09/03/2025
Mwezi wa Ramadan ni kipindi cha ibada na mfungo. Ukirejea kauli ya mtume Muhammad (s.a.w) kuwa "Fungeni, mpate afya".. hivyo katika mwezi huu ni muhimu kuchagua vyakula vinavyosaidia mwili kupata nguvu, maji ya kutosha, na virutubisho muhimu kwa afya bora.
Hapa kuna miongozo ya lishe bora kwa waumini wa Kiislamu wanaofunga:
1. Wakati wa Kufuturu (Iftar).
Fungua kwa vyakula vyepesi vinavyorejesha nguvu haraka, k**a vile:
Maji – Ili kuzuia upungufu wa maji mwilini.
Tende – Husaidia kurejesha sukari mwilini na ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi na madini.
Juisi ya matunda – Husaidia kuongeza viwango vya sukari na maji mwilini.
Uji wa nafaka (mtama, ulezi, mahindi) – Rahisi kumeng’enywa na hutoa nishati ya haraka.
Baada ya futari, kula chakula chenye virutubisho kamili:
Wanga wa afya: Mchele wa sme (brown rice), ndizi mzuzu, viazi vitamu, ugali wa dona, au mkate wa ngano nzima.
Protini bora: Samaki, nyama ya kuku, mayai, maharagwe, dengu, na kunde.
Mboga na matunda: Mchicha, matembele, karoti, nyanya, pilipili hoho, parachichi, papai, machungwa, tikiti maji.
Mafuta mazuri: Karanga, mbegu za maboga, n**i, na mafuta ya mizeituni.
2. Wakati wa Daku
Daku ni muhimu kwani husaidia kudumu mchana wote bila njaa kali. Vyakula vya kuzingatia ni:
Wanga wenye nyuzinyuzi nyingi: Oats, ugali wa dona, wali wa brown, au mkate wa whole wheat.
Protini: Mayai, samaki, maziwa, siagi ya karanga, au kunde.
Maji na maziwa: Kunywa maji ya kutosha na epuka chai au kahawa nyingi ili kuzuia upungufu wa maji.
Mboga na matunda: Husaidia mmeng’enyo wa chakula na kuzuia kukosa choo.
3. Vyakula vya Kuepuka
Vyakula vyenye sukari nyingi: Soda, p**i, keki, na sharubati zenye sukari nyingi.
Chakula cha mafuta mengi: Chips, maandazi, vitumbua vya mafuta mengi.
Vyakula vya viwandani (processed foods): Vyakula vilivyosindikwa k**a soseji, biskuti, na juisi za madukani.
Chumvi nyingi: Chipsi, dagaa wenye chumvi nyingi, na vyakula vya makopo ili kuzuia kiu kupita kiasi.
4. Usimamizi wa Maji
Kunywa angalau glasi 8 za maji kuanzia futari hadi daku.
Epuka vinywaji vyenye kafeini nyingi k**a vile chai nyeusi, soda na kahawa kwani huongeza upotevu wa maji mwilini.
Kwa kufuata miongozo hii, waumini wanaweza kuwa na Ramadan yenye afya, kuzuia uchovu mwingi, na kudumisha nguvu mwilini.