AFYA NI MTAJI

AFYA NI MTAJI AFYA NDO MTAJI WAKWANZA WA MWANADU

UGONJWA WA U.T.I (URINARY TRACT INFECTION) – CHANZO, DALILI & TIBAUTANGULIZI – UJUE UGONJWA WA U.T.I (URINARY TRACT INFE...
15/09/2022

UGONJWA WA U.T.I (URINARY TRACT INFECTION) – CHANZO, DALILI & TIBA

UTANGULIZI – UJUE UGONJWA WA U.T.I (URINARY TRACT INFECTION)

U.T.I ni maambukizi kwa njia ya mkojo na huathiri mfumo wa mkojo na mfumo wa uzazi, wadudu huathiri sana kibofu na urethra. Jina U.T.I ni kifupi cha URINARY TRACT INFECTION (Neno la kingereza) watu wengi huzoea kuita hivyo wakijua ni jina la kiswahili, imeshazoeleka hivyo. Jinsia ya k**e wana hatari kubwa kuliko jinsia ya kiume. Maambukizi yakwenye kibofu huleta maumivu makali, madhara makubwa hutokea maambukizi yakifika mpaka kwenye figo. U.T.I husababishwa na wadudu wadogo sana ambao ni bakteria waitwao Escherichia coli (E. coli), wanapoingia mwilini na kuenda kuathiri mfumo wa mkojo.

U.T.I hutibika haraka kwa mtu ambaye atatumia dawa na pia yaweza kuleta madhara makubwa isipotibika huweza kuathiri mfumo wa uzazi, kibofu, na sehemu mbalimbali, tunashauri mtu mwenye U.T.I inatakiwa awe msafi na kubadili mienendo iliyo hatarini.

UTI+Header
MGAWANYO WA U.T.I

Kuna mgawanyo wa aina mbili za U.T.I

Maambukizi ya Upande wa juu – Hii hujumuisha Figo na Ureta
Maambukizi ya Upande wa chini – Hii hujumuisha Kibofu na Urethra
CHANZO CHA MAAMBUKIZI YA U.T.I

U.T.I husababishwa na wadudu wadogo sana ambao ni bakteria waitwao Escherichia coli (E. coli), wanapoingia mwilini na kuenda kuathiri mfumo wa mkojo, vitu vifuatavyo vinaweza kukuingiza kwenye hatari ya kupata U.T.I;

Kinga ya mwili kuto kuwa imara
Kutumia Vifaa au Dawa za kuzuia mimba
Kwa wa k**e; Kupungua kwa homoni ya estrogeni
Mtu mwenye kisukari
Kutumia choo kichafu na kutumia idadi kubwa ya watu
Kuwa na tatizo la mmeng’enyo na tatizo la choo
Kukaa kwa mda mrefu bila kutembeatembea
DALILI ZA MTU MWENYE U.T.I

Dalili za mtu mwenye tatizo la U.T.I hutokea tofauti kulingana na umri, jinsia na sehemu iliyoathiriwa. Hizo dalili ni k**a;

urinary_tract_infections-1
Kujihisi mchovu na kutokujisikia vizuri
Kukojoa kwa shida na kujilazimisha
Maumivu wakati wa kukojoa
Kukojoa kiasi kidogo na mara kwa mara
Mkojo kutoa harufu kali
Mkojo kuwa na rangi tofauti zisizo za kawaida kwa mfano wekundu kiasi
Kichefuchefu au kutapika
Maumivu ya tumbo, au pande za mwili karibu na tumbo mpaka sehemu za misuli
Joto laweza kuongezeka
JINSI YA KUEPUKANA NA U.T.I

Kunywa maji mengi
Acha kutumia dawa za uzazi wa mpango
Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
Kojoa hata kidogo baada ya kujamiiana
Punguza au acha kunywa pombe na kutumia sigara huchochea kuathiri kibofu
Kuwa msafi hasa sehemu za siri ili kutoruhusu bakteria
Usipulizie spray kwenye sehemu za siri
TIBA YA UGONJWA WA U.T.I

U.T.I hutibika kwa kuwaondoa bakteria na fangasi sehemu zilizoathirika kwa kutumia dawa, mtu mwenye U.T.I hupata shida sana na mpaka humpelekea kutokuwa na raha. Mtu mwenye U.T.I asipoitibu husababisha vimelea kuzaliana na kuwa vingi hii huitwa U.T.I sugu yuko hatarini kuwa na tatizo kubwa na pia hukaribisha magonjwa mengi.

DAWA

Tuna dawa ya kutibu U.T.I ambayo ni ya asili isiyo na kemikali ambayo hufanya mtu kupona na kuimarika kabisa. : Dawa hiyo hutibu kwa mda kulingana na mda wa tatizo, tatizo halirudi tena maana huondoa chanzo pamoja na ugonjwa sio kituliza maumivu, ukianza kutumia baada ya siku 5 huonesha mabadiliko, pia mgonjwa anapewa mfumo wa maisha ambao inatakiwa autumie kwasababu kuna mtindo wa maisha unaendelea kuongeza tatizo pia kuna mtindo unapunguza hatari ya ugonjwa.

Tunamshukuru Mungu kwa uumbaji wake na kutupa dawa ambazo alizileta ili kutuimarisha na kutuponya, Mungu hakuumba dawa nyingine zaidi ya mimea na vitu vingine vya asili, japo wengi hudharau. Mungu tunaomba utuokoe na kutuponya.

MAWASILIANO
0710264170
0755804170

🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝CHANZO CHA FUNGUS UKENI NA TIBA ZAKE  Habari za leo ndugu msomaji wa makala za *Dr kyando* leo nimependa kuzungum...
15/09/2022

🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝
CHANZO CHA FUNGUS UKENI NA TIBA ZAKE



Habari za leo ndugu msomaji wa makala za *Dr kyando* leo nimependa kuzungumzia ugonjwa wa fangasi ukeni ambao ni common hususani kwa wanawake,
maambukizi ya fangasi sehemu za siri imekua ni tatizo kubwa sana Duniani 75%ya wanawake wote Duniani wanasumbuliwa na tatizo hili
maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na fangasi aina ya CANDIDA ALBICANS, maambukizi haya pia hujulikana k**a YEAST INFECTIONS /THRUSH
CANDIDA ALBICANS hupatikana katika midomo, mpira wa kupitishia Chakula (PHARYNX), kibofu cha mkojo, uume au katika uke pia.
~bacteria Hawa huishi katika sehemu hizo Bila kuleta madhara, isipokua pale mazingira ya eneo husika, yanapobadilika, MFANO mabadiliko katika Hali ya PH tutambue PH ya mwanamke ndani ya uke ni 4.0_4.5 au uwiano wake na vimelea (microorganisms) wengine, hivyo huharibiwa kutokana na sababu mbalimbali k**a vile MATUMIZI YA MADAWA YA ANTIBIOTICS k**a AMPICILLINE, CIPROFLAXINE, AMOXYLINE, DOXYCYCLINE, ERTHROMYCINE, NK pia kupungua kwa Kinga kutokana na magonjwa mbalmbali .
~maambukizi ya fangasi ukeni yamegawanyika katika sehemu KUU mbili nazo ni ÷
(1)MAAMBUKIZI YASIYO MAKALI (UNCOMPLICATED THRUSH)
~katika aina hii mgonjwa hupatwa na maambukizi Mara moja hadi nne kwa mwaka pia Dalili zake huwa si za kuogopesha na maambukizi haya husababishwa na fangasi aina ya CANDIDA ALBICANS
(2)MAAMBUKIZI MAKALI (COMPLICATED THRUSH)
Katika kundi hili mgonjwa hupatwa na maambukizi Zaidi ya Mara nne au Zaidi kwa mwaka pia Dalili zake huwa ni za kuogopesha k**a maambukizi yatakua yametokea kipindi cha UJAUZITO, ugonjwa wa VVU, ugonjwa wa sukari nk

VIHATARISHI VYA MAAMBUKIZI YA FANGASI KATIKA UKE
· Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini ambazo husababisha mabadiliko katika sehemu za siri
· magonjwa ya saratani ya tezi koo la Chakula (thyroid cancer)
· wanawake wenye umri wa miaka 20_30 wapo katika hatari ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi (menopause) na wale ambao hawajaanza kupata hedhi hawako katika hatari kutokana na mazingira na vitu wanavyotumia
· upungufu wa Kinga mwilin kutokana na magonjwa hatar ya saratani, kisukari, ugonjwa wa mononucleosis nk
· matumizi ya vidonge vya majira
· msongo wa mawazo
· kujamiana kwa njia ya kawaida Mara tu baada ya kujamiiana kupitia haja kubwa (a**l s*x)
· matumizi ya glycerin wakati wa kujamiiana husababisha maambukizi pia
· kuwa na historia ya kupata matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy)
~ujauzto (husababisha kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini
~kuwa na utapiamlo (malnutrition
~kuvaa nguo za ndani ziszo kauka vzur
~kuvaa mavazi yanayoleta sana joto sehem za siri

DALILI ZA UGONJWA WA FANGASI UKENI
· kuwashwa sehem za siri
· kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana (superficial dysapareunia)
· kuhisi kuwaka moto sehemu za siri Mara baada ya kutoka kufanya tendo la ndoa au kutoka kukojoa (burning sensation
· kupata vidonda ukeni (soreness
· kuvimba na kuwa mwekundu katika mdomo wa nje wa uke (l***a minora
· kupata maumivu wakati wa kukojoa
· kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa MWEPESI au MZITO au majimaji
NOTE :Dalili na viashiria hivi huwa mbaya Zaidi mwanamke anapokua mwezini

MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU WA FANGASI UKENI
Matibabu ya ugonjwa huu wa fangasi hupatikana kwa urahisi Tanzania na tiba hupatikana na kutolewa kupitia vipimo vya uchunguzi na majibu yalivyotoka pamoja na hayo matibabu ya ugonjwa huu hospital sio ya uhakika kwasababu dawa za hospital hazitibu chanzo cha tatizo hivyo ndio maana tatzo hili huwa Linajirudia baada ya muda fulani, pamoja na hayo ugonjwa huu unaweza kujiknga nao kwa kuepuka mambo mbalimbali na kufanya mambo yatakayotusaidia kutopata ugonjwa huu kwa kuzingatia kanuni ya afya na USAFI
· Vaa chupi ambazo hazibani na zilizotengenezwa kwa pamba au hariri epuka kutumia chupi aina ya synthetic underwear.
· epuka kufanya mapenzi na mpenzi wako mwenye maambukizi haya
· kula mlo wenye virutubsho muhimu
· epuka kuoga maji ya moto sana (Hot baths) tumia maji ya uvuguvugu
· osha sehemu zako za siri kwa kutumia maji Safi na jikaushe kwa kutumia taulo au kitambaa Safi
· epuka mavazi yote ya kubana ukeni.
· tumia ped na pantiliner zenye anions chip zenye uwezo wa kufyonza haraka zenyewe zinaitwa NEPLILY SANITARY PADS ambazo mara nyingi hazipatikani madukani, hvyo basi tujulishe tuweze kukutumia pale ulipo.
· kunywa maziwa aina ya mtindi yenye live culture Mara kwa Mara yatakusaidia kuepusha maambukizi ya fangasi ukeni
· epuka matumizi ya vifaa vya kupanga uzazi na vifaa vya kufanyia mapenzi (s*x toys, diaphragm cervical caps) husababisha maambukizi ya fangasi ukeni
· epuka kutumia sabuni za kemikali/dawa kuoshea ukeni nakushaur utumie lady intimate sabuni ya asili isiyo na kemikal na inayoboresha uke wako .
Kwa ushauri na matibabu wasiliana nami
0710264170
0755804170

*UGONJWA WA PID* (Pelvic Inflammatory Disease)au Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi waMwanamke.Magonjwa ya zinaa ndio saba...
11/08/2020

*UGONJWA WA PID* (Pelvic Inflammatory Disease)
au Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi wa
Mwanamke.
Magonjwa ya zinaa ndio sababu kuu ya
wanawake kupata maambukizi katika mfumo wa
uzazi yani (PID). Mwanamke 1 kati ya wanawake 8 walipota PID katika wakati wowote ndani ya maisha yao hupata tabu kushika mimba

*(PID) NI NINI?*
PID ni maambukizi katika mfumo wa uzazi wa
mwanamke na mara nyingi husababishwa na
magonjwa ya zinaa k**a gonorrhea na
chlamydia ila kuna aina ya maambukizi mbali na
magonjwa ya zinaa yanaweza kusababisha
maambukizi ya PID.

*JE! MWANAMKE HUAMBUKIZWAJE PID?*
Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza
kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na:
- K**a una ugonjwa wa zinaa na haijatibiwa
- Kufanya ngono zembe isiyo salama (yani kulala
na wanaume tafauti tafauti)
- Kuwa na mpenzi ambaye ana wanawake wengi
nnje
- K**a umekuwepo na historia ya PID hapo
nyuma
- Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara
baada ya kujifungua (au postpartum period)
- Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya
kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post
abortion) au mara baada ya mimba kutoka
(miscarriage)
- Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa
uzazi (IUCD) k**a njia mojawapo ya uzazi wa
mpango
- Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya
PID
- Kutumia (Vaginal Dauche)

*UTAJUAJE UKO NA (PID)?*
Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID.
Miongoni mwa dalili hizi ni:
- Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa
maeneo ya chini ya kitovu
- Kupata maumivu ya mgongo
- Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za
siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- Kupata maumivu au kutokwa na damu wakati
wa tendo la ndoa
- Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
- Kupata homa
- Kupata damu innje ya siku zako zako za-
kawaida kupata damu ya hedhi
- Wakati fulani kuhisi kichefuchefu k**a
mwanamke mja mzito na kutapika

*VIPIMO VYA PID*
Hakuna vipimo maalum kudhibitisha mwanamke
ameathirika ila Dactari hujua mwanamke
ameathirika baada ya kuchukua historia ya
muhusika na kufanya vipimo vingine k**a:
- Kuchunguza mkojo ili kufahamu k**a mgonjwa
ana mimba. Kipimo hiki ni muhimu hasa kwa
mwanamke aliye katika umri wa kuzaa au
mwenye uwezo wa kubeba mimba
- Uchunguzi wa mkojo kwenye darubini ili
kutambua aina za vimelea vinavyomletea
mgonjwa uambukizi. Aidha mkojo huweza
kuoteshwa katika maabara kwa ajili ya kutambua
aina nyingine za vimelea viletavyo uambukizi huo.
- Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza jinsi aina
mbalimbali za chembe za damu zilivyoathiriwa na
uambukizi huo au k**a kuna mwingiliano na
magonjwa mengine yaliyojificha. Kipimo hiki kwa
kitaalamu huitwa (Full Blood Picture).
- Kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi
na kuuotesha kwa ajili ya utambuzi wa aina za
vimelea viletavyo maambukizi hayo. Kipimo hiki
huitwa (Cervical culture)
- Aidha ni muhimu pia kufanya vipimo vingine kwa
ajili ya utambuzi wa magonjwa yaambukizwayo
kwa njia ya kujamiiana, k**a vile virusi vya
ukimwi na kisonono.
- Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa ultrasound ya
nyonga ili kuangalia k**a kuna athari yeyote
katika mfumo wake wa uzazi.

*JE PID INAWEZA KUTIBIWA?*
Jibu ni ndio k**a itagunduliwa mapema inaweza
kutibiwa na ikaisha, ila ieleweke k**a tayari
ilikuwa imeharibu njia za uzazi uharibifu ule
haiwezi kurekebishwa. Kila mara ukichelewesha
kutibu PID ndivyo itaharibu mfumo wako wote wa
uzazi sasa ni muhimu ukiona mojawapo wa dalili
nilizozitaja utembelee daktari ili upate tiba. Hata
k**a utatibiwa na zile dalili zikapotea hakikisha
kila mara unashauriana na daktari wako na
ukipata mume mwingine ni muhimu umueleze ili
mpate matibabu msi-ambukizane mara kwa
mara. Ijulikane k**a ulikuwa na PID awali
inaweza kurudi mara kwa mara.

*MATIBABU*
Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa
ameathiriwa na ugonjwa huu, dawa za jamii ya
antibayotiki huweza kutumika kwa ajili ya kuua
vimelea vya ugonjwa .
Ieleweke pia mara nyingi ugonjwa hujirudia mara
kwa mara k**a mwanamke atapewa tiba na
mume asitibiwe. Na k**a maambukizi imekuwa
sugu inabidi muathiriwa amueleze daktari ili
apate kutumia anti-biotics kwa mda mrefu kuliko
kawaida. Lakini muhimu sana mwanaume apewe
dawa wakati mwanamke anatibiwa. Ikiwa
mwanamke peke yake atapata tiba pindi atakapo
lala na mwanaume yule yule maambukizi
yatarejelea.
*MADHARA YAKUTO-FWATA MATIBABU*
- Maumivu ya mfuko wa uzazi wakudumu
- Utapata ugumu wa kushika mimba
- Ectopic pregnancy (mtoto kuwa innje ya mfuko
wa uzazi)
- Kuziba kwa njia ya uzazi

*JINSI YA KUZUIA MAAMBUKIZI*
Kuna njia kadhaa za kuzuia maambukizi katika
mfumo wa uzazi. Njia hizi ni pamoja na:
- Njia hakiki ya kujizuia na maambukizi haya ni
kuwacha ngono zembe na kufanya ngono salama
- Kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili
za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza au pindi tu
unapogundua kuwa mwenzi wako ana dalili za
magonjwa ya zinaa au anatembea na wanawake
wengine
- Kufanya vipimo mara kwa mara hasa vya
mfumo wa uzazi, pamoja na vipimo vya
maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa
njia ya ngono (STI) khususan ugonjwa wa
chlamydia ufanyie vipimo kila mwaka mara 1
- Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua,
mimba kutoka au mara baada ya kutoa mimba ili
kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga
vema.
Ahsante

08/08/2020

*JINSI YA KUTATUA CHANGAMOTO YA KISUKARI*

K**a wewe ni mgonjwa wa KISUKARI naomba uniskilize kwa umakini maana huu ni ujumbe mzuri sana mwaka huu.......

Nasema hili kwa sababu zaidi ya wagonjwa 250 hawaumwi na kusumbuliwa tena na kwenda kwenda hospitali sababu sukari yao iko normal sasa......

Kabla hatujazungumzia suluhisho 👉Kwanza nikupe POLE SANA sababu najua maumivu na shida unazozipata, kwani hata baba yangu alikutana na hii changamoto mpaka akataka kupoteza maisha *sababu hakuweza kula vyakula anavyovihitaji*, miguu kufa ganzi , na shida zingine nyingi

Nataka nikupe USHAURI BURE/elimu BURE ....nipigie simu BURE /whasap BURE ........

Natoa ofa kwa watu wa mwanzo 10 tu ndani ya siku mbili tu na ukipitwa na huu muda basi utakua umepitwa na hii ofa na utapewa elimu kwa shilingi elfu 15.......

Ili kupata ofa piga no 0755804170/0676001543

30/07/2020

RANGI YA UTE AU UCHAFU UNAOTOKA ILI KULINDA MAENEO YA UKE

Ni kawaida kushangaa endapo k**a rangi au uchafu unatoka mara kwa mara ukeni kuwa ni wa kawaida au unahitaji kuchunguzwa. Uchafu utokao ukeni unaweza kuwa na rangi nyingi, na viashiria mbalimbali ili kuonyesha kuwa mwili una afya.

Katika makala hii tunaenda kujifunza ili tujue je, ute unalinda maeneo ya uke unakuwa na rangi gani?

Je, Uchafu Unaotoka Ukeni Huwa Ni Kitu Gani?


Uchafu utokao ukeni huwa ni majimaji fulani yanayotengenezwa kutoka kwenye tezi ndogo zinazokuwa ukeni na kwenye mlango wa kizazi. Maji maji haya huvuja kutoka ukeni kila siku ili kuondoa seli zilizochoka pamoja na mabaki, ili kuufanya uke pamoja na njia ya mfumo wa uzazi uwe katika hali yenye afya nzuri.

Kiwango cha uchafu unaotoka ukeni kinaweza kutofautiana kwa kila mwanamke. Rangi, uzito, na kiwango vinaweza pia kubadirika kila baada ya siku, kutegemeana na mazingira ya mwanamke anapokuwa hedhini:


Siku ya 1-5


Mwanzoni mwa mzunguko wa hedhi, uchafu unaotoka ukeni mara nyingi huwa mwekundu au wenye damudamu, kadiri mwili unavyotumia nguvu kuliondoa gamba laini linalokuwa juu ya ukuta wa mfuko wa kizazi.



Siku ya 6-14


Kipindi cha hedhi kinachofuata, mwanamke anaweza kuona damu kidogo ikitoka ukeni kuliko kawaida. Yai linapoanza kukua na kukomaa, basi ute utelezi unaokuwa kwenye mlango wa kizazi utabadirika na kuwa wenye rangi ya kijivu au mweupe au wa njano. Unaweza ukawa mzito.

Siku ya 14-25

Siku chache baada ya yai kupevuka, ute utelezi hubadirika na kuwa mwepesi wenye kuteleza, k**a ute wa yai la kuku vile. Baada ya yai kupevuka, ute hubadirika na kuwa wenye rangi ya kijivu, mweupe au wa njano, na wenye kunata

Siku ya 25-28:


Ute utelezi unaokuwa kwenye shingo ya kizazi hubadirika na kuwa mwepesi, na mwanamke anaweza kuuona kidogo tu, kabla hajaingia kwenye kipindi kingine cha hedhi.

Uchafu Wenye Rangi Nyekundu



Uchafu huu mwekundu unaweza kutofautiana, kwani unaweza kuwa wenye rangi yenye kung’aaa au nyekundu sana. Uchafu mwekundu huwa ni matokeo ya damu ya hedhi kuanza kutoka.

Damu ya hedhi hutokea, kwa wastani, kwa kila mzunguko wa siku 28, ingawa kiwango cha kati huwa ni siku 21 na 35. Hedhi huwa ni ya siku 3-5.



NUKUU: Mwanamke yeyote anayepata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja, anapaswa afike hospitali mapema ili kumuona daktari. Ingawa kuna visababishi vingi hafifu vya kumfanya mwanamke apate hedhi mara mbili kwa mwezi, lakini navyo vinaweza wakati mwingine kuwa viashiria vya matatizo mabaya baadaye.

Mwanamke yeyote aliyefikia hali ya kukoma hedhi na kutokuona hedhi kwa takribani mwaka mmoja, anapaswa amuone daktari mapema ikiwa k**a anapatwa na hali ya kutokwa na damu ukeni. Hii yaweza kuwa ni dalili ya salatani.


Uchafu Mweupe

Uchafu mweupe unaweza kuongezeka, unaweza ukawa k**a maziwa vile au wa njanonjano kwa mbali. Endapo mwanamke hatakuwa na dalili zingine, basi uchafu mweupe unaweza kuwa kiashiria kabisa cha kilainishio kizuri chenye afya ukeni mwake. Utakuta uke wake uko katika hali nzuri hata anapokutana kimapenzi na mwezni wake hakutakuwa na shida yoyote zaidi ya kufurahia tendo la ndoa

NUKUU: Hata hivyo, endapo k**a uchafu mweupe utakuwa mzito k**a maziwa mtindi vile na kuwa na harufu mbaya, basi hii yaweza kuwa dalili za maambukizi. Muhusika anapaswa afike hospitali haraka bila kuchelewa ili kumuona daktari wa vipimo.

Uchafu mweupe wenye kunata, na wenye harufu mbaya mara nyingi huwa ni wenye maambukizi ya fangasi, ambao pia unaweza kusababisha muwasho ukeni.


Uchafu Wenye Rangi Ya Njano Na Ukijani

K**a uchafu una rangi ya njano njano, inaweza isiashirie tatizo kwako. Hali hii hasa inaweza ikasababishwa kubadirika kutokana na vyakula unavyotumia.



Uchafu ambao ni wa njano kabisa, unjano wenye ukijani, au kijani yenyewe, mara nyingi huwa ni dalili za bakteria au maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Jitahidi kumuonda daktari mapema endapo k**a uchafu ni mzito na wenye harufu mbaya.

Uchafu Wenye Rangi Ya Pink


Uchafu unaweza kuwa wenye rangi ya pinki kwa mbali au kabisa. Mara nyingi huwa unakuwa na damudamu kidogo. Uchafu wenye rangi ya pinki kwa kawaida hujitokeza huku ukiwa na matone ya damu damu kabla ya kipindi cha hedhi kuwadia. Hata hivyo, inaweza pia kuwa ishara ya damu kutoka pale yai linapojipachika kwenye ukuta wa tumbo la uzazi ujauzito unapoingia.

NUKUU: Baadhi ya wanawake hutokwa na matone ya damu damu baada ya yai kupevuka, hali ambayo pia inaweza kusababisha kutokwa na uchafu wa pink. Uchafu unaweza kuwa wenye rangi ya pink baada ya kufanya tendo la ndoa, endapo k**a tendo lenyewe limesababisha maumivu kidogo au muwasho ukeni au maeneo ya mlango wa kizazi.


Uchafu Msafi

Uchafu wa kawaida huwa ni msafi mweupe. Unaweza kuwa mwepesi au ukawa na uzito k**a ute wa yai vile. Mwanamke anaweza akatokwa na uchafu mweupe msafi, mwepesi kabla yai halijapevuka, au wakati hisia au nyege zinapompanda, au anapopata ujauzito.

Uchafu Wenye Rangi Ya Ukijivu

Uchafu unaotoka ukeni huku ukiwa na rangi ya kijivu huwa sio mzuri, na inaweza kuwa dalili za maambukizi ya bakteria wajulikanao k**a, “Bacterial Vaginosis(BV)”.

Bakteria hawa kwa Kiasi husababisha dalili zingine ukeni k**a vile;


Muwasho

Hali ya k**a moto ukeni


Harufu mbaya ukeni


Hali ya wekundu maeneo ya mashavu ya uke au mlango wa uke


NUKUU: Mwanamke yeyote anayetokwa na uchafu wenye rangi k**a ukijivu pamoja na dalili zake hizo anapaswa kufika hospitali haraka sana bila kuchelewa.

Je, Ni Lini Unapaswa Kumuona Daktari?

Nakushauri umuone daktari ikiwa k**a uchafu una harufu au muonekano usi wa kawaida . Mwanamke napaswa pia kutafuta tiba endapo k**a anapatwa na dalili k**a zifuatazo:

Muwasho

Maumivu au kutojisikia raha

Uchafu mzito k**a maziwa ya mgando


Kutokwa na damu mara mbili kwa mwezi au baada ya hedhi kukoma


Kutokwa na damu baada ya kufanya tendo la ndoa


Kutokwa na damu kila mara baada ya kufanya tendo la ndoa


Kutokwa na uchafu wenye rangi ya njano, ukijivu, au kijani


Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya


Kuhisi maumivu makali wakati wa kukojoa

DAWA MBADALA 6 ZINAZOTIBU GANZI MIKONONI NA MIGUUNIGanzi mikononi na miguuni inamaanisha kukosekana kwa fahamu katika se...
26/06/2020

DAWA MBADALA 6 ZINAZOTIBU GANZI MIKONONI NA MIGUUNI

Ganzi mikononi na miguuni inamaanisha kukosekana kwa fahamu katika sehemu hizo. Hisia ndiyo inakosekana sababu kunakuwa hakuna damu na neva zinakosa mawasiliano ya moja kwa moja na ubongo.

Ni jambo la kawaida linalowapata watu wengi sana miaka ya hivi karibuni.

Kinachosababisha ganzi mwilini ni pamoja na:

1. Shinikizo la muda mrefu kwenye miguu na mikono
2. Kuwa karibu na vitu vyenye baridi sana kwa kipindi kirefu
3. Mabadiliko ya muda mfupi kwenye neva
4. Ajali kwenye neva
5. Kunywa pombe kupita kiasi
6. Uvutaji wa sigara na bangi
7. Uchovu sugu
8. Kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara
9. Ukosefu wa vitamini B12 na Magnesiamu
10. Ugonjwa wa kisukari nk

Kwa kawaida ganzi inayotokea kwa dakika kadhaa na kupotea huwa haina shida yoyote lakini onana na daktari mapema ikiwa inakutokea mara kwa mara na pia ikiwa inakutokea na kudumu kwa muda mrefu. Inaweza kuwa ni ishara ya ugonjwa fulani ambao unahitaji matibabu ya haraka.

Kuumwa ganzi kwenye miguu na mikono yako linaweza kuwa ni jambo linaloudhi sana hata hivyo hapa mimi leo nimekuandalia dawa za asili unazoweza kuzitumia kuondokana na tatizo hili.

Endelea kusoma …

Dawa mbadala zinazotibu tatizo la ganzi mwilini:

1. Massaji

Kufanya mazoezi ya massaji wakati unapopatwa na ganzi ni namna nzuri ya kutibu ganzi. Massaji inaongeza msukumo na mzunguko wa damu jambo ambalo mwisho ni tiba kwa tatizo la ganzi. Zaidi masaji inasaidia kusisimua neva na misuli na hivyo kuimarisha na kuongeza mzunguko wa damu kwa ujumla.

*Kwa matokeo ya uhakika weka mafuta ya n**i au ya zeituni au ya mharadali (mustard oil) kwenye viganja vya mikono yako .

*Pakaa sehemu unapopata ganzi

*Massaji maeneo hayo na mikono yako kwa dakika 5 mpaka 7 hivi

*Fanya mara 3 hata 5 kwa siku.

2. Mazoezi ya viungo

Mazoezi husaidia kuimarisha mzunguko wa damu na kuongeza oksijeni sehemu zote za mwili na hivyo kuzuia mwili kupata ganzi.

Mazoezi ndiyo namna pekee ya bure ya kujikinga

12/04/2020

Afya ndo mtaji wa mwanadamu yeyote yule na mengine huja ..lakini afya yako isipokua vizur huwez ishi kwa amani na piaa kinachoharibu afya zetu Ni mwenendo mbovu au mbaya was maisha ya kila sku

Address

Dodoma

Telephone

+255755804170

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AFYA NI MTAJI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to AFYA NI MTAJI:

Share