AFYA YAKO kwanza.

AFYA YAKO kwanza. Health education

07/08/2021

FAHAMU UGONJWA WA P.I.D

(PELVIC INFLAMMATORY DIDEASE)

Huu ni ugonjwa unaoshambulia sana njia ya uzazi, mlango wa mfuko wa uzazi(cervicitis), mfuko wa uzazi(endometritis), mirija za uzazi(salpingitis), mahali mayai yanako zalishwa(oophoritis).
Maambukizi haya hasa husababishwa na Bacteria (Gonorrheal and clamydial organism), na wakati mwingine huweza kusababishwa na fangasi, virusi na wadudu wengine.

Ugonjwa huu unapokua umefika mbali zaidi husababisha matatizo ya uzazi k**a vile kutokupata ujauzito, vidonda katika mirija ya uzazi, maumivu makali kiunoni yenye kujirudia, mimba kutunga nje ya kizazi. Pia k**a umefika mbali zaidi husababishwa mtu kuondolewa sehemu ya njia ya uzazi au kizazi chote (Hesterectomy)

DALILI ZAKE.
Uonapo dalili yoyote au zote kati ya hizi usipuuzie.
1)Maumivu maeneo ya kiunoni
2)Maumivu wakati wa tendo la ndoa
3)Kutokwa na uchafu/majimaji sehemu za siri ambayo huwa mweupe k**a maziwa mgando(usio na harufu) au wanjano,kijani au rangi ya brown wenye harufu.
4)Homa
5)Kukosa hamu ya kula
6)Kichefuchefu au kutapika.
7)wakati mwingine mimba kuharibika
8)Muwasho sehem za siri
9)Wakati mwingine maumivu wakati wa haja ndogo.

MATIBABU
Kwa maelezo zaidi na matibabu usisite kunitafuta piga/sms/whatsapp kwa namba...
0742251673

Weka appointment na daktari kwa sh elf kumi tu (10000). Piga kwa namba iliotajwa kupata utaratibu wa malipo kabla ya huduma.

LIKE kisha SHARE na rafiki zako wapate elimu hii

14/06/2021
Sasa ni rahisi kwa tatizo lolote unaweza wasiliana na Daktari wako muda wowote kupitia namba 0742251673, sms au WhatsApp
09/04/2021

Sasa ni rahisi kwa tatizo lolote unaweza wasiliana na Daktari wako muda wowote kupitia namba 0742251673, sms au WhatsApp

KWA GHARAMA NAFUU PATA TUBA SAHIHI
30/03/2021

KWA GHARAMA NAFUU PATA TUBA SAHIHI

FIBROIDS (UVIMBE KATIKA KIZA)Huu ni uvimbe ambao mara kwa mara huonekana katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Uvimbe huu k...
28/05/2020

FIBROIDS (UVIMBE KATIKA KIZA)

Huu ni uvimbe ambao mara kwa mara huonekana katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Uvimbe huu kitaalamu unaweza kuwa Uterine myomas, leomyomas, au fibromas. Asilimia 20 hadi 50 ya wanawake walio katika umri wanoweza kubeba mimba hupata uvimbe huu katika mfumo wa uzazi hivyo kupelekea matatizo katika mfumo wao wa uzazi.

SABABU YA KUTOKEA KWA UVIMBE KATIKA MFUMO WA UZAZI.

Hakuna sababu maalum inayoelezwa katika kutokea kwa uvimbe huu isipokua uvimbe huu huchipua na kukua kwa haraka kutoka kwenye misuli laini ya mfumo wa uzazi. Ukuaji wake wa haraka ni kwasababu ya uwepo wa homoni ya estrogen kwa wingi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke.

DALILI ZA UVIMBE KWENYE MFUMO WA UZAZI. (FIBROIDS)

Uonapo dalili moja wapo kati ya hizi usipuuzie

1. Kutokwa na damu nyingi wakati wa siku zako.
2. Kuwa katika siku zako kwa muda mrefu isiyo kawaida (zikizidi siku 3-5, wengine hadi 7 )
3. Kutokwa kwa damu isiyo ya kawaida katika mizunguko yako ya hedhi.
4.Maumivu ya nyonga(kiuno)
5. Kupata haja ndogo mara kwa mara
6. Maumivu chini ya mgongo
7. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
8. Kuwepo kwa uvimbe unaoonekana au unaoweza kuupapasa chini ya kitovu.

MATIBABU

Madhara yake ni makubwa sana katika mfumo wa uzazi ambayo huweza kusababisha kutokua na uwezo wa kubeba mimba na wakati mwingine kutolewa kizazi k**a mtu hatopata matibabu ya mapema.

Malipo ni sh. Elf kumi (10000) tu kumuona daktari, piga namba hio chini kujua utaratibu wa malipo kabla ya huduma.
Usisite kunipigia/sms/whatsapp kwa namba 0742251673. NITAKUSIKILIZA NA KUKUSAIDIA.

LIKE, SHARE pia na wenzako wapate faida hii.

12/05/2020

It's world nurse day

FAHAMU KUHUSU UVIMBE KATIKA OVARI (OVARIAN CYST).O***y ni sehemu katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwaajili ya utengenez...
12/05/2020

FAHAMU KUHUSU UVIMBE KATIKA OVARI (OVARIAN CYST).

O***y ni sehemu katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwaajili ya utengenezwaji wa mayai ya uzazi kila mwezi. Ovarian cysts hutokea pale vifuko vinavyobeba mayai (follicles) kujaa maji kabla au baada ya kutoa yai kwenda kwenye mirija ya uzazi (falopian tubes)

AINA ZA UVIMBE KATIKA SEHEMU YA UTENGENEZWAJI WA MAYAI.
(TYPES OF OVARIAN CYST)
>Kuna aina sita za ovarian cyst ambazo ni Dermond cysts, Endometrioma cyst, Cystadenomas, Follicle cyts, corpus luteum cysts, Polycystic Ovarian Syndrome (PCOS)
Katika aina hizi mara nyingi mtu huweza kuwa nayo moja kati ya hizi na asipate dalili. Dalili huanza kuonekana Cyst hizi zikianza kukua.

DALILI ZA OVARIAN CYSTS

1). Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi kila mwezi
2).Maumivu chini ya kitovu pembeni kwenye nyonga na chini ya mgongo
3). Maumivu wakati wa tendo la ndoa
4). Maumivu kwenye matiti
5). Maumivu ya kiuno kabla au wakati wa hedhi

DALILI ZINAZO HITAJI MATIBABU YA HARAKA ZAIDI

Kwa dalili hizi huwenda uvimbe umepasuka na kuvuja. Mtu huweza kupoteza mpaka maisha au kusababisha madhara makubwa zaidi k**a atachelewa matibabu aonapo dalili hizi:

1). Maumivu makali sana ya nyonga au kiuno.
2). Kujiskia kizunguzungu au kupoteza fahamu
3). Homa
4). Kupumua haraka haraka
5). Kupungua uzito kwa haraka bila sababu
6). Uvimbe chini ya kitovu.

MADHARA YA OVARIAN CYSTS.

Cysts hizi huja na kuondoka zenyewe bila kuonesha dalili, zikianza kukua huonesha dalili zilizotajwa hapo juu.
Madhara ni k**a yafuatayo k**a mtu hatopata matibabu ya mapema

1). Kupoteza uwezo wa kuzalisha mayai ya uzazi(hatoweza kubeba mimba).
2). Kansa ya mfumo wa uzazi
3). Kupoteza maisha kabisa.

MATIBABU

Asilimia kubwa ya wanawake hupata ugonjwa huu bila kujua. Cysts huweza kutokea kila mwezi na kuondoka zenyewe bila kuonesha dalili zozote. Zinaposhindwa kuisha zenyewe hukua na kuleta madhara makubwa na dalili k**a ilivyoelezwa hapo juu

Ovari zote zinapokua zimeharibika sana hulazimika mtu kufanyiwa operation na kutolewa kizazi

Kumuona daktari malipo ni sh. Elf kumi tu (10000). Piga namba chini hapo kupata utaratibu wa malipo kabla ya huduma.

Matibabu ya mapema yapo. Wasiliana nami muda wowote nikusikilize kwa namba
0742251673.
issues_afya

MENSTRUAL CRAMP(MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA HEDHI) MAUMIVU YA TUMBO huwapata wanawake wengi sana kila wanapokaribia hedhi...
10/05/2020

MENSTRUAL CRAMP
(MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA HEDHI)

MAUMIVU YA TUMBO huwapata wanawake wengi sana kila wanapokaribia hedhi au wakiwa ndani ya hedhi. Maumivu haya ya tumbo wakati wa hedhi kitaalam tunaita Dysmenorrhea ambayo huanza taratibu na baadae kuwa makali zaidi ambayo huisha ndani ya siku 2 hadi 4.

MAUMIVU haya wanawake wengi huchukulia ni kawaida na wakati kitaalamu si kawaida.

AINA ZA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI

1) Primary menstrual cramp.
Aina hii ya maumivu husababishwa na homoni ''prostaglandins" ambayo husababisha kujikunja kwa mfuko wa uzazi hivyo kupelekea damu kutofika kwa wakati katika kuta za mfuko wa uzazi. Aina hii pia huweza kusababishwa na kuwepo kwa wingi wa homoni " leukotrines" .

2)Secondary menstrual cramp
Aina hii ya maumivu husababishwa na magonjwa mbalili mbali katika mfumo wa uzazi ambayo huweza kuwa Uvimbe katika mfumo wa uzazi (Endometriosis, Uterine fibroids) au mashambulizi ya bakteria au fangasi katika mfumo wa uzazi(pelvic inflammatory disease(PID))

●Tabia zinazoweka kupelekea pia maumivu haya ni pamoja na Mtu kukaa muda mrefu bila kulala, mawazo na lishe pia.

DALILI.

Dalili hutofautiana na mtu anaweza pata zote au baadhi:

1. Maumivu makali chini ya kitovu na kiuno
2. kichefuchefu na nakutapika
3. kutokwa jasho
4. kuharisha au kutopata choo kabisa
5. kichwa kuuma
6. Kujihisi kizunguzungu na wengine hupoteza fahamu.

MATIBABU

Wanawake wengi huchukulia ni kawaida kwako kuteseka na hali hii kila mwezi. Maumivu haya si kawaida na huenda yakaashiria madhara makubwa katika mfumo wa uzazi mfano Uvimbe katika kizazi au maambukizi au homoni kuzalishwa kwa wingi ambayo si kawaida.

Kumuona daktari malipo ni sh. Elfu kumi tu (10000), piga namba hio chini kujua utaratibu wa malipo kabla ya huduma.

Usichukulie poa. Kwa yeyote mwenye dalili hizi matibabu yapo.
Nipigie/meseji/whatsapp kwa namba: 0742251673
nikusikilize upate ufumbuzi pia wa tatizo hili.

WAKATI WOWOTE KARIBUNI

Fahamu afya yako ya uzazi. Muda wote mtaalamu wako yuko nawe.
10/05/2020

Fahamu afya yako ya uzazi. Muda wote mtaalamu wako yuko nawe.

TB inatibika bila kujali wewe ni mgonjwa mpya au ulishawahi kutibiwa ikarudi tena. Kwa sasa serikali kwa kushirikiana na...
06/03/2020

TB inatibika bila kujali wewe ni mgonjwa mpya au ulishawahi kutibiwa ikarudi tena. Kwa sasa serikali kwa kushirikiana na wadau na mashirika mbalimbali wameboresha matibabu..uonapo dalili nilizozitaja katika somo lililopita tafadhali fika kituo cha afya chochote kilichopo karibu yako kwaajili ya kupima na kuanza matibabu

NJIA ZA KUEPUKA UGONJWA WA KIFUA KIKUU(TB)1. Epuka kukaa karibu na MTU anayeumwa au kudhaniwa kuumwa kwa kuelekeana USO ...
04/03/2020

NJIA ZA KUEPUKA UGONJWA WA KIFUA KIKUU(TB)

1. Epuka kukaa karibu na MTU anayeumwa au kudhaniwa kuumwa kwa kuelekeana USO kwa USO na kwa ukaribu.

2. Epuka sehemu za misongamano k**a sokoni, kwenye dalala n.k

3. Unapokohoa au kupiga chafya. Ziba mdomo kwa kitambaa kuepuka kusambaza wadudu wa kifua Kikuu.

5. K**a ni muathirika wa UKIMWI hakika unatumia dawa za kuzuia kifua kikuu( ISONIAZID) K**a ulivyoelekezwa kwa kipindi chote cha miezi sita.
6. Epuka matumizi ya dawa za kupunguza kinga ya mwili kwa muda mrefu. Mfano dawa aina ya Steroids k**a vile prednisolone

7. Hakikisha nyumba unayoishi ina mzunguko wa hewa wa kutosha.

8. Epuka tabia hatarishi k**a unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara au madawa ya kulevya.

Moja ya malengo ya maendeleo endelevu ni kutokomeza janga la ugonjwa wa kifua kikuu au TB ifikapo mwaka 2030. Mkakati wa...
02/03/2020

Moja ya malengo ya maendeleo endelevu ni kutokomeza janga la ugonjwa wa kifua kikuu au TB ifikapo mwaka 2030. Mkakati wa shirika la afya ulimwenguni, WHO wa kutokomeza TB unataka kupunguzwa kwa vifo vitokanayvo na ugonjwa huo kwa asilimia 90 na kupunguza visa vyake kwa asilimia 80. Malengo haya yatafikiwa iwapo tiba sahihi itapatikana kwa wakati sahihi kwa wagonjwa, pia mikakati ya kuzuia kueneza ugonjwa. Je nchini Tanzania upatikanaji wa huduma ya TB ukoje? Basi ungana nasi kujifunza zaidi kuhusu kujikinga, tiba, ushauri na namna ya kuutokomeza ugonjwa huu katika jamii yetu

Kuwa mzazi ni jambo jema, ila kulea mtoto si kitu rahisi, haswa akiwa ndio mtoto wa kwanza. Wengi wetu tunalea watoto ku...
30/10/2019

Kuwa mzazi ni jambo jema, ila kulea mtoto si kitu rahisi, haswa akiwa ndio mtoto wa kwanza. Wengi wetu tunalea watoto kutokana na maelekezo ya watu wenye uzoefu na malezi kwa muda mrefu. Tatizo linakuja pale ambapo mbinu wanazotumia zinapoleta madhara makubwa kuliko faida. Ni vizuri mzazi akiwa na muda wa kujua nini hasa atakacho mtoto kabla ya kufuata ushauri usio wa kitaalamu na kusababisha madhara makubwa.

Je ulishawahi kushauriwa kumkaba mtoto wakati anapogoma kula ? K**a ulishaambiwa basi fahamu si ushauri mgeni. Si kila mbinu inaweza kufanya kazi kwa kila mtoto, hivyo ni bora kuchanganya akili yako katika kila ushauri unaopewa kabla ya kuufanyia kazi.

Kwanini watoto wanakataa chakula ?

kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kumfanya mtoto akatae kula, hizi hapa ni chache tu:

• Mtoto anakuwa ameshiba na hajisikii hamu ya kula. Hii inawezekana kusababishwa na mtoto kula vitu vidogo vidogo mara nyingi hivyo kuzuia njaa na kumzuia kula chakula vizuri.
• Hapendi chakula anachopewa sababu hajakizoea au hakifurahii. Watoto wengi wanaweza kukataa kula mboga za majani, lakini ni muhimu sana ale sababu ni chakula pekee kinachomfanya akue vizuri.
• Anaumwa na amepoeza hamu ya kula. Ugonjwa ni moja ya sababu kubwa za kumfanya mtoto kugoma kula.
• Amechoka chakula anachopewa hivyo kutokifurahia tena. Kula chakula cha aina moja muda mrefu inaweza kuwa ni sababu kubwa ya mtoto kugoma kula. Hata k**a anafurahia chakula, wakati mwengine anaweza asipende tena kula. Hivyo ni vizuri kuweka vyakula tofauti ili mtoto apate ladha na virutubisho tofauti.
Ni muhimu kuzingatia kuwa, katika mazingira yeyote yale usimlazimishe mtoto kula na ni hatari kubwa kumkaba ili ameze chakula. Kulazimisha mtoto kula ni kumjengea tabia ya kuchukia chakula. Mtoto akishajenga tabia hii hawezi kuacha sababu atakuwa anahusisha chakula na adhabu. Sababu hakuna mtu anayependa adhabu, atakuwa anachukia chakula cha aina yeyote. Matokeo yake ni kuwa mtoto atajenga tambia mbaya zaidi ya kukataa kula chakula cha aina zote. Pia, kumkaba mtoto kunaweza kuleta matatizo makubwa k**a vile kufanya chakula kuingia kwenye njia ya hewa, hii itakuletea kesi zisizo za lazima.

Jinsi ya kutatua tatizo

Katika njia muhimu ni pamoja na hizi hapa:

1. Kubadilisha vyombo vya chakula vya mtoto

mtoto huvutiwa zaidi na rangi, hasa kwenye vitu anavyotaka kula. Mtoto anaweza kuchoka kula chakula sababu anatumia chombo kimoja kila siku, hii haijalishi k**a chakula kinabadilika au la. Ni muhimu kumuandalia mtoto chakula kwenye vyombo vyenye rangi na maumbo tofauti. Hii inamfanya mtoto kuona utofauti wakati wa kula, na kumfanya apate hamu ya kula.
Mfano, unaweza kutumia bakuli, vikombe, sahani, vijiko vyenye rangi tofauti ili kumfanya aone anakula katika mazingira tofauti na hii humfanya awe na hamu kula chakula zaidi.

2. Watoto wale pamoja na familia

Watoto hupenda kuiga wazazi. Mara nyingi sana watoto hupewa vyakula wale wakiwa wenyewe wakati watu wengine wanaendelea na shughuli za kawaida. Hii inaweza kumfanya mtoto kupendelea zaidi kucheza kuliko kula. Ni muhimu kumlisha mtoto wakati familia nzima imekaa mezani au jamvini tayari kwa kula. Katika muda huu mtoto atakula vizuri bila vikwazo, maana kila mmoja anakula.

Vilevile, watoto wengine (umri wa miezi 10 hadi miaka 2) hupendelea kula vyakula wanavyokula watu wazima, hata k**a haviwafai, na kugoma vyakula vya watoto. Ni bora kumuandalia chakula kinachofanana na unachokula wewe na kumpa ili apate kufurahia. Huwezi kubishana na mtoto, ingawa huwezi kumpa kila kitu anachotaka pia. Ila jaribu kutumia mbinu tofauti ili apate kula na kuridhika. Afya yake ni bora kuliko kitu kingine kwenye maisha yake kwa muda huu.

3. Jaribu kumsoma mtoto anapenda nini


Kila mzazi ana jukumu la kumsoma mwanae anapendelea nini. Ili kuweza kumfanya mtoto ale vizuri, ni vyema kubadilisha vyakula kila wakati, siyo kila siku.

Mara nyingi watoto huchukua muda kuzoea chakula, hivyo ni vizuri kumpa mtoto chakula kwa muda wa siku 2 hadi 3 na kumbadilishia na chakula kingine. Hii inasaidia mtoto kuonja ladha ya chakula. Anaweza kukipenda au kukichukia. K**a atakataa ladha ya chakula kipya, usikate tamaa, jaribu kumpa tena baada ya siku moja au mbili, unaweza kukuta akaipenda ladha na akala chakula bila tatizo.

Usikate tamaa kwenye kumpa mwanao upendo wako k**a mzazi. Jaribu kila njia unayoweza na usife moyo. Watoto ni wagumu kuwaelewa na inachukua muda, lakini pale unapofikia hatua ya kujua anachopenda utakuwa umepata jibu zuri jinsi ya kuendelea kumlea mwanao.

4. Epuka kumpa vitu vitamu kati ya milo


Watoto wengi wanapenda kula vitu vidogo vidogo (p**i, biskuti, juisi, keki n.k.) kila mara. Hivi vitafunwa vinaweza kumfanya mtoto azibe njaa na kutokuwa na hamu ya kula chakula muda unapowadia. Ili kuzuia hii tabia, ni bora kuacha kumpa mtoto vitu vidogo vidogo kati ya milo ili kumfanya kuwa na hamu ya chakula muda unapowadia.

Mara nyingi inashauriwa kumlisha mtoto mara 4 hadi 5 kwa siku. Hii ni vizuri sababu mwili wa mtoto unakuwa unahitaji virutubisho vingi mara kwa mara kwa kusaidia kukua. Ni vizuri kumpa mtoto chakula bora kuliko kumjaza tumbo na vyakula vyenye sukari zisizokua muhimu katika kujenga afya yake

5. Msikilize mtoto anachotaka


Mara nyingi mzazi au mlezi unaweza kudhani kuwa unajua zaidi kiwango cha chakula anachotakiwa kula mtoto kuliko hata mtoto mwenyewe. Hili linaweza kuwa tatizo kubwa litakalopelekea mzazi kumlazimisha mtoto kula chakula kingi kupita kiasi. Fahamu kuwa, watoto wanajua kiwango cha chakula kinachowatosha na wakati gani ni muafaka wa kula.

Hivyo, itakuwa rahisi kwako k**a ukimsikiliza mtoto anataka nini, kuliko kulazimisha kile unachotaka wewe. Hakuna mtoto anayeweza kuvumilia kukaa na njaa. Watoto wote huhitaji chakula ili kucheza na kufurahi na wenzao. Hivyo basi, pale anakuwa na njaa atasema, au kulia, na ndio muda muafaka wa kumpa chakula unachotaka.

Swala muhimu la kuzingatia ni kuwa, katika mazingira yeyote, usimlazimishe mtoto kula. Usimkabe. Kulazimisha mtoto kula ni kumjengea tabia ya kuchukia chakula. Na akishajenga tabia hii hawezi kuacha sababu atakuwa anahusisha chakula na adhabu. Hakuna mtu anayependa adhabu. Hivyo, watu wengi wanaopenda kulazimisha mtoto kula kwa kumkaba huwa wanajenga tatizo kubwa zaidi ya lile la kula tu.

Follow
Facebook “Health issues-AFYA”

Like my page on instagram (afya_na_malengo)
16/09/2019

Like my page on instagram (afya_na_malengo)

MATATIZO YA UZAZIHupaswi kukata tamaa, afya njema ni haki yako na uamuzi upo mikononi mwako.Kwa matatizo ya uzazi na mag...
31/05/2019

MATATIZO YA UZAZI

Hupaswi kukata tamaa, afya njema ni haki yako na uamuzi upo mikononi mwako.

Kwa matatizo ya uzazi na magonjwa mbali mbali ya wanawake, wasiliana na mtaalam wa afya mapema aweze kukuskiliza kwaajili ya elimu, ushauri na tiba.

Weka appointment na daktari kwa sh. Elf kumi tu (10000). Piga namba chini hapo kupata utaratibu wa malipo kabla ya huduma.

Mawasiliano: 0742251673/ whatsapp/sms/ call

AFYA YAKO, MALENGO YAKO.

Address

Dodoma

Telephone

+255742251673

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AFYA YAKO kwanza. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to AFYA YAKO kwanza.:

Share