
18/12/2023
Mshtuko wa Moyo (Heart Attack)
Utangulizi
Mshtuko wa Moyo hutokea wakati mshipa au mishipa ya damu inayoenda kwenye misuli ya moyo inapoziba na kushindwa kuipatia oksijeni misuli hiyo. Mishipa hiyo huziba kutokana na kuongezeka kwa mafuta aina ya kolesterol kwenye kuta za mishipa hiyo iitwayo coronary arteries.
Mshtuko wa moyo ni tatizo la dharura ambalo lisiposhughulikiwa kwa haraka husababisha kifo.
Dalili
• Kupata maumivu makali ya kifua, mikono hasa wa kushoto,shingoni, mgongoni au kwenye taya ghafla na kuhisi k**a kugandamizwa na kitu kizito kifuani,
• Kuhisi kichefu chefu,maumivu ya tumbo,
• Kutokwa na jasho la baridi,
• Kupatwa na kizunguzungu,
• Kuhisi uchovu wa ghafla,
• Kushindwa kupumua.
Sio kila mtu hupatwa na dalili hizi. Wengine husikia maumivu kidogo huku wengine dalili ya kwanza ni moyo kusimama.Lakini mara nyingi mtu akipatwa na dalili kadhaa kati ya hizo hapo juu kuna uwezekano mkubwa kuwa amepatwa na mshtuko wa moyo.
Sababu
K**a nilivyosema kwenye utangulizi,mshtuko wa moyo hutokea baada ya misuli ya moyo kukosa hewa ya oksijen. Hii hutokea kwa sababu mbalimbali k**a vile;
• Mishipa kuziba kutokana na kuwa na mafuta mengi ndani yake,
• Mishipa ya damu kusinyaa,
• Damu kuganda ndani ya mishipa,
• Misuli kuwa mikubwa kutokana na ugonjwa sugu wa moyo(chronic heart failure).
Watu wenye hatari ya kupata mshtuko wa moyo;
• Watu wanene-hutokana na wao kuwa na mafuta mengi katika viungo k**a vile maini,moyo,mishipa na ngozi,
• Watu wenye kisukari- kisukari huzuia mwili kutumia mafuta hivyo kusababisha limbikizo la mafuta. Lakini pia sukari nyingi husababisha damu kuwa nzito hivyo kuhatarisha mishipa kuziba,
• Watu wenye shinikizo la damu,
• Uvutaji wa sigara,
• Umri-kadri umri unavyoongezeka ndio kuna hatarishi ya kupata mshtuko wa moyo,
• Matumizi ya madawa ya kulevya k**a kokain ,
• Historia ya familia- mshtuko wa moyo ni miongoni mwa magonjwa ya kurithi ingawa sababu zake bado hazijulikani kitaalamu,