Maalim Omary Mzungu

Maalim Omary Mzungu Mganga wa tiba asili kutoka Tanzania, nikitoa suluhisho la asili kwa afya na ustawi wa jamii.

Ninalenga kuleta afya bora na maisha yenye furaha kwa wengine kwa njia ya tiba asilia na maarifa ya kitamaduni.

MAELEZO YA NYOTA YA MBUZI CAPRICORNMAWASILIANO - 0678 752 883Hii ni nyota ya kumi katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii...
18/04/2024

MAELEZO YA NYOTA YA MBUZI CAPRICORN

MAWASILIANO - 0678 752 883
Hii ni nyota ya kumi katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 Disemba na 19 Januari au wenye majina yalio anza na herufi J au V.
Asili yao ni Udongo.Siku yao ya bahati ni Jumamosi. Namba yao ya bahati ni 8.
Sayari yao ni Saturn (Zohal).
Malaika wake anaitwa Cassiel au Kafyaeel, na Jini anayetawala Jumamosi anaitwa, Abuu Nuhu au Aratron.Herufi ya Jumamosi ni Z.
Rangi zao ni Nyeusi na Bluu iliyoiva Wenye nyota hii wanashauriwa wapake rangi zifuatazo kwenye nyumba zao, rangi ya Kahawia (Brown) Rangi ya Kijivu (Grey) au Nyeusi (Black).
Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Hudhurungi (Puce) na Fedha (Silver).
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Rangi ya Samawi (Ultramarine).
Kito (Jiwe) ni Black Onyx. Madini yao ni Risasi (Lead).
Manukato yao ni yale yatokanayo na Msonobari (Pine), Maua yanayofanana na ya Jamii ya Choroko, Njegere au Dengu (Sweet pea) na Magnolia.
MAMBO MUHIMU:-
Sifa ya Nyota hii ni Uongozi.
Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye Uchangamfu na Furaha.
Maadili yao ni Uvumilivu, Utiifu, Ustaamilivu, Kuratibu, Kuandaa na Uwezo wa kuona mbali.
Matakwa yao ni Kutawala, Kusimamia na Kuongoza.
Tabia za kujiepusha nazo ni Kutokutegemea kuwa mambo mabaya yatatokea, Kuwa na masikitiko, Kutokupenda mabadiliko na Kupenda vitu na mali kupita kiasi.
USHIRIKIANE NA NANI?
★Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Ng’ombe na Mashuke.
★Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Punda, Kaa na Mizani.
★Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mizani.
★Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Punda.
★Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Ndoo.
★Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Ng’ombe.
★Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Kaa.
★Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Ng’ombe.
★Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Mashuke na Mshale.
KIPAJI CHA MBUZI:
Mbuzi wana kipaji cha kuchambua mambo kidogo kidogo au kufuatilia kitu bila watu kujua na kupata ufumbuzi wa uhakika mwishoni.Gradual
TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Mbuzi wanapenda kuwajibika, ni wenye bidii ya kazi, katika kazi yeyote watakayofanya hata k**a ikiwa ni ya kipuuzi.
Ni viumbe waaminifu sana, watu wastahamilivu na wenye kuweza kuvumilia matatizo yeyote.
Kwa upande mwingine ni watu wenye tamaa kubwa ya kimaisha na kimaendeleo, na kwa sababu ya kutekeleza malengo yao basi huwa wanakuwa wabinafsi na wenye uroho na uchu.
Watu wenye nyota hii wanakuwa ni watu wenye aibu sana kwa wapenzi wao, lakini aibu ikishawaondoka huwa ni wapenzi wa kutisha, kwa maana ya kwamba kwa vile wao ni waaminifu wanataka wapenzi wao wawaunge mkono katika hisia zao za kimapenzi.
Ni watu wanaoogopa sana kuachwa na wapenzi wao hivyo basi huwa wanakuwa waangalifu sana katika kuchagua wapenzi.
Jambo jingine ni kuwa huwa wao wenyewe hawajiamini kimapenzi, mara nyingi wanashindwa kuingia katika mapenzi kwa woga tu hivyo kukosa nafasi nzuri ya kupendwa.
Kwa ujumla ni wapenzi makini na huwa hawaoi mpaka wapate uhakika wa kutosha kutoka kwa wapenzi wao. Ni wapenzi makini, waaminifu na wanaoweza kuaminiwa. Lengo lao katika mapenzi ni usalama.
KAZI NA BIASHARA ZA MBUZI:
Mbuzi kitu muhimu katika maisha yake ni kazi na maisha mazuri na yanayoeleweka ambayo yako katika mpangilio wanaoutaka wao.
Ni watu ambao wan**ingatia sana muda wa maisha na wana mpangilio maalum kwamba katika umri fulani awe amepata nini au awe na fedha kiasi gani.
Ni wenye kupenda utekelezaji wa kazi wa hali ya juu na wao wanapoagizwa hufanya hivyo.Kazi zao zinazowafaa ni zile za kutumia akili, Uhandisi, Usanifu Majengo, Saveya, kazi za Serikali, Siasa na Daktari wa Meno.
MAVAZI NA MITINDO:
Mbuzi wanatakiwa wavae nguo za mitindo, zilizoshonwa kwa ustadi. Nguo hizo ziwe za rangi ya kijivu au Kijani iliyoiva au hudhurungi nzito.Kitambaa kiwe cha kitani (Linen) au cha ngozi.
Nguo ziwe ni suti na ziambatane na saa za mikononi.
MAGONJWA YA MBUZI:
Nyota hii inatawala Mifupa, Magoti na Ngozi.Matatizo yao makubwa ya kiafya huwa yanasababishwa na muda mrefu ambao wanafanya kazi au kujishughulisha
Hii ni kwa sababu hawamwamini mtu mwingine afanye shughuli zao ambazo zina mipangilio ya muda mrefu,nguvu nyingi, na akili hutumika.
Shughuli zao nyingi za mizunguko na kufikiria huwaletea maradhi k**a Baridi Yabisi (rheumatism).
Maradhi yao mengine makubwa ni ugonjwa wa Ngozi, matatizo ya Magoti na maradhi ya mifupa.
VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA MBUZI:
Mbuzi wanashauriwa wapende kula vyakula au matunda yafuatayo.ambayo ndio yanatawaliwa na nyota yao.Wapende sana vyakula vya N**i na Nyama yeyote. Vile vile wapendelee kula Viazi Vitamu na Samaki Gamba (Shellfish).
Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa watu wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee miji au nchi zifuatazo ambayo inatawaliwa na nyota ya Mbuzi.
Miji hiyo ni Brussels (Ubelgiji) na Oxford (Uingereza) au nchi za Mexico na India.
MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Mbuzi ni Risasi (Lead). Vito vyao vya kuvaa katika pete ni k**a vilivyoonyeshwa katika picha hapa chini.
Mafusho ya Mbuzi ni Miatun- saila. unachoma siku ya Jumamosi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.
★KWA WENYE★
matatizo ya kinyota, mahusiano, mateso ya majini wa kila aina magonjwa mbali mbali majini mahaba kusafisha Nyota mivuto ya biashara ♥Mapenzi wasiliana Nami - 0678 752 883

MAELEZO YA NYOTA YA MSHALE SAGITTARIUS.MAWASILIANO _ 0678 752 883 Hii ni nyota ya tisa katika mlolongo wa nyota 12. Nyot...
18/04/2024

MAELEZO YA NYOTA YA MSHALE SAGITTARIUS.

MAWASILIANO _ 0678 752 883
Hii ni nyota ya tisa katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Novemba na 20 Disemba au wenye majina yalio anza na herufi I na U.
Asili yao ni Moto.Siku yao ya Bahati ni Alkhamisi. Namba yao ya Bahati ni 3
Sayari yao ni Jupiter (Mushtara).
Malaika wake anaitwa Sachiel au Israfeell na Jini anayetawala alkhamisi aanaitwa Shamhuurush Kadhi wa Majini au Bethor
Herufi Ya Alkhamisi ni DH.
Rangi zao ni Bluu na Bluu iliyokolea. Wenye nyota hii wanatakiwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara rangi zenye kusisimua na uchangamfu na zinazoashiria hali ya kumkaribisha mgeni. Rangi hizo ni Nyekundu iliyochangamka (Warm Red) rangi ya Zambarau (Purple) na rangi ya hudhurungi au kahawia (Brown).
Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Njano na Njano-machungwa.
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Nyeusi na Bluu iliyoiva.
Kito (Jiwe) ni Feruzi (Turquoise) na Kito chekundu (Carbuncle).Madini yao ni Bati.
Manukato yao ni Yasmini (Jasmine), Manemane (Myrrh).
MAMBO MUHIMU:-
Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye uwezo wa Kuongoza, Kuratibu, Kuandaa, Kupanga na Kusikiliza kwa makini.
Maadili yao ni Ukweli, Kuona mbali, Ukarimu na Kuwa na uwezo wa kusikiliza mawazo ya wenzake japokuwa siyo lazima akubaliane nayo.
Matakwa yao ni Kupanuka kimawazo.
Tabia za kujiepusha nazo ni Kutegemea mambo kuwa yatakuwa mazuri siku zote, Kutia chumvi mambo na Kuzidisha Ukarimu kwa kutegemea hela za watu wengine.
USHIRIKIANE NA NANI?
★Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Punda na Simba.
★Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Mapacha, Mashuke na Samaki.
★Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mashuke.
★Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Samaki.
★Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mbuzi.
★Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Punda.
★Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Mapacha.
★Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Punda.
★Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Simba na Nge.
KIPAJI CHA MSHALE:
Mshale wana kipaji cha kutabiri na kujua mambo ambayo yatatokea mbele au muda utakaokuja, na mara nyingi wanalolisema huwa linatokea hata likiwa la kipuuzi.(Prophetic)
TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Mshale ni wenye tabia ya kuwa na matumaini ya mafanikio kwa lolote wanalolitegemea. Wanapenda kuwa na uhuru wa kupenda na kuchagua na wanapenda watu wengine wawe k**a wao.
Hawapendi mambo nusunusu.
Ni watu ambao wako wazi na wanaopenda kusoma. Ni wakweli na ukitaka kuelewana nao na wewe uwe mkweli.
Mshale ni watulivu, waaminifu na wanapenda uadilifu,.hawapendi kuamrishwa kufanya jambo kwa sababu wanaamini kwamba wao wenyewe wana uwezo mkubwa wa kutekeleza jambo lolote, lakini likiwaudhi wanakuwa wakaidi na wasioweza kutii amri.
Wenye nyota hii hawaoni taabu kusema lolote bila kujali athari zake, mradi jambo hilo liwe la kweli.
Pamoja na kwamba wenye nyota hii wanapenda wawe huru na wenye kujiamulia mambo yao wenyewe, huwa wana starehe na kuona raha wanapokuwa ndani ya uhusiano wa kimapenzi wanapenda sana kujihusisha na makundi makundi lakini huwa wanapata muda wa kuwa na wapenzi wao. Katika mapenzi ni wachangamfu na wenye kupenda lakini tabia yao ya kutojali inawafanya wapenzi wao wajione kwamba wanakosa ulinzi wa kimapenzi.
Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu. Mwanzoni wanakuwa wagumu sana kujihusisha. Wanapenda sana wakati wote kuwa na wapenzi wapya au mapenzi ya kawaida kwa sababu wanaamini mapenzi ya kudumu yanawanyima uhuru.
Wapenzi wao wanaponyesha dalili ya kuwapenda basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu ya kubanwa na kutokuwa na uhuru.
Ni watu wanaopenda kufanya ngono kwa muda mrefu na hisia zao ziko mbali, inashauriwa kwamba wapenzi wao wawe wamekula kabla ya tendo la ndoa vinginevyo itakuwa taabu.
KAZI NA BIASHARA ZA MSHALE:
Mshale ni waaminifu wanaopenda sana mafanikio, wako tayari wakati wowote katika kazi. Kutokana na hili wana bahati ya kuwa katika sehemu muafaka na katika muda unaotakiwa.
Wenye nyota hii ni wafanyakazi waaminifu na hawapendi kuwasimamia watu katika kazi. Wanawaamini wafanyakazi wao na wanapokuwa ofisini huleta mazingira ya urafiki na kuaminiana.
Kazi zinazowafaa ni za usafiri, kazi za sheria, Wakili au Hakimu, kazi za uandishi, ualimu, dini, sheikh au padri au makanisani au misikitini, michezo, kazi za kijeshi na uuzaji.
MAVAZI NA MITINDO:
Mshale wanatakiwa wavae nguo zenye kuathiri na za mzaha mzaha k**a koti au blauzi isiyo rasmi au nguo za kitamaduni zilizoongezwa ongezwa vitu vingi k**a maua au nakshi nakshi.
Rangi ya nguo zao iwe ya Zambarau au rangi ya Hudhurungi iliyochangamka au rangi ya blue.
Vitambaa viwe vya sufu. Nguo ziambatane na mikanda, na viatu viwe vya buti. Wanawake wapendelee kuvaa sketi.
MAGONJWA YA MSHALE:
Nyota hii inatawala sehemu ya chini ya kiuno. Wenye nyota hii hawapendi kuugua. Lakini huwa wanapata maradhi kutokana na kujishughulisha kupita kiasi na kutumia nguvu zao na akili zao kwa muda mrefu bila mapumziko Wanathamini sana mizunguko kuliko mapumziko.Vile vile ni watu wasiopenda ushauri kuhusiana na afya zao.
Tatizo lao lingine ni kuwa wanapenda sana kula na kunywa na hiyo huwaletea unene usiotakiwa. Wakitaka kujikomboa na matatizo wanashauriwa wawe na tabia ya kujipumzisha.
Magonjwa yanayohusiana na nyota hii ni majereha na maradhi ya nyonga, mapaja, maradhi ya ini (Liver Disorder) kupooza kwa miguu (paralysisi of limbs) na ugonjwa wa kuumwa mishipa au misuli ya nyuma ya paja.
VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA MSHALE:
Wenye nyota hii wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao. Nyama mwitu, kun**i za rangi ya bluu, maboga na juice ya mapera.
Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota zao.
Nchi hizo ni USA na SPAIN na miji ni Budapest (Romania) na Cologne (Ujerumani).
MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Mshale ni Chuma. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni k**a vilivyoonyeshwa katika picha hapa chini.
Mafusho ya Mshale ni Udi Kafur. unachoma siku ya Alkhamisi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.
MAWASILIANO - 0678 752 883

MAELEZO YA NYOTA YA NG'E SCORPIOMAWASILIANO - 0678 752 883Hii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kw...
18/04/2024

MAELEZO YA NYOTA YA NG'E SCORPIO

MAWASILIANO - 0678 752 883
Hii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Oktoba na 22 Novemba au wenye majina yaliyoanza na herufi H au T.
Siku yao ya Bahati ni Jumanne, Namba yao ya bahati ni 9.Asili yao ni Maji.
Sayari yao ni Pluto.
Malaika anayetawala nyota hii anaitwa Samael au Israeel na Jini wa siku hii anaitwa Abuu Muhriz al Hammar au Phaleg.
Herufi ya Jumanne ni S, Jina la Jumanne ni lile linaloanza na S,mfano, Shakur au Simon au Stella.
Rangi zao ni Urujuani nyekundu. Ng'e wanashauriwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi nzito yenye kutia shauku na kuvutia k**a rangi ya damu ya mzee (Maroon).
Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi ya Kijani.
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Bluu.
Kito (Jiwe) ni Bloodstone, Malachite, Topaz. Ruby,Rhodochrosite, Kunzite, Moldavite, Opal, Diamond, Selenite, Quartz.
Madini yao ni Chuma, Radiamu (Radium) na Chuma cha pua (Steel).
Manukato yao ni ya Msandali (Sandalwood), Tikiti maji (Watermelon), N**i (Coconut), Mcheri (Cherry Blossom).
MAMBO MUHIMU:-
Sifa ya Nyota hii ni Kuwa Imara.
Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni uwezo wa kuangalia na kujua mambo kwa upana zaidi.
Maadili yao ni Utiifu, Kuwa Imara, Kuazimia jambo, Ujasiri na Undani.
Matakwa yao ni Kuingilia undani wa kitu na kukibadilisha.
Tabia za kujiepusha nazo ni Wivu, Kulipiza kisasi, Kutokubali Kusamehe, kutoshawishika au kutobadilika, kuwa mbishi, mng’ang’anizi.
USHIRIKIANE NA NANI?
*Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Kaa na Samaki.
*Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Ng’ombe, Simba na Ndoo.
*Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Simba.
*Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Ndoo.
*Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mshale.
*Nyota inayomsaidia katika Ubunifu ni nyota ya Samaki.
*Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Ng’ombe.
*Nyota bora ya Kujifurahisha ni nyota ya Samaki.
*Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Kaa na Mizani.
KIPAJI CHA NG'E:
Ng'e wana kipaji na uwezo wa kiroho wa kuwasiliana na watu katika kutekeleza mambo wanayohitaji. Mystical.
TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Ng'e wana uwezo mkubwa wa muvuto au kuvutia watu katika mambo yao. Ni wenye uelewa mkubwa, majasiri katika kukabiliana na matatizo ambayo wengine yamewashinda.
Wana tabia ya kutilia mkazo mambo yao, tena kwa ukali na ikibidi kutumia ukatili ili jambo litimie wao wako tayari.
Ni wasiri na wanaopenda kufanya mambo yao kwa siri sana. K**a ilivyo alama ya nyota yao hawaogopi kiza. Wana uwezo na kipaji cha asili cha kutekeleza mambo yao na wakafanikiwa.
Ni wenye akili nyingi, waerevu na wepesi sana kuelewa mambo.
Ng'e vile vile wanaweza kujidhuru wao wenyewe. Mambo yanapowawia magumu.
Wanapenda sana kutumia fursa ya kufanya mapenzi k**a njia mojawapo ya kuonyesha ujasiri wao katika mapenzi na namna wanavyojua kufanya tendo la ndoa.
Kwao mapenzi au tendo la ndoa ni kiungo muhimu sana katika maisha yao hasa ikizingatiwa kwamba nyota ya Ng'e inatawala sehemu za siri.
Inashauriwa wale wenye moyo mdogo wasifanye mapenzi na Ng'e sivyo watajuta. Kitu kingine ni kwamba ni watu ambao hawayumbi na hawakubali kushindwa upesi.
Ni watu wenye ashki na hasira wakiwa wamedhalilishwa au wameumizwa na wapenzi wao na wanapofanya tendo la ndoa hasira zao huisha mara moja.
Ni watu wasiri sana katika masuala ya mapenzi na wanakuwa hivyo ili waweze kuwapata wapenzi wengi kukidhi matakwa au kiu yao kubwa ya ngono.
KAZI NA BIASHARA ZA NG'E:
Ng'e ni watu makini sana katika kazi na wanafanya kazi kwa kutilia mkazo na ushupavu wakihakikisha wanatekeleza malengo yao. Ni waerevu na wenye kung’amua mambo upesi. Ni wafanyakazi wazuri na wanaheshima kwa wafanyakazi wenzao.
Kazi zinazowafaa wenye nyota hii ni kazi za madawa au tiba, kazi za upelelezi, kazi za utafiti, kazi za fundi bomba, kazi za elimu ya kale, na kazi za ushauri wa mambo ya mapenzi na ngono au biashara zinazoendana na mambo hayo.
MAVAZI NA MITINDO:
Ng'e wanatakiwa wavae nguo zenye rangi inayong’ara, zenye kuonekana na maridadi, zilizo katika hali ya suti au mbili kwa pamoja. Nguo ziwe za rangi nyekundu au shati jekundu au skafu nyekundu. Kitambaa kiwe cha sufi au cha fulana au chenye kumeremeta. Mavazi yaendane na kofia na wanawake wapendelee sana kuvaa suruali.
MAGONJWA YA NG'E:
Nyota hii inatawala kifuko cha mkojo, uume, uke, kifandugu au kitonoko (coccy), mlango wa kizazi (cervix) na sehemu ya haja kubwa. Vile vile inatawala mfumo wa mkojo na tezi kibofu (prostate).
Matatizo yao makubwa ya kiafya yanatokana na sehemu zilizotajwa ambazo zinatawaliwa na nyota yao wenye nyota hii wanapenda kujizoesha sana mambo ya mapenzi na ngono.
Magonjwa makubwa ya wenye nyota ya Ng'e ni maradhi yanayohusiana na kibofu cha mkojo, maradhi ya kuziba mkojo, kansa ya tezi kibofu (prostate Cancer), matatizo ya damu ya k**e na mabusha.
VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA NG'E:
Ng'e wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao, Mananasi, wapende sana vitunguu vibichi na vilivyopikwa, Nyama ya Kondoo mchanga na vyakula viambatane na viungo vikali.
Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota hii.
Miji hiyo ni Liverpool (Uingereza) na New Orleans(Marekani) na nchi za Poland na Switzerland.
MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Ng'e ni Chuma. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni k**a vilivyoonyeshwa katika picha hapa chini.
Mafusho ya Ng'e ni Qist. unachoma siku ya Jumanne kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

MAWASILIANO 0678 752 883

NYOTA YA MIZANI (LIBRA)0678 752 883Hii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12. Na ni ya watu waliozaliwa  kati ya ...
18/04/2024

NYOTA YA MIZANI (LIBRA)

0678 752 883
Hii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12. Na ni ya watu waliozaliwa kati ya tarehe Septemba 23 na Oktoba 23 au wenye majina yalio anza na herufi G na S.
Sayari yako ni VENUS (ZUHURA).
Siku yako ya Bahati ni Ijumaa.
Namba ya Bahati ni 6.
Rangi ya Bahati ni Kijani isiyoiva.
Asili ya nyota hii ni Hewa.
KIPAJI CHA MIZANI
(Extra Sensory Perception)
Wenye nyota hii wana kipaji cha kufumbua mafumbo na kujua siri za watu bila kuambiwa.
TABIA ZA MIZANI:
Wenye nyota ya Mizani wana tabia yatapungua kupenda usuluhishi, amani na upatanishi. Ni watu wasikivu, watiifu, na wepesi kuongozwa. Ni wenye maumbo ya kupendeza hasa wanawake. Kwa ujumla ni watu wenye roho nzuri na wanajua kupenda na wenye mahaba mengi.
Ni watu wastraabu, wenye adabu heshima na ni wakarimu kwa mtu yeyote na wanajipenda sana.
Katika maisha yao wajipenda sana.
TABIA YA MIZANI KATIKA MAPENZI
Kujihusisha na suala la mapenzi kwa wenye nyota hii ni kitu cha kawaida kabisa pamoja na kwamba wenye nyota hii wanachukua muda mrefu kufanya maamuzi na inawawia vigumu sana kuchagua kati ya wapenzi wawili yupi anaefaa. Kwao kuishi vizuri ni kuwa na mpenzi au uhusiano wa kimapenzi.
Watu wa mizani wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda sana kujionyesha kwamba wanapendwa.
Kwa sababu hizo wengi sana wanapumbazwa na mapenzi na ndoa zao zinakuwa zina
matatizo na zisizo na raha kwa sababu ya kuoa mapema bila kuangalia. Wenye nyota hii wanaonelea bora kuishi katika ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.
Katika suala la mahaba (Romance) na ngono (S*x) wao ni mabingwa. Wanajua sana
kumpendeza mwanamke kwa maneno matamu yenye mpangilio na zawadi za thamani na wawapo kitandani wanatumia muda mrefu kuwachezea wapenzi wao sehemu nyeti.
Kwa ujumla wenye nyota ya Mizani wanapenda kuishi vizuri na wanapenda wapenzi wao nao waishi katika hali nzuri
MADINI YA MIZANI Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa LAPIS LAZULI. Mawe k**a nye rangi ya Bluu iliyokoza, wamisri wanayaita mawe ya peponi. Yakiwekwa k**a kito kwenye pete ya dhahabu yanaleta mizani kwa wenye nyota hii.
UHUSIANO WA KIMAPENZI
(Punda na Mizani)
Tabia ya Punda ya haraka haraka. Vishindo na kutumia nguvu bila kufikiria, hulainishwa au kuzimwa na diplomasia, uerevu na ujanja wa mizani. Punda vile vile hupendezwa na uwezo au kipaji cha mahaba walichonacho wenye nyota ya mizani.

MAWASILIANO - 0678 752 883

MAELEZO YA NYOTA YA NDOO AQUARIUSMAWASILIANO - 0678 752 883Hii ni nyota ya kumi na moja katika mlolongo wa nyota 12. Nyo...
18/04/2024

MAELEZO YA NYOTA YA NDOO AQUARIUS
MAWASILIANO - 0678 752 883

Hii ni nyota ya kumi na moja katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 20 Januari na Februari 18 au wenye majina yalio anza na herufi K au W.
Asili yao ni Upepo.Sayari yao ni Uranus. Siku yao ya bahati ni Jumamosi. Namba yao ya bahati ni 8
Malaika wake anaitwa Cassiel au Kafyaeel, na Jini anayetawala Jumamosi anaitwa, Abuu Nuhu au Aratron. Herufi ya Jumamosi ni Z
Rangi zao ni Bluu, Kijivu na Samawi ya Bluu (Ultramarine blue). Wenye nyota ya Ndoo wanatakiwa wapake nyumba zao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi zilizotulia k**a Bluu au Kijivu.
Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Dhahabu na Machungwa.
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Aqua.
Kito (Jiwe) ni Lulu Nyeusi, Obsidian, Opali (Opal) na Johari (Sapphire).
Madini yao ni Risasi (Lead).
Manukato yao ni yale yatokanayo na Mgadenia (Gardenia) na Azalea.
MAMBO MUHIMU:-
Sifa ya nyota hii ni Uimara na Kutoyumba.
Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa Wachangamfu na Wenye hisia.
Maadili yao ni Uwezo mkubwa wa Kiakili, Uwezo wa Kuwasiliana, na Kuelewa mambo ya muhimu, Kupenda mambo Mapya.
Matakwa yao ni Kujua na Kuleta mambo mapya.
Tabia za kujiepusha nazo ni Kutojali, kutoshawishika au kutobadilika, kuwa na mawazo yasiyobadilika.
USHIRIKIANE NA NANI?
*Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Mapacha na Mizani.
*Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Ng’ombe, Simba na Nge.
*Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Nge.
*Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Ng’ombe.
*Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Samaki.
*Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mapacha.
*Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Simba.
*Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mapacha.
*Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Mizani na Mbuzi.
Siku yake nzuri katika wiki ni siku ya Jumamosi.
KIPAJI CHA NDOO:
Ndoo wana kipaji cha kutoa tafsiri sahihi ya jambo lolote linalotokea wakati wowote, Sudden Revelation.
TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Ndoo ni watu wachangamfu, wavumbuzi na wenye akili za kubuni jambo au kitu. Ni watu ambao wenye furaha wakati wote lakini inakuwa vigumu wakati mwingine kuwa karibu nao. Ni waaminifu na wakweli na wako tayari wakati wowote kutoa msaada unaohitajika.
Kwa upande mwingine ni watu ambao hawatabiriki hasa wanapokasirika, wanaweza kuwa wakaidi, wenye kushikilia jambo hata likiwa baya, ni wapotovu wa nidhamu na waasi.
Ni watu ambao hawajali Dunia inasema nini au inafikiria nini, wakati mwingine hukataa shughuli za kijamii na kujihusisha katika mambo yasiyo na maana yeyote.
Kwa ujumla ni watu wenye Roho nzuri ya kibinaadamu wanapenda kutoa msaada pamoja na kwamba wakati mwingine wanakuwa siyo dhahiri.
Ndoo ni watu wanaopenda uhuru na hawawezi kabisa kukubali kudhibitwa katika mapenzi, mawazo yao na miono yao inaweza kubadilika mara moja na kuwa wakaidi na wasumbufu. Pamoja na kwamba ni waaminifu na wanatoa msaada mkubwa kwa wapenzi wao.
Wako tayari kutulia katika mapenzi iwapo watahakikishiwa uhuru wao na haki ya kutoingiliwa katika mambo binafsi. Ni watu ambao hawapendi kuonyesha hisia zao halisi na wanachukua muda mrefu kuingia kikamilifu katika uhusiano wa kimapenzi.
Mara nyingi inakuwa vigumu kwao kuwaamini wapenzi wao lakini wakisha waamini wanakuwa waaminifu.
Ni watu ambao husema mambo bila kuficha na mara nyingi hawaeleweki kwa wapenzi wao.
Katika ngono, kwa sababu ya kupenda uhuru huwa wanapenda kufanya mambo wanavyotaka wao na hawakubali kuingiliwa.
Wakati mwingine hushindwa kuelewa hisia za wapenzi wao jambo ambalo linawafanya wapenzi wao washindwe kuwaelewa.
KAZI NA BIASHARA ZA NDOO:
Ndoo ni watu wenye akili nyingi na wenye malengo maalum katika shughuli fulani. Ni wawekezaji asili na wana uwezo wa kuwabadilisha watu tabia zao kutoka mbaya kuwa nzuri.
Kwa uhakika mawazo yao saa zote yanafanya kazi. Ni watu ambao muda wote wanafikiri njia mpya na za uhakika za kutekeleza wajibu wao na kikazi.
Kazi zao wan**ifanya kwa upole na uhakika, pamoja na kwamba wanafanya kazi kwa bidii mara nyingi huwa wanaonekana hawajafanya kitu au sifa huenda kwa watu wengine.
Watu wa Ndoo ni wenye mawazo ya ubunifu na wenye kugundua njia mpya na zenye uhakika katika kazi.
Kazi zinazowafaa ni za uhandisi wa umeme, kompyuta, utafiti wa Sayansi, utabiri, huduma za jamii na utafiti wa mambo ya kale.
MAVAZI NA MITINDO:
Ndoo wanatakiwa wavae nguo za mitindo, zilizoshonwa kwa ustadi. Nguo hizo ziwe za rangi ya Kijivu, au Kijani iliyoiva au hudhurungi nzito. Kitambaa kiwe cha kitani (Linen) au cha ngozi. Nguo ziwe ni suti na ziambatane na saa za mikono.
MAGONJWA YA NDOO:
Nyota hii inatawala kifundo na ugoko. Wenye nyota hii wana mawazo mapana ya kufanya mabadiliko ya Dunia na hii inawasababisha wajisahau hasa katika afya zao na mara kwa mara hupata matatizo ya kuugua.
Kutokana na ubishi wao mara nyingi wanakuwa wabishi kupokea ushauri kuhusiana na hali zao za kiafya.
Matatizo yao makubwa yanasababishwa na kuchoka kwa misuli kutokana na kazi nyingi, kwa kawaida ni wagonjwa wabishi wasiopenda ushauri.
Wanapofanya mazoezi wanashaurwa wasiwe na hasira kwani hiyo inawafanya wajiumize au wapate ajali ndogo ndogo hasa sehemu za miguu, ugoko, vifundo na uvimbe katika sehemu hizo.
Vile vile matatizo yao mengine ya kiafya ni mzunguko wa damu na mishipa ya miguu.
VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA NDOO:
Ndoo wanashauriwa wepende kula vyakula au Matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota zao, vyakula vya n**i na nyama aina zote. Vile vile wapendelee kula Viazi Vitamu na Samaki Gamba.
Ili kupata mafaniko ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota zao. Nchi hizo ni Sweden na Zimbabwe na Miji ni Humburg (Ujerumani) na Leningrad (Urusi).
MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Ndoo ni Risasi (Lead). Vito vyao vya kuvaa katika pete ni k**a vilivyoonyeshwa katika picha hapa chini.
Mafusho ya Ndoo ni Miatun- saila. unachoma siku ya Jumamosi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

MAWASIALIANO - 0678 752 883

MAELEZO YA NYOTA YA MASHUKE VIRGOMawasiliano - 0678 752 883Hii ni nyota ya sita kwenye mlolongo wa nyota 12 na ni ya wat...
18/04/2024

MAELEZO YA NYOTA YA MASHUKE VIRGO
Mawasiliano - 0678 752 883
Hii ni nyota ya sita kwenye mlolongo wa nyota 12 na ni ya watu waliozaliwa kati ya Tarehe 22 Agosti na 22 Septemba au wenye majina yalio anza na herufi F na R.
Asili yao ni Udongo.Siku yake nzuri katika wiki ni Jumatano. Namba yao ya bahati ni 5.Sayari yao ni Mercury (Attwarid).
Malaika wake anaitwa Raphael au Mikyaail na Jini anayetawala siku ya Jumatano anaitwa, Barkaan au Ophiel,
Herufi ya Jumatano ni T
Rangi zao ni Rangi ya udongo, Njano na Rangi ya machungwa. Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi Nyeupe au rangi ambazo siyo nzito au zenye kuonekana sana.
Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi Bluu.
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Rangi ya Kijani kibichi.
Kito (Jiwe) ni Cuprite, Diamond, Sugilite, Moss Agate, Quartz, Peridot,
Madini yao ni Quicksilver (Zebaki).
Manukato yao ni ya Mrujuani (Lavender) na Lilaki (Lilac).
MAMBO MUHIMU:-
Sifa ya Nyota hii ni wanakuwa na uwezo wa kubadilika badilika.
Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye uwezo kuangalia mambo kwa mtizamo mkubwa zaidi.
Maadili yao ni Uchambuzi, Wepesi wa Akili, Uwezo wa kuwa makini na Uwezo wa Kuponya.
Matakwa yao ni kuwa wenye uwezo wa Kutumika.
Tabia za kujiepusha nazo ni ukosoaji usiokuwa na malengo mazuri.
USHIRIKIANE NA NANI?
Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Ng’ombe na Mbuzi.
Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Mapacha, Mshale na Samaki.
Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mapacha.
Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Mshale.
Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mizani.
Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mbuzi.
Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Samaki.
Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mbuzi.
Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Simba.
KIPAJI CHA MASHUKE:
Mashuke wana kipaji cha kuhisi, kufikiri, kutambua tatizo au ugonjwa au kupata picha ya wazi akilini ya kutambua jambo lolote. Vilevile wana uwezo wa kuponya na wana uwezo wa kusoma michoro yeyote.
TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Mashuke ni watu ambao wanaopenda kusoma. Wana akili nzuri ambayo inatumika zaidi katika kupambanua njia ya asili ya mpangilio wa mambo. Kwa ujumla ni watu ambao wanapenda kufuata kanuni na kufanya mambo kwa usahihi kabisa. Ni waangalifu sana hasa katika mambo madogo madogo na wanapenda kushutumu hasa mambo yanapokwenda vibaya. Wanatabia ya kuchunguza mambo na kuhakikisha mpangilio unafuatwa kikamilifu. Wanajituma na kujishughulisha na wanapenda sana kufuata sheria au mpangilio maalum ulioainishwa.
Katika Mapenzi ni watu wenye aibu kwa undani lakini wanajiamini, wanapokuwa katika mapenzi hunawiri.
Ni watu ambao inawawia vigumu kuonyesha penzi lao. wana mtizamo wa kufikiri kabla ya kujitumbukiza ndani ya penzi lolote, wanachunguza kwa makini matokeo ya penzi lenyewe. Wanapotafuta mpenzi wanaweza wakakupumbaza na maneno matamu na raha zisizo na kifani.
Ni vizuri kufikiria mara mbili kabla hujajiingiza katika mapenzi na Mashuke. Inawawia vigumu wao kukuanza wewe kimapenzi kwa sababu wana uhakika kwamba watashindwa. Kinachowasaidia ni subira na kuwaelewa wapenzi wao ndio maana mapenzi yanakua. Mara wakishapata mpenzi wa kweli wanakuwa waaminifu sana na watafanya kila njia kuhakikisha mapenzi yanakuwa hai na yenye kupendeza.
Hata hivyo wanaweza kuwa wasumbufu, wenye kulalamika na wenye mtizamo wa makosa ya mpenzi wake ili amshutumu. Kwa sababu ya hali yao hii mara kwa mara kunakuwa na ugomvi wa wapenzi ambao wanataka kutekeleza malengo yao.
KAZI NA BIASHARA ZA MASHUKE:
Mashuke ni tegemezi, wenye bidii ya kazi na tabia ya kufanya kazi bila ya kuchoka. Wanapenda sana kazi zenye mpangilio na ambazo kila kitu kiko katika mpangilio maalum.Wanapenda kuwa huru katika kazi zao na kujitosheleza katika kila wanachokifanya, hufurahi kufanya kazi bila ya kusimamiwa.
Kazi zao ni zile zinazohusiana na uchapishaji, utangazaji, afya, udaktari, kazi za unesi, kazi za uongozi, elimu na kufundisha, biashara yoyote au kazi za ukatibu muhtasi.
MAVAZI NA MITINDO:
Mashuke wanatakiwa kuvaa Nguo zenye Mitindo ya kisanii, nguo ziwe Nyepesi na zilizonyooka Ziwe za Rangi ya Njano na Nyeupe. Kitambaa kiwe k**a hariri, chepesi na chenye kumeremeta. Wake kwa waume wapendelee kuvaa Suti na ikiwezekana wasikose kuvaa Gloves
MAGONJWA YA MASHUKE:
Nyota hii inatawala utumbo, sehemu ya uvunguni mwa utumbo na neva zote zilizo chini ya kitovu.Kutokana na asili hiyo wale wenye nyota hii huwa wanapata sana matatizo ya maradhi ya ugonjwa wa tumbo au tumbo la uzazi au matatizo ya kizazi.Magonjwa ya mwili kushindwa kusaga chakula tumboni au magonjwa ya kujikunja utumbo na maambukizo ya utumbo.
VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA MASHUKE:
Mashuke wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndio vinavyotawaliwa na nyota yao, kuku, rasiberi, karoti na uduvi. Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota ya Mashuke wanashauriwa watembelee au waishi katika nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota yao; nchi hizo ni Austria na Norway na miji hiyo ni Jerusalem na Paris.
MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Mashuke ni Quicksilver (Zebaki). Vito vyao vya kuvaa katika pete ni k**a vilivyoonyeshwa katika picha hapa chini.
Mafusho ya Mashuke ni Kashuu Muhlib (kachiri). unachoma siku ya Jumatano kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana

Mawasiliano - 0678 752 883

Address

Ilala, Dar Es Salaam
Ilala
12101

Telephone

+255678752883

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maalim Omary Mzungu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Maalim Omary Mzungu:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram

Category