17/06/2025
*FAHAMU UHUSIANO ULIOPO KATI YA BINZARI (MANJANO) na MDALASINI KATIKA AFYA YA UZAZI WA MWANAMKE.*🤰🤱
Licha ya kuwa viungo bora kwenye chakula kwa muonekano wake, radha yake na harufu yake nzuri ya kuvutia binzari (manjano) na mdalasini ni tiba nzuri sana katika afya zetu. Vina uwezo mkubwa wa kuleta utulivu wa akili, kutibu gesi tumboni na kiungulia, kusaidia kwenye urembo wa ngozi, kupunguza uzito lakini vina faida nyingi zaidi katika afya ya uzazi wa mwanamke.
*Faida zake katika afya ya uzazi kwa mwanamke:*👇
1. Hutibu uvimbe maji kwenye mayai yaani Ovarian Cyst.
2. Hupevusha na kukomaza mayai ili ubebe ujauzito kiurahisi.
3. Kuponya maumivu ya hedhi yaani chango la uzazi.
4. Inaondoa sumu ya uzazi wa mpango mwilini.
5. Huzibua mirija iliyoziba, mirija iliyojaa maji na mirija iliyojaa uchafu.
6. Inatibu makovu kwenye kizazi na kwenye mirija.
*FANYA HIVI:*👇
Chukua binzari (manjano) nyingi kisha usage unga wake ambao utakuwa unatumia kila unapohitaji.
Vilevile chukua mdalasini mwingi kisha usage unga wake ambao utakuwa unatumia kila unapohitaji.
*MATUMIZI YAKE:*👇
1. Chemsha maji kikombe kimoja yapate uvuguvugu kisha epua na uweke kwenye kikombe, ongeza kijiko kimoja cha unga wa mdalasini, kijiko kimoja cha unga wa binzari (manjano) na kijiko kimoja cha asali. Kisha koroga kwa pamoja chai hii na unywe kikombe kimoja asubuhi na kimoja jioni kwa siku 30 mfululizo kupata matokeo mazuri.
2. Chemsha maziwa fresh kikombe kimoja kisha epua weka kwenye kikombe, ongeza kijiko kimoja cha unga wa mdalasini, kijiko kimoja cha unga wa binzari (manjano) na kijiko kimoja cha asali. Kisha koroga kwa pamoja chai hii na unywe kikombe kimoja asubuhi na kimoja jioni kwa siku 30 mfululizo kupata matokeo mazuri.
Chagua njia mojawapo kati ya hizo mbili itakayokuwa rahisi kwako.
Usiweke sukari.❌
* *