27/06/2020
Je wajua ni wakati gani Wa kumuona mtaalamu Wa Afya ya UZAZI ama kwenda kliniki unapohisi hali ya utofauti pale unapo kuwa MJAMZITO?
Zipo dalili ama viashiliya vingi vya kukufanya uweze kumuona mtaalamu wa Afya ya Uzazi, ama kufika kliniki ikiwezekana hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kubaini tatizo na hatimaye kulitibu. Hapa nimeorodhezesha baadhi ya dalili (5) ingawa zipo nyingi lakini hizi nimezipa kipaumbele.
1.Mara unapojihisi kuwa mjamzito inakupasa wewe na mwenza wako kufika sehemu ya kutolea Huduma za Afya (clinics),hospitali ili kuweza kupewa ushauri, kufanyiwa vipomo na uchunguzi mbalimbali ili kubaini k**a kuna shida yeyote ya kiafya na kuweza kupatiwa matibabu na namna ya kutunza huo ujauzito n.k.
2.unapo hisi maumivu ya kichwa,macho kuuma ama kushindwa kuone vizuri, kuvimba kwa miguu, kujihisi kizunguzungu, inakupasa ufike clinic ama Hispitali ili uweze kutibiwa kwani hilo ni tatizo
3.unapopata maumivu makali ya tumbo hasa chini ya kitovu, kuharisha zaidi ya Mara tatu ndani ya muda mfupi, nyonga (kiuno) kuuma kupita kiasi, inakupasa umuone mtaalamu Wa Afya (uzazi) ili kuweza kufanyiwa uchunguzi.
4.kutokwa na damu ama maji sehemu za sili wakati Wa ujauzito pia ni dalili mbaya hivyo inakupasa umuone mtaalamu Wa Afya ama kliniki, fika hospitali iliyokaribu na wewe kwa uchunguzi zaidi
5. Unapohisi mabadiliko ya kucheza ama kutosikia mtoto akicheza fika kliniki iliyokaribu yako kwa uchunguzi zaidi.