17/05/2021
KISUKARI [DIABETES MELLITUS TYPE 2, DM-2]
Hiki ni aina ya kisukari ambacho kipindi cha nyuma kilijulikana k**a ‘kisukari cha watu wazima, japo katika zama za sasa hata watoto wadogo bado wanaathirika.
Kisukari ni ugonjwa ambao unaambatana na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu, pamoja na kufeli kwa mwili kutumia homoni ya insulin (homoni hii ndio inayohusika kwenye matumizi ya sukari au
glucose mwilini), pamoja na kufeli kwa kongosho kutoa homoni ya insulin, na utoaji wa homoni nyingi ya glucagon (homoni hii inafanya kazi kinyume cha insulin hivyo inaongeza sukari ndani ya damu).
Kwa DM-2, mgonjwa hatategema matumizi ya Insulin maisha yake yote k**a ilivyo kwa DM-1, ingawaje wagonjwa watakuja kutumia hii homoni k**a dawa kipindi fulani.
DALILI KUU ZA ‘KISUKARI CHA WATU WAZIMA'
• Kukojoa mara kwa mara, kuhisi kiu sana mara kwa mara, pamoja na njaa, na kupoteza au kuongezeka uzito
• Kuona kwa tabu
• Kuhisi hali isiyo ya kawaida kwenye miguu.
Kwa mgonjwa wa kisukari, kiwango cha sukari mwilini kinatakiwa kuwa au zaidi ya 11.1 mmol/L kwenye kipimo maalum muda wowote kituo cha afya ama nyumbani.
KISUKARI KITOKANACHO NA UJAUZITO (GESTATIONAL DIABETES)
Ni kiwango chochote cha sukari mwilini kilichozidi kuliko kiwango cha kawaida kinachojulikana wakati
wa ujauzito.
Hata ivyo, kuongezeka kidogo kwa sukari ni sehemu ya kawaida ya ujauzito.
Kisukari hichi kisipotibiwa kinaweza sababisha madhara kwa mtoto k**a kuzaliwa na uzito uliozidi,
kuwa na kiwango kidogo cha sukari mwilini, kiwango kidogo cha madini ya calcium mwilini pamoja na
kuwa na manjano kwenye ngozi au machoni.
Vilevile, mwanamke anayepata kisukari kipindi cha ujauzito yupo hatarini zaidi kujifungua kwa upasuaji (Cesarean delivery).
MATIBABU NA MALENGO YA MATIBABU:
Malengo ya matibabu ya kisukari yanalenga sehemu kuu tatu (3);
1. Kuzuia au kupunguza athari za mishipa midogo ya damu kwenye macho na figo kwa kuweka sahawia viwango vya sukari na shinikizo la damu.
2. Matibabu ya kuzuia au kupunguza athari kwenye mishipa mikubwa ya damu kwenye moyo, kichwani na mikononi na miguuni kwa kuweka sahawia viwango vya mafuta mwilini, pamoja na shinikizo la damu, na kuacha uvutaji wa sigara.
3. Kuzuia na kutibu athari mwili kushindwa kumeng'enya chakula, pamoja na matatizo ya neva kwa kuweka sahawia kiwango cha sukari mwilini.
MAPENDEKEZO YA KITABIBU KATIKA MATIBABU YA KISUKARI:
1. Matibabu maalum yanayolenga kushusha kiwango cha sukari mwilini
2. Lishe, mazoezi na elimu k**a msingi wa matibabu
3. Matumizi ya dawa ya metformin k**a dawa ya kwanza (first- line treatment) hadi itakavyopendekezwa vingine.
4. Baada ya matumizi ya metformin, nyongeza ya dawa moja au mbili ya vidonge ama sindano
katika juhudi za kupunguza mathara kwa kadri itakavyowezekana.
5. Matumizi ya Insulin yenyewe au ikichanganywa na dawa nyingine pindi juhudi zaidi zitahitajika
katika kuweka sahawia kiwango cha sukari kwenye damu.
6. K**a itawezekana, maamuzi ya matibabu yanaweza kumhusisha mgonjwa mwenyewe, kwa kuzingatia vitu ambavyo mgonjwa atapendelea, na atakavyohitaji.
7. Uangalizi maalum katika mfumo wa moyo na mishipa ya damu katika juhudi za kupunguza athari za ugonjwa kwenye mfumo huo.
MIKABALA KATIKA KUZUIA MATATIZO YA MUDA MREFU YA KISUKARI
• Upimaji wa kiwango cha hemoglobin (protini ya kwenye damu inayotoa rangi nyekundu) HbA1c kila baada ya miezi mitatu mpaka sita
• Vipimo vya macho
• Kucheki kiwango cha protini (microalbumin) mara kwa mara
• Uangalizi na vipimo vya miguu
• Shinikizo la damu kwa kuzingatia kiwango kiwe chini ya 130/80 mmHg
• Matumizi ya dawa ya Statin (dawa inayoshusha kiwango cha mafuta mwilini).
MATATIZO YANAYOAMBATANA NA KISUKARI
1. Matatizo ya ya mfumo wa moyo na usafirishaji wa damu mwilini. Hii husababishwa na
kuongezeka kwa kiwango cha cholesterol isiyohitajika mwilini (bad cholesterol- LDL) na kushuka kwa kiwango cha cholesterol nzuri mwilini (HDL).
2. Mwili kushindwa kutumia homoni ya insulin inayotolewa na kongosho (insulin resistance) na hivyo kusababisha mlundikano wa mafuta kwenye ini na misuli.
3. Kupungua kwa uwezo wa kupokea na kuchakachua mawazo, pamoja na kutoa mawazo au maamuzi (cognitive decline). Hii utokana na kupungua kwa ukuaji wa seli za ubongo na kusababisha ugonjwa wa Alzheimer na kiharusi.
KISUKARI KINACHOTOKANA NA MAGONJWA MENGINE:
1. Magonjwa yanayoathiri seli za kongosho
2. Matatizo na magonjwa ya homoni za mwili ambayo yanaingilia utolewaji wa homoni ya insulin.
3. Magonjwa ya mwilini yanayosababisha mwili kushindwa kuchekecha au kuitumia homoni ya insulin kutoka kwenye kongosho. Dawa za matibabu ya mshtuko wa ubongo, aleji na dawa ya estrogen.
MAENDELEO, NA ATHARI ZA MUDA MREFU MWILINI MWA MGONJWA WA KISUKARI
1. Matatizo ya macho (Diabetic retinopathy)
Kwa tafiti za Marekani, kisukari ndio ugonjwa unaoongoza kwa kusababisha upofu kwa watu wazima kati ya umri wa miaka 20 hadi 74.
Ugonjwa huu husababisha kuharibika kwa mishipa ya damu iliyopo upande wa nyuma wa jicho (retina), sehemu ambayo inahusika na kupokea mwanga kutoka nje ya jicho kuingia ndani katika jitihada za kusaidia jicho kuona.
2. Ugonjwa wa figo usiotibika (End Stage Renal Disease, ESRD)
K**a ilivyo kwa upofu, kufeli kwa figo kwa kiwango kisichoweza kutibika husababishwa na
kisukari zaidi ya ugonjwa wowote mwingine katika nchi zilizoendelea k**a Marekani.
3. Kisukari ndio ugonjwa unaoongoza katika athari za ukataji wa miguu kwa binadamu (pasipo
kuzingatia ajali).
4. Ugonjwa wa mishipa ya damu ya moyo (Coronary Heart Disease, CHD). Wagonjwa wenye kisukari wapo hatarini sana kuugua huu ugonjwa baada ya muda mrefu kuliko mtu asiye na kisukari.
Vilevile, ugonjwa hatarishi zaidi kwa wagonjwa wa kisukari ni Ugonjwa wa moyo na mishipa yake ya damu (Cardiovascular Disease). ⅔ ya vifo vitokanavyo na kisukari hutokana na matatizo ya moyo.
5. Kufeli kwa moyo (heart failure) ndio athari kuu ambayo huibuka kwa vijana wadogo ambao huugua aina hii ya kisukari (DM-2)
6. Saratani pia ni moja ya tatizo ambalo husadikika kusababishwa na kisukari. Saratani maarufu zaidi ni saratani ya kibofu cha mkojo, ambayo huibuka zaidi kwa watumiaji wa dawa ya kutibu
kisukari iitwayo pioglitazone.
7. Homa ya mapafu (pneumonia). Wagonjwa wengi wa kisukari pia huugua kirahisi homa ya mapafu, k**a moja ya magonjwa yanayoathiri hawa wagonjwa. Fangasi ndio kisababishi kikuu
cha magonjwa ya kuambukizwa kwa wagonjwa hawa.