
15/08/2025
BIASHARA 20 ZA KUANZA NA LAKI MBILI NA KUJENGA MAFANIKIO
1. Genge la matunda na mbogamboga na vitu vya nyumbani.
Tafuta sehemu yenye makazi/ wanaopita watu wengi (hasa wanaotoka kazini), nunua matunda na mboga sokoni kwa jumla, uza kwa bei ya rejareja.
Hii ni biashara nzuri na huwa inaonekana ya watu wa hali ya chini lakini imewatoa wengi mnooo
2. Biashara ya urembo wa bei nafuu
Nunua hereni, shanga, vikuku, pete kwa jumla Kariakoo au mitandaoni, uza kwa marafiki, chuoni, mtaani kwako,kazini, au siku za gulio.
Hii mtaji mdogo tu hata laki mbili au chini ya hapo unaanza. Hakuna mdada asiyependa kupendeza na hawezi shindwa nunua kwako wajati ni 2000 wewe umenunua kitu kwa buku.
Chimbo wanaotoa China 0765135589
3. Nguo za ndani
Nunua kwa jumla (bra, chupi, boxer) kutoka Kariakoo, makumbusho, tandika kwa staili nzuri. K**a mtaji mdogo nunua zile za bukubuku,1300 adi 1500 na wewe kauze Tsh 2000 adi 30000 tu. Usiweke faida kubwa, lengo ni laki yako ikupe laki nyingine.
Chimbo stoo za makumbusho 0743356395 au 0763356395.
4. Vitafunwa (viazi, maandazi, sambusa, chapati)
• Namna ya kuanza: Nunua vitu, pika nyumbani au sehemu ndogo, uza ofisini, shuleni, mitaani pika kwa oda kwenye sherehe, harusi, vikao au mafundi wa mitaani
5. Mikoba ya bei nafuu
Nunua mikoba midogo na mikubwa kutoka kwa wauzaji jumla, na fungua duka lako au uza online, zungusha kwenye magulio, kwenye maofisi, vyuoni, makazini, nk
Target wanafunzi wa vyuo na wanawake wa kazini au wa nyumbani.
Nikupe chimbo. Chimbo ni Dukani kwangu mwenyewe natoa china kukuletea kwa bei ndogo. Duka liko makumbusho Plaza Duka namba 26
6. Juisi na vinywaji baridi
• Namna ya kuanza, Nunua blender, chupa, na matunda, tengeneza juisi safi, uza barabarani au ofisini.
Hii ni Biashara nzuri na yenye mafanikio makubwa kwa watu wengi hasa maeneo ya mijini.
Nikupe chimbo la Blender original unayopata warranty mwaka mzima? Ni kariakoo mtaa wa Pemba. Chimbo Brenda hata moja 0620191536
7. Kuuza mitumba
Nunua bale ndogo ya nguo za mitumba, chagua nzuri, uza online na mtaani. Watanzania wengi huvaa nguo za mtumba.
Unapata wapi? Pata Ilala Boma mtaa wa Tabora na Pangani utapata belo safi nguo aina zote na mkoani utatumiwa Piga 0769297877
K**a huna uwezo wa belo Amka asubuhi naapema nenda Ilala Boma utapata.
Piga picha nzuri na uza kwa staili ya “story telling” mitandaoni. Zunguka kwenye magulio au fungua kibanda au uza mtaani kwako
8. Chipsi na mayai
Tafuta sehemu yenye msongamano wa watu, nunua vifaa na mahitaji mengine anzisha. Kwa Watu wa Dar hii ni fursa zaidi na walio karibu na vyuo au stend
9. Kuuza viatu vya mitumba
Nunua kiatu kwa bei ya jumla 5,000–7,000, uza 12,000–15,000.
Chagua viatu safi na vya kuvutia. Iwe vya k**e, kiume au wanawake ni deal
10. Sabuni na bidhaa za usafi
Nunua sabuni kwa jumla, pack kwenye mifuko midogo, uza majumbani na sokoni.
11. Mayai ya kuchemsha
Nunua tray ya mayai, chemsha, uza kwenye vikombe na chumvi
Sehemu yenye wanafunzi na wafanyakazi na stend au sehemu za mikusanyiko kuna soko kubwa zaidi.
12. Uuzaji wa maua na mapambo
13. Biashara ya kanga na vitenge
Nunua kanga na vitenge kwa jumla, uza mtaani au online.
14. Simu na accessories
simu viswaswadu Nunua chaja, earphones, kava za simu kwa jumla, uza mtaani au kibanda
Uwe na vitu vipya vinavyotoka sokoni.
15. Biashara ya kufunga zawadi
16. Perfume
Nunua perfume refill, pack kwenye chupa ndogo, uza bei ya 2,000–5,000.
17. Uuzaji wa mafuta ya kupikia kwa rejareja
Nunua dumu la mafuta, uza kwenye chupa ndogo ndogo. unaweza kutoa Singida
18. Vifaa vya watoto
Nunua chupa za watoto, toys ndogo, mabegi ya shule.
19. Biashara ya mashuka na mapazia.
Unaweza anza na pisi chache tu.
Machimbo ya mashuka na mapazia ni kariakoo mtaa wa mchikichi na sikukuu. +255 744 334 554 mwingine +255 789 612 741
20. Kuuza biskuti na p**i
Nunua kwa jumla kutoka Kariakoo, uza mitaani au kwenye maduka na maeneo wanapopita wanafunzi wengi.
Kwenye hizi Biashara 20. Ni ipi umeipenda na unatamani niichambue zaidi?
Biashara gani nyingine ya mtaji mdogo ila ina faida nzuri sijaiandika ila unaijua tuambie kwenye comment tujifunze