Kulwa Daniel

Kulwa Daniel KUFANIKIWA KUNATOKA NDANI YAKO

AINA TANO ZA HOBBIE (5) AMBAZO KILA MTU ANATAKIWA KUWA NAZO KWA AJILI YA MAENDELEO BINAFSI.📌HOBBIE INAYOKUTENGENEZEA/ KU...
12/06/2023

AINA TANO ZA HOBBIE (5) AMBAZO KILA MTU ANATAKIWA KUWA NAZO KWA AJILI YA MAENDELEO BINAFSI.

📌HOBBIE INAYOKUTENGENEZEA/ KUKUONGEZEA KIPATO
hii ni kufanya kitu unachokipenda huku kikikuingizia kipato.
Inaweza kuwa unapenda kupika, unapenda kucheza na kufatilia soka, unapenda kucheza game, kuvaa nguo nzuri na kupendeza vyote hivi unaweza kuvifanya kuwa sehemu yako ya kipato.

Unaweza kujifunza hobbie au kuendeleza uliyo nayo na kuifanya kuwa sehemu ya kukuongezea kipato

Kuna raha yake jamani kufanya kitu unachokipenda kwa sababu utafanya bila kuchoka na inakuwa rahisi kukubali makosa na kuyafanyia marekebisho

Hobbie yako inaweza kuwa suluhu yako ya matatizo ya kiajira au kukuongezea kipato.

HOBBIE INAYOKUONGEZEA UBUNIFU
Jifunze hobbie itakayokufanya wakati wote uwe mbunifu katika biashara, kazi, stadi za maisha, mahusiano ya jamii n.k

Sisi wote ni wabunifu na kila eneo la maisha linaubunifu lakini huwezi kuwa mbunifu kwa kitu ambacho hujaanza kukifanya hivyo unatakiwa kuanza kwanza ndo ubunifu uje.

K**a unapenda kuchora, kupangilia vitu, kushona, kusuka hata kuandika n.k inaweza kuwa sehemu nzuri ya kuanzia

Imedhibitishwa kitabibu kuwa ubunifu unaongeza afya ya akiri hivyo kuleta maendeleo mazuri katika mwili.

HOBBIE INAYOIMARISHA MWILI

Miili yetu ni k**a vyombo vya moto hivyo inahitaji kushughulishwa ili iwe active k**a utakaa tu bila kufanya mazoezi mwili unakuwa na uvivu mwingi na utasongwa na magonjwa

Hivyo tafuta hobbie ya kuufanya uwe na mwili imara k**a kukimbia, kunyanyua vyuma, kuruka kamba, kuendesha baiskeli nk

Mwili hauimarishwi kwa mazoezi tu bali kwa chakula pia, pendelea kula kwa kiasi chakula chenye virutubisho vyote k**a matunda, mboga mboga za majani, kunywa maji mengi na ya kutosha, mwisho kabisa kula nyama

Hapa unaweza kuwa na hobbie ya kulima bustani ya mboga mboga au matunda na kuitunza, kufuga ndege(kuku, njiwa, bata n.k) na wanyama hii itakupunguzia gharama za kununua mboga kila wakati pia itakuongezea kipato

NB: kuwa mwembamba haimaanishi una afya bora, na kuwa mnene sana haimaanishi una afya, kuwa na misuri mikubwa haimaanishi una afya bora. zingatia vyakula unavyokula na kula kwa kiasi, kunywa maji na fanya mazoezi.

Kula vyakula vyenye wanga,protein na mafuta mengi(fat)haviharibu afya yako kwani protein na fat vinahitajika kujenga mwili wako, vinavyoharibu mwili wako ni kiasi au kiwango cha chakula unachokula, kula kwa kiasi au kidogo kuboresha afya yako, usifunge kwa ajili ya kujikondesha madhara yake ni makubwa zaidi k**a kupata Madonda ya tumbo.

HOBBIE YA KUKUONGEZEA MAARIFA

Tafuta hobbie itakayokuongezea maarifa, maarifa ni chanzo cha kila kitu. Jiulize kwa mwaka umefanya nini kuongeza maarifa yako? Je baada ya kumaliza masomo tu kila kitu ulitupa na kusema hutosoma tena ? Labda nikwambie kwamba maarifa huexpire usipoyanoa. kila unapoishi na muda unavyoenda unahitaji maarifa ili kuboresha ubongo na ufahamu wako

Tafuta hobbie itakuyokufanya kuongeza maarifa yako k**a kusoma, kuhudhurulia warsha, semina na makongamano yatakayokuongezea maarifa.

Unaweza kuongeza maarifa kwa kuhusiana na watu wengine, tafuta wako kwenye kitu unachokifanya au unachotaka kufanya husianana nao kwa namna moja au nyingine watakuongezea maarifa

Elimu haina mwisho usichoke wala kuacha kujifunza.

HOBBIE YA KUJENGA MAHUSIANO

Address

Mtwara

Telephone

+255783914484

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kulwa Daniel posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Kulwa Daniel:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram