Magonjwa ya Wanawake

Magonjwa ya Wanawake You're health is our concern , Call us +255769600821 or +255655562181

FAHAMU UNDANI KUHUSU UGONJWA WA ACID REFLUX/TINDIKALI YA TUMBO (GERD-GastroEsophagaelRefluxDesease)+255655562181 , +2557...
10/07/2025

FAHAMU UNDANI KUHUSU UGONJWA WA ACID REFLUX/TINDIKALI YA TUMBO

(GERD-GastroEsophagaelRefluxDesease)

+255655562181 , +255769600821

• Ni tatizo linalotokea katika mfumo wa mmeng'enyo na kusababisha hitilafu ya chakula au maji kurudi katika koo la chakula (*Umio*) mara baada ya kuwa chakula Hiko kimeshamezwa au Ni kitendo cha kupanda kwa acid ( *tindikali* ) ya tumbo hadi kwenye Koo /Umio la chakula kwa muda mrefu na kusababisha kiungulia ( *HEARTBURN* ).

• Kiungulia hiki huanza muda mfupi baada kumaliza kula na kuisha baada ya masaa mawili.
• Pia dalili za tatizo hili kwa watoto hujionesha pale m tototo anapotapika kupita kiasi au kupaliwa mara kwa mara wakati wa kula chakula.

_*Dalili zingine ni k**a*_

• Tumbo kuunguruma na Kukosa hamu ya kula chakula na kuhisi kichefuchefu.
• Mdomo kunuka kutokana na kurudi juu kwa chakula cha tumboni chenye tindikali.
• Kupata hali ya kuunguza kwenye kifua karibu na moyo, hali inayotokea Muda Mfupi baada tu ya kula na kupata shida wakati wa kumeza chakula.
• Kucheuwa Maji Maji Yenye Tindikali Ukiwa Usingizini Hasa Baada Ya Kulala Muda Mfupi Baada Ya Kula.
• Kukohoa au kupaliwa mara kwa mara ikiambatana na kuweweseka Kwa Kukosa Pumzi.
• Mdomo kuwa mchachu muda mwingi.
•Kuvimba Kwa Tezi za Shingoni K**a Vile Tonses na Goita.
• Mdomo kukauka.
• Meno kupoteza uimara na kuanza kumomonyoka kutokana na uwepo wa tindikali.
• Tumbo kujaa Gesi , Kupata Choo K**a Tope Kunakoambatana kujamba sana.
• Tumbo Kuunguruma Hasa Muda Mfupi Baaada Ya Kula.

• Tatizo la Acid / Tindikali Ya Tumbo Linatibika na Kupona Kabisa.

-📞"Wasiliana nasi kuhusu afya - Kupitia Simu Namba 0655562181 / 0769600821

°Au Kuchart Nasi Moja Kwa Moja Watssapp Bofya link hapo chini 👇👇
http://.wa.me/255655562181

- Pia Waweza Jiunga na Group letu la Afya la WhatsApp Kwa Kubonyeza Link Hii hapa 👉👉👉 https://chat.whatsapp.com/C4qdsFaTDTB7tUPplBak8Q

, & Usaidie na Wengine

"VYAKULA 16 VINAVYOONGEZA KINGA YA MWILI"✒ Watu wengi tumekuwa tukijiuliza kinga ya mwili ni kitu gani na je ni nini tuf...
12/04/2025

"VYAKULA 16 VINAVYOONGEZA KINGA YA MWILI"

✒ Watu wengi tumekuwa tukijiuliza kinga ya mwili ni kitu gani na je ni nini tufanye ili kuiongeza hiyo kinga ndani ya miili yetu. Suala la kuimarisha na kuiongeza kinga ya mwili linapaswa kuwa ni jambo endelevu la kila siku.

✒ Hakuna dawa au chakula cha kula siku moja na kuponya tatizo la kushuka kinga ya mwili milele. Kinga ya mwili huongezeka ama kupungua kila siku kutegemea na umekula nini, umekunywa nini au hali ya ubongo wako kwa ujumla ipoje kwa siku hiyo, mathalani k**a umeshinda una hasira hasira tu kutwa nzima lazima na kinga yako itapungua.

✒ Mwili ulibuniwa na Mungu uweze kujitibu wenyewe bila kuhitaji DAWA YOYOTE. Ulivyo ni vile unavyokula na kunywa. Shida ni kuwa watu wengi hatujuwi tule nini kwa ajili ya nini, mara nyingi tunakula ili tushibe.

✒ Fanya chakula kiwe ndiyo dawa zako na dawa zako ziwe ni chakula unachokula. Kinga yako inapokuwa na nguvu na ya kutosha huwezi kuugua ugonjwa wowote kirahisirahisi.

Vifuatavyo ni vyakula na mitishamba 16 inayoweza kukusaidia kuongeza kinga ya Mwili wako

👉 Vyakula vinavyoongeza Kinga ya mwili"

1. MTINDI (yoghurt).

✒ Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na matakwa yako, yogati pengine ndio chakula kinachoongoza kwa kuogeza kinga ya mwili wako

👉 2. MATUNDA.

✒ Yanapatikana sehemu yoyote duniani kwa bei unazozimudu, katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, mtu asiyekula matunda ana hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda.

✒ Unaweza kuamua pia moja ya mlo wako katika siku k**a ni wa jioni au wa mchana au wa asubuhi uwe ni matunda tu na si kitu kingine zaidi. Jaza kwenye sahani yako ndizi, embe, papai, nanasi, tikiti maji, parachichi nk, sahani iwe na matunda tu kula hadi ushibe matunda tu.

👉 3. Tui la N**i:

✒ N**i ikiliwa na binadamu hugeuza aina hizo za mafuta kuwa tindikali ambayo kitaalamu huitwa ‘medium chain fatty acids’ au kwa kifupi (MCFA’s) ambazo huwa na uwezo wa kuiimarisha kinga ya mwili na hivyo kuupa mwili uwezo wa kuyashinda maradhi mbalimbali".

✒ Matumizi ya n**i k**a tiba ya kuimarisha kinga ya mwili duniani yalishika kasi mwaka 1990 mara baada ya mtafiti wa tiba kutoka Iceland, Bw. Halldor Thormar, kubaini maajabu ya tiba hii. Waathirika wa UKIMWI toka sehemu mbalimbali duniani waliotumia n**i walitoa ushuhuda wao wa namna walivyopata nafuu mara baada ya kutumia n**i k**a tiba.

✒ Dozi yake ni rahisi, kunywaji glasi nne za tui la n**i kila siku kwa muda wa kati ya miezi mitatu hadi minne, huweza kuondoa maradhi yote yanayosababishwa na kupungua kwa kinga ya mwili na pia hung’arisha ngozi na kuifanya kuwa nyororo.

✒ Kula n**i kwa wingi kadiri uwezavyo, k**a kinga yako imepunguwa basi anza kunywa tui la n**i glasi nne kwa siku na utaona maajabu ndani ya miezi mitatu tu. K**a tayari una vidonda visivyopona basi paka mafuta ya n**i kila utokapo kuoga, na matokeo utayaona bayana.

👉 4. VITUNGUU SWAUMU".

✒ Hupatikana kwa wingi Tanzania! Japokuwa vitunguu swaumu vimekuwa vikitumika sana kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali toka enzi za mababu, wataalamu wameshauri pia vitunguu hivi ni chanzo muhimu kwa kinga ya binadamu. Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.

✒ Chukuwa kitunguu swaumu kimoja, Kigawanyishe katika punje punje, chukua punje 6 hivi, Menya punje moja baada ya nyingine. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu, Meza k**a unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala au fanya kutwa mara 2.

👉 5. Mlonge:

✒ Mlonge au Moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana k**a mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean. Mti huu umeripotiwa kutibu zaidi ya magonjwa 300 ikiwemo magonjwa mbalimbali sugu.

✒ Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika k**a dawa. Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa k**a mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.

✒ Mbegu za mlonge zimekuwa dili kubwa duniani kwa sasa, zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Marekani na China na kwa mjibu wa taarifa ni kuwa zinauzwa mpaka shilingi 45000 ya Tanzania kwa gramu 500. Walikuja pia wachina kuzinunua kwa wingi na walipokuwepo hapa Tanzania bei ya mbegu za mlonge ilifika mpaka 11000 kwa kg kwa bei ya jumla yaani kwa anayechukua kg 100 au 500 au 1000 na kwenda juu.

✒ Taarifa zisizo rasmi zinadai Wachina hawa walikimbia nchini baada ya serikali kuanza kufuatilia na kuwak**ata wakwepaji kodi bandarini. Isingekuwa hivi mpaka leo mlonge ungekuwa umeshatoweka wote Tanzania.

✒ Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani. Kile ulikuwa hujuwi ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajili ya binadamu na wanyama.

👉 MLONGE UNA:

*Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe
*Potasiamu mara 15 zaidi ya ile ya kwenye ndizi
*Una vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti
*Una protini nyingi mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi (Yogurt)
*Una Klorofili (kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea) mara 4 zaidi ya ile ya kwenye nyasi au majani ya ngano (wheatgrass)
*Una madini chuma (iron) mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach
*Una vitamini A mpaka Z,
*Una Omega 3, 6, na 9
*Una asidi amino zile mhimu zaidi zinazohitajika na mwili
*Una kiasi cha kutosha cha madini ya Zinc ambayo ni madini mhimu katika kuongeza homoni za kiume na nguvu za kiume kwa ujumla

👉 MLONGE NDICHO CHAKULA CHENYE AFYA ZAIDI KULIKO CHAKULA KINGINE CHOCHOTE JUU YA ARDHI;

👉 6. Asali yenye Mdalasini

✒ Asali ni dawa kwa kila ugonjwa, zingatia tu unapata asali mbichi na nzuri ya asili kwani endapo utauziwa asali iliyochakachuliwa kuna hatari ya kuharibu afya yako zaidi. Katika kila lita moja ya asali ongeza vijiko vikubwa vya chakula 8 vya unga wa mdalasini na uchanganye vizuri kisha lamba kijiko kimoja cha chakula cha mchanganyiko huo kila siku kutwa mara tatu kwa mwezi mmoja hivi kinga yako ya mwili itarudi katika hali yake nzuri.

👉 7. UYOGA:

✒ Usishangae! Ndio.. hiki ni moja ya vyakula muhimu zaidi kuimarisha afya yako kwani huchangia kiasi kikubwa kuimarisha seli nyeupe za damu zinazofanya kazi ya kupambana na magonjwa mbalimbali!

👉 8. SUPU YA KUKU:

✒ Wengi watahisi ni gharama lakini si kubwa kuzidi gharama ya kumuona daktari! Unywaji wa supu ya kuku ya moto husaidia kuzuia kupungua kwa seli nyeupe za damu vilevile hupunguza uwezekano wa kupata matatizo yanayohusiana na mapafu na mfumo wa hewa kiujumla!

✒ Mhimu ni kuwa supu hii ya kuku hakikisha ni ya kuku wa kienyeji tu.

👉 8. Mafuta ya habbat soda

✒ Unaweza kutumia mafuta ya habbat soda kuimarisha kinga yako ya mwili kwa ujumla na hivyo kuongeza ulinzi wa mwili wako dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo dhidi ya bakteria na virusi. Mafuta ya habbat soda ndiyo bidhaa pekee ya asili iwezayo kuimarisha kinga yako ya mwili kwa muda mfupi.

✒ Ukiacha hili la kuongeza kinga ya mwili, Habbat soda ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo.

👉 9. Ubuyu:

✒ Pata kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku (kumbuka uwe ubuyu halisi). Ubuyu una vitamini C nyingi zaidi kuliko ile ipatikanayo kwenye machungwa au maembe.

✒ Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa.

1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
4. Ina virutubisho vya kulinda mwili
5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.
6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
7. Huongeza nuru ya macho
8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

✒ Unywe kiasi gani? Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.

✒ Ili upate faida za juisi ya ubuyu, zinazoelezwa hapa, lazima upate ule ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.

👉 11.VIAZI VITAMU(mbatata):

✒ Unaweza kuhisi ngozi sio sehemu ya muhimu katika kinga ya binadamu lakini ukweli ni kwamba ngozi ni sehemu ya muhimu sana kwa mwili wa binadamu. Kwa kinga kamili ya mwili wa binadamu tunahitaji Vitamin A ambayo hupatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu

👉 12. KAROTI:

✒ Karoti zina ziada kubwa ya vitamin pengine kuliko tunda lolote lile hivyo jitahidi kujumuisha karoti k**a kiungo kwenye chakula au unaweza kuitafuna ikiwa mbichi!

👉 13. SAMAKI:

✒ Husaidia seli nyeupe kuzalisha ctokins zinatohusika kuzuia baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na virusi hasa yale yanayohusiana na mfumo wa hewa nk.

👉 14. MATIKITI:

✒ Wengi Hudharau lakini tunda hili ni muhimu sana katika afya ya kila siku ya binadamu kwani husaidia kuongeza kiasi cha maji mwilin, madini chuma na kuimarisha seli nyeupe za damu.

✒ Tunda linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.

👉 Faida 13 za tikiti maji kiafya

• Asilimia 92 yake ni maji
• Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
• Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili,
• Huponya majeraha,
• Hukinga uharibifu wa seli
• Huboresha afya ya meno na fizi
• Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema
• Hubadilisha protin kuwa nishati
• Chanzo cha madini ya potasiamu
• Husaidia kushusha na kuponya shinikizo la damu
• Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
• Huondoa sumu mwilini
• Huongeza nguvu za kiume hasa ukila pamoja na mbegu zake

👉 15. MAJI YA KUNYWA:

✒ K**a kuna Kitu cha kwanza kwa uhai wa binadamu basi ni maji. Bila kunwya maji ya kutosha bado utakuwa katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali. Angalau glasi 8 hadi 10 za maji kwa siku ni muhimu kwa afya yako!.

✒ Kila mtu ana kiasi cha maji anachohitaji kunywa kila siku kwa mjibu wa uzito wake.

👉 16. Mbegu za Maboga:

✒ Mbegu za maboga pia zina kiasi kingi cha madini ya Zinki (Zinc). Madini haya yana faida lukuki mwilini, ikiwa ni pamoja na kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha ukuaji na uundaji wa chembechembe hai za mwili, kuboresha usingizi, kuboresha ladha mdomoni na harufu, huboresha afya ya macho na ngozi, hurekebisha sukari na huboresha nguvu za kiume pia.

✒ Upungufu wa madini ya Zinc mwilini una uhusiano mkubwa sana na matatizo ya kuzaa watoto njiti, kuota chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo darasani kimasomo na matatizo mengine mengi ya kimwili na kiakili.

👉 Namna nzuri ya kula mbegu za maboga:

✒ Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo k**a dakika 15 hivi na huwa n**ichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.

✒ Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa k**a nusu kikombe cha chai hivi kwa siku.

✒ Vitu vinavyoharibu na kushusha kinga ya mwili

1. Msongo wa mawazo (stress)
2. Vilevi vyote
3. Lishe duni (chakula kichache)
4. Kutokufanya mazoezi ya viungo
5. Kutumia dawa za kupunguza maumivu kila mara bila ushauri wa kitaalamu.

🔅Mawasiliano :☎️ 0655562181 au 0769600821

Ku chart Nasi Moja Kwa Moja WhatsApp Bonyeza Hapa 👉🏿 https://wa.me/255655562181

"Ili Kuwa Karibu Nasi Saa 24 ( 24hrs ) Kwa Msaada na Ushauri Wa Magonjwa Mbali Mbali , Jiunge na Group Letu la Whatsaapp .. Bonyeza Link hii hapa >>>>> https://chat.whatsapp.com/KCYfdXeCyVI1fVufcFbaVf

SHARE post hii kwa ajili ya wengine

--""MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOKUWA NA MIAKA 40 AU ZAIDI ""--       +255655562181 / +2557696008211 A. Mambo mawili ya kupi...
06/04/2025

--""MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOKUWA NA MIAKA 40 AU ZAIDI ""--

+255655562181 / +2557696008211

A. Mambo mawili ya kupima mara kwa mara:

(1) Msukumo wa damu(presha)
(2) Sukari kwenye damu

B. Mambo sita ya kupunguza kabisa kwenye chakula chako:

(1) Chumvi
(2) Sukari
(3) Vyakula vya makopo na vilivyokaa muda mrefu
(4) Nyama nyekundu kipekee ya kuchoma
(5) Bidhaa za maziwa
(6) Vyakula vyenye wanga

C. Vitu vinne vya kuongeza kwenye vyakula:

(1) Mbogamboga
(2) Maharage
(3) Matunda
(4) Karanga, korosho, macadamia, almond(nuts)

D. Mambo matatu unayotakiwa kuyasahau:

(1) Umri wako
(2) Yaliyopita
(3) Majonzi yako

E. Mambo manne ya lazima kuwa nayo, bila kujali hali yako:

(1) Marafiki wanaokupenda kweli
(2) Familia inayokujali
(3) Mawazo chanya
(4) Nyumba yenye furaha.

F. Mambo manne ya kufanya ili kuwa na afya njema:

(1) Kufunga
(2) Kutabasamu na kucheka
(3) Kutembea/mazoezi ya mwili
(4) Kupunguza uzito

G. Mambo sita ya kutofanya:

(1) Usisubiri hadi upate njaa ili ule.
(2) Usisubiri upate kiu ndio unywe maji
(3) Usisubiri upate usingizi ndio ulale.
(4) Usisubiri uchoke kabisa ndipo ulale
(5) Usisubiri uugue ndipo uende hospitalini kupima afya yako la sivyo utajutia baadae
(6) Usisubiri uwe na tatizo ndipo umwombe Mungu akusaidie

JIJALI

Utaweza kutimiza ndoto zako ukizingatia hizi dondoo na kuwaona watoto wa watoto wako.

Asante kwa kusoma na kushea 🙏🏿🙏🏿🙏🏿

☆Unaposhea kontenti k**a hii unawezesha watu wengi zaidi kipekee marafiki zako kufahamu jinsi ya kuwa na afya njema na maisha bora zaidi.

Jali Afya Yako +255655562181 / +255769600821

🕳 Kwa msaada zaidi :- Tafadhali Usisite Kuwasiliana Nasi Kuhusu Tiba Kwa Njia za Kisasa Kabisa na Ushauri wa Masuala Mbali Mbali Ya Afya.

𝐊𝐀𝐑𝐈𝐁𝐔 𝐍𝐈𝐊𝐔𝐒A𝐃𝐈𝐄 𝐏𝐈𝐆𝐀 & 𝐖𝐇𝐀𝐓𝐒𝐀𝐏𝐏

Call➖text&sms➖whatsapp👇

➖ Ili Kupata Ushauri Bure na Msaada Zaidi Kuhusu Matatizo Mbali Mbali Kiafya - Mawasiliano - +255655562181 au +255769600821

➖ Jiunge na Group letu la Afya la WhatsApp Kwa Kubonyeza Link Hii hapa 👉👉👉

WhatsApp Group Invite

UKIWA NA DALILI HIZI USISEME UNA VIDONDA VYA TUMBO~ +255655562181 , +255769600821 ~• Kupatwa na kiungulia mara kwa mara ...
04/04/2025

UKIWA NA DALILI HIZI USISEME UNA VIDONDA VYA TUMBO

~ +255655562181 , +255769600821 ~

• Kupatwa na kiungulia mara kwa mara ambapo huambatana na koo la chakula kuwaka moto pia maumivu ya kifua na hali hii huzidi zaidi pale mtu anapolala kichwa kimeinama au kulalia tumbo.

• Kiungulia hiki huanza baada ya lisaa limoja na kuisha baada ya masaa mawili baada ya kula.

• Pia dalili za tatizo hili kwa watoto hujionesha pale mtoto anapotapika kupita kiasi au kupaliwa mara kwa mara wakati wa kula chakula ,Kikohozi kisichopona au kupaliwa na kukosa pumzi akiwa usingizini.

•Dalili zingine ni k**a;

• Tumbo kuunguruma na Kukosa hamu ya kula chakula na kuhisi kichefuchefu.
• Kutokwa na makohozi kooni mara kwa marq.
• Kutoa mabaki ya chakula wakati was kupiga mswaki.
• Mdomo kunuka kutokana na kurudi juu kwa chakula cha tumboni chenye tindikali.
• Kupata hali ya kuunguza kwenye koo , kifua na karibu na moyo, hali inayotokea Muda Mfupi baada tu ya kula na kupata shida wakati wa kumeza chakula.
• Kucheuwa Maji Maji Yenye Tindikali Ukiwa Usingizini Hasa Baada Ya Kulala Muda Mfupi Baada Ya Kula.
• Kukohoa au kupaliwa mara kwa mara ikiambatana na kuweweseka Kwa Kukosa Pumzi.
• Mdomo kuwa mchachu muda mwingi hasa baada ya kutoka usingizini.
• Kupata usingizi kwa shida kutokana na maumivu ya tumbo na Koo.
• Kuvimba Kwa Tezi za Shingoni K**a Vile Tonses na Goita.
• Mdomo na koo kukauka.
• Meno kupoteza uimara na kuanza kumomonyoka kutokana na uwepo wa tindikali.
• Tumbo kujaa Gesi , Kupata Choo K**a Tope Kunakoambatana kujamba sana.
• Tumbo Kuunguruma Hasa Muda Mfupi Baaada Ya Kula.

• Hii inaitwa ACID REFLUX au GERD
( *GastroEsophagaelRefluxDesease* na siyo vidonda vya tumbo k**a wengi wanavyodhani , Kwa sababu Ugonjwa huu unafanana sana na Vidonda vya Tumbo.
• Watu wengi wanao jitambulisha kuwa wana Vidonda vya tumbo baada ya vipimo vya Kumulika tumboni kufanyika na Kuonyrsha “Kuta ni Nyekundu. Lakini pia huonyesha Gesi imejaa tumboni”. Kitalamu wanaangukia kwenye GERD na Gastritis na Siyo Vidonda vya Tumbo.
:
ENDOSCOPY - Vipimo vya Kuingiziwa Kumulika ndani haviwezi kukwambia CHANZO CHA TATIZO halisi cha Tatizo na ndiyo maana wagonjwa wengi wamekuwa wakijitafsiri wana Madonda ya tumbo kwa sababu wameanzishiwa dawa za Kutibu dalili (Gesi na Kiungulia) bila Kuchunguzwa chanzo.

• Kibaya zaidi Watalamu wengi wamekuwa wakikimbilia kutibu H Pylori na kusahau kuna vyanzo Vingi Vinavyo sababisha Mtu kuwa na GERD na Gastritis.

• Katika mfumo wa chakula kuna bakteria rafiki ambao husaidia kumeng’enya chakula vizuri. Maisha ya Pombe, sigara, Vyakula vya kukaanga, Soda Na juisi Huathiri hawa bakteria na Kusababisha vimelea maadui kuota katika kuta na kushambulia ukuta wa Mfumo wa chakula. Kitalamu husababisha SIBO (Small Intestine Bakteria and Yeast Overgrowth) Hali hio Huvimbisha Mfumo wa chakula Gut Inflammation na Unaweza Kuibua mzio sugu, Kukosa usingizi, Mvurugiko wa homoni kwa sababu ya Kudhoofika kwa Mfumo wa Chakula.

“Uhai na Kifo vipo katika Mfumo wa Chakula”

•.Vyakula Vya Sukari na wanga kwa mtu k**a uwezo wa mwili Kutumia wanga huo ni Mdogo. Husababisha wanga kukaa tumboni muda mrefu badala ya kuwa Dighested kwa wakati na kusababisha kuchachuka haraka na Kuongeza makali ya gesi na kiungulia.

• Hivyo katika matibabu Mgonjwa huwa tunampampatia Suluhisho kwa Kuondoa changamoto ziluzopo jwa kusafisha mfumo wake wote na kuufanyia repair ili kurudisha hali yake ya asili ndani ya muda mfupi Sana.

♐Tatizo la Acid / Tindikali Ya Tumbo Linatibika na Kupona Kabisa.

🕳 Kwa msaada zaidi :- Tafadhali Usisite Kuwasiliana Nasi Kuhusu Tiba Kwa Njia za Kisasa Kabisa na Ushauri wa Masuala Mbali Mbali Ya Afya.

𝐊𝐀𝐑𝐈𝐁𝐔 𝐍𝐈𝐊𝐔𝐒A𝐃𝐈𝐄 𝐏𝐈𝐆𝐀 & 𝐖𝐇𝐀𝐓𝐒𝐀𝐏𝐏

Call➖text&sms➖whatsapp👇

➖ Ili Kupata Ushauri Bure na Msaada Zaidi Kuhusu Matatizo Mbali Mbali Kiafya - Mawasiliano - +255655562181 au +255769600821

➖ Jiunge na Group letu la Afya la WhatsApp Kwa Kubonyeza Link Hii hapa 👉👉👉 https://chat.whatsapp.com/C4qdsFaTDTB7tUPplBak8Q

➖ SHARE kwenye MA GROUP NA WATU MBALI MBALI UWASAIDIE WENGI WANAO TESEKA 🙏🙏🙏 kisha tuandikie maoni yako au ushauri hapo chini

𝐊𝐀𝐑𝐈𝐁𝐔 𝐀𝐒𝐀𝐍𝐓𝐄.

TAFADHALI : USISAHAU KU SHARE.

*JINSI YA KUONDOA KITAMBI AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE*  +255655562181 / +255769600821- Wanawake wengi miaka...
15/01/2024

*JINSI YA KUONDOA KITAMBI AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE*

+255655562181 / +255769600821

- Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa.

- Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana k**a ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi.

- Karibu , tumekuandalia darasa la siku tatu BURE la kuondoa kitambi bila kutumia dawa wala mazoezi kwa Wanawake - GUSA HAPA ILI KUINGIA DARASANI SASA HIVI 👇👇👇👇👇👇 👉👉👉👉 https://chat.whatsapp.com/C4qdsFaTDTB7tUPplBak8Q

*MFUMO WA UMENG’ENYAJI CHAKULA*   +255655562181 / +255769600821- Mfumo wako wa umeng’enyaji chakula umeundwa na njia ya ...
10/01/2024

*MFUMO WA UMENG’ENYAJI CHAKULA*

+255655562181 / +255769600821

- Mfumo wako wa umeng’enyaji chakula umeundwa na njia ya utumbo (gastrointestinal. GI) , ini, kongosho na kibofu cha nyongo. Njia ya GI ni safu ya viungo vya mashimo ambavyo vimeunganishwa kutoka mdomoni hadi kwenye tundu ya nyuma. Viungo vinavyounda njia yako ya GI, kwa utaratibu wa kuwa vimeunganishwa, ni pamoja na mdomo wako, umio, tumbo, utumbo mdogo, utumbo mkubwa na tundu ya nyuma.

*JINSI MFUMO WA UMENG’ENYAJI CHAKULA HUFANYA.*

- Mfumo wako wa usagaji chakula umeundwa kwa namna ya kipekee kufanya kazi yake ya kugeuza chakula chako kuwa virutubisho na nishati unayohitaji ili kuwa na afya njema.

Usagaji chakula ni muhimu kwa sababu mwili wako unahitaji virutubisho kutoka katika chakula unachokula na vinywaji unavyokunywa ili kuwa na afya nzuri. Virutubisho ni pamoja na wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji.
Mfumo wako wa usagaji chakula husaga na kufyonza virutubisho kutoka katika chakula na vimiminika unavyotumia ili kutumika k**a vile nishati, ukuaji na ukarabati wa seli.

*MAGONJWA YANAYOWEZA KUTOKANA NA MFUMO WA MMENG'ENYOWA CHAKULA*

- Kutokana mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kuwa chanzo kikuu cha mahitaji ya mwili inapelekea mfumo huu unapopata shida magonjwa mengi kuibuka bila mfumo huu kuhusishwa kwamba ndiyo chanzo cha moja kwa moja kutokana na baadhi ya mifumo kujitenga lakini kuwa na uhusiano wa kimahitaji na kiutendaji kazi kwa namna moja au nyingine.

- Mfano - Uwepo wa sumu nyingi mwilini unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mfumo huu , lakini madhara yanaweza kuhusisha uzazi upende wa homoni , mzunguko wa damu ,moyo na fahamu, magonjwa ya ngozi ikiwemo saratani, mabadiliko ya mfumo wa Kinga mwili na mengineyo mengi.

*Miongoni mwa magonjwa mengine ni pamoja na*:-

~Kansa ya Utumbo.
~Uzito uliozidi na kitambi.
~Bawasiri i(*Vinyama sehemu ya haja kubwa*).
~Maumivu ya Kiuno ,Nyongq, Magoti,, Mgongo , Mabega , Kichwa , Misuli.n.k.
~Kukosa usingizi(*Insomnia*)
~Kukosa hamu ya kula (*Loss of appetite*).
~Tumbo kujaa gesi.
~Vidonda vya tumbo (*Ulcers*).
~Upungufu wa nguvu za kiume.
~Kushindwa kubeba mimba au kuzaa ( *Ugumba* ).
~Kupasuka kwa utumbo.
~Ileocecal valve incompetence.
~Kutoa harufu mbaya mdomoni na unapojamba.
~ Msongamano wa Hewa Kwenye Mapafu ( *Kubanwa Mbavu na Kukosa Pumzi*).
~ Maumivu ya tumbo Mara kwa Mara.
~ Muwasho Njia ya Haja Kubwa .
~ Maumivu ya Koromeo ( *Kuhisi Kitu Kinapanda Kooni na Kushuka* ).
~ Kiungulia (*ACID REFLUX*).
~ Magonjwa ya Ngozi.
~ Ngiri (*HERNIA*).
~ Kiharusi
~ Pressure.
~ Hormone imbalances
~ Kisukari. Magonjwa ya figo.
• Na Mengine Mengi Sana.

- 𝗞𝗪𝗔 𝗧𝗜𝗕𝗔 𝗡𝗔 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗭𝗔𝗜𝗗𝗜-
- Tembelea Ofisi Zetu Zilizopo Kijitonyama Dar es salaam jirani na Stand ya Makumbusho na Mlimani City au Tupigie Sasa Kupitia ☎️ +255769600821 au +255655562181

Kuchart Nasi Moja Kwa Moja Watssapp Bofya link hapo chini 👇👇
http://.wa.me/255655562181

➖ *Ili Kufahamu Mengi Kwa Undani Zaidi BOFYA HAPA.* 👉 👇👇 https://chat.whatsapp.com/C4qdsFaTDTB7tUPplBak8Q

➖ *SHARE kwenye MA GROUP NA WATU MBALI MBALI UWASAIDIE WENGI WANAO TESEKA* 🙏🙏🙏 *Kisha tuandikie maoni yako au ushauri hapo chini*

🕳 *UCHAFU UNAOTOKA UKENI NA MAANA ZAKE* 🕳 +255655562181  /  +255769600821    *Chanzo.*~Kitaalamu Hali ya mwanamke kutokw...
02/01/2024

🕳 *UCHAFU UNAOTOKA UKENI NA MAANA ZAKE* 🕳

+255655562181 / +255769600821

*Chanzo.*

~Kitaalamu Hali ya mwanamke kutokwa na maji yenye rangi nyeupe au njano ni Hali ya kawaida na sio tatizo Lakini endapo maji yanatoka yapo katika Hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali au kuwasha hapo una tatizo.

~Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha au kutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nnje ya mwili pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maaambukizi ya bacteria.

~Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa hayawashi na huwa na rangi nyeupe au njano pia huwa na asidi ya LACTIN ambayo huzuia bacteria kuzaliana.

~Mwanamke hutoa kiasi cha grams 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye mji wa kizazi na grams 3 za ute mwepesi kila siku, kiwango hicho kinaweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi pia Kuna wakati ute huwa mwepesi na unaovutika na Kuna wakati pia huwa mzito wa rangi ya njano hautoi harufu.

*VISABABISHI VYA TATIZO HILI.*

- Sababu za kutokwa na uchafu ukeni una vyanzo vingi sana vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo hili.

1. *BACTERIA VAGINOSIS.*

Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijafanikiwa kuwa wazi,kinachotokea ni kuongezeka kwa ghafla kwa idadi ya ya bacteria hawa na kubadilisha uwiano wa kawaida katika mazingira ya uke, wanawake wenye wapenzi wengi na wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo Wana hatari ya kupata tatizo hili.

2. *TRICHOMONAS.*

Maambukizi haya hutokana na Aina ya protozoa wa seli moja, trichomonas mara nyingi huambukizwa kwa njia ya ngono, protozoa huyo huweza kukaa kwenye unyevu unyevu kwa Muda wa saa 24 Bila kufa hivyo kufanya taulo na chupi zisizokauka kuwa chanzo kingine cha tatizo hili.

3. *YEAST INFECTION.*

- Kwa kawaida Kuna kiwango kidogo cha yeast (candida albicans) katika uke, huwa tunasema Kuna maambukizi pale kiwango kinapozidi Hali ambayo inatokana na kubadilika kwa Hali ya hewa ukeni (Change in the PH balance of va**na).

*Maambukizi ya yeast hayatokani na tendo la ndoa.*

*Mambo ambayo huchangia tatizo hili ni:-*

(a) *MATUMIZI YA DAWA ZA KUZUIA MIMBA*
(b) *MAWAZO*
(c) *UJAUZITO*
(d) *KISUKARI*
(d) *MATUMIZI YA ANTIBIOTICS*

4. *VAGINAL OR CERVICAL CANCER.*

- Mtu anapokua na kansa ya uke, hutokwa na maji ya harufu mbaya, hivyo ni heri uwe unafanya check up ili kujua Afya yako na Kwa kuwa cancer ya kizazi inapona hivyo ni vema ukatambua mapema uanze tiba.

5. *S*XUAL TRANSMITTED DESEAS (STDs).*

- Kuna baadhi ya magonjwa k**a vile KASWENDE NA KISONONO yanasababishwa na ngono na kuwa chanzo cha tatizo hili.

6. *POOR HYGIENE.*

- Tatizo la kutokwa na maji wakati mwingine husababishwa na muhusika kua mchafu yan mtu unaoga kwa siku mara moja, chupi moja ndio hiyo hiyo mwaka mzima, pads unakaa nayo saa 24, ukienda kukojoa ujitawadhi na maji masafi hivyo unategemea utakua salama kweli??? Zingatia usafi mrembo.

*DALILI ZA TATIZO HILI.*

- Kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na kuwashwa au kutokewa na vipele, hii hutokana na kuharibika kwa uwiano wa bacteria hivyo kuwa na madhara na uchafu hutoka wa aina tofauti hapa chini nitaelezea kila Aina ya uchafu na dalili zake.

1. *UCHAFU WENYE RANGI YA KAHAWIA AU DAMU.*

- Huu uchafu huonyesha dalili ya kuwa mzunguko wako wa hedhi umevulugika na wakati mwingine ni dalili ya kansa ya kizazi, mwanamke anayepata tatizo hili hutoa damu nyingi kuumwa sana nyonga.

2. *UCHAFU WENYE RANGI YA NJANO /KIJANI WENYE HARUFU MBAYA.*

- Endapo uchafu huo utatoka k**a povu na wenye rangi ya kijani au njano na ukiambatana na harufu mbaya huwa ni dalili ya ugonjwa wa trichomonas, maambukizi ya parasite yanatokana na ngono zembe, dalili Yake nyingine ni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo.

3. *UCHAFU MWEUPE MZITO K**A JIBINI.*

Mara nyingi hii huwa ni dalili ya maambukizi ya fangasi(YEAST INFECTION) na dalili nyingine huwa ni kuvimba sehemu ya nje ya siri, kuwashwa na kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.

4. *UCHAFU MWEUPE/KIJIVU WENYE HARUFU YA SAMAKI.*

-Uchafu wa Aina hii ni dalili ya maambukizi ya bacteria vaginosis, mara nyingi mwenye tatizo hili husikia muwasho na maumivu sehem ya nnje ya uke.

5. *MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUEPUKA TATIZO HILI NA TIBA YAKE*.

- Matibabu ya tatizo hili hufanyika baada ya kugundua chanzo cha tatizo na mara nyingi tiba Yake ni tiba ya dawa za antibiotics kitu ambacho si tiba nzuri zaidi kwa sababu tatizo huweza kujirudia kila wakati na kusababisha matatizo zaidi hivyo tiba nzuri ni kuepuka hili tatizo kwa kufanya yafuatayo:-

👉 *EPUKA KUJIINGIZA VIDOLE MARA KWA MARA UKENI*
👉 *EPUKA MATUMIZI YA DAWA ZA ANTIBIOTICS MARA KWA MARA*
👉 *PUNGUZA KULA VYAKULA VYENYE SUKARI NYINGI*
👉 *TUMIA PADS ZENYE ANIONS NI SALAMA KWA AFYA YAKO*
👉 *SAFISHA VIZURI NGUO ZAKO ZA NDANI NA UZIANIKE JUANI NA HATA KUZIPIGA PASI*
👉 *KUNYWA MAZIWA MTINDI ,JUICE YA APPLE,STRAWBERRY, NANASI KWA WINGI*
👉 *EPUKA KUFANYA NGONO ZEMBE*
👉 *HAKIKISHA UNAJISAFISHA KILA UNAPOMALIZA KUJISAIDIA KWA KUANZIA MBELE KISHA NYUMA*
👉 *EPUKA KUTUMIA DAWA ZA KUZUIA MIMBA*
👉 *EPUKA KUTUMIA SABUNI AU VITU VYA MANUKATO UKENI*
👉 *EPUKA KUINGIZA VITU HOVYO UKENI KWA KISUNGIZIO CHOCHOTE , K**A KUONGEZA LADHA AU UKAVU*
👉 *EPUKA KUWEKEWA MATE WAKATI WA TENDO AU NGONO YA UKE KWA MDOMO* / *ORAL S*X*

*NOTED* : Wanawake wengi mnapenda kutumia baadhi ya dawa kwa lengo la kuongeza vionjo kwenye mapenzi pia kufanya uke kunukia vizuri, au kukaza uke rafiki uke una harufu nzuri sana ambayo haipatkan kokote hivyo haihitaji kuwekwa pafyumu Wala kusafishwa kwa sabuni za kemikali kwani huwa panajisafisha hivyo ni heri ukaacha kutumia kwani madhara Yake hayaonekani sasa ila baada ya Muda huonekana.

- 𝗞𝗪𝗔 𝗧𝗜𝗕𝗔 𝗡𝗔 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗭𝗔𝗜𝗗𝗜-
- Tembelea Ofisi Zetu Zilizopo Kijitonyama Dar es salaam jirani na Stand ya Makumbusho na Mlimani City au Tupigie Sasa Kupitia ☎️ +255769600821 au +255655562181

Kuchart Nasi Moja Kwa Moja Watssapp Bofya link hapo chini 👇👇
http://.wa.me/255655562181

➖ *Ili Kufahamu Mengi Kwa Undani Zaidi BOFYA HAPA.* 👉 👇👇 https://chat.whatsapp.com/C4qdsFaTDTB7tUPplBak8Q

➖ *SHARE kwenye MA GROUP NA WATU MBALI MBALI UWASAIDIE WENGI WANAO TESEKA* 🙏🙏🙏 *Kisha tuandikie maoni yako au ushauri hapo chini*

Address

Ilala Boma
Ilala

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Magonjwa ya Wanawake posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Magonjwa ya Wanawake:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram