Ewe mwanaume au mwanamke ijenge afya yako

Ewe mwanaume au mwanamke ijenge afya yako Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Ewe mwanaume au mwanamke ijenge afya yako, Medical and health, Mbeya.

ni kwa ajili ya wanaume na wanawake kuishi na kujua afya zao na kudumisha mausino au ndoa zao tafadhali ukijiunga au kujijoini fuata Shelia haturuhusuwi kupost vitu vyovyote mbali na afya ya MWANAUME by
Dr Braitoni
0714780308

22/02/2022
UJUE UGONJWA WA PID (Pelvic Inflammatory Diseases)Pelvic Infalammatory Disease (PID) ni maambukizi kwenye viungo vya uza...
20/02/2022

UJUE UGONJWA WA PID (Pelvic Inflammatory Diseases)

Pelvic Infalammatory Disease (PID) ni maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke. PID hutokea pale bakteria waenezwao kwa ngono wanaposambaa kutoka kwenye uke (va**na) hadi kwenye nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na ovari.

Dalili za PID huweza kuwa ni ngumu kueleweka. Baadhi ya wanawake hawaoni dalili zo zote. Kwa maana hiyo, unaweza usihisi cho chote hadi pale utakaposhindwa kupata ujauzito au hadi utakapoanza kupata maumivu ya kiuno.

PID MAENEO YA pid

Dalili Za PID
PID inaweza isilete dalili zo zote mbaya na ndogo zikitokea zinaweza kuwa ngumu kuzigundua. Baadhi ya wanawake hawapati dalili zo zote. Pale zinapojitokeza, zinaweza kuwa:
Maumivu – yanayoweza kuwa madogo au makali – maeneo ya chini ya tumbo au nyonga Uchafu usio wa kawaida au mzito ambao unaweza kuwa na harufu mbaya Kutokwa damu kusiko kwa kawaida, hasa wakati wa tendo la ndoa, au katikati ya siku za hedhi Maumivu wakati wa kujamiiana Homa, wakati mwingine kusikia baridi Maumivu wakati wa haja ndogo, haja ndogo ya mara kwa mara au haja ndogo kutoka kwa shida.

Chanzo Cha PID
Kuna bakteria wa aina nyingi wanaoweza kusababisha PID, lakini maambukizi ya gonorrhea na chlamydia ndiyo yanayoonekana zaidi. Bakteria hao huambukiza wakati tendo la ndoa linapofanyika bila ya kutumia kinga.

kusambaa kwa PID

Aghalabu, bakteria hawa huingia kwenye viungo ya uzazi vya mwanamke pale ulinzi wa kwenye shingo ya kizazi (cervix) unapovurugwa. Hii inaweza kutokea mathalani, wakati wa hedhi na baada ya kuzaa, mimba kuharibika au kutoa mimba. Mara chache bakteria huweza kujipenyeza wakati kifaa cho chote cha tiba kinapoingizwa kwenye nyumba ya uzazi.

Mazingira Hatarishi
Kuna vipengele ambavyo huweza kukuweka kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata PID, navyo ni:
Kuwa mwanamke uliye chini ya miaka 25 unayeshiriki ngono Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja Kuwa na mahusiano na mpenzi mwenye wapenzi zaidi ya mmoja Kufanya mapenzi bila kinga Kujisafisha na maji mara kwa mara Kuwa uliwahi kupata PID kabla au magonjwa mengine ya ngono

Madhara Yatokanayo Na PID
PID ambayo haikupata tiba inaweza kusababisha makovu na vifuko vyenye maji yenye wadudu kwenye mkondo wa njia ya uzazi ya mwanamke. Vitu hivi vinaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye viungo vya uzazi.

PID magonjwa

Madhara yanayoweza kutokea ni pamoja na:
Mimba nje ya mirija (ectopic pregnancy). PID ndiyo sababu kubwa ya mimba kutunga nje ya kizazi. Mimba huweza kutunga nje ya kizazi endapo PID imesababisha makovu ndani ya mirija ya uzazi. Makovu haya husababisha yai lililopevushwa kushindwa kusafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye nyumba ya uzazi. Badala yake yai hunata ndani ya mirija ya uzazi . Mimba nje ya kizazi husababisha utokaji wa damu usio wa kawaida unaoweza kukatisha maisha ya mwanamke.
Ugumba. Uharibifu wa viungo vya uzazi huweza kusababisha ugumba – kushindwa kupata ujauzito. Kadiri unavyozidi kupata PID mara nyingi zaidi, ndivyo hatari ya ugumba inavyozidi. Kuchelewa kupata tiba ya PID kunaongeza hatari ya ugumba.
Maumivu sugu ya nyonga. PID inaweza kusababisha maumivu ya nyonga yanayoweza kudumu kwa miaka mingi. Makovu ndani ya mirija ya uzazi na viungo vingine vya uzazi huweza kuleta maumivu wakati wa kujamiiana na wakati yai linadodondoshwa (ovulation).
Tubo-ovarian abscess. PID huweza kusababisha kutunga kwa usaha na kufanya majipu ndani ya njia ya uzazi. Mara nyingi majibu haya hutokea ndani ya mirija ya uzazi na ovari, ingawa huweza kuota ndani ya nyumba ya uzazi na shingo ya kizazi. K**a tiba haitatolewa, unaweza kupata maambukizo hatarishi kwa maisha.

Tiba Ya PID

Kutana na Dr Braitoni kwa ushauri na tiba ya ugonjwa huu wa PID ambao umewatesa wengi na wengi kupoteza maisha
Wasiliana nasi kwa no
Tell 0766626773
WhatsApp 0714780308/0628296954

Tunapatikana mbeya mwanjelwa century plaza

TEZI DUME UMEKUWA NI UGONJWA UNAOWAKUMBA SANA HASA WANAUME UMRI WA MIAKA 40 ..NA INATIBIKA BILA UPASUAJI KALIBU UKUTANE ...
04/02/2022

TEZI DUME UMEKUWA NI UGONJWA UNAOWAKUMBA SANA HASA WANAUME UMRI WA MIAKA 40 ..NA INATIBIKA BILA UPASUAJI KALIBU UKUTANE NA
DOKTA BRAITON
0766626773/0714780308
MWANJELWA MBEYA CENTURY PLAZA

04/02/2022
04/02/2022

Address

Mbeya

Telephone

+255766626773

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ewe mwanaume au mwanamke ijenge afya yako posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Ewe mwanaume au mwanamke ijenge afya yako:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram