
18/04/2022
Nimeishi na mke wangu na kuzaa nae watoto watatu, wakiume 2 na wakime 1. Tulipendana Sana na tulikuwa tukiishi kwa amani na upendo. Baada ya ukaguzi wa serikali kuhusiana na vyeti nilisimamishwa kazi kwa kuonekana nilifoji cheti cha form 4. Ukweli ni kwamba cheti changu kilitumiwa na ndugu yangu kuombea ajira kwenye Taasisi fulani na hapo ndipo niliposimamishwa kazi nakutakiwa nilete cheti original cha form 4. Wakati naendelea kufuatilia cheti ambacho kilikuwa kwa wazazi wangu ilemela jijini mwanza, Mke wangu alibadilika Sana na kuanza kunidharau. Hali ya maisha kwa miezi kadhaa ilikuwa ngumu sana kiasi cha kuwa na madeni mtaani. Mke wangu alinikimbia na kuacha watoto ambao kwa wakati huo walikuwa wakimuhitaji Sana. Nilipambana na watoto wangu na kwa bahati nzuri niliweza kurudishwa kazini baada ya miezi sita. Nililipa madeni ya watu na Karo za watoto wangu. Wakati huo mke wangu alianzisha mahusiano na jamaaa mwingine na akapewa uja uzito. Huyo jamaa ameukana ujauzito na kumtimua nyumbani kwake. Mke wangu amenipigia simu na kuniomba radhi nimemkatalia na kumwambia anipe muda. Kinachonishangaza juzi ameniripoti Dawati la jinsia kuwa nimetelekeza familia ikiwemo kumfukuza yeye na anadai watoto wake ambao yeye mwenyewe ndie alie waacha na kwenda kuanzisha maisha mengine.