Afdek-centre

Afdek-centre Welcome to our mental health consultation centre to help you achieve your best self.

USIRUHUSU WATU KUTUMIA HISTORIA YAKO KUKUNYANYASA!Kuna mambo mengi ambayo uliyafanya kipindi cha nyuma, kuna hatua nying...
10/02/2024

USIRUHUSU WATU KUTUMIA HISTORIA YAKO KUKUNYANYASA!

Kuna mambo mengi ambayo uliyafanya kipindi cha nyuma, kuna hatua nyingi ulipitia, zipo nzuri zipo mbaya, kuna mambo mengi ambayo unatamani kuyasahau katika maisha yako lakini huwezi, kuna mambo mengi unatamani kuyabadilisha katika maisha yako lakini huwezi. Yameshatokea na ni sehemu ya maisha yako, haya tunayaita historia, si sehemu tena ya maisha yako, wewe ni mtu mpya, huwezi kubadilisha historia lakini usijihukumu au kuruhusu watu kukuhukumu kutokana na historia yako.

Ulikua Malaya kweli, ulikua mwizi kweli, umetoka katika familia ya kimasikini, ulikua mshamba, ulikua unadanga, ulikua marioo na chochote kile ambacho ulikua, k**a umeshapita katika hali yoyote mbaya na sasa hauko huko cha kufanya ni kuangalia historia na kumshukuru Mungu hauko kule tena. Acha kujihukumu, acha kujisikia vibaya na kubwa kabisa usiruhusu watu kukufanya ujisikie vibaya.

Anaweza kuwa mume au mke, wanaweza kuwa majirani au ndugu, watataka kukudharau kwakua ulikua flani, watataka kukudhalilisha kwakua unatokea katika hali flani, watataka kukukatisha tamaa kwakua huna elimu flani. Huna haja ya kuwasikiliza, huna sababu ya kuwapa akili yako, wala huna sababu ya kujielezea kwako. Wewe ni mtu mpya hivyo acha kulia, acha kuhuzunika, acha kujiona mbaya, acha kujiona umepungukiwa kwakua tu historia yako si tamu.

Share na Mungu akubariki!!

Address

Dodoma

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afdek-centre posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Afdek-centre:

Share