21/01/2023
GAUTI (Gout) ni aina ya ugonjwa unaoathiri viungo vya mwili unaosababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa kuliko kawaida cha tindikali ya Urea (uric acid) katika damu. Ongezeko la uric acid husababisha madhara katika jointi (joint) (jointi ni sehemu ya mwili inapokutana/ inapoungana mifupa miwili).
Gauti inaweza kutokea ghafla, kitaalamu huitwa acute gout au ikawa sugu yaani chronic gout.
Hali hiyo hutokea iwapo mwili wa mgonjwa unatengeneza uric acid nyingi kuliko kawaida au unashindwa kutoa uric acid mwilini k**a inavyotakiwa.
Ongezeko hili husababisha mrundikano wa uric acid katika majimaji yanayozunguka jointi yanayoitwa synovial fluid na hatimaye kutengeneza vijiwe vidogo vidogo vya tindikali ya urea yaani uric acid crystals ambavyo husababisha jointi kuvimba na hatimaye kuathirika.
Aidha unywaji pombe pamoja na matumizi ya baadhi ya madawa k**a vile dawa za kutoa maji mwilini husababisha ongezeko la kiwango cha uric acid katika damu.
Vihatarishi vingine vya gauti ni pamoja na kuwa na ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya figo, unene uliopitiliza, ugonjwa wa sickle cell anemia au aina nyingine za upungufu wa damu, pamoja na saratani ya damu (leukemia).
DALILI
Dalili za gauti kwa kawaida huhusisha jointi moja au jointi chache. Jointi zinazoathiriwa zaidi ni pamoja na kidole kikubwa cha mguuni, magoti au kiwiko cha mguu.
Wagonjwa huwa na maumivu yanayoanza kwa ghafla hususan nyakati za usiku. Mara nyingi mgonjwa hudai anasikia maumivu makali k**a kitu kinachokata, kupwita au mifupa inayosagana. Jointi hubadilika na kuwa na joto, kuvimba na kuwa na nyekundu. Kwa kawaida mgonjwa hulalamika maumivu makali ikiwa ataguswa kwenye jointi yenye matatizo.
Wagonjwa wenye gauti kwa muda mrefu huwa pia na vinundu chini ya ngozi inayozunguka jointi zilizoathirika. Vinundu hivi kwa kitaalamu huitwa trophy.
MATIBABU
Matibabu ya gauti hujumuisha matumizi ya dawa, lishe pamoja na mabadiliko katika mfumo wa maisha wa mgonjwa. Dawa hutumika mara tu mgonjwa anapopata shambulio la ghafla. Lakini kwa ukosefu wa maarifa kuhusu ugonjwa huu watu wengi wanatumia dawa za kupunguza maumivu halafu badae maumivu huendelea k**a mwanzo. Dawa hizo ni pamoja na codeine na paracetamol,
USHAURI
Kwa matibabu ya uhakika changamoto ya gauti wasiana nami kwa namba 0759305096.