
14/12/2023
KUTOKUZINGATIA taratibu za usafi wa kinywa ni miongoni mwa sababu za tatizo la kulegea, kuoza, kutoboka na kutoa harufu ya kinywa linalowakabili watoto na watu wazima katika Jamii.
Asilimia kubwa ya tatizo la meno yanayowakabili watoto na watu wazima yanasababishwa na kutokusafisha meno vizuri, kuoza na kutoboka kunasababishwa pia na matumizi ya sukari ilio sindikwa inayopatikana katika vyakula mbalimbali zikiwemo chocolate, p**i, biscuits na soda.
Sukari ilio sindikwa ambayo hupatikana katika vyakula vingi ndio chanzo cha meno kutoboka, kulegea pamoja na kuoza kutokana na matumizi ya sukari hio, hii hutokea kwa watoto na watu wazima wanaotumia vyakula vya Aina hio kwa wingi.
ILI kuepuka madhara hayo yanayosababishwa na matumizi ya sukari ilio sindikwa, unapaswa kuzingatia hatua mbalimbali za kusafisha kinywa ili kuondoa kabisa mabaki ya vyakula hivyo katika meno.
Kuna hatua nne za kufuata zinazoweza kukukinga meno yako dhidi ya matatizo yanayosababishwa na ulaji wa sukari zilizosindikwa k**a zitafuatwa kikamilifu, utabaki na meno mazuri na yenye afya.
Wakati unasafisha meno unapaswa kuanza na fizi za ndani kwa meno yote kabla ya Kuja katika hatua ya pili ambayo ni katikati ya meno hasa yakutafunia chakula.
Hatua ya tatu ni kusafisha sehemu ya nje ya meno na fizi zake na hatua ya mwisho ni kusafisha sehemu ya juu ya ulimi. Kupitia hatua hizo meno yako yatasalia kuwa masafi na salama na utaepuka meno kuoza, kutoboka au kinywa kutoa harufu mbaya.
Taratibu za kiafya inatakiwa Kila mtu kusafisha kinywa kila baada ya kula pamoja na asubuh baada ya kuamka.
KWA TATIZO LOLOTE LA MENO AU KINYWA USISITE KUWASILIANA NASI ILI UPATE MSAADA WA TATIZO LAKO.
Piga 📞 +255624416652