25/02/2026
TANGAZO TANGAZO TANGAZO
HABARI NJEMA KWA WAKAZI WOTE WA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI.
Madaktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Ujerumani (INTERPLAST) kwa Ushirikiano na Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Kilutheri llembula - Njombe, watatoa huduma za Upasuaji kwa wenye matatizo k**a MAKOVU BAADA YA KUUNGUA MOTO (BURN CONTRACTURE), Matatizo ya Mikono (Hand Surgery), Mdomo uliopasuka (Cleft lip) yanayohitaji upasuaji kuanzia tarehe 22/03/2026 mpaka tarehe 02/04/2026.
UTARATIBU
Tarehe 22/03/2026 mpaka tarehe 23/03/2026 kupima wagonjwa
kuanzia saa 02:00 asubuhi.
Tarehe 24/04/2026 mpaka tarehe 02/04/2026 upasuaji
GHARAMA
Usajili wa mgonjwa shilingi 10,000/=
Upasuaji wote utafanyika BURE
NB: BIMA ZA AFYA ZITATUMIKA KULIPIA GAHARAMA TAJWA HAPO JUU.
Kwa maelezo zaidi wasiliana kwa namba hii:
0755797295 (Dr. Pangamawe) na
0787882205 (Dr. Victory)
Atakayesoma au kusikia Tangazo hili amwambie na mwenzake.