
25/07/2025
Wakati mwingine ni vyema tu kumruhusu mtu aondoke maishani mwako k**a hataki kukuelewa, Kutokuwepo kwake kutakufundisha vitu ambavyo Huwezi jifunza akiwepo.
Acha kujiumiza kwa kulazimisha Mahusiano au ndoa ambayo wewe ni Shahidi siyo sahihi kwako, Huwezi kufanya mtu akujali, awe mwaminifu au kuwabadilisha unavyotaka.
Wakati mwingine mtu unayelazimisha kuwa naye ndo hukupaswa kabisa, wakati mwingine watu huja kwa sababu tu nakupita, waache waende.
Kuwa makini usipoteze utu na nafsi yako kurekebisha jambo ambalo kamwe hutaliweza. Huwezi pata Upendo / mapenzi toka kwa mtu ambaye hayupo tayari kukuthamini.
Ni ngumu sana ukiwa unafikiri mtu uliye naye " Ni sahihi" halafu anakuwa ndo anakuuza kabisa, Utapona tu na kupata mtu mwingine.
Kumbuka ni Bora kuwa "single" - Kuishi mwenyewe kuliko kupoteza utu wako, K**a mtu anakufanya k**a wewe mbadala, kamwe usimfanye kipaumbele chako.
, , ,