
24/06/2025
*Madhara ya kutumia P2 (Postinor 2) mara kwa mara:*
P2 ni dawa ya kuzuia mimba ya dharura (emergency pill) ambayo hufanya kazi ndani ya saa 72 baada ya tendo la ndoa bila kinga. Ingawa ni salama kwa matumizi ya dharura, matumizi ya mara kwa mara yana madhara yafuatayo:
🔴 *Madhara ya Muda Mfupi (baada ya kutumia):*
- Kichefuchefu na kutapika
- Maumivu ya kichwa au kichomi
- Maumivu ya matiti
- Maumivu ya tumbo (k**a hedhi)
- Hedhi kubadilika (kuchelewa au kutoka mapema)
🔴 *Madhara ya Matumizi ya Mara kwa Mara:*
1. *Kuvuruga mzunguko wa hedhi*
- Hedhi huja bila mpangilio au kutokuwepo kabisa kwa miezi kadhaa.
2. *Kuchanganya homoni*
- Inaweza kusababisha homone imbalance: chunusi, unene kupita kiasi, hasira au mabadiliko ya kihisia.
3. *Kupunguza uwezo wa kushika mimba baadaye (kwa baadhi ya wanawake)*
- Ingawa si kwa kila mtu, matumizi ya mara kwa mara yanaweza kuathiri uzazi.
4. *Kuongeza hatari ya mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi (ectopic pregnancy)*
5. *Kuathiri ini na figo* kwa matumizi ya muda mrefu bila uangalizi.
---
✅ Ushauri:
- Tumia P2 *tu* kwa dharura — si njia ya kawaida ya uzazi wa mpango.
- K**a unahitaji kinga ya muda mrefu, zingatia njia salama k**a vidonge vya kila siku, sindano, kitanzi (IUD), au kondomu.
Afya ya uzazi tz
0719699760