Afyaclass-Afya/Uzazi

Afyaclass-Afya/Uzazi Karibu kwenye Official Page ya Afyaclass,Upate Ushauri,Elimu na Tiba juu ya Magonjwa mbali mbali,Pamo

11/12/2022
UCHOMAJI WA SINDANO YA ANTI-D(Rho) KWA MAMA MJAMZITO NA MAMA BAADA YA KUJIFUNGUABaada ya mama mjamzito kuanza Kliniki na...
10/12/2022

UCHOMAJI WA SINDANO YA ANTI-D(Rho) KWA MAMA MJAMZITO NA MAMA BAADA YA KUJIFUNGUA

Baada ya mama mjamzito kuanza Kliniki na kupima group la Damu,moja ya vitu vikubwa ambavyo wataalam wa afya huangalia ni pamoja na Rhesus factor ya mama na baba,ambapo huweza kuwa POSITIVE au NEGATIVE,mfano kwenye makundi ya damu utaona yameandikwa hivi; A+ au A-, B+ au B-, AB+ au AB-, O+ au O-, hizo positive na negative ndyo tunasema Rhesus factors.

Sasa basi, endapo Baba ana kundi lolote la damu Rhesus factor positive mfano; A+,B+,AB+ au O+, na mama mjamzito akawa na kundi lolote la damu rhesus factor negative mfano; A-,B-,AB- au O-, hapa tayari kuna tatizo,

Mama huyu mjamzito yupo kwenye hatari ya kupatwa na matatizo k**a vile; mimba kutoka zenyewe au kuzaa mtoto mwenye matatizo k**a vile kukosa hewa ya oxygen kwenye ubongo,mtoto kuishiwa na damu,mtoto kufariki muda mfupi baada ya kuzaliwa pamoja na matatizo mengine yanayohusu damu yaani hemolytic diseases hasa kwenye ujauzito wake wa pili.

Sasa kutokana na matatizo hayo,ndipo swala la kutumia sindano za Anti-D linapoanza ili kumsaidia mama huyu pamoja na ujauzito wake aliyobeba kumkinga na matatizo hayo.

INAENDELEA.. Google Website Afyaclass,Kisha Search Title hii hapa chini

UCHOMAJI WA SINDANO YA ANTI-D(Rho) KWA MAMA MJAMZITO NA MAMA BAADA YA KUJIFUNGUA

Wanawake wengi baada ya kujifungua husubiri kwanza waone hedhi ndipo waanze kuchukua tahadhari ya kujikinga na Mimba,Kum...
09/12/2022

Wanawake wengi baada ya kujifungua husubiri kwanza waone hedhi ndipo waanze kuchukua tahadhari ya kujikinga na Mimba,

Kumbuka hedhi ni matokeo ya kutokuwa na urutubishaji wa Yai, endapo yai limerutubishwa huwezi ona hedhi k**a ulivyokuwa unasubiria ndipo uanze kujikinga,

Hii imepelekea wanawake wengi kubeba mimba ambazo hazijapangwa baada ya kujifungua,

Una mimba nyingine na huku bado unanyonyesha,

JIKINGE NA MIMBA AMBAZO ZIPO NJE YA MPANGO

Kipanda uso(Migraine) ni tatizo ambalo huhusisha mtu kupatwa na maumivu makali sana ya kichwa ambayo hutokana na sababu ...
12/11/2022

Kipanda uso(Migraine) ni tatizo ambalo huhusisha mtu kupatwa na maumivu makali sana ya kichwa ambayo hutokana na sababu mbali mbali k**a vile;

hali ya kutanuka kwa mishipa ya damu kichwani k**a vile mishipa aina ya Artery,

mabadiliko ya mfumo wa damu yaani Blood stream na mabadiliko ya vichocheo k**a vile; kichocheo aina ya Serotonin ambacho huhusika na kudhibiti kiwango cha maumivu kwenye mfumo wa fahamu.

Vyote hivi huchangiwa na sababu mbali mbali k**a vile;

✓ Mtu kuwa na msongo wa mawazo

✓ Matumizi ya pombe kali kupita kiasi

✓ Kunywa vinywaji vyenye caffeine nyingi k**a kahawa N.k

✓ Kukosa muda wa kutosha wa kulala

✓ Matumizi ya dawa mbali mbali k**a vile; vidonge vya uzazi wa mpango n.k

✓ mabadiliko ya hali ya hewa mfano; Kuwa na jua kali pamoja na joto sana

N.k

DALILI ZA TATIZO LA KIPANDA USO(MIGRAINE) NI PAMOJA NA;

Siku moja au mbili kabla ya tatizo hili kutokea,mtu huweza kupata mabadiliko k**a vile;

• Kuanza kupata choo kigumu

• Kupoteza mood

• Shingo kukak**aa

• Kiu ya maji kuongezeka sana pamoja na mtu kukojoa sana

• Mtu kupiga miayo sana

• Kuanza kupata shida ya kutokuona vizuri au kuona marue rue

NDIPO BAADAE dalili zingine hujitokeza mfano;

- Maumivu makali ya kichwa

- Mshipa kucheza cheza upande mmoja wa kichwani

- Kupatwa na hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika

- Mtu kupata kizunguzungu kikali

- Kuhisi sauti za makelele masikioni

- Kupata shida ya kuongea

- Mwili kutetemeka

- Mwili kukosa nguvu

- Dalili za kuchanganyikiwa

N.K

MATIBABU YA TATIZO HILI LA KIPANDA USO

• Zipo dawa mbali mbali za kuondoa maumivu haya k**a vile; Ibuprofen, Paracetum N.k

japo endapo mtu hupata dalili mbaya zaidi k**a kushindwa kuongea,mwili kutetemeka, n.k ni vizuri kuwaona wataalam wa afya.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Kucha kutumika kutambua baadhi ya Magonjwa1.Ikiwa kucha zako zina mstari mmoja ambao umechimba kidogo na upo mlalo(horiz...
11/11/2022

Kucha kutumika kutambua baadhi ya Magonjwa

1.Ikiwa kucha zako zina mstari mmoja ambao umechimba kidogo na upo mlalo(horizontal) huweza kuashiria;

• Tatizo la utapiamlo

• Shida ya measles(surua)

• Kisukari ambacho hakijadhibitiwa(uncontrolled diabetes)

• Shida ya Pneumonia

• Upungufu wa Madini ya Zinc.

2. Kucha kuwa nene na kutuna, kuwa na kitu k**a mgongo,huweza kuashiria;

• magonjwa ya moyo(cardiovascular disease)

• magonjwa ya Ini(Liver diseases)

• Shida kwenye mapafu

• Shida ya upungufu wa kinga mwilini(AIDS)

3. Kucha kuingia ndani na kupinda k**a Kijiko,huweza kuashiria;

• Upungufu wa damu unaotokana na upungufu wa madini chuma(Iron-deficiency anemia)

• Magonjwa ya Moyo

• shida ya hypothyroidism n.k

4. Kucha kuwa na mistari miwili mlalo, hii huweza kuwa shida ya sumu au Arsenic poisoning

5. Kucha kuwa za njano(yellow nail syndrome), hii huweza kuashiria;

• Shida ya rheumatoid arthritis

• Chronic bronchitis

• Shida ya Pleural effusions n.k

MAELEZO ZAIDI,Google Website@afyaclass

VIDOLE VYA MIKONO KUFA GANZI(Chanzo chake)1. Ugonjwa wa kisukari, hapa nazungumzia Diabetes neuropathy, ambapo baada ya ...
05/11/2022

VIDOLE VYA MIKONO KUFA GANZI(Chanzo chake)

1. Ugonjwa wa kisukari, hapa nazungumzia Diabetes neuropathy, ambapo baada ya ugonjwa wa kisukari kutokea huharibu nerves hasa kwenye maeneo ya miguuni na mikononi,

ndyo maana wagonjwa wengi wa kisukari hupatwa na tatizo hili la vidole vya mikono pamoja na miguu kufa ganzi.

2. Matatizo yote ambayo yanahusu kuharibiwa kwa nerves kwenye maeneo ya shingoni, mikono na miguuni k**a vile; Carpal tunnel,Cervical radiculopathy,Ulnar nerve entrapment n.k

3. Tatizo la Raynaud's Disease, Huu ni ugonjwa ambao husababisha mishipa ya ARTERIES Kwenye mikono kuwa mwembamba zaidi,hali ambayo hupunguza flow ya damu kwenye nerves zilipo kwenye mikono ikiwemo na vidole,

Hii husababisha upungufu wa damu kwenye nerves kisha kupelekea vidole pamoja na mikono kuanza kupata tatizo la ganzi.

4. Hali ya baridi sana, hali hii ya baridi sana huweza kusababisha mpaka vidole vya mikono kufa ganzi, japo haidumu kwa muda mrefu sana tatizo hili huondoka lenyewe

5. Shida ya Emotional Distress, kuna baadhi ya watu wakiwa kwenye hali isiyo na utulivu kihisia huweza kupata pia shida ya vidole kufa ganzi.

6. Vidole vya mikono kubanwa sehemu kwa namna yoyote ile k**a kukaliwa, n.k

7. Tatizo la Rheumatoid arthritis(RA), hii ni autoimmune disordrer ambayo huweza kuleta uvimbe,maumivu kwenye joints, ganzi kwenye vidole vya mikono, hali ya kuungua kwenye mikono n.k

Soma zaidi. Google:Afyaclass

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA INBOX +255758286584.

Hizi hapa ni baadhi ya dalili ambazo huweza kukuonyesha kwamba una shida ya Mzio au allergies kwenye baadhi ya Vitu.1. K...
05/11/2022

Hizi hapa ni baadhi ya dalili ambazo huweza kukuonyesha kwamba una shida ya Mzio au allergies kwenye baadhi ya Vitu.

1. Kuvimba Pua muda mfupi baada ya kutoka nje, hii ni allergic rhinitis, ambapo mtu hupata reaction dhidi ya particles ndogo kwenye hewa anayovuta.

Kuvimba pua baada ya kukaa sehemu zenye vumbi,kula chakula flani,dawa n.k

2. Mtu kupiga chafya sana hata baada ya kula kitu chochote,

3. Kuwashwa Sana Mwilini, na wakati mwingine kupata vipele kwenye ngozi

4.macho kutoa machozi yenyewe, na baadhi ya watu hupata shida hii baada ya kuanza kunywa dawa ambazo hawajawahi kuzitumia kabsa.

5. Mtu kuvimba Mdomo baada ya kula baadhi ya vyakula

6. Mtu kuwashwa sana masikio au Mdomo, hasa baada ya kula chakula flani

7. Mtu kuvimba mdomo,uso,pua n.k baada ya kuoga kwa kutumia baadhi ya sabuni

8. Kupata shida ya kupumua,kila unapokula nyama au chakula flani

9.Ngozi kubadilika rangi,kuwasha,kuwa na vipele,baada ya kula baadhi ya vyakula,dawa n.k

10. Kupata kichefuchefu,kutapika,maumivu ya tumbo au Kuharisha,kila unavyokula baadhi ya vyakula

11. Mtu kuvimba Ulimi au Lips za mdomo baada ya kula baadhi ya vyakula,Dawa n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Kahawa huweza Kupandisha Presha(shinikizo la Damu)Hushauriwi kutumia kahawa k**a tayari una tatizo la Presha ya kupanda,...
04/11/2022

Kahawa huweza Kupandisha Presha(shinikizo la Damu)

Hushauriwi kutumia kahawa k**a tayari una tatizo la Presha ya kupanda,

mbali na kwamba baadhi ya watu hutumia kahawa kwa lengo la kupoteza Usingizi,lakini kahawa pia inaweza kupandisha presha yako ndani ya muda mfupi baada ya kutumia.

Machapisho zaidi ya 34 ya tafiti mbali mbali yanaonyesha kwamba;

200–300 mg za caffeine kutoka kwenye Kahawa sawa na makadirio ya kikombe kimoja na Nusu(1.5) mpaka vikombe viwili(2) vya kahawa,

huweza kuongeza presha kwa kiwango cha 8 mm Hg na 6 mm Hg kweny systolic na diastolic blood pressure,

Na mabadiliko hayo yalionekana ndani ya masaa 3 tu baada ya mtu kutumia Kahawa,

Ongezeko hilo hutokea kwa watu wote,walio na presha ya kawaida(normal bp), walio kwenye hatari ya kupata presha, na ambao tayari wanashida ya presha.

Lakini pia kwa kadri mtu anavyozoea kutumia Kahawa mara kwa mara hutengeneza kitu kinaitwa caffeine tolerance mwilini,

Ndo mana matokeo ya kahawa kwa siku za mwanzo,ni tofauti kadri unavyotumia mara kwa mara, hata kwenye swala la presha ni hivo hivo.

Tatizo la Mdomo Sungura kwa watoto husababishwa na nini?Tatizo la Mdomo sungura ambapo kwa kitaalam hujulikana k**a clef...
04/11/2022

Tatizo la Mdomo Sungura kwa watoto husababishwa na nini?

Tatizo la Mdomo sungura ambapo kwa kitaalam hujulikana k**a cleft lip and palate ni aina ya ulemavu ambao chanzo chake ni sehemu ya uso na mdomo kushindwa kufunga wakati wa uumbaji wa mtoto akiwa tumboni.

Tatizo la mdomo sungura mara nyingi hutokea katika wiki ya tano hadi ya nane ya ukuaji wa mtoto anapokua tumboni ambapo sehemu tatu za uso yaani sehemu ya juu, pembeni na chini hushindwa kukutana,

Tatizo hili huwapata baadhi ya watoto bila kujali jinsia yao.

CHANZO CHA MDOMO SUNGURA NI NINI?

Wakati mwingine inaweza kuwa vigumu kujua sababu halisi ya mtoto kuzaliwa na hali hii ila Zipo sababu mbali mbali ambazo huongeza uwezekano wa watoto kuzaliwa na tatizo la Mdomo sungura, na sababu hizo ni k**a vile;

- Sababu ya Kigenetic, hapa huhusisha uwepo wa Vinasaba vya tatizo hili la Mdomo Sungura

- Mama mjamzito kunywa Pombe kupita kiasi,Unywaji pombe kipindi cha ujauzito huweza kusababisha madhara makubwa kwa mtoto wako aliyetumboni

- Mama mjamzito kuvuta Tumbaku,Sigara,pamoja na matumizi ya Ugoro kipindi cha ujauzito.

- Tatizo la kupata Lishe duni kwa mama mjamzito, hali ambayo hupelekea mama mjamzito kukosa virutubisho muhimu k**a vile vitamini,foliki asidi n.k.

virutubisho hivi ni muhimu sana kwenye uumbaji wa uti wa mgongo, ubongo,mfumo mzima wa fahamu pamoja na maeneo mengine ya mwili wa mtoto k**a vile Uso n.k.

- Matumizi ya baadhi ambazo haziruhusiwi kwa mama mjamzito,hasa katika miezi mitatu ya kwanza,ambapo uumbaji wa viungo mbali mbali vya mtoto hufanyika yaani Organogenisis.

MATIBABU YA TATIZO HILI LA MDOMO SUNGURA

Tiba kubwa ya tatizo hili ni UPASUAJI, Watoto wenye ulemavu huu wa mdomo Sungura hufanyiwa upasuaji na kurudisha viungo vilivo athirika katika hali yake ya kawaida.

MAELEKEZO ZAIDI,GOOGLE WEBSITE AFYACLASS.

Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD),chanzo,dalili,TibaTatizo hili hujulikana kwa jina Lingine k**a Acid Ref...
04/11/2022

Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD),chanzo,dalili,Tiba

Tatizo hili hujulikana kwa jina Lingine k**a Acid Reflux, tatizo hili hutokea pale ambapo Acid kutoka Tumboni hupanda juu kwenye mrija unaounganisha tumbo na Mdomo yaani esophagus,

Hali hii ya acid kupanda juu kutoka tumboni ndyo huanza kuleta shida mbali mbali.

DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;

- Mtu kuhisi Kiungulia(heartburn) mara kwa mara, hasa baada ya Kula, ambapo huzidi sana wakati wa Usiku au wakati wowote ukiwa umelala

- Mtu kupata shida ya chakula alichomeza au kinywaji alichokunywa kupanda juu au kurudi mdomoni yaani regurgitation

- Mtu Kupata maumivu ya tumbo juu ya kitovu karibu na mbavu au kupata maumivu ya Kifua(kichomi)

- Mtu kupata shida ya Kumeza Kitu yaani dysphagia

- Mtu kuhisi k**a kuna kitu kimebakia Kooni

- Wakati mwingine unaweza kupata kikohozi ambacho hakiishi,hasa k**a shida hii ya Acid Reflux hutokea wakati wa Usku

NB: SOMA ZAIDI MAKALA HII KWA KINA GOOGLE WEBSITE AFYACLASS

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

MATATIZO YA HEDHI1.kuumwa na Tumbo sana wakati wa Hedhi2.Kuvuja Damu nyingi na kwa mda mrefu mfano wiki moja,mbili n.k3....
28/12/2020

MATATIZO YA HEDHI

1.kuumwa na Tumbo sana wakati wa Hedhi

2.Kuvuja Damu nyingi na kwa mda mrefu mfano wiki moja,mbili n.k

3.Kublid mara mbili au zaidi kwa Mwezi

4.Kukaa zaidi ya mwezi mmoja bila kupata Hedhi

5.Kupata hedhi ya mabonge mabonge,nyeusi na wengine kunatoka vipande k**a vya maini.

KWA MATATIZO HAYA YOTE YA HEDHI CHECK INBOX 0758286584 UPATE MSAADA,TUMA UJUMBE UTAJIBIWA KWA HARAKA ZAIDI.

➡️ TATIZO LA KUWASHWA KWENYE NGOZI PAMOJA NA SEHEMU ZA SIRIUgonjwa huu umekuwa ukiwasumbua watu wengi siku hizi,bila kuj...
12/12/2020

➡️ TATIZO LA KUWASHWA KWENYE NGOZI PAMOJA NA SEHEMU ZA SIRI

Ugonjwa huu umekuwa ukiwasumbua watu wengi siku hizi,bila kujali umri au jinsia.

ZIPO SABABU MBALI MBALI KITAALAM AMBAZO HUCHANGIA HALI HII IKIWEMO;

-Swala la allergy ambayo hutokana na vitu mbali mbali k**a Maji(ya kisima,mvua n.k), baadhi ya mafuta ya kula,vyakula k**a aina ya flani ya nyama mfano ya mbuzi,ng'ombe,kuku n.k. KUNA WATU WANA ALLERGY KUTOKANA NA VITU HIVI.

-Swala lingine ni Magonjwa k**a FANGASI YA NGOZI, AU DAMU.ambayo hii matokeo yake huonekana moja kwa moja kwenyengozi na hali ya miwasho isiyoisha hujitokeza.

K**A UNAPATA MUWASHO WA NGOZI AU SEHEM ZA SIRI PIA,TUWASILIANE +255758286584 UPATE MSAADA.

Address

Moshi

Telephone

+255758286584

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afyaclass-Afya/Uzazi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Afyaclass-Afya/Uzazi:

Share