21/09/2022
KUTOKWA NA UCHAFU NA HARUFU MBAYA UKENI (VAGINOSIS)
Nimekuwa nikipata simu nyingi sana kuhusiana na tatizo hili pamoja na namna ya kutibu pia. Nikaona si vibaya kuliweka hapa ili kila mtu iwe rahisi kujifunza
Wanawake wengi wanasumbuliwa na tatizo la kutokwa na uchafu ukeni na uchafu huo huwa sambamba na harufu kalia au bila harufu na upo k**a maziwa ya mgando
Kitaalamu hali ya kutokwa na maji maji ukeni (viginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano ni hali ya kawaida na sio tatizo ila endapo majimaji hayo yapo katika hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au k**a mgando wa maziwa na yanatoa harufu kali sambamba na muwasho basi hiyo sio hali ya kawaida ni ugonjwa uitwao VAGINOSIS
majimaji ya ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha na kutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili. Pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi ya bacteria au fangasi wanaosababisha magonjwa. Kawaida huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au njano. Na pua huwa ni asidi ya Lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na huzalishwa kwenye tezi za Bartholin zilizopo kwenye shingo ya mlango wa uzazi (Cervix)
SABABU ZA KUTOKWA UCHAFU NA HARUFU MBAYA UKENI
-maambukizi ya bacteria k**a Trichomoniasis, candidiasis, Gonorhea, uambukizo wa bacteria candida albicans, vaginosia bacteria ambao husababisha kutoa harufu
-mabaki ya vitambaa, pedi, pamba na tishu ambazo hazikutolewa wakati wa hedhi
-kutumia tishu wakati wa kumaliza kujisaidia, hivyo kuacha mabaki ambayo yanasababisha tatizo hilo
-usafi wa sehemu za siri usipozingatiwa hasa baada ya hedhi kumalizika huweza kuwa mazalia mazuri ya bacteria wanaosababisha harufu
-kukaa muda mrefu na pedi bila kubadili
-kuvaa chupi mbichi, chafu na nguo nyinginezo za ndani mara kwa mara na bila kuzifua.
DALILI YA UGONJWA HUU
1: kutokwa ute au majimaji yasiyo ya kawaida yenye harufu kali k**a shombo ya samaki
2: maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu
3: kutokwa na uchafu wenye rangi k**a ya kijani
4: kuwashwa sehemu za siri na kutokwa vidonda mpaka mapajani k**a hutatumia dawa
5: kutokwa ute uliochanganyika na damu hata k**a haupo kwenye hedhi.