The Cotex Medicine

The Cotex Medicine Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from The Cotex Medicine, Medical Center, Morogoro.

The Cotex Medicine (the centre for Cure Coaching and Rehabilitation) ni kituo kinachotoa ushauri, usimamizi na mapendekezo juu za afya za wagonjwa wa moyo, presha na matatizo mengine ya kiafya.

27/05/2025
We are Active.Call/sms/whatsaap 0678640098
29/04/2024

We are Active.

Call/sms/whatsaap 0678640098

*Dawa Si Kila Kitu Kwenye Matibabu,Dawa Ni Sehemu Ya Matibabu.* Dawa si kila kitu kwenye Matibabu,dawa ni sehemu ya Mati...
23/04/2023

*Dawa Si Kila Kitu Kwenye Matibabu,Dawa Ni Sehemu Ya Matibabu.*

Dawa si kila kitu kwenye Matibabu,dawa ni sehemu ya Matibabu.
Usishikirie na kuikumbatia dawa usiku na mchana na kuacha kufuata utaratibu sahihi wa kula na kunywa kuendana na hali yako.

Mara nyingi Magonjwa yanayochangiwa na mfumo wa chakula,yanahitaji dawa na yanahitaji pia uangalifu mzuri pindi unatumia hiyo dawa.

Kufuata utaratibu sahihi wa kula na kunywa wakati wa kutumia dawa ina faida nyingi, ikiwa ni pamoja na:

*1.Kuhakikisha ufanisi wa dawa:*

Kufuata maagizo ya daktari wako juu ya jinsi ya kula na kunywa wakati unatumia dawa husaidia kuhakikisha kuwa unapata faida kamili ya matibabu yako. Hii ina maanisha kuwa dawa ina nafasi ya kufanya kazi vizuri zaidi ikiwa ulaji wako utaendana na hali yako.

*2.Kuongeza uwezekano wa dawa kukupatia matokeo:*

Kufuata maagizo ya daktari wako kwenye ulaji kutakuepusha na vyakula ambavyo haviendani na dawa unayotumia na ambavyo vinaweza kupunguza ufanisi wa dawa au kufanya dawa isifanye kazi kabisaa.

*3. Kuongeza uhakika wa matibabu:*

Kufuata utaratibu sahihi wa kula na kunywa wakati wa kutumia dawa husaidia kuongeza uhakika wa matibabu yako na kurahisisha safari yako ya kupona.

*4. Kukuepusha na upoteza pesa:*

Kufuata maagizo ya daktari wako kunaweza kusaidia kuzuia upotevu wa pesa.Hii hutokea pale ambapo mtu ametumia dawa bila kufuata utaratibu sahihi wa kula na kunywa na hatimae dawa kutokumpatia matokeo sahihi.

*5. Kupunguza hatari ya kurudia matibabu:*

Kufuata utaratibu sahihi wa kula na kunywa wakati wa kutumia dawa kunaweza kupunguza hatari ya kurudia matibabu. Hii inamaanisha kuwa unapunguza hatari ya kusumbuliwa na tatizo lako la kiafya tena baada ya kupona.

Kwa ujumla, kufuata utaratibu sahihi wa kula na kunywa wakati wa kutumia dawa ni muhimu sana kwa afya yako na usalama wa matibabu yako. Ni muhimu kuzingatia maagizo ya daktari wako ili kuhakikisha kuwa unapata faida kamili ya matibabu yako.

Call/sms/WhatsApp
0678640098

*VISABABISHI VYA MAGONJWA YA MOYO NA PRESHA(CAUSES OF CARDIOVASCULAR DISEASES& BLOOD PRESSURE)*Visababishi vya magonjwa ...
17/04/2023

*VISABABISHI VYA MAGONJWA YA MOYO NA PRESHA(CAUSES OF CARDIOVASCULAR DISEASES& BLOOD PRESSURE)*

Visababishi vya magonjwa ya moyo na presha ni pamoja na:

1.🖇️ *Ulaji usio sahihi:* Kula vyakula vyenye mafuta mengi yasiyofaa, sukari nyingi(vyakula vya wanga) na chumvi kunaweza kusababisha shinikizo la damu na kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo.

2.🖇️ *Kutofanya mazoezi ya kutosha:* Kutofanya mazoezi ya kutosha kunaweza kusababisha unene kupita kiasi, shinikizo la damu na hatari ya magonjwa ya moyo.

3.🖇️ *Uvutaji wa sigara:* Uvutaji wa sigara unaweza kusababisha uharibifu wa mishipa ya damu na kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo.

4.🖇️ *Matumizi ya pombe:* Matumizi ya pombe kupita kiasi kunaweza kusababisha shinikizo la damu na kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo.

5.🖇️ *Msongo wa mawazo:* Msongo wa mawazo unaweza kuathiri afya ya moyo na kusababisha shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.

6.🖇️ *Ugonjwa wa kisukari:* Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababisha uharibifu wa mishipa ya damu na kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo.

7.🖇️ *Historia ya familia:* K**a kuna historia ya magonjwa ya moyo katika familia yako, hatari yako ya kupata magonjwa ya moyo inaweza kuwa kubwa zaidi.

Nutr Sood
+255 678640098
Morogoro mjini & Ilala Dsm.
*TANZANIA.*

*DALILI ZA MAGONJWA YA MOYO NA PRESHA (CARDIOVASCULAR DISEASES& BLOOD PRESSURE)*⚫Dalili za magonjwa ya moyo hutofautiana...
17/04/2023

*DALILI ZA MAGONJWA YA MOYO NA PRESHA (CARDIOVASCULAR DISEASES& BLOOD PRESSURE)*

⚫Dalili za magonjwa ya moyo hutofautiana kulingana na aina ya ugonjwa wa moyo,ukubwa wa tatizo na mtu husika kwa ujumla.
Baadhi ya dalili za kawaida ni:

1.🖇️ *Maumivu au kubana kifuani:* Hii ni dalili ya kawaida zaidi ya magonjwa ya moyo na inaweza kuhisi k**a shinikizo, kubana au msukumo katika kifua.

2.🖇️ *Kupumua kwa shida:* Kupata shida ya kupumua au kuhisi k**a huwezi kupata pumzi, hasa wakati wa shughuli za kimwili au hata wakati wa kupumzika.

3.🖇️ *Uchovu:* Kuhisi uchovu au udhaifu, hata baada ya kupumzika vya kutosha.

4.🖇️ *Kizunguzungu au kuhisi kichwa kuenda mduara:* Kuhisi kizunguzungu au kuona vumbi, hasa unaposimama au unapojitahidi.

5.🖇️ *Kuvimba miguu, vifundo vya miguu au miguu:* Kujaa maji mwilini kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi vizuri kunaweza kusababisha uvimbe katika viungo vya chini.

6.🖇️ *Moyo kupiga kasi au kutokuwa na mpangilio:* Hali ya moyo kupiga haraka au kutokuwa na mpangilio.

7.🖇️ *Kichefuchefu, matatizo ya tumbo au maumivu ya tumbo:* Dalili hizi zinaweza kutokea wakati wa shambulio la moyo, hasa kwa wanawake.

8.🖇️ *Jasho baridi:* Kutokea kwa jasho ghafla ambalo si kwa sababu ya mazoezi au joto.

9.🖇️ *Maumivu sehemu nyingine za mwili:* Maumivu au kubana katika mikono, shingo, taya, mgongo au tumbo pia inaweza kuwa dalili ya shambulio la moyo.

*CHUKUA HATUA MAPEMA*

Nutr Sood
+255 678640098
Morogoro mjini & Ilala Dsm
TANZANIA.

*HATUA ZA KUFUATA KUZUIA NA KUTIBU MAGONJWA YA MOYO*1.🖇️ *Kupunguza uzito na kula lishe bora:* Kupunguza uzito kupitia m...
16/04/2023

*HATUA ZA KUFUATA KUZUIA NA KUTIBU MAGONJWA YA MOYO*

1.🖇️ *Kupunguza uzito na kula lishe bora:* Kupunguza uzito kupitia mazoezi na kula lishe bora inaweza kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo. Lishe bora ni kuachana kabisa na wanga ikiwa tayar una tatzo na k**a bado haujawa na tatzo basi dhibit kwa kupunguza kabsa matumizi ya wanga na k**a huna bas tumia wanga ambao haujakobolewa,matunda na sio juice ya matunda nk

2.🖇️ *Kufanya mazoezi ya mara kwa mara:* Mazoezi ya mara kwa mara yanaweza kuboresha afya ya moyo na kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.

3.🖇️ *Kuacha uvutaji wa sigara:* Kuacha uvutaji wa sigara ni hatua muhimu katika kuzuia magonjwa ya moyo.

4.🖇️ *Kupunguza/kuacha matumizi ya pombe:* Kupunguza/kuacha matumizi ya pombe kunaweza kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.

5.🖇️ *Kudhibiti shinikizo la damu:* Kudhibiti shinikizo la damu ni muhimu katika kuzuia magonjwa ya moyo.

6.🖇️ *Kudhibiti kisukari:* Kudhibiti kisukari ni muhimu katika kuzuia uharibifu wa mishipa ya damu na magonjwa ya moyo.

7.🖇️ *Matibabu ya dawa:* Daktari anaweza kuagiza dawa za kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo au kudhibiti hali zinazosababisha magonjwa hayo.(NAKUSHAURI KUPATA DAWA MBILI ZA ASILI KATIKA MATIBABU YA MOYO YAANI *CARDIOMEGAL & CARDIAC SOLUTION)* Ni dawa nzuri sana zenye kutibu kabisa magonjwa ya moyo ikiwa mgonjwa atazingatia maelekezo.

8.🖇️ *Upasuaji:* Katika hali mbaya, upasuaji unaweza kuwa muhimu katika kutibu magonjwa ya moyo *(Usisubiri kufikia hatua hii kwani ni hatua mbaya sana)*

Nutr Sood
*+255 678640098*
Morogoro &Ilala Dsm
*TANZANIA*

Kila nikiamka asubuhi miguu inavimba Ila baada ya masaa 3 hadi manne miguu inarudi kwenye hali yake?Hii hali inajirudia ...
10/04/2023

Kila nikiamka asubuhi miguu inavimba Ila baada ya masaa 3 hadi manne miguu inarudi kwenye hali yake?

Hii hali inajirudia kila asubuhi nikiamka, inaweza kuwa inachangiwa na nini,zipi ni sababu zake?

Sababu kuu ya uvimbe wa miguu kuwa mbaya zaidi usiku ni kwa sababu ya mvutano wa graviti. Wakati wa siku, mvutano wa graviti unavuta maji na damu kuelekea chini ya miguu. Lakini wakati wa usiku, wakati tunalala na miguu yetu iko sawa, mvutano wa graviti unaruhusu maji na damu kukaa katika miguu kwa muda mrefu zaidi, ambayo inasababisha uvimbe kuwa mbaya zaidi. Wakati tunapoamka na kuanza kutembea, shinikizo la miguu yetu linasaidia kusukuma maji na damu kurudi kwenye moyo na mfumo wa limfu, ambayo inapunguza uvimbe.

Kuvimba kwa miguu mara nyingi hutokea kwa sababu ya kuziba kwa damu au maji katika tishu za miguu. Sababu za kawaida za uvimbe wa miguu ni pamoja na:

1. Kukaa kwa muda mrefu sana: Kukaa kwa muda mrefu sana bila kusimama au kutembea kunaweza kusababisha uvimbe wa miguu.

2. Upungufu wa maji mwilini: Upungufu wa maji mwilini unaweza kusababisha uvimbe wa miguu.

3. Matumizi ya dawa: Baadhi ya dawa k**a vile dawa za shinikizo la damu, dawa za homoni, na dawa za maumivu zinaweza kusababisha uvimbe wa miguu.

4. Magonjwa: Magonjwa k**a vile ugonjwa wa figo, ugonjwa wa moyo, na ugonjwa wa ini yanaweza kusababisha uvimbe wa miguu.

5. Ujauzito: Uvimbe wa miguu ni kawaida wakati wa ujauzito, hasa katika miezi ya mwisho.

Ni muhimu kupata ushauri wa matibabu ikiwa uvimbe wa miguu unaendelea kuwepo kwa muda mrefu au unaambatana na dalili zingine k**a vile maumivu, joto, na rangi nyekundu au nyeusi.

Call/sms/WhatsApp
Nutr Sood
0678640098

Tiba Ya Pumu(Asthma).Dawa hii ni maalum kwa wenye changamoto ya pumu wakike kwa wakiume. *Mahitaji.*1.Tangawizi vijiko 4...
05/11/2022

Tiba Ya Pumu(Asthma).

Dawa hii ni maalum kwa wenye changamoto ya pumu wakike kwa wakiume.

*Mahitaji.*

1.Tangawizi vijiko 4
2.Uwatu vijiko 2
3.Mdalasini vijiko 4
4.Karafuu kijiko 1
5.Asali nusu Lita.

*Maandalizi.*

-Hakikisha dawa zote ziko katika unga, changamoto mchanganyiko huo kwenye nusu Lita ya asali.

-Koroga vizuri ili kuhakikisha mchanganyiko umechanganyika vizuri.

*Matumizi.*

-Chukua kijiko kutoka kwenye mchanganyiko wa asali na tumia kwa asubuhi,chukua kingine tumia mchana na kingine tumia kwa usiku.

*Note.*

Kijiko hiki ni kijiko kikubwa cha chakula.
Itumie dawa ipasavyo na kheri itapatikana.

Wako,

*Nutr.Sood*
0678640098.

23/09/2022

Jizoeshe Utaratibu Huu, Utaratibu Huu Utakusaidia Kupunguza Uzito Mkubwa/Kilo nyingi/Kitambi/Obese.

⤵️⤵️⤵️

➡️Jiwekee utaratibu wa kuruka kamba 500 hadi 600 kwa siku.

➡️Achana na vitu vyenye kuandaliwa kwa mafuta au sukari nyingi k**a maandazi,vitumbua au chapati.Badala yake tumia chai ya kijani au maziwa yasiyo na mafuta (skim milk/fat free milk) na ulaji wa vyakula vilivyoandaliwa kwa kuchemshwa au kuokwa k**a ndizi za kuchemsha au magimbi.

➡️ Asubuhi push up 15 hadi 20 na jioni pia

➡️Kula matunda na mboga mboga zaidi.

➡️Shughulisha mwili wako kwa kutembea hatua 500 au zaidi.

➡️ Punguza matumizi na ulaji wa vyakula vya wanga, punguza ulaji wa ugali wali viazi ndizi mihogo tambi n.k.Jazia mlo wako kwa kula mboga mboga na matunda zaidi,mboga zaidi k**a maharage kunde au samaki.

➡️Ikiwa we ni mpenzi wa supu,tumia supu itokayo na vyanzo vya baharini k**a supu ya samaki n.k

➡️Tumia lita moja ya maji kila asubuhi,maji ambayo umeweka ndimu kidogo au umekamulia limao.

➡️Kula mlo wako wa usiku kwa utofauti wa masaa 4 hadi 5 kabla ya kulala na ikiwa kanuni hii itakuwa ngumu kuifikia kula matunda na mboga mboga k**a mlo wako wa siku muda wowote kabla ya kulala.

➡️ Epuka matumizi ya pombe,sigara,soft drinks,kahawa/chai ya rangi n.k

➡️Pata wasaa mzuri wa kulala na kupumzika.

Note:

Ukitaka kubadilika,yakupasa ubadilishe utaratibu wako wa awali na uanze utaratibu mpya.Hakuna kazi rahisi kwenye uwanja wa vita.

Usiseme huoni mabadiliko huku bado hujaweza kuacha Yale yaliyokufanya uwe na kilo nyingi au uzito mkubwa.

For more clarification,

Nutr Sood
Call 0678640098

Address

Morogoro

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Cotex Medicine posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to The Cotex Medicine:

Share

Category