
12/10/2023
JINSI YA KUJIPONYA TATIZO LA ACID AU TINDIKALI YA TUMBO - GERD
https://shorturl.at/gESW5
Hili ni tatizo linalotokea katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula linalosababisha hitilafu ya chakula au maji kurudi katika koo la chakula (umio) mara baada ya kuwa chakula Hiko kimeshamezwa. Au Ni kitendo cha kupanda kwa acids (tindikali) ya tumbo hadi kwenye Koo /Umio la chakula kwa muda mrefu na matokeo yake husababisha kiungulia (HEARTBURN) AU MAUMIVU YA KOO
-Kawaida Mara baada ya mtu kutafuna chakula au kunywa maji,chakula husafirishwa kupitia mrija wa chakula (Esophagus) hadi tumboni lakini juu kidogo kati ya tumbo na mrija huu wa chakula kuna kizuizi kilicho na sura ya bangili ( lower esophageal spincher )
kibangili hiki hufanya kazi ya kuzuia chakula kisurudi mdomoni au kwenye koo baada ya kuwa kimeshamezwa.
-Baada ya chakula kuingia tumboni huchanganyikana na vimeng'enya pamoja na tindikali ambayo hufanya kazi ya kuua vimelea vyote vilivyoingia tumboni pamoja na chakula
mchanganyiko huu husababisha chakula kupata chachu(acids) ambayo matokeo yake huwa ni rahisi sana kuweza kurudi katika koo la chakula endapo kizuizi cha juu ya tumbo kitakua kimepata hitilafu au maambukizi.
CHANZO CHA MATATIZO HAYA NI NINI ?.
Uchunguzi unaonyesha kuna sababu nyingi zinazoweza kuambatanishwa na matatizo haya ambayo ni;
1. Kudhohofika kwa utendaji kazi wa kizuizi cha juu ya tumbo ( Lower esophageal sphincter)
• Kudhohofika kwa kizuizi hiki husababishwa na utumiaji wa madawa k**a nitrates , isphosphonates , Estrogen , Oral Contraceptives , Progesterone , n.k. Baadhi ya dawa zimeonekana kuharibu sana utendaji kazi wa kizuizi hiki.
2.Mfumo dhaifu wa mmeng'enyo wa chakula :-
• Mfumo wa mmeng'enyo huwa dhaifu kutokana na lishe kuwa mbovu
watu wanaokula zaidi vyakula vilivyosindikwa, sukari, chocolate, vyakula vyenye caffeine k**a kahawa wapo kweye hatari zaidi ya kupata matatizo haya
3.Tindikali ( Hydrochloric acid) kuzidi tumboni.
4.Upungufu wa madini k**a Magnesium na Potassium mwilini
5.Uzito mkubwa na kitambi na msongo wa mawazo kupita kiasi ni chanzo cha kupata matatizo haya.
6.Wamama wajawazito na wazee wenye umri mkubwa wako kwenye hatari zaidi ya kupata matatizo haya
7.Wenye historia ya kuwa na ugonjwa wa hernia(ngiri) pia wapo katika hatari zaidi ya kupata matatizo haya
8. Uwepo wa bacteria wabaya tumboni k**a H.pyrolly na wengineo huwa ni chanzo cha magonjwa haya ya mmeng’enyo wa chakula
DALILI ZA GASTROESOPHAGEAL REFLUX DISEASE AU KUZIDI KWA TINDIKALI YA TUMBO
1 kupatwa na kiungulia mara kwa mara ambapo huambatana na koo la chakula kuwaka moto pia maumivu ya kifua na hali hii huzidi zaidi pale mtu anapolala kichwa kimeinama.
2 Kwa watoto hujionesha pale mtoto anapotapika kupita kiasi au kupaliwa mara kwa mara wakati wa kula chakula.
3 Tumbo kuunguruma na Kukosa hamu ya kula chakula na kuhisi kichefuchefu.
4 Mdomo kunuka kutokana na kurudi juu kwa chakula cha tumboni chenye tindikali.
5 Kupata hali ya kuunguza kwenye kifua karibu na moyo, hali inayotokea Muda Mfupi baada tu ya kula na kupata shida wakati wa kumeza chakula.
6 Kucheuwa Maji Maji Yenye Tindikali Ukiwa Usingizini Hasa Baada Ya Kulala Muda Mfupi Baada Ya Kula.
7 Kukohoa au kupaliwa mara kwa mara ikiambatana na kuweweseka Kwa Kukosa Pumzi.
8 Mdomo kuwa mchachu muda mwingi.
9 Kupata usingizi kwa shida kutokana na maumivu ya tumbo na Koo.
10 Kuvimba Kwa Tezi za Shingoni K**a Vile Tonses na Goita.
11 Mdomo kukauka.
12 Meno kupoteza uimara na kuanza kumomonyoka kutokana na uwepo wa tindikali.
13 Tumbo kujaa Gesi , Kupata Choo K**a Tope Kunakoambatana kujamba sana
KIUNGULIA (HEARTBURN)NI NIN I?
-Ni hali ya kukera inayoweza kumtokea mtu yoyote na husababisha maumivu makali kwenye kifua na upande wa juu wa tumbo.
Hali hii inaendana kwa ukaribu wa kupanda kwa tindikali(acid reflux).
Lakini pia Kuna utofauti kati ya acid reflux na heartburn.
K**a tatizo likiendelea zaidi basi hufikia hatua ya tatu na kuitwa gastroesophageal reflux disease (GERD), kwa hiyo kadiri kiungulia kinachukua muda mrefu mpaka kuathiri tishu za Utumbo au Umio GERD ni hatari zaidi kwa sababu inaweza kupelekea uwezekano wa kupata Madonda Tumboni au Saratani ya Koo.
𝐊𝐀𝐑𝐈𝐁U TUKUSAIDIE – TUMEKUANDALIA DARASA MAALUMU LA KUJIFUNZA JINSI YA KUJIPONYA NA MAGONJWA HAYA KWA MWEZI MMOJA – DARASA HILI NI BURE CHA KUFANYA BONYEZA LINKI UNAZOZIONA KWENYE TANGAZO HILI KUJA DARASANI SASA HIVI
https://shorturl.at/gESW5
AU PIGA SIMU AU WHATSAP MOJA KWA MOJA