
28/03/2021
*KARIBUNI wadau tuangalie kwa ufupi jambo hili.* UTOKAJI WA MAJIMAJI UKENI 👉Tezi zilizo ukeni hutengeneza maji maji. Majimaji haya hutiririka kila siku na kutoka nje ya mwili. Majimaji toka ukeni huchukua seli zilizokufa na bacteria na kuzitoa nje ya mwili kila siku. Hii ni njia mojawapo ya kusafisha na kutunza via vyako vya uzazi kila siku. Yanaweza kuwa maji maji yasiyo na rangi au yenye rangi ya maziwa lakini yasiyo na harufu yoyote. Kiwango na rangi ya maji maji yatokayo ukeni hutofautiana kulingana na mzunguko wako wa kila mwezi.👉Ukiwa na hisia za kufanya mapenzi maji maji mazito hivi hutoka. Lakini pia 👉wakati unanyonyesha na wakati wa hedhi kiwango na rangi huweza kuwa tofauti. 👉HITIMISHO Mwanamke yeyote endapo atatoka majimaji ukeni ambayo hayana harufu wala muwasho, hilo siyo tatizo na maambukizi, ni mabadiliko tu ya mwili.ILA K**a utokaji huo huambatana na muwasho na dalili zingine ni vyema kutafuta matibabu haraka.
zungumza nasi