03/08/2024
Unene unanyemeleaga jamani 😅😅😅
Unaongezeka taaaaratibu bila kushtuka,mwili unaongezeka kidogo kidogo na sio rahisi kushtuka.
Zingatia hivi vitu
1.Kuanza kubanwa na nguo zilizokua size yako (uschukulie poa)
2.Kuanza kubadilisha aina ya mavazi ili uwe huru zaidi (hutaki kubanwa banwa)
3.Kubadilika ubora wa ngozi yako (pimples)
4.Kushindwa kufanya au kufanya kwa ugumu shughuli mbali mbali zinazohitaji kutumia nguvu au haraka haraka
(Mimi ukisikia nasema sipendi kukimbia najua nimeshaongezeka)
5.Uchovu wa kudumu hata ukipumzika hauondoki (fatigue)
6.Maumivu ya Viungo (Mgongo,kiuno ,Miguu)
7.Uvivu/Uzembe (Hata kufanya vitu vidogo vidogo)
8.Mapigo ya Moyo kwenda mbio (Kuhema Juu Juu)
9.Kuwa tegemezi wa vinywaji Vya kuongeza nguvu ili uweze kufanya kazi vizuri (Kahawa,Energy drinks)
10.Kula hovyo,kutamani vyakula flani flani vyenye sukari,mafuta au wanga kwa wingi (cakes,soda,sweets,pizza,chips)
Na viashiria vingine vingi Kulingana na mtu na mtu.
Haya Mimi huyu na kilo zangu 70.1 hata mimi nimeshangaaa!😱
Muonekano usikudanganye,jua ndani ni nini kinaendelea.
Natakiwa kuondoa kilo 10 ili niwe katika Hali bora zaidi ya ufanisi ya mwili wangu.Uzuri ni kuwa najua cha kufanya,Mchakato Umeanza.
Jambo la kuzingatia,Jipende,Jipende sana,usithubutu kujiruhusu kujichukia kwa muonekano uzito uliokuletea,huo Mchakato utakua mgumu sana.Jipende jithamini na lengo Kuu liwe kuboresha Afya,muonekano utakuja pamoja na Afya.
#