16/11/2025
TATIZO LA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE
Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke (low libido au hypoactive sexual desire)
Ni ile hali ambapo wanamke anakuwa hana matamanio kabisa ya mwanaume hasa ikija katika swala la hisia ya hamu ya tendo la ndoa.
Hii ni hali ambayo imeanza kuwa Tatizo na changamoto kubwa sana kwa siku za hivi Karibu na linaendelea kukua kila siku.
Leo naomba tuangalie kwa mapana zaidi Sababu zinazopelekea, Namna ya kufanya Vipimo na Matibabu pia nitakushauri nini cha kufaya kujisaidia Mwenyewe nyumbani
π΄ Sababu Kuu Zinazosababisha Mwanamke Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa
1. Mabadiliko ya Homoni
π Kupungua kwa homoni ya estrogen, hasa baada ya kujifungua, wakati wa kunyonyesha, au kuingia menopause. Lakini pia homoni hii inaweza ikapungua kutokana na ulaji mbovu usio zingatia afya Yako
π Matatizo ya homoni ya thyroid. Homoni ya Estrogen haiwezi fanya kazi k**a Tezi ya Thyroid imepunguza utendaji kazi ama haina ufanisi Kabisa.
2. Msongo wa Mawazo (Stress) na Uchovu
π Shughuli nyingi, kazi nzito, majukumu ya familia, au matatizo ya kifedha.
π Kukosa usingizi wa kutosha.
3. Hisia na Mahusiano
πMigogoro baina ya wenzi.
π Kutokuhisi kupendwa, kuthaminiwa au kuungwa mkono.
π Msongo wa kihisia, huzuni, au mshtuko (trauma).
π Historia mbaya ya kimahusiano mfano kubakwa au kutendwa
4. Magonjwa au Maumivu
π Kisukari, shinikizo la damu, upungufu wa damu, maumivu ya ukeni, fangasi, PID n.k.
π Ukavu wa uke unaosababisha maumivu wakati wa tendo.
5. Matumizi ya Baadhi ya Dawa
π Vidonge vya uzazi wa mpango (kwa baadhi ya wanawake).
π Dawa za presha, antidepressants, na baadhi ya dawa za usingizi.
6. Mitazamo ya Kisaikolojia
π Hofi ya kushindwa kumridhisha mwenzi.
π Hisia hasi kuhusu mwili (body image).
π Uzoefu mbaya wa kingono zamani.
π’ Matibabu na Ufumbuzi wa Tatizo Hili
1. Tiba ya Kimwili na Kitabibu
π Kupima homoni, damu, thyroid, na magonjwa mengine yaliyofichika.
2. Kubadili Dawa
Ikiwa tatizo limetokana na dawa fulani, daktari anaweza:
π Kubadilisha dawa, Kupunguza dozi, Au kupendekeza mbadala salama.
3. Tiba ya Kisaikolojia / Ushauri Nasaha
π Kumaliza migogoro ya uhusiano.
π Kushughulikia msongo wa mawazo au huzuni. Utashauliwa namna Nzuri ya kushughulikia hilo na Dakitari wako
π Tiba ya wanandoa ikiwa tatizo linatokana na mawasiliano duni.
4. Kuimarisha Mtindo wa Maisha
π Kupunguza stress (mazoezi, mawasiliano mazuri, kupumzika).
π Unashauri kupata mda mzuri wa kupumzika ili upate Usingizi wa kutosha kwa siku.
π Kula vyakula vinavyoongeza nguvu na mzunguko wa damu k**a:
Parachichi, mbegu (chia, ufuta), karanga, boga, samaki wenye omega-3, majani mabichi.
5. Tiba za Asili (Kwa Uangalizi)
Baadhi ya mimea huongeza mzunguko wa damu na hamu ya tendo kwa wanawake:
π Moringa,
π Ginseng,
π Mdalasini,
π Mbegu za maboga
Ni muhimu kutumiwa kwa uangalifu na kufuata ushauri wa mtaalam wa tiba mbadala. ( Unaweza ukatupigia Simu )
6. Kuboresha Mazingira ya Kimapenzi
π Kuongea na mwenzi kuhusu vitu vinavyomfurahisha.
π Kukuza ukaribu wa kihisia kabla ya tendo.
π£ Lini Umuone Daktari?
π Tatizo limeanza ghafla bila sababu.
π Limesababisha mgogoro wa ndoa.
π Kuna maumivu makali wakati wa tendo.
π Kukosa hedhi au mabadiliko ya homoni yanayoshukiwa.
π₯ Ikiwa unahitaji kuondoka kabisa na Tatizo hili na umetumia njia nyingi lakini bado linakusumbua unaweza ukawasiliana nasi kupitia Namba
πππ
βοΈ 0743 824 015
π 0714 538 903
Tunatuma Dawa popote pale Ndani ya Tanzania kwa uaminifu mkubwa. Pia unaweza ukafika katika ofisi zetu zilizopo NYEHUNGE BUCHOSA MWANZA na MASWA SIMIYU MTAA WA SOKONI.