07/04/2025
Kwa miaka mingi sana, Manjano hutumika k**a kiungo cha chakula, dawa ya asili na pia katika urembo wa ngozi!
Kwa upande wa scrub ya manjano imekuwa moja ya msaada bora zaidi kwa urembo na afya ya ngozi kwa wengi!
Manjano yana wingi wa virutubisho k**a curcumin na antioxidants, ambayo husaidia katika kupunguza uvimbe, lakini pia katika kung'arisha ngozi, pamoja na kusawazisha rangi ya ngozi na kuleta mwanga wa asili.
Scrub ya manjano ina ina faida nyingi sana kwa urembo wa ngozi na afya kwa ujumla. Hizi hapa ni baadhi ya faida kuu za Scrub ya manjano kwa ngozi yako
FAIDA ZA SCRUB YA MANAJANO
1. Kupunguza Uvimbe
Curcumin, kiungo kinachopatikana kwenye manjano, husaidia kupunguza uvimbe na uwekundu, na pia kutuliza hali za ngozi k**a chunusi au eczema.
2. Kung'arisha Ngozi
Manjano husaidia kupunguza madoa meusi, rangi isiyo sawa ya ngozi, na kutoa mwangaza wa asili.
3. Kinga dhidi ya kuzeeka mapema (Anti-aging)
Manjano Ina viambato vya kuzuia uharibifu wa ngozi unaosababishwa na radicals huru, hivyo kupunguza dalili za mikunjo, kuchakaa na kuzeeka kwa ngozi mapema.
4. Kupambana na Chunusi
Pia manjano yanaaminika kuwa na viambata vya antibakteria ambavyo husaidia sana kwenye kuzuia chunusi kwa kuweka vinyweleo vyako vya ngozi vikiwa safi dhidi ya uchafu, mafuta na kuua bakteria ambao hupelekea chunusi.
5. Kusafisha Ngozi
Katika scrub, manjano husaidia kuondoa seli zilizokufa, na kufanya ngozi iwe laini na yenye afya.
Simu au Whatsapp: 0785868744 au 0759362030
Tupo Dodoma, Barabara ya kwenda Nanenane,
baada ya AZAM Unaingilia PETROL STATION ya kwanza
KUSHOTO COMPOUND yenye GHOROFA YA KIJANI KIBICHI