18/11/2025
Mwenyekiti kamati ya wazazi Shule ya Msingi Unubini, Temeke, Albinus Masalu akitoa ahadi ya kuendelea kuhamasisha wazazi na walezi kuchangia huduma ya chakula wanachopewa watoto shuleni mara baada ya kupewa semina elekezi kuhusu umuhimu wa lishe iliyotolewa kwa wazazi na walezi wa shule hiyo.
Semina hiyo imetolewa na wataalamu kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) pamoja na Manispaa ya Temeke kupitia mradi wa Afya na Lishe unaotekelezwa katika shule za msingi 15 za Manispaa ya Temeke kupitia uwezeshaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).