
09/06/2025
📌Kumeza folic acid (au folate) kabla ya kubeba mimba kuna faida nyingi muhimu sana kwa afya ya mama na mtoto. Hapa chini ni baadhi ya faida kuu:
1. Kuzuia matatizo ya neva ya mtoto (neural tube defects)
Folic acid husaidia kuzuia matatizo k**a:
Spina bifida (mgongo wa mtoto kutokufunga vizuri)
ubongo wa mtoto kutokukua vizuri
📌Haya matatizo hutokea wiki za mwanzo kabisa za ujauzito (wiki ya 3 hadi 4), mara nyingi hata kabla mama hajajua k**a ni mjamzito — ndiyo maana ni muhimu kuanza kutumia kabla ya kushika mimba.
2. Kusaidia ukuaji mzuri wa mtoto tumboni
Folic acid ni muhimu kwa ukuaji wa seli mpya, hasa wakati mtoto anapokua haraka mwanzoni mwa ujauzito.
3. Kupunguza hatari ya mimba kuharibika (miscarriage)
Utafiti unaonyesha kwamba wanawake wanaotumia folic acid qwana uwezekano mdogo wa mimba kuharibika mapema.
4. Kuzuia matatizo ya kuzaliwana matatizo ya moyo
Inaweza kusaidia kupunguza hatari ya matatizo ya moyo kwa mtoto.
5.kumsaidia mama kutokupata changamoto ya upungufu wa damu kipind cha ujauzito.singano_afya