06/07/2025
Taasisi ya Mafunzo ya Afya ya Kimataifa Ifakara (Tanzanian Training Centre for International Health) - TTCIH iliyopo mjini Ifakara Mkoani Morogoro inawatangazia umma kwamba sasa inapokea maombi ya kujiunga na Chuo kwa mwaka wa masomo 2025/26 kwa kozi zifuatazo;
1. Stashahada ya Utabibu
2. Stashahada ya Ufamasia
3. Stashahada ya Optometria
Sifa za Muombaji
Stashahada ya Utabibu - Ufaulu angalau D ya Biology, Chemistry na Physics
Stashahada ya Ufamasia - Ufaulu angalau D ya Biology na Chemistry
Stashahada ya Optometria - Ufaulu angalau D ya Biology, Chemistry, Basic Mathematics, English na Physics/Engineering Sciences
TTCIH imesajisajiliwa NACTVET kwa namba HAS/003. Chuo kina mazingira tulivu na mazuri kwa kujifunza ikiwa pamoja na wakufunzi waliobobea katika fani za afya na tafiti, hospitali ya kujifunzia kwa vitendo, mtandao wa uhakika, na kutoa mafunzo kupitia Mfumo wa Mafunzo kwa Njia ya Masafa unaosimamiwa na Wizara ya Afya (National eLearning Platform for Health).
Kwa kujaza fomu moja kwa moja Chuoni na maelekezo zaidi piga simu namba zifuatazo: 0781,845374, 0718 552 164, tembelea tovuti yetu www.ttcih.ac.tz au tutumie barua pepe info@ttcih.ac.tz
/26