03/04/2022
*NILICHOKITHIBITISHA KWENYE NDOA Miezi 6*
*Kuna kitu nimekuja kukihakikisha kwenye ndoa, hichi kitu bhana alinambiaga mentor wangu M***a Suleiman enzi hizo nikiwa single wakati ule sikumwelewa lakini saizi ndio namwelewa...
Sasa from experience ya ndoa ya miezi 6 ngoja nishuhudie kitu, hapa nataka kuongea na Wanawake wenye bonge za ndoto walioolewa na wanaotarajia kuolewaga....
Maana ya kuwa mke ni kuwa msaidizi na sio hivyo tu Biblia inasema Waefeso 5:22"Enyi wake watiini waume zenu k**a kumtii Bwana wetu.23:Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe,k**a Kristo naye ni kichwa cha kanisa, naye ni mwokozi wa mwili. (English version inasema"Wives, submit to your own husband,as to the Lord." Hapa nilitaka tu hili Neno "Submit"neno submit limetokana na Neno "Submission"
Hili neno submit kwa namna nyingine tunaweza sema "Wives understand and support your husband in ways that show your support for Christ"
Submit iliyoelezewa Kwa Kiswahili Kwa maana ya kutii ina maana nyingi.
Kutii haimaanishi kuheshimu tu,bali ina upana mkubwa Sana unaobeba uhalisia wa mume Kwa ujumla.
Sasa hapa mimi katika kusoma soma na kutafakari nikagundua Submission ndani yake ina maana ya "submit your vision, under his vision"
Ili mwanamke uendane na kusudi la Mungu la Ndoa,
Ili ndoa yako iwe na Amani,
Ili Ndoa yako ibarikiwe,
Ili uendelee kutimiza ndoto zako hata kwenye ndoa( maana hapa kuna wanaosema Mimi siolewi, maana nikiolewa ndoto zangu zitakufa. Hii hata Mimi nilikuwa nayo.
Yani nilikua na ndoto hizo jamani😄mpaka nyingine kuziongea tu zinaweza kukuangusha chini, sijui nifungue mashule, makampuni, mahotel, nawaza ndoto zangu, nikiolewa zitakufa, nilikua naangalia walioolewa wakiwa Moto baada ya ndoa wakazima ghafla, nikajisemea siunaona fulani,fulani kumbe nilikuwa na mawazo mgando,)
Sikuzote napenda kusema *Ukimjua Mungu atakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea atakushauri jicho lake likikutazama* Mungu si akaanza kunifundisha na sio tu kunifundisha alininyoosha haswa mpaka yale mawazo yangu ya alinacha yakayeyuka, akanipondaponda akanifanya k**a atakavyo Yeye lakini ni baada ya Kumwambia BABA nimefika mwisho wa akili zangu naomba akili zako🙇♀️🙌🏽 )
Nikaja kugundua sio kwamba vinakufa lakini ni wao hawajaelewa maana ya Submission k**a mke ndani ya ndoa, hasa ukitaka kuishi katika ndoa ya Kusudi la Mungu.
Nikagundua tena kumbe ndio maana ndoa nyingi za Leo zina migogoro na talaka,yani kila kukicha talaka, mpaka mahusiano tu sikuizi yana talaka🙆🏻♂️.
Hii inatokana na mfano k**a huu, utamkuta mwanamke anaingia kwenye ndoa na ndoto zake/ huduma na anataka asimamie ndoto zake tuu asiambiwe kitu kingine, na mwanaume ukimwambia kitu utasikia niache nina ndoto zangu, my dear hapa utalia sana na hakuna siku hiyo ndoto itatimia na mwisho wa siku utaishia kupigwa vibuti.
Hujawahi kuona mtu ameolewa ana huduma/kipaji mwisho ndoa inamshinda??
*Sasa tuendelee kwenye submission*
Ili Ndoa yako iwe Sawa na vile tulivyoviona pale juu ikiwemo ndoto zako mwanamke kutimia ni lazima ukubali kusubmit vision/ndoto zako chini ya vision za mume wako.
Kivipi???
Ni Rahisi sana, Ukishajua mume wako ana vision gani, hakikisha unaisimamia vision yake kwa kuchomeka vision yako ndani yake mpaka vision/ndoto zake zitimie.
Kumbuka Mwanzo Mungu alipomuumba Adamu alimpa Kazi ya kufanya, kazi Mungu aliyompa Adamu ndio vision yenyewe, Mungu akaona Adamu pekee hatoweza kuikamilisha vision hiyo ni lazima amfanyie msaidizi wa kumsaidia kuitimiza.
Ndipo akamuumba mwanamke.
Wakati Mungu anamuumba mwanamke alimpa vifaa vyote(equipments) za kuhakikisha maono ya Mungu kwa Adamu yanatimia, mfano kuna (enqubation ability, hichi ni kifaa mojawapo walichopewa wanawake chenye nguvu na Uwezo wa kuatamia ndoto/maono ya mume,watoto, yakwake mpaka yatimie)
*Kuna kitabu kimoja nakiandika ni bonge ya kitabu kwa wanandoa✍🏼hasa Wanawake..stay tuned*
Sasa turudi kwetu, waume zetu wamepewa maono na MUNGU na Sisi ndio wenye vifaa vya kukamilisha maono hayo, ikitokea mwanamke umeligundua hili nakuhakikishia utakuwa na ndoa ya baraka na mfano duniani na Mbinguni.
Cha kufanya mwanamke, yale maono yako uliyokuwa nayo tokea ukiwa single ukiolewa hakikisha unayasubmit kwenye maono ya mumeo sio uyaache hapana, nakupa mbinu hapa👇🏼
*Simamia,Fanya, Pambania,Ombea, Tia moyo, sisitiza, wekeza nguvu, muda wako,akili yako Kwa maono ya mume wako*
Nakuhakikishia ukipambania maono ya mume wako yakatimia, yakwako yanakuwa yameshatimia automatically yani pasipo hata kutumia nguvu.
Mimi nimeanza kuiishi hii baada tu ya kuolewa, na nimejikuta kuna vingine vizuri zaidi vinaongezeka kwenye maono yangu, kuna vitu mume wangu ananiambia tufanye ambavyo ndio Vilevile vilivyokuwa ndoto zangu na nguvu imekuwa kubwa kuliko ambavyo ningepambana mwenyewe lakini hii ni baada tu ya kukubali kusubmit my vision under his vision. Kitu ambacho nisingesubmit ningebaki palepale na kudumaa na huenda hayo mandoto yangu yasingekaa yatimie.
"Make your man's vision shine and your vision will shine automatically"
*Mwisho*
Nikwambie bonge la Siri
Hakuna kitu kinamshinda Mzee wa Siku nikmaanisha Mungu, Jamani Mungu anabadilisha, Mungu anaweza kufanya mambo ambayo akili zetu zilishafikaga mwisho.
Na kingine hakuna ndoa ngumu, hakuna mwanaume mkorofi, hakuna mwanamke mbabe mbele ya huyu Mwamba💪🏼, wewe mpeleke tu mbele zake uone.
*USHUHUDA WANGU*
Jamani hakuna mtu alikuwa mkorofi, mbabe na mjeuri hasa kwenye mahusiano k**a Mimi, Kwa nje ulikua ukiniona hutaamini.
Yaani tunaweza ingia kwenye mahusiano asubuhi na mchana tukaachana🙄
Ilikuwa ni Mimi na misimamo yangu ninachokitaka Mimi ndio kitafuatwa, ukileta mchezo hasa ukiingia kwenye 19 za ndoto zangu yaani hutaamini.
Yaani utanikosea wewe msamahaa utaomba wewe na kuachana naanza mimi🙆🏻♂️.
Ulifika wakati nikaona mahusiano yananichelewesha kwenye ndoto zangu, nikafunga ukurasa huo na sio tu nilifunga ukurasa wa mahusiano Bali nilifunga mpaka wa ndoa, nikasema sitaki kabisa kuolewa maana nikiolewa ndoto zangu zitakufa🙄.
Nilikua nikiwaza mwanaume gani atanioa Mimi maaana ukorofi ule nilikuwa namuonea huruma sana, nikasema labda nipate mwanaume mkali, mbabe, mkorofi zaidi yangu tofauti na hapo ningekuja piga mtoto wa watu afu nivunjwe mbavu bure😨maana ukorofi gunia mwili sindano😄.
*Lakini nilipotaka na kutafuta kumjua sanaaa Mungu maana nilikua namjua lakini siyo Ile aliyosema yeye sanaa,Ile ya kushuka mpaka mavumbini, kunyenyekea mbele zake,kuwa si kitu kabisa mbele zake, Ile ya kupungua haswa na Mungu aongezeke sana Kwa maisha yako* nikamwambia BABA naomba unifinyange unifanye k**a utakavyo wewe nikasurrender🙇♀️🙌🏽mbele zake.
Kweli Mungu ni mwaminifu sana kwa wale wamtafutao Kwa bidii ni lazima aonekane, Mungu akaingila Kati maisha yangu akashuka Yeye mzima mzima🙌🏽🙌🏽hakusema hata amtume malaika, Mungu akaninyoosha haswaaa, akanipondaponda akanifanya k**a atakavyo Yeye, akaniondolea ukorofi wote, ubabe, misimamo ya hovyoo, sijui ndoto za mavitu gani sijui magari, manyumba, makampuni kwamba niyapate kwanza haya ndio niolewe tofauti na hapo nilikuwa nasema siolewi.
Wakati Mungu ananifundisha alinibananishaga kwenye Kona hiyo sitasahau na akanambia
"Winnie mwanangu hivyo unavyovitaka hutokaa uvipate mpaka utakapoolewa, Akaendelea kuniambia si unaona unavyopambana na hakuna ulichopata, kanambia Kwa jinsi ulivyo na juhudi usingekuwa mtu wa kukosa hata kagari wala kanyumba lakini vyote hivyo sikupi maana nikikupa hutowaza kabisa kuolewa na ujeuri utaongezeka na ili kusudi langu kwako litimilike na kile nilichoweka ndani yako kiwe chenye Utukufu wangu ni lazima uolewe.
Akaendelea kuniambia nakuahaidi hivi unavyovitaka siku ukiolewa utavipata na zaidi maana ulivyonavyo akilini mwako ni tuvitu tudogo saaaanaa kuliko vile nilivyoweka mbele yako ukiwa na familia.
Mfano wa kwanza akanioneshea, kweli nilivyoinua mikono nikasema Baba nakubali🙌🏽 kufuata ratiba yako, nikamkubali kijana aliyemleta kwangu wakati ule, nikashangaa🙄lile gari langu nilikuwa nimelichora kichwani Mungu siakampa huyo jamaa🤨
Sijakaa sawa process za ndoa zikaanza, Ile nyumba yangu iliyokuwa kwenye ndoto zangu ikamdondokea tena huyo jamaaa🤨, nikasema kweli Mungu ni hatari🙌🏽🙌🏽
Nikakubal ndoa ikafungwa baada ya ndoa tukahamia kwetu, Mungu kanikumbusha unaona uliyokuwa unapambana mwenyewe ungezeekea kwenu pasipo baiskeli wala banda la kuku🙆🏻♂️.
(Hii ni kwangu sisemi masingle ladies msinunue magari wala kujenga nyumba, mkiweza jengeni haswaa lakini k**a ratiba ya Mungu inataka tofauti lazima usarende).
Sasa juzi hapo nilikuwa naenda kanisani bodaboda akachelewa kunifuata, nikakasirika kweli😣
Nikasikia sauti ndani ikiniambia "yaani wewe siulikuwa unalilia gari haya leo gari imepack hapo huna hata mpango nayo, ona Sasa ivi unavyoiona ya kawaida!kitu kidogo hivi ndio kilikuwa kinakufunga usifikilie hatima alizokuandalia Mungu?? !
*Mungu akanifundisha kitu kikubwa Sana hapa, kwamba tunakuwa na vijimipango vyetu ambavyo vinatufunga kufikilia makusudi yake makubwa Sana hasa mabinti/Wanawake kumbe Mungu katuandalia mabonge ya mipango ni sisi tu kumwambia Mungu nataka kutembea kwenye mipango yako🙌🏽 niongoze Baba.*
Turudi baada ya ndoa Sasa,baada ya kukubali kufuata ratiba ya Mungu, niulize leo zile ndoto zangu naziona kumbe vilikuwa vijindoto tu, kuna mabonge ya mindoto bhana na mavision ukitembea kwenye mipango ya Mzee wa Siku🙌🏽
Yaani tena hiyo mindoto mnaijadili wawili kila mmoja anaweka point mezani mkianza kuitekeleza acha kabisa huwa ni kutelezaa tuuu. Hapa ndipo nilithibitisha kumbe ni haikika na kweli Ndoa ni Kusudi halisi na kuu Sana la Mungu Kwa maisha yetu.
Na uzuri mmoja mkijua Sana Mungu yaani anawaambia kabisa hapa wanangu fanyeni hivi na anakupa mtu ambaye mtaendana hata kimandoto unashangaa mume anakuambia Kwa ukubwa wa hili mke wangu hapa tuweke ghorofa kitu wewe uliwaza room moja na store😄.
Mabinti, Wanawake, Wanaume tujifunze Kumkabidhi Mungu njia zetu na mawazo yetu yatathibitika tukaze Sana kumjua Yeye ili atufundishe na kutuonesha njia tutakazoziendea atatushauri jicho lake likikutazama🙌🏽🙌🏽🙌🏽
*FOR GOD'S GLORY*