09/08/2022
Unalifahamu kundi lako la damu na mwenzi wako??!
Ukiwa na mpenzi msiwaze tu kupima VVU,bali pimeni pia mjue makundi yenu ya damu.
Mwanaume akiwa na damu yenye + ( mfano A+, B+, AB+ au O+ ) anaweza kuoana na mwanamke yeyote mwenye damu group yenye + ( mfano A+, B+, AB+ au O+ ) na watapata watoto bila tatizo lolote.
Mwanaume akiwa na group mfano ( A+, B+, AB+ au O+) akioa msichana mwenye A-, B-, AB- au O- Mtoto wa kwanza atazaliwa vizuri, na ikitokea MWANAMKE AMEJIFUNGULIA NYUMBANI au NJE YA HOSPITAL, ambako hakugundulika kwamba ana damu negative... Mtoto wa kwanza ataishi vizuri kabisa na afya nzuri. ila watoto wanaofata hawataweza kuishi au watakufa kabla hawajazaliwa kwa sababu, Msichana mwenye negative blood group ( Rh-) yaani hana D antigen, alipojifungua mtoto wa kwanza mwili wake unakuwa sasa umeandaa kujikinga (antibodies kupambana na D antigen ( Rh +) kwa baadae
MTOTO WA PILI akitungwa mwili wa mama tayari una Antibodies dhidi ya Rh+ ( mtoto anazo hizi Rh+), hivyo matokeo yake ni kuwa seli nyekundu za mtoto zitashambuliwa na kufa.
Mtoto akibahatika kuzaliwa hai, atapoteza uhai muda sio mrefu kwa vile anakuwa hana seli nyekundu za kusambaza damu mwilini.
Endapo Mwanamke huyu alijifungulia MTOTO WA KWANZA HOSPITAL, madaktari wanakuwa wameshajua kwamba ana damu negative, hivyo wanasaidiana na mmewe kufanya maandalizi ya sindano yenye dawa ( SIITAJI HAPA )
alafu msichana akijifungua tuu MTOTO WA KWANZA anachomwa hiyo sindano
na akija kupata mimba baada atachomwa hiyo sindano wakati wa mimba na pindi anapojifungua.