ya maji taka kwa mfuniko imara
Safisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama
Kujikinga na kuumwa na mbu

*Tumia dawa za kufukuza mbu �mosquito repellants�
Vaa nguo ndefu kujikinga na kuumwa na mbu

* Tumia vyandarua vyenye viuatilifu (hata kwa wale wanaolala majira ya mchana).

*Weka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi.

03/04/2019

JINSI YA KUMTULIZA MTOTO MCHANGA ANAYELIA

20/08/2018

MAJANI YA MPERA NA FAIDA ZAKE MWILINI. 🍊
----------------------
1. Chai ya majani ya mpera inaponyesha kifua na kikohozi.
2. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu muwasho uliotokana na mzio (allergy).
3. Pia majani haya ya mpera yakichemshwa k**a chai yanaondoa cholesterol iliyozidi mwilini.
4. Chai ya majani ya mpera inapunguza kiwango cha tatizo la sukari mwilini.
5. Chai ya mpera ni dawa nzuri kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume.
6. Pia inatumika k**a scrub ya uso.
Chukua majani ya mpera saga kisha tia maji kiasi na inasaidia kuondoa uchafu usoni.

7. Pia majani ya mpera yakichemshwa ni dawa ya kuponyesha tumbo la kuhara.
8. K**a umejikata kidogo unaweza kutumia majani ya mpera yalioshwa na kusagwa vizuri kwa kupunguza maumivu na kukulinda na maambukizi ya bakteria.
9. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu eneo la mwili lililong'atwa na mdudu na kupunguza maumivu.
10. Chai ya majani ya mpera inaaminika kuwa ina uwezo wa kutibu tezi dume.
11. Kutokana na kuwa na vitamini C kwa wingi majani ya mpera yana uwezo mkubwa wa kutibu chunusi.
12. Chai ya majani ya mpera inasaidia kupunguza uzito mwilini na kuzuia uharibifu sukari ndani ya mwilini.
13. Majani ya mpera yanajaza nywele na kurefusha nywele kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele, unasaga na kuchemsha kisha acha yapoe ndio upake kichwani kutoka chini ya ngozi ya kichwa hadi kwenye ncha ya nywele zako.
14. Ukiwa na tatizo la vidonda kwenye ufizi, maumivu ya jino na ufizi tafuna majani ya mpera na utaona maajabu ya majani haya.
15. Chukua majani ya mpera saga vizuri mpaka yawe laini kabisa ongeza na maji kidogo kisha tumia kupaka usoni k**a scrub inatibu ngozi inayoanza kuzeeka mapema.
16. Chai ya mpera inasaidia kwa kutibu mvurugiko wa tumbo.
Pamoja na majani hayo kuwa msaada wa kutibu maradhi mbalimbali , halikadhalika juisi ya mapera nayo husaidia sana kutibu mgolo au bawasiri, figo na hata kuondoa mafuta katika moyo.
Kimsingi mti wa mpera karibu kila sehemu yake ni tiba kwani hata mizizi yake inapochemshwa na kutumia kwa kunywa huenda kuwasaidia wanawake wenye matatizo ya hedhi au wenye matatizo ya kutokwa na maji yenye harufu mbaya sehemu zao za siri.
17. Majani ya mpera yanaondoa tatizo la kukatika kwa nywele. Chemsha majani kisha wacha yapoe na ukande kwenye paji na eneo la ngozi taratibu kwa dakika 15, Wacha kwa dakika 30 kisha osha na maji safi bila shampoo au sabuni. Fanya hivyo mara 3 kila wiki.

NAMNA YA MATUMIZI

Kuitengeza chai ya majani ya mpera. Kuna namna mbili.
- Aidha chemsha maji k**a glasi nne mpaka itokote sana, chukua majani k**a 10 ya mpera, weka ndani ya yale maji moto kisha funika kwa dakika 10 - 15 koroga, chuja, chai yako tayari.

- Aina ya pili ni chemsha maji hayo pamoja na majani yakiwa ndani. Ikitokota ondoa kwenye moto, wacha kwa dakika 10 -15 chuja, chai tayari. Waweza ukatumia majani yaliyo kauka pia. Zingatia ukichanganya na ASALI badala ya sukari ndio bora zaidi.

ASANTENI SANA……………

Usiache ku-SHARE na wengine wapate elimu hii.

JARIBU NA TWAKUTAKIA UPONYAJI BORA..

MAJI YA VITUNGUU NA UTUNZAJI NYWELEWanawake na mabinti, wadada wanatambua umuhimu wa mwonekano mzuri hukamilika pale wan...
23/06/2018

MAJI YA VITUNGUU NA UTUNZAJI NYWELE

Wanawake na mabinti, wadada wanatambua umuhimu wa mwonekano mzuri hukamilika pale wanapokuwa na nywele nzuri za kutosha na zenye afya yake ya asili. Tatizo la kupotea kwa nywele au upara (wengine hupenda hali hii) limekuwepo tangu enzi na enzi. Kipara kinaweza kuja kwa sababu za kimaumbile na kuwa la kawaida ama sababu zifwatazo.

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kupotea kwa nywele k**a vile:

* Sababu za kimazingira
* Kuzeeka
* Msongo wa mawazo (stress)
* Kuvuta sigara kupita kiasi
* Lishe duni,
* Homoni kutokuwa sawa
* Kurithi vinasaba,
*Maambukizi kwenye ngozi ya kichwa
* Matumizi yasiyo sahihi ya vipodozi vya nywele
* Baadhi ya dawa za hospitali
* Matatizo katika kinga ya mwili
* Upungufu wa madini chuma, na
* Magonjwa mengine sugu

Kitunguu maji kina kazi nyingi katika mwili wa binadamu kwani hutibu magonjwa mengi k**a kikohozi, vidonda vya tumbo na mifupa, ngozi, koo, figo, na pia kina virutubisho vingi vya vitamini C.

Kitunguu hiki huwa na salfa (sulphur) ambayo husaidia kutengeneza tishu za ‘collagen’ katika mwili ambapo huipa nywele na ngozi nuru ya aina yake.

Hivyo naweza kusema kuwa juisi ya kitunguu maji husaidia kukuza nywele na kwa wale wenye nywele za kukatika, kupaka kitunguu maji mara kwa mara kunaweza kusaidia kupambana na tatizo hilo.

Jinsi ya kuandaa

Chukua kitunguu kimoja au viwili kutegemea na na ukubwa wa kitunguu chenyewe

Osha vizuri kitunguu au vitunguu na kisha ukimenye au uvimenye

Kata kitunguu au vitunguu vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kusaga au kutwanga

Saga kwenye blenda au uvitwange kwenye kinu.

Visage au vitwange mpaka vilainike kabisa ili uweze kutoa maji kwa urahisi.

Vichuje vizuri ili upate majimaji. Hakikisha kwamba huongezi maji kwa hivi vitunguu.


Jinsi ya kupaka

Nywele sio lazima ziwe safi maana unapaswa kuziosha baada ya kupaka maji ya vitunguu.

Chukua pamba ambayo utatumia kupaka hayo maji ya vitunguu kwenye nywele zako. Paka zile sehemu ambazo nywele zimekatika. Unaweza pia paka kichwa kizima.
Baada ya kupaka unapaswa kuvaa kofia ya plastiki na kitambaa kichwani ili uweze kupata joto.
Ukae hivyo kwa muda wa saa 4 - 5
Baada ya hapo unaweza kuosha na kukausha nywele zako.


Hitimisho

Ni vyema kufanya shughuli hii ya kupaka vitunguu angalau mara mbili kwa mwezi.

Ikiwa harufu ya kitunguu ni kali, unaweza kuongezea asali kidogo kwenye maji ya vitunguu.

Kwa matokeo mazuri ya kukuza na kutunza nywele zako, tumia vitunguu vidogo kufanya jinsi nilivyoeleza hapo juu.

Nipe matokeo kwa kukomenti hapo chini ama nipigie kupitia +255743753561

Wataalamu wa afya ya kinywa na meno wanashauri tubadili miswaki tunayotumia kila baada ya miezi sita. Ufanisi wa mswaki ...
22/05/2018

Wataalamu wa afya ya kinywa na meno wanashauri tubadili miswaki tunayotumia kila baada ya miezi sita. Ufanisi wa mswaki hupungua unapoutumia kwa zaidi ya kipindi hiki.

Tukumbushane huo wa kwako ulianza kuutumia lini?!

Kulala umefunika kichwa husababisha seli nyingi za ubongo kufa haraka kwa kukosa hewa safi (oksijeni) hivyo kuathiri ute...
22/04/2018

Kulala umefunika kichwa husababisha seli nyingi za ubongo kufa haraka kwa kukosa hewa safi (oksijeni) hivyo kuathiri utendaji wa ubongo mfano kuharibu mfumo wa utunzaji kumbukumbu!

JINSI YA KUWA MWANAUME MASHINE KIASILI !!Natumaini mu wazima Wa afya tele mkiendelea na harakati za kulijenga Taifa letu...
27/03/2018

JINSI YA KUWA MWANAUME MASHINE KIASILI !!

Natumaini mu wazima Wa afya tele mkiendelea na harakati za kulijenga Taifa letu kwa kasi kubwa !! Mungu akapate kubariki kazi ya mikono yako na Taifa letu

Twende pamoja sasa !!!

Wanaume tumekua katika wakati mgumu sana ile jioni tunapotoka katika mihangaiko yetu na wakati mgumu sana pale unapokua Muda Wa kulala umefika na Wakati mgumu zaidi pale unapotambua mwenzi wako anakuitaji kimwili !! Hapa ndipo Hofu ile inapoanzia hofu inayokupa maswali Mengi, maswali yanayokuumiza kichwa na kujiona k**a mwanamme Mnyonge sana mbele ya mwanamke wako !!!

Sijui Leo nitafanya Mara ngapi?? Je nitampa kamoja tu??? Je nitamwaga ndani ya dakika mbili k**a Jana ??? Je Leo pia Uume utakua lege lege?

Je, nitamfanya afike kileleni (Hili ni somo lingine. Naufahamu asilimia 90 ya wanawake hawajawahi kufikishwa kileleni au kukojoleshwa, wengi wao huwa wanaigiza kukojoleshwa) Mmmmhhhhh mambo yan**idi kua mambo.

Tuendelee zetu wakuu !!! Mdogo mdogo k**a lkn tutafika

Hayo yote ni maswali machache ambayo hutufanya kuona chumba ni kidogo na usiku ni mrefu!!! Usilie Leo nakupa mavitu ya KITAALAM zaidi na Utafurahi na atakufurahia na utanipa majibu mazuri zaidi. Piga makofi basi.

SASA naomba Muscles, Brain, Nerves zako zote uwe makini ktk haya nitakayoyasema!!!, Utaenda kuyatibu matatizo yako yote ya tendo la ndoa, No matter una kibamia au mpini!!!!

Haya ndiyo mambo yakufanya Ambayo hutotumia garama na nirahisi kufanya na hayatumii muda na yanasaidia 98% tuseme tu 100% au sio wakuuuu ,!!! Kuanzia Leo naamini utaimarisha misuli ya Uume wako ,,utaufanya kua na nguvu ,, utaufanya usimama haraka baada ya kumwaga ,,kwaiyo mtafurahishana sana kwakua hamu utakua pale pale na Uume utakua wenye nguvu !! Naam tuendelee sasa .

1) MAZOEZI YA KEGELI .
KEGELI ni nini ??? Kegeli ni msuli Wa chini unaopatikana katikati ya A**s na sc***um( mahali ambapo kifuko cha kubebea korodan kinaanzia ). Mkuu Bado tu hujapapata ???? Usijali twende pamoja !!! Je Umewahi kua unakojoa alafu ukasimamisha mkojo gafla usitoke kisha ukaendelea kukojoa ???? K**a bado Leo wakati unakojoa ,, jaribu kusimamisha mkojo usitoke kisha endelea kukojoa ,,simamisha tena ,,kisha kojoa ,,alafu simamisha tena ,,kisha acha utoke ,, ,,Msuli uliokusaidia usimamishe mkojo japokua kibofu bado kinamkojo ndio unaitwa KEGELI !! hapa naamini wakuu tunaenda pamoja sasa !!!.
Sasa baada ya kujua Msuli Wa kegeli Fanya ivi ,,,Hakikisha upo mahali ambayo haiyofanya misuli mingine yamwili kufanya kazi,, datz umekaa mahali popote hata ofsin au garin ,,popote yaan ..eeeeeehhhhhhh

Kisha anza kufanya km UNASIMAMISHA MKOJO usitoke ( hapa unajua hukojoi ) yaan una ashumu km unakojoa lkn hukojoi ,,lengo nikuanza kuuvuta huu msuli,, Simamisha kwa sekunde anza 2-3-4-5-----9 unaposimamisha unahold on kwa izo sekunde kisha unaachia unahold on unaachia ,, Fanya ivo kwa Mitupio thelathini kila unapopata muda ( usipungue mitupio 30 Mara tatu kwa siku ,,yaan uanzia angalau mitupio 90 kwa siku )
Faida ..... 

-Kegeli hukomaza misuli ya Uume .
-Kegeli hukomaza mishipa ya dam uumeni .
-Nirahisi ,,sio garama ni time saver !!

2/ BAKIA KUA MWENYE MAJI MWILINI .

wanaume wenzangu Kua wakavu mwilin umekua sababu kubwa ya uume kua legelege kusimama .

Naomba mjue kua ili Uume usimame vzuri nilazima kuwepo na Flow nzuri ya Damu mwilin nakiasi kingi cha damu mwilin....asilimia 70 ya damu nimaji .... Ivyo unavyokua unakunywa maji unaonheza kiwango cha damu ,,unaongeza na flow yadam ,, kwaiyo inasaidia sana wakati watendo dam kuflow nyingi uumeni nahuo ndo mwanzo wauume kusimama haraka na ulojaa na wenye nguvu !!!!

Kuanzia Leo hakikisha unakua MTU wakunywa maji k**a Rey kwajili ya Uume wako !!!!! Mavitu hayoooo !!!.

3/ MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI .

Hivi nivitu ambavyo wengi tunavidharau ,,kuvitumia mpaka tuwe tunauumwa ???? Khaaaahh brother haupo serious na mwanamke wako !!!

MATUNDA na MBOGA ,, ni kitu vyenye utajiri mkubwa Wa Vitamin,, Madini ,, Phytochemicals,, Antioxidants ... Vitu hivi kwa pamoja Husaidia Nerves kufanya kazi vzur ,, husaidia misuli kufanya kazi vzuri na mwisho vinatumika kutengeneza Damu ...

N.b ,, The More the low amount of blood the low the kudidisha Uume wako

4)-MAZOEZI YA VIUNGO .
Aisee hapa sizungumzi kunyanyua mivyuma mizito utazan unajiandaa kupambana na ile mijitu mikubwa kwwnye muvi ya " Jack and the Giants Slayer "" .. Kufanya mazoezi yaviungo husasani yanayohusiana na upumuaji ( pumzi ) ni vzuri sana !!! Kwan Pumzi nimuhimu mno ktk suala ndoa. Na pia mazoezi yaaina hii husaidia misuli kuunguza nishati kwa kasi nzuri .

Fanya mazoezi bro , otherwise Juma mcheza mpira atakupigia mwanamke !!.

5/BAKIA KUA MTU POSTIVE .
Wakuu hakikisha huwi MTU Wa mawazo na HUNA mawazo wakati upo mapajani mwa mwanamke ,,Stress kills s*x ,, nanaomba utambue S*x start in Mind ,, kwaiyo usiwe namawazo ,, Jiamin,, jiongoze ,, jione we ni great lover mzuri ,,, nakuhakikishia Mwili wako lazima utafuata mawazo yako tu kaka !!! Na mtoto utampa huduma matata KIASI kwamba kila akiwaza s*x ,,anakuwazia kufanya s*x Naww tuuu.

6// TABIA YA KIAFYA .
Wakuu kwa ubora mzuri kitandan nivema ukaachana na tabia ya uvutaji sigara ,, pombe ,, nakadhalika ,, kwa kua hivi nivitu vinavyoathiri Reproductive system moja kwa moja !!!!.

Namwisho ngoja niwape kitibabu kidogo.

KITUNGUUUUUUU KITUNGUUUUU KITUNGUUUUUUUU.

Wakuuu km suala LA kudidisha nitatizo ....Uume legelege ,, HUNA ham ya kurudia tendo ,,ukiwa nayo Uume unasimama km mlenda ,, Baada ya kufanya mambo hayo juu niloyataja ,,

Nunua vitunguu na Asali ,,weka kwako .... Chukua vitunguu viwili ,to a maganda ,, kisha toboa kitundu kidogo juu ya kichwa cha kitunguu na chini kwenye eneo LA mizizi ..viweke kwenye kibakuli ,,, mwagia asali katika kitundu cha kichwan mwa kitunguu hakikisha kila kitunguu kimewekwa asali ,,, kisha vifunike .....USIKU BAADA YA KULA CHAKULA CHA USIKU CHUKUA KIMOJA TAFUNA ,,ENDELEA NA RATIBA NA MWENZI WAKO ,,ASUBUHU TAFUNA KILICHOBAKI ,,NA ANDAA VYAUSIKU UNAOFUATA ,,FANYA IVYO KWA MWEZI NAHATA UKIONA KIKA SIKU NISAWA TU MAANA VITUNGUU VINATIBU NAMAGONJWA MENGI NAHAVINA ATHARI ....KWA KUFANYA IVYO UTAKUA UMEEPUKANA NA MATATIZO YOTE YATENDO LANDOA ..UWE UMEZALIWA HUSIMAMISHI !!!

naomba mkishafanya hayo ,, msisite kunipa FEEDBACK wakuuu !!!!

Ni vyema kuanza siku asubuhi kwa kunywa maji ya kutosha (kuanzia glasi moja).Hii itakusaidia kuamsha mwili, utakuwa na n...
25/03/2018

Ni vyema kuanza siku asubuhi kwa kunywa maji ya kutosha (kuanzia glasi moja).
Hii itakusaidia kuamsha mwili, utakuwa na nguvu, mwepesi na mwenye umakini wa akili siku nzima

NB:Unaweza ongeza ndimu kipande kimoja ndani ya maji (yakiwa na uvuguvugu inafaa zaidi)

Address

Nyerere Road, Ukonga
Dar Es Salaam

Telephone

+255743753561

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya ni Utajiri posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Afya ni Utajiri:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram