26/03/2026
UZIMA PROJECT NDANDA, kwa kushirikiana na wataalam wa afya kutoka hospitali ya Rufaa Ndanda, Pamoja na viongozi wa Serikali ya Kijiji Cha Njenga.
Tulimtembelea magonjwa anayeumwa ugonjwa wa Figo, Wilaya ya Nachingwea Kijiji Cha Chemchu.
HISTORIA.
Mgonjwa anaitwa Ally Selemani Chilindo ni mkazi wa wilaya ya Nachingwea Kijiji Cha chemchemu.
Mgonjwa alikuwa shehe mkuu aliyemiliki kata saba (7), akiwa k**a kiongozi wa kuongoza wauminini wa dini ya kiislamu.
Wakati anaendelea kuongoza umma wa kiislamu alianza kuumwa nyuma. Hadi Ilipofika 2023, mgonjwa hali yake ya afya ilikuwa sio mzuri, hapo familia ikaamua kumepeleka hospitali kwa Matibabu zaidi.
Baada ya Matibabu na vipimo vya kina kwa mgonjwa ndipo aligundulika kuwa ana tatizo la Figo ( kidney failure).
Baada ya hapo familia walikubaliana na majibu ya watalamu wa matibabu yalianza hospitali na wanaporudi nyumbani huku wakifuata taratibu za huduma kwa mgonjwa waliziambiwa.
Wakati Matibabu yanaendelea familia waliomba Msaada sehemu mbalimbali mpaka serikalini kwa ajili ya Matibabu mgonjwa wetu ( Ally Salemani) , waliosaidia walimsaidia lakini bado hali iliendelea kuumwa.
Mwaka 2024, mgonjwa alifika tena hospital ya rufaa Ndanda kwa Matibabu,
Lakini tayari ilishafikia stage ya kuchuja Figo(dialysis) kwa mgonjwa.
hapo ndipo ikaanza kutumika hela kwa kiasi kikubwa hadi baadhi ya Mali k**a vile mashamba, mifugo ikaanza kuuzwa kwa ajili ya Matibabu ya mgonjwa wetu lakini bado hali ya mgonjwa hakupata unafuu wa kupona kabisa k**a matarajio yao.
Takribani miaka mitatu(3), tangu 2024-2026, hali iliendelea na walikuja kuishi Ndanda mtaa wa majengo kwa ajili ya kupata Matibabu hospitali ya rufaa Ndanda.
ila bado hali ilikuwa mbaya,
Wakati wa Matibabu yake hapa Ndanda, shirika la Uzima walitembelea mgonjwa huyo na kuonana na familia yake kwa ajili ya kumsadia kwa upande wa UZIMA PROJECT NDANDA.
familia walikubali na alisajiliwa kwa ajili ya kupata huduma ya Tiba shufaa( Palliative care), kwa lengo la kumpata dawa za kutuliza maumivu.
Kwa muda mrefu wa matibabu yake hapa Ndanda, matibabu yalivyo na hali ya wataalamu wa tiba shufaa walishauri familia warudi na mgonjwa nyumbani kwa ajili huduma ya nyumbani na tuendelee kumpa dawa maumivu mgonjwa akiwa nyumbani.
Maana tayari fedha nyingi imetumika na mgonjwa hali haiko sawa, na wamezunguka miaka mingi kwa matibabu lakini hamna tiba yake ya kupona moja kwa Moja.
Ndipo tarahe 24/03/2026, Jopo, au Timu ya wataalamu wenye taaluma mbalimbali tuliamua kumtembelea mgonjwa kumuona na kuongea na familia kuhusu mgonjwa.
Familia walitupokea vizuri na wataalamu walimuona mgonjwa na walitoa huduma na elimu ya dawa kwa mgonjwa na kuwaomba familia kuungana pamoja kusaidiana kumuuguza mgonjwa wetu.
Familia walishukuru Sanaa na tulimuacha mgonjwa ametabasamu. Ahsante Team
Update
Muungwana One tv