25/05/2024
Je, hapa ndo wengi tunapokosea kwenye kudhibiti kisukari kwa vyakula?
Lengo la kuandika kitabu hiki ni kusaidia wagonjwa kudhibiti kisukari kwa kuwapa maarifa na muongozo wa lishe bora.
Lishe bora husaidia kudhibiti kisukari na kuboresha afya ya moyo na mishipa ya damu.
Wagonjwa wengi wamekuwa wakipata tabu kwasababu wafundishaji tumekuwa tukisisitiza sana kuhusu virutubisho vilivyomoโฆtunafundisha kula virutubisho, wakati mtu hula vyakula.. Tunakubaliana kwamba protini, wanga, madini, vitamini ni virutubisho muhimu kwa mtu kufahamu.
Je, kusisitiza kuhusu virutubisho tu badala ya vyakula tunavyokula katika mazingira yetu ya kila siku kuna shida? Kujibu swali hili nitakupa mfano, waelimishaji tumekuwa tukisisitiza kwa mfano usile vyakula vya wanga badala yake endelea kula vyakula vya protini k**a maharage.
Siku mtu ukifahamu kuwa maharage pia yana wanga unapata shida kwa sababu unachanganyikiwa namna ya kupanga chakula chako.
Hapa ndo pale unaposikia watu wakisema, huwenda si wewe, madaktari bana kila kitu wanasema usile! Na hapa ndipo unakuja umuhimu wa kitabu hiki.
Nimehakikisha kukuelekeza kwa kuzingatia maisha yetu ya uhalisia. Nimezingatia kwamba k**a nilivyo mimi, na wewe pia mwanzo huona aina ya chakula na si kirutubisho kilichomo ndani yake. Yani kabla hujaona protini, umeona nyama.
Kufahamu virutubisho vilivyomo kwenye chakula ni vizuri na unapata manufaa mengi. Lakini, ni rahisi kuelewa na kupanga mlo wako kwa kutumia uhalisia kwa sababu kuu tatu.
ukweli usiopingika kwamba tunapokwenda sokoni tunalenga kununua mchicha na si Vitamin A na pia tunanunua nyama tunapo kwenda buchani badala ya kusema nakwenda kununua protini.
Kiwango cha virutubisho hutofautiana kutokana na aina ya vyakula mtu alavyo, lakini ya tatu na ya muhimu zaidi ni kwamba,
Vyakula karibia vyote huwa na aina tofauti ya virutubisho. Namaanisha kwa mfano maharage yana protini, wanga na mafuta na vitamini mbalimbali vilevile muhindi una wanga, mafuta na protini na vitamini mbalimbali.
Nidyo maana tunaamini kwa kurahisisha kuandika kitabu kwa kuzingatia maisha yetu ya kila siku tunaweza kukusaidia msomaji kufahamu kwa uhakika na kuweza kupanga bila hofu aina ya mlo unaoutaka ili kuweza kuboresha afya yako bila kuathiri kiwango chako cha sukari.
Kitabu hiki kitakusaidia wewe na wengine pamoja na mimi pia k**a rejea. Katika kitabu hiki tumezingatia makundi yote ya vyakula ambavyo wewe na mimi tunakula: nafaka (ugali, wali, makande, maharage nk), mboga za majani, mchicha, spinachi, tembele; matunda, nyama, na maziwa.
๐Pata kopi yako leo kwa bei ya offer:
Umeacha vyakula uvipendavyo kufuata masharti lakini bado hujaweza kudhibiti kisukari? Nina habari ni njema kwano...