24/08/2022
UGONJWA WA KUPOTEZA KUMBUKUMBU
Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Dementia) unapata zaidi watu wenye umri zaidi ya miaka 65 na ni ugonjwa ulio
endelevu kwa maana dalili zake huwa
zinazidi kuongezeka taratibu kadri muda/umri unavyokwenda.
Dalili za mwanzo kabisa za tatizo hili ni kusahau matukio au mazungumzo ya hapa karibuni na Kadiri ugonjwa unavyoongezeka, mtu atapata matatizo makubwa zaidi ya kumbukumbu na kumfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake ya kila siku
*DALILI ZA UGONJWA WA KUPOTEZA
KUMBUKUMBU ZINAWEZA KUWA :
1. Kukosa kumbukumbu k**a vile kusahau tarehe muhimu au matukio muhimu
2. Kupata shida katika kufanya mambo ya kawaida, k**a kukumbuka sheria za mchezo unaoupenda au kuendesha gari kuelekea sehemu unayoifahamu vizuri
3. Kupata shida katika mazungumzo na wenzako au katika kuandika, kwa mfano kupata shida katika kukumbuka maneno sahihi au majina ya watu na sehemu mbalimbali
4. Kupoteza mwelekeo wa muda na mahali, k**a kusahau sehemu ulipo, kutojua msimu wa mwaka, tarehe, na muda uliotumia katika shughuli
5. Kupungua uwezo wa kutoa maamuzi k**a kukosa usafi, kushindwa kutoa maamuzi ya pesa n.k.
6. Matatizo katika kuona k**a matatizo katika kusoma au kukadiria umbali
7. Kupungua kwa uwezo wa kutatua matatizo na kuweka mikakati k**a ufuatiliaji wa bili mbalimbali au kukumbuka mapishi
8. Kupoteza vitu kila wakati au kusahau villipowekwa
9. Mabadiliko katika tabia
10. Kukosa ubunifu au kujitoa kwenye shughuli za jamii