Golden GATE Sanitarium Clinic

Golden GATE Sanitarium Clinic HIKI NI KITUO CHA SAYANSI YA TIBA MBADALA.

TUNATOA HUDUMA ZA TIBA KWA MAGONJWA MBALIMBALI KAMA VILE VIDONDA VYA TUMBO,MAGONJWA YA AKINA MAMA YOTE ALKADHALIKA NA WANAUME BILA KUSAHAU MAGONJWA YA ZINAA,MOYO,FIGO,INI,MAGONJWA YA MIFUPA NK.

12/08/2019

TUNAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID WAISLAM WOTE

10/08/2019

TUMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA AJALI YA MOTO ILIYOCHUKUA UHAI WA WATANZANIA WENZETU. HUU NI MSIBA MKUBWA KWA TAIFA, POLEN NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI MLIOPOTEZA WATU WA KARIBU. POLE KWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI, MKUU WA MKOA MOROGORO NA SECTOR BINAFSI WOTE THAMANI YETU NI SAWA MAUMIVU YAMETUFIKA SOTE KWA UJUMLA. NARUDIA TENA POLEN SANA

19/11/2018

TATIZO LA MIGUU KUWAKA MOTO (FOOT NEUROPATHY)
Tatizo hili huwafanya watu wasisinzie japo wanakuwa na usingizi.
Sababu za tatizo hili
1.Kudhoofika kwa neva za miguuni hivyo kupelekea kupoteza utendaji Kazi
2.Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu
3.Kuwa na sumu nyingi mwilini
4.Kurithi
5.Mwili kushindwa kufanya kazi zake vizuri
DALILI ZA TATIZO HILI
1.Kuhisi ganzi
2.Joto kali miguuni
3.Maumivu makali
4.Kuhisi kuchomwa na kitu chenye ncha kali miguuni
VITU VINAVYOWEZA KUPELEKEA KUTOKEA KWA TATIZO HILI
1.Matumizi ya dawa zenye kemikali kwa muda mrefu, mfano dawa za TB na HIV
2.Upungugu wa mkusanyiko wa virutubisho mwilini( Vitamin B complex)
3.Matatizo ya moyo
4.Matatizo kwenye mishipa ya damu
5.Kisukari,shinikizo la damu na fangasi
6.Uzito mkubwa mwilini
JINSI YA KUEPUKA TATIZO HILI
1.Kufanya mazoezi
2.Kuwa na uzito unaoendana na kimo chako
3.Ondoa sumu au kemikali mwilini mara kwa mara
4.Usafi wa viatu na soksi
5.Kula vyakula vyenye vitamin B complex
6.Chua miguu kwa vitu k**a limau na asali mbichi ili kusaidia mzunguko mzuri wa damu
7.Tumbukiza miguu kwenye maji ya vuguvugu yenye chumvi

 - *Pelvic Inflammatory Disease PID* UNAFAHAMU VIPI KUHUSU PID?Pelvic inflammatory disease,  ugonjwa huu unafahamika k**...
09/11/2018

- *Pelvic Inflammatory Disease PID*
UNAFAHAMU VIPI KUHUSU PID?

Pelvic inflammatory disease, ugonjwa huu unafahamika k**a PID, ni maambukizi kwenye via vya uzazi wa mwanamke . PID ni miongoni kwa magonjwa hatari sana kwa mwanamke una madhara makubwa na unaambukizwa kwa njia ya kujamiiana.
Ugonjwa huu unaweza ukapelekea uharibifu mkubwa kwenye mfuko wa uzazi,mayai ,mirija ya uzazi au sehemu nyingine za uzazi wa mwanamke
Na pia Pid ni moja ya chanzo cha ugumba kwa mwanamke ambacho kinaweza kuzuilika.

*TAKWIMU ZINAONESHA*
Kila mwaka,zaidi ya wanawake milioni moja nchini marekani wanapatwa na ugonjwa huu wa PID,
Matokeo yake zaidi ya wanawake 100000 wanakuwa wagumba kila mwaka.
Zaidi ya hayo idadi kubwa ya mimba zaidi ya 100000 inatungiwa kwenye mirija ya uzazi(ectopic pregnancy) inahusishwa na tatizo hilo la PID.
Kiwango kikubwa cha maambukizi ni kwa wasichana wadogo

*VISABABISHI VYA PID*
Kwa kawaida mlango wa uzazi (cervix) inazuia bakteria ambao wameingia ukeni wasisambae sehemu zingine za ndani za uzazi
K**a mlango wa uzazi cervix umepatwa na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana k**a kisonono na/au clamydia
Mlango huo wa uzazi cervix unaathirika na unakuwa na uwezo mdogo
wa kuzuia kusambaa kwa bakteria sehemu za ndani za uzazi.
PID inatokea pale vimelea vya magonjwa vinaposafiri kutoka kwenye mlango wa uzazi cervix kwenda sehemu za juu za uzazi.
Aslimia 90 ya PID husababishwa na kutotibiwa ugonjwa wa kisonono na klamidia
Visababibishi vingine vya PID
šŸ‘‰Kutoa mimba
šŸ‘‰Kujifungua
šŸ‘‰Vipimo kwenye mlango wa uzazi

DALILI ZA PID
Dalili za PID zinatofautiana,zinaweza kuwa zifuatazo
šŸ‘‰Maumivu ya tumbo sehemu ya chini au upande wa kulia
šŸ‘‰Kutokwa kwa uchafu ukeni usio wa kawaida wenye rangi ya kijani au ya njano na wakati mwingine una harufu isiyo ya kawaida
šŸ‘‰Kichefuchefu na kutapika
šŸ‘‰Homa
šŸ‘‰Maumivu wakati wa tendo la ndoa
šŸ‘‰Maumivu wakati wa kukojoa
šŸ‘‰Maumivu sehemu ya kulia upande wa juu wa tumbo

*HATARI ZA MWANAMKE KUPATA PID*
Kuna baadhi ya vitu ambavyo vinamuweka mwanamke katika hatari ya
kupata PID ni k**a vifuatavyo

1.Wanawake wenye magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana k**a kisonono na klaimidia wako hatarini sana kupata PID
2.Wanawake ambao waliwahi kupata PID wako hatarini kupata tena
3. Wasichana wadogo wapo hatarini kupata PID kuliko wazee.
4.Wanawake wenye wapenzi wengi wako katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa na PID

Baadhi ya tafiti zinaeleza uoshaji wa uke unachangia kupata PID.Kuosha uke( Douching) kunaweza pelekea kusukuma bakteria sehemu za juu za via vya uzazi na kuzuia kutoka kwa uchafu ambao mwanamke angeweza kutumia k**a ishara ya kwenda kuonana na wataalamu wa Afya mapema

*MADHARA YA PID*
Kutokea /kujirudia kwa PID kunaweza kusababisha
kutokea kuharibika mirija ya uzazi ambayo inaweza kupelekea
šŸ‘‰Ugumba
šŸ‘‰Mimba kutunga kwenye mirija ya uzazi(ectopic pregnancy)
šŸ‘‰Maumivu makali kwenye shingo ya kizazi
Kati ya wanawake nane (8) wanaougua PID mmoja(1) unakuwa mgumba

*JINSI YA KUJIKINGA NA PID*
PID inaweza kuzuilika kabisa ,kisababishi kikubwa cha pid ni magonjwa ya zinaa Mambo ya kuzingatia ili uweze kujikinga na PID
šŸ‘‰Epuka kufanya mapenzi na watu wengi
šŸ‘‰Tumia njia za uzazi wa mpango(barrier) k**a kondomu
šŸ‘‰Tumia spermicides kwa kila tendo la ndoa hata k**a unameza vidonge vya uzazi
šŸ‘‰ Usitumie IUDs k**a unawapenzi wengi.


IUDs ni vitu vinavyowekwa ndani ya uke kuzuia mimba
šŸ‘‰Wahi matibabu ukiona dalili zozote za PID au za magonjwa ya zinaa k**a kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni,maumivu kiunoni nk
šŸ‘‰Pia fanya uchunguzi wa afya ya uzazi mara kwa mara ili k**a kuna tatizo ligundulike na litibiwe kabla halijasambaa kwenda kwenye viungo vya ndani vya uzazi

*MATIBABU YA PID*
Antibiotics hutumika kutibu PID kwa awali na kwa matibabu ya PID ya awali antibiotics za kunywa hutumika.
K**a tatizo limekuwa kubwa mgonjwa atapewa antibiotics ya kunywa na pia ya sindano,k**a utagundulika na tatizo hili mwenza wako au wenza wako watibiwe hata k**a hawana dalili zozote vinginevyo tatizo litaweza kujirudia mtakaposhiriki tendo la ndoa
TATIZO LIKIZIDI LIKAWA KUBWA YANI USAHA UKAVIMBIA ITAKUBIDI UFANYIWE UPASUAJI.
*HATUCHOKI KUWAELIMISHA*

01/11/2018

Warm and heartfelt wishes to the Golden gate sanitarium clinic family members.

PROSTATE PROBLEM: TEZI IPO KARIBU NA KIBOFU CHA MKOJOBY DR KAVISHE0715-030962/ 0756-097022Wengi wanatambua k**a tatizo l...
14/04/2018

PROSTATE PROBLEM: TEZI IPO KARIBU NA KIBOFU CHA MKOJO

BY DR KAVISHE

0715-030962/ 0756-097022

Wengi wanatambua k**a tatizo la kibofu cha mkojo
HALI HALISI: Ni kokwa ambayo ipo chini ya kibofu cha mkojo ambapo mrija wa kupitisha mkojo hupita ndani yake

DALILI ZIONEKANAZO KWA MTU MWENYE TATIZO HILI:
1. Matatizo yanaoambatana na kukojoa
a) Kubanwa na mkojo mara kwa mara (hasa usiku zaidi)
b) Damu kwenye mkojo
c) Maumivu wakati wa kukojoa
d) Maumivu baada ya kukojoa au wakati mtu anamalizia kukojoa
e) Kushindwa kukojoa (kubanwa mkojo lakini ukienda chooni mkojo hautoki)
f) Matone ya mkojo kutoka yenyewe au mtu kushindwa kujizuia na kukuta mkojo umetoka

2. Matatizo ya uzazi au matatizo ya nguvu za kiume
a) Maumivu wakati wa tendo la ndoa (hasa wakati mbegu za kiume zinapotoka nje).
b) Kupungukiwa na nguvu za kiume
c) Wakati mwingine inafikia kipindi mtu a**lalamika kuwa amepungukiwa na nguvu za kiume na kuamua kutafuta dawa za kuongeza nguvu. Atapata dawa hizo, na baada ya muda tatizo hujirudia, kumbe inakuwa hajatibu au hajaliondoa tatizo

3. Maumivu sehemu ya chini ya mgongo
4. Maumivu sehemu ya chini ya tumbo (wengine hulalamika kwamba wanapata maumivu kwenye kibofu cha mkojo).
5. Maumivu kwenye mapaja
6. Maumivu kwenye nyonga au hips

ANGALIZO: Mtu mwenye shida hii anaweza akajihisi k**a amepungukiwa na nguvu za kiume au anaweza kudhani ni tatizo la UTI ambapo wengi hutibiwa na tatizo kuendelea kuwepo. Hii husababishwa na ile hali ya yale maji maji (semen) yanayosafirisha mbegu za kiume kutokuwepo (kutokana na prostate gland kupata tatizo), hatimaye mbegu hizo huishia njiani.
Hali ikizidi kuwa mbaya inaweza ikasababisha mtu kufanyiwa upasuaji.

MAWASILIANO: 0715 030961/0756-098022
Email goldgatesanitarium@gmail.com

🌳🌲* *MAUMIVU YA TUMBO KIPINDI CHA HEDHI* * Kuumwa tumbo wakati wa hedhišŸ€Tumbo la hedhi au maumivu wakati wa hedhi (perio...
25/11/2017

🌳🌲* *MAUMIVU YA TUMBO KIPINDI CHA HEDHI* *

Kuumwa tumbo wakati wa hedhi

šŸ€Tumbo la hedhi au maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo. Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huanza pale mayai yanapotoka katika mirija (fallopian tubes) na kuteremka chini ya mirija hiyo wakati wa Ovulation.

*Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili* . šŸ€Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea) ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.

šŸ€Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea) ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba k**a vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.

šŸ€Takribani nusu ya wanawake wote waliopo katika umri wa kuweza kupata mototo wanakumbana na maumvu wakati wa hedhi, maumivu ambayo huanza siku chache kabla ya hedhi na kuendelea kwa siku kadhaa. Baadhi ya wanawake hupata maumivu ya kawaida lakini kwa wengine maumivu huwa makali sana hadi kupelekea kushindwa kufanya shuguli zao. Hii ni moja ya sababu watoto wa shule kukosa vpindi kwa siku kadhaa. Ili kupata tiba basi wanawake wengi hukimbilia kunywa dawa za kupunguza maumivu na baadhi ya madactari hutoa ushauri wa kunywa vidonge ili kuzuia hedhi ili kupunguza makali ya maumivu, njia zote hizi mbili zikiwa na madhara na pia kutoweza kutoa suluhisho ala kudumu la tatizo husika.

šŸ€Uchunguzi unaonyesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.

šŸŒ±ā€¢ Kuwa na umri wa chini ya miaka 20.

šŸŒ±ā€¢ Kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo.

šŸŒ±ā€¢ Kutoka na damu nyingi wakati wa hedhi. (suala hilo linaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali ya kitiba).

šŸŒ±ā€¢ Wanawake ambao hawajawahi kuzaa.

*Maumivu ya Tumbo la Hedhi... Sehemu ya Pili*

🌿Hii inahusisha magonjwa ambayo husababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:

šŸŒæā€¢ Endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuota nje ya fuko hilo, au hta sehemu nyinginezo.

šŸŒæā€¢ Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaoota katika mfuko wa uzazi.

šŸŒæā€¢ PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga

šŸŒæā€¢ Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.

šŸŒæā€¢ Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.

🌿Baada ya kujua baadhi ya matatizo ya wanawake yanayoweza kusabibisha hedhi inayoambatana na maumivu ya tumbo,

⁉ *hebu sasa na tuzijue tumbo la mwezi linaumaje?* ⁉

⚔1. Maumivu mara nyingi si makali.

⚔2. Muumivu huja na kuondoka, na kwa kiwango tofauti

⚔3. Maumivu zaidi huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo.

⚔4. Huchanganyika na maumivu ya sehemu ya chini ya mgongoni ambayo husambaa mpaka mapajani.

⚔5. Kujihisi kutapika, kichefuchefu na wakati mwingine hata kutokwa jasho.

⚔6. Kupata choo kilaini au hata kuharisha.

⚔7. Kufunga choo.

⚔8. Tumbo kuwa kubwa au kuwa gumu.

⚔9. Kuhisi maumivu ya kichwa.

⚔10. Kutojihisi vizuri au kujisikia kuchoka.

Wasiliana nami kwa maoni zaid.
0715-030961/
0756-098022.

MAUMIVU MAKALI YA MGUU, MGONGO, BEGA AU MKONO.SPINAL DISC (DISC ZA UTI WA MGONGO) ZINAVYOLETA MAJANGASpinal Disc ni disk...
19/10/2017

MAUMIVU MAKALI YA MGUU, MGONGO, BEGA AU MKONO.

SPINAL DISC (DISC ZA UTI WA MGONGO)
ZINAVYOLETA MAJANGA

Spinal Disc ni disk zinazokaa kati kati ya pingili ā€œSpinal Vertebraeā€ za uti wa mgongo. Kuna wakati disk hizo hutoka sehemu yake na kusogea pembeni tatizo ambalo linajulikana kwa majina kadhaa k**a vile DEGENERATIVE DISC DISEASE au HERNIATED DISC au SLIPPED DISC. Tatizo hili husababisha maumivu makali ya mguu, mgongo, bega au Mkono. Maumivu haya huwa ni makali mno, katika mazingira mengine huuja na kutoweka, katika mazingira mengine maumivu haya huwa endelevu.

Naamini wengi wetu tumeshawahi kusikia au kuona ndugu, rafiki, jamaa, jirani fulani akiumwa mguu, mkono, bega au mgongo tena kwa maumivu makali sana.

Wengi wamehangaika hospitali nyingi bila mafanikio, wengine wamekimbilia kwenye huduma za maombezi na wengine wamekimbilia kwenye tiba mbadala na wengine wamekimbilia kwa Sangoma.

Kote huko wamekosa ufumbuzi wengine wamepoteza maisha na wengine wamepata kupooza kabisa mguu au miguu wakiwa wameshatuoa fedha nyingi sana na mateso makali.







Nilibahatika kufanya mazungumzo na baadhi ya waliowahi kupatwa na matatizo k**a haya. Ndugu Selemani Mkoba alinielezea tatizo hilo lilivyomtesa na baada ya kuhangaika hospitali kwa zaidi ya miezi 3 wakati wote kiteseka kwa maumivu makali na kupoteza hela nyingi bila mafanikio aliamua kwenda kwa waganga wa kienyeji. Anasema Mganga alimpa matumaini makubwa lakini wiki kadhaa zikawa zinapita bila kupata unafuu wowote. Anasema Mgonga alikuwa akimpa matumaini kwa kumwambia ugonjwa unaingia ghafla lakini kutoka unatoka taratibu sana . Ndugu Mkoba anasema kwa bahati alipomwelezea tatizo hilo mmoja wa rafiki zake ambaye si daktari alimwambia aondoke haraka huko na kuwahi Muhimbili. Rafiki yake huyo alimweleza kuwa a**lifahamu tatizo hilo.

Ndugu Mkoba amasema alienda Muhimbili k**a alivyoshauriwa na rafiki yake, akafanyiwa kipimo cha MRI ambapo waligundua tatizo hilo katika uti wa mgongo na kupangiwa siku ya upasuaji. Alifanyiwa upasuaji na alipozinduka alikuwa na maumivu makali ya wastani yatokanayo na upasuaji tu .. maumivu ya mguu hayakuwepo tena. Maumivu yatokanayo na upasuaji yaliendelea kupungua na sasa ni miezi mitatu amebakiwa na maumivu madogo sana mbayo yanaendelea kupoteza huku akiendelea na mazoezi. Anaweza kuendesha Gari, anaweza kutembea na kufanya shughuli zake ambazo zilisimama. Aidha Ndugu Mkoba anasema angependa watu wajue hili ili wasi mateso aliyoyapata yeye na walio kwenye mateso hayo wapate ufumbuzi haraka maana ni mateso yanayotisha.

MGAWANYIKO WA UTI WA MGONGO NA MATOKEO YA DISCK ZINAPOCHEZA

Uti wa mgongo umegawanyika katika aina kuu zipatazo nne (4) za pingili ā€œSpinal Vertebraeā€

Cervical Curve: Hili ni eneo la juu la uti wa mgongo, Eneo hili linaanzia uti wa mgongo unpokutana na kichwa na kuishia eneo la mwisho la Shingo, kwa lugha nyepesi ndilo eneo linalomiliki shingo, pingili zilizopo katika eneo hili zinaitwa ā€œCervical Vertebraeā€.

• Maeneo yanayoathiriwa na Disc kucheza katika eneo hili ā€œCervical Disc Herniationā€ ni Mikono au Mabega au kifua, moja wapo ya viungo hivi vitapata maumivu makali sana.

Thoracic Curve: Hili ni eneo la uti wa mgongo linalofuatia kuelekea chini likianzia inapoishia Shingo, Eneo hili linaishia katikati ya mgongo, kwa lugha nyepesi eneo hili ndilo linalomilike mbavu. Pingili zinazopatikana katika eneo hili zinaitwa ā€œThoracic Vertebraeā€.

• Kucheza kwa disck katika eneo hili kutakusababishia maumivu makali ya Mgongo eneo la juu ya Kiuno.

Lumbar Curve: Eneo hili linaanzia inapoishia Thoracic Curve na kuelekea chini na kukutana na Eneo linaloitwa Sacral Curve au eneo la kiuno linapoanzia. Eneo la Lumba linazungukwa na ma matumbo na mazagazaga mengine yasiyokuwa na mifupa. Pingili za uti wa mgongo zinazopatikana katika eneo hili zinaitwa ā€œLumbar Vertebraeā€

• Ikiwa Disc zitacheza katika eneo hili mhusika atapata maumivu makali ya mguu maumivu ambayo yaukumba mguuu wote kuanzia sehemu ya ndani ya tako na kushuka chini mpaka mwisho wa mguu kwenye kisigino.

Sacral Curve: Eneo hili linaanzia pale Lumbar Curve inapoishia hadi mwisho wa uti wa mgongo kwa chini. Katika lugha nepesi eneo hili ndilo linalomiliki kiuno. Pingili zinazopatikana katika eneo hili zinaitwa ā€œSacral Vertebraeā€

SABABU ZA MATATIZO HAYA

• Ajali ya Gari
• Kuanguka
• Kupigwa/kupigana
• Michezo
• Ajali katika sehemu za kazi
• Kasoro wakati wa kuzaliwa
• Kubeba vitu vizito
• Ukaaji mbaya wa muda mrefu
• Misukosuku mbali mbali ya mwili k**a

MATIBABU

Tatizo hili linatibika ikiwa mgonjwa atawahi kufanyiwa uchunguzi sahihi na tatizo hilo kugundulika. Kuna matibabu ya namna tofauuti ambayo daktari anaweza kukupa lakini hali inapokuwa mbaya Madaktari hulazimika kufanya upasuaji. Mgonjwa anatakiwa kupimwa kwa vipimo sahihi na kipimo kinachoAMINIWA zaidi ni MRI. Aidha kwa bahati Tanzania moja ya nchi chache barani Afrika zenye mitambo hii ya MRI na moja ya nchi chache barani Afrika zenye madaktari bingwa wa matatizo haya.

Wadau badala ya ya kutumia fedha nyingi kwa waganga wa kienyeji tuwahi hospitali hususani Muhimbili kuonana na mabingwa wa NEURAL. Rai yangu kwa serikali pamoja na kuwa sisi tumekuwa moja katika nchi chache zenye huduma hii, mahitaji ya Madaktari hawa ni makubwa sana bado, Serikali ipeleke Madaktari zaidi nje kwa ajili ya kupatiwa ujuzi huu na kuongeza mashine za MRI angalau zifike 10.

NAMNA YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI

Matunzo mazuri ya ujauzito
Kuepuka kipigana au kupigwa, usimpige mwenzako kwasababu unaweza kumsababishia tatizo baadae
K**a unaendesha gari ama piki piki kuepuka mwendo unaoweza kukusababishia ajaili
Uangalifu katika michezo na mazoezi mazito
Kujilinda kiafya ili kujiepusha na maradhi yasiyotambulika
Tujiepusha na ukaaji mbaya wa muda mrefu katika sehemu zetu za kazi, pendelea kutafuta maelekezo jinsi ya kukaa katika sehemu yako ya kazi.
Pendelea kuangalia afya mara kwa mara na kupata ushauri wa madaktari.

Imeandaliwa na MD Dr Richard Kavishe
0715-030961/0756-098022
goldgatesanitarium@gmail.com

BAWASILI{HEMORRHOIDS}Bawasili ni hali ya kuvimba au kutanuka kwa mishipa ya vena{varicose viens} iliopo ndani ya njia ya...
17/10/2017

BAWASILI{HEMORRHOIDS}
Bawasili ni hali ya kuvimba au kutanuka kwa mishipa ya vena{varicose viens} iliopo ndani ya njia ya haja kubwa. Katika ile misuli imara inayozungunguka na kutengeneza muundo wa njia ya haja kubwa pamoja na puru{rectum}ambapo sasa ugawanywa katika aina mbili ya ndani na ya nje.
Bawasili ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi.
Kuna aina mbili za Bawasiri

Nje: Aina hii ya bawasili hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Hali hii huwa na maumivu makali sana na ngoziyake ugeuka kuwa ya blue au zambarau. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina fulan ambalo kitaalamu linaitwa Thrombosed hemorrhoid.

Ndani: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?

• Tatizo sugu la kuharisha
• Kupata kinyesi kigumu
• Ujauzito
• Uzito kupita kiasi (obesity)
• Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (a**l s*x)
• Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.kunyanyua vitu vizito, kikohozi cha muda mrefu nk
• Umri mkubwa,
• Vyakula vya kukoboa,
• Kufanya kazi ukiwa umekaa kwa muda mrefu.
• Kuchuchumaa kwa muda mrefu wakati wa kujisaidia.
• Mtu mwenye tatizo la ini
•

Dalili za bawasili

• Damu kwenye kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
• Maumivu au usumbufu njia ya haja kubwa
• Kinyesi kuvuja.
• Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
• Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
• Kujitokeza kwa kinyama (bawasili) wakati wa haja kubwa

Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri

• Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
• Strangulated hemorrhoids
• Kushindwa kujisaidia kwa amani

Njia za kuzuia Bawasiri

• High fibre diet {makapi lishe}, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
• Kunywa maji mengi kiasi cha kutosha.
• Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.
• Fanya mazoezi
Utofauti wa hemorrhoids na re**al fissures
• Bawasili ni hali ya kuvimba kwa mishipa ya vena iliopo ndani ya haja kubwa. Re**al fissures ikiwa ni hali ya kuchanika au kuwa na vidonda kwenye njia ya haja kubwa. Na ikiwa ni tatizo ambali hutokana na kupata kiasi kikubwa kupita uwezo wa njia yenyewe. Hivyo basi k**a kutaingia bacteria basi hili huwa ni tatizo la kudumu eneo husika.
Prepared by Golden gate sanitarium clini
Under Dr. Ritchard kavishe
Hotline 715-030961 /0756-098022
• Email goldgatesanitarium@gmail.com

Leo saa tatu hadi nne kamili. Utakuwa nami katika kipindi cha afya tukidadavua ugonjwa wa fangas, vyanzo, dalili, kinga ...
30/07/2017

Leo saa tatu hadi nne kamili. Utakuwa nami katika kipindi cha afya tukidadavua ugonjwa wa fangas, vyanzo, dalili, kinga na madhara yatokanayo na ugonjwa huo. Afm92.9 Dodoma na kanda ya kati. Hata kwa njia ya mtandao utatupata loud and clear.

21/07/2017

Tangazo tangazo tangazo.

Kuna matapeli wanawaibia watu kwa kutumia jina langu. Wanawapa dawa alafu kibaya zaidi wanawapa namba zangu. Ili kukiwa na tatzo wanitafte, samahani sana k**a jina lako halipo katika daftari la mahudhurio. Hatukutambui na utakuwa umeibiwa. Tuna taratibu za kufuata kabla ya kupewa dawa hivyo basi k**a hukufuata taratibu hizo wewe utakuwa umetapeliwa. Unatakiwa upewe namba ya card itakayokutambulisha muda wote wa matibabu.
Huyo anayekuhudumia k**a mmekutana njiani au hujaona nembo na jina LA Golden Gate Sanitarium Clinic jua umeibiwa.

Address

2244 Moshi
Dodoma

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Telephone

+255715030961

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Golden GATE Sanitarium Clinic posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Golden GATE Sanitarium Clinic:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram