09/02/2024
SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
Shingo ya kizazi (cervix) ni kiungo cha mwili kinachopatikana kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke. Ni sehemu ya mji wa mimba (Uterus) inayotokezea kwenye uke (tupu) wa mwanamke. Tazama picha
SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI NI NINI?
Ni mabadiliko hasi (yasiyo ya kawaida) ya chembechembe hai zilizopo kwenye shingo ya kizazi. Mara nyingi saratani hii ikiwa inaanza haionyeshi dalili yoyote hivyo mgonjwa hawezi kuchukua hatua yoyote kukabiliana na tatizo hili kwa wakati huu.
Kwa kiasi kikubwa saratani hii husababishwa na maambukizi ya mda mrefu (persistence infection) ya virusi viitwavyo Human papilloma, ambavyo huenezwa kwa njia ya kujamiiana. Kawaida mwili una uwezo wa hudhibiti maambukizi haya yaingiapo mwilini, lakini yasipodhibitiwa kikamilifu na kuwepo mwilini kwa mda mrefu husababisha ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.
MAMBO MENGINE YANAYOCHANGIA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
Kufanya ngono zembe
Kuwa na wapenzi wengi
Kukoma siku katika umri mkubwa
Utumiaji mafuta mengi katika chakula.
Kutokufanya mazoezi ya mara kwa mara.
Unene kupita kiasi
Uvutaji sigara.
Utumiaji wa pombe kupita kiasi.
Historia ya saratani ya matiti katika familia.
DALILI ZA UGONJWA WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
Dalili za ugonjwa huu huanza kujitokeza baada ya tatizo kuanza kukomaa, zifuatazo ni baadhi ya dalili
Kutokwa na maji maji yenye harufu ukeni
Kutokwa damu baada ya kujamiiana
Kutokwa damu kusiko kwa kawaida (siyo damu ya hedhi)
Kuumwa mgongo na kiuno
Kuumwa miguu
Kizunguzungu na kuishiwa nguvu
NINI KIFANYIKE?
Saratani ya shingo ya kizazi inazuilika au kutibika kabisa endapo itagundulika ikiwa kwenye hatua za awali.
Hivyo ni muhimu kufanya uchunguzi wa afya yako kwa kadiri utakavyoshauriwa na wataalam wa afya
Wanawake wote walio na umri kuanzia miaka 30 na kuendelea wanatakiwa kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi.
Kumbuka: Wakati wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi ni sasa usisubiri hadi uone dalili
Whatsaap 0659905019