26/10/2022
FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA KISUKARI, CHANZO, DALILI, MADHARA NA TIBA YAKE.
KISUKARI (diabetes mellitus ) ni ugonjwa wa uwepo wa kiasi kingi cha sukari katika damu. Sababu yake kubwa ni uhaba wa homoni ya insulini mwilini au upungufu wa uwezo wa mwili kuzalisha insulini ambayo husaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini.
Kipi kinatokea mpaka mtu kupata ugonjwa wa sukari au kuongezeka kwa kiwango cha sukari mwilini?
Ugonjwa wa sukari hutokea baada ya ulaji wa wingi wa vyakula vyenye sukari (wanga), hasa zaidi vyenye sukari rahisi.
Mfano wa vyakula vitoavyo sukari mwilini ni k**a:- Ugali, wali, viazi, ndizi, mkate, chapati n.k
Ulaji wa wingi wa vyakula vyenye sukari au vitoavyo sukati kwa wingi, kwa kutofuata taratibu za kitabibu k**a kula kiasi kingi cha chakula baada ya saa kumi na moja jioni, ulaji wa chakula kingi katika mlo mmoja na utumiaji wa vyakula vyenye mafuta mengi hupelekea mtu kupata tatizo hili(Type 2 diabetes).
Wakati mwingine unaweza kupata tatizo la sukari kutokana na kurithi, historia ya sukari kwenye familia au kuzaliwa na upungufu wa uzalishaji wa kiwango cha insulini mwilini (Type 1 diabetes).
Sababu zingine zinazopelekea kupata tatizo hili ni Umri mkubwa, kuwa na uzito mkubwa, presha ya kupanda,historia ya sukari wakati wa ujauzito na magonjwa yanayoweza kupelekea kuharibika kwa ufanisi kazi wa insulini mwilini kiasi cha kushindwa kurekebisha kiwango cha sukari mwilini.
Sababu zote kwa pamoja hupelekea watu kupata kisukari, unapopata tatizo hili hakikisha unachukua hatua za haraka kukabiliana na changamoto hii.
Ugonjwa huu unakadiriwa kuua karibu watu million 1.5 kila mwaka duniani kote (WHO, 2019).
⏹️DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI.
1.Kushikwa na kiu cha mara kwa mara/kupatwa na kiu kikali.
2. Kukojoa mara kwa mara.
3. Kutokwa jasho jingi bila hata kufanya shughuli yeyote.
4. Uchovu usiokwisha pamoja na kupungua uzito licha ya kula vizuri.
5.Kupatwa na njaa ya mara kwa mara/njaa kali.
6. Mkojo kuwa na ladha ya sukari.
7.K