
21/07/2022
UGONJWA WA ARTHRITIS NI NINI?
Arthritis ni ugonjwa unaotokana na namna yo yote ya hitilafu katika maungio ya mifupa ya binadamu ambao husababisha maumivu na pengine kuvimba katika sehemu moja au zaidi ya maungio hayo.
Neno arthritis halilengi ugonjwa mmoja bali jamii ya magonjwa ambayo kwa ujumla yapo mengi (zaidi ya 1).
Tabia kuu ya magonjwa haya ni maumivu kwenye maungio ya mifupa (joints) ambayo ni endelevu na ambayo hutokea eneo hilo moja.
CHANZO CHA ARTHRITIS NI NINI?
¶Kwanza tutazame muundo wa joint au sehemu mifupa miwili inapokutana.
Mtano, goti ambapo mifupa miwili mmoja wa paja na mwingine wa mguu vinapokutana:
¶ Ligaments: Ndicho kitu kinachoshikilia mifupa hii miwili pamoja.
Hii ni k**a utepe wa plastiki au mpira unaonyumbuka uliozunguka eneo hilo kwa nje, ukikunja goti inanyumbuka na ukinyoosha mguu inarudi.
¶ Cartilage: Huu ni utando unafunika eneo ambalo mifupa hugusana ili kuzuia mifupa hii isisuguane moja kwa moja.
Utando huu ambao kwa kiswahili tunauita gegedu huyawezesha maungio hayo kufanya kazi kiulaini pasipo kusababisha maumivu.
¶ Capsule: Hiki ni kitu kinachofunika maungio haya kikizunguka pande zote.
Ndani ya mfuko huu wa capsule kuna synovial fluid ambayo huzalishwa na synovial membrane.
¶ Synovial fluid ni ute wa kulainisha sehemu hiyo ya maungio na synovial membrane ni utando ulio kwenye kuta za ndani za capsule.
Ugonjwa wa arthritis unasababishwa na hitilafu yoyote katika sehemu hizo za maungio ya mifupa.
Inaweza kuwa cartilage inalika, upungufu wa synovial fluid, maambukizi ya vijidudu katika moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo.
Virutubisho lishe vimeonekana kutibu kabisa changamoto bila kufanyiwa upasuaji. Nitafute nikushauri na nikupatie tiba pia.