30/12/2025
Kliniki ya mama, baba na mtoto ina mchango mkubwa katika kutoa elimu kuhusu umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto mchanga.
Kupitia kliniki hizi, wazazi hupata elimu sahihi juu ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo, namna sahihi ya kumnyonyesha mtoto, na jinsi ya kuepuka matumizi ya vyakula au vinywaji vingine visivyofaa.
Kwa ujumla, kliniki ya mama, baba na mtoto huimarisha uelewa, hubadili mitazamo potofu na kuhamasisha jamii kukubali unyonyeshaji k**a njia bora na salama ya lishe kwa mtoto mchanga.