26/05/2025
MAGONJWA YA ZINAA (Sexually Transmitted Infections −STIs)
Yapo magonjwa mengi yanayosababisha mtu kukojoa udenda (usaha), uume kuuma au kuwasha wakati wa kukojoa. Magonjwa yanayosababisha hali hiyo kwa sana ni pamoja na klamidia (Chlamydia), kisonono (Gonorrhea), Trichomoniasis na magonjwa mengine yanayoathiri njia ya mkojo (Nongonococcal Urethritis).
Klamidia (Chlamydia)
Klamidia (Chlamydia) ni moja ya magonjwa ya zinaa. Ugonjwa huu unasababishwa na viini vya bakteria wanaojulikana kitalaamu k**a Chlamydia Trachomatis na waweza kuathiri uke, mrija wa kupitisha mkojo, uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa.
Klamidia (Chlamydia) ndio ugonjwa wa zinaa unaotokana na bakteria unaoongoza kwa maambukizi mengi zaidi duniani ukifuatiwa na ugonjwa wa kisonono (gonorrhea).
Ugonjwa wa Klamidia (Chlamydia) huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiana. Ugonjwa huu ni wa hatari kwa sababu mama mjamzito anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa ujauzito.
Njia nyingine za maambukizi ni pamoja na,
Kuchangia vifaa vya kuogea k**a taulo vya mtu mwenye maambukizi,
Kuchangia vyoo vya kukaa na mtu mwenye maambukizi na
Kukumbatiana na mtu mwenye maaambukizi.
Vile vile ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kupitia mbwa, kupitia vinyesi vya ndege k**a kuku, bata na kasuku walioambukizwa klamidia (chlamydia) inayopatikana kwa wanyama ijulikanayo kitaalamu k**a Chlamydophila psittaci na kusababisha aina ya homa ya mapafu au homa ya kasuku (psittacosis).
Klamidia huathiri sehemu tofauti za mwili wa binadamu k**a macho, mfumo wa upumuaji, sehemu za siri k**a makalio, viungo vya uzazi na tezi (lymph nodes).
Huchukua siku 1-14 tangu maambukizi hadi kuonekana kwa dalili. Asilimia 75 ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume wanaopata maambukizi ya ugonjwa huu huwa hawaonyeshi dalili za moja kwa moja.
Ishara na dalili (Signs and symptoms).
Kwa wanaume,
Ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitishia mkojo uzuri ni kwamba dalili huonekana wazi, k**a vile;
Uume kuwasha,
Uume kutokwa na ute na kusikia maumivu wakati wa kukojoa.
Sehemu ya tundu kwenye uume kuwa nyekundu,
Kuvimba na kuwasha pia kuhisi maumivu kwenye korodani.
Tezi zilizopo sehemu za uume ambazo huvimba na kuambatana na maumivu.
Kwa wanawake dalili hazionekani kwa urahisi.
Ubaya ni kuwa ugonjwa huo unaweza kuathiri fallopian tubes – yaani mirija ya kupitia mayai kutoka kwenye Ovari hadi kwenye nyumba ya uzazi hivyo basi kusababisha ugumba/utasa.
Wakati mwingine dalili hii unaweza kuiona - kutokwa na majimaji ya ukeni yasiyo ya kawaida na kuhisi maumivu wakati wa kukojoa.
Dalili za ugonjwa huu k**a umeathiri makalio (puru) kwa wanawake na wanaume ni k**a
Kuwashwa na kutokwa na damu kwenye puru,
Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa.
Kutokwa uchafu k**a k**asi kutoka kwenye puru.
Iwapo vimelea vya klamidia vitaathiri macho, wanawake na wanaume huwa na dalili k**a;
Kuvimba macho,
Macho kuwa mekundu, Kuwasha na hata kutokwa na majimaji machoni.
Klamidia inayoambukiza kwenye macho hujulikana kitaalamu k**a Chlamydia conjunctivitis au Trakoma (trachoma) na ndiyo inayoongoza kwa kusababisha upofu duniani.
Dalili za klamidia kwa watoto wachanga hutokea katika kipindi cha wiki mbili kwenye macho, na iwapo ni homa ya mapafu dalili zake hujitokeza katika kipindi cha wiki mbili hadi miezi 3 baada ya kuzaliwa.
Husababishwa na viini vya bacteria na waweza kuathiri uke, mrija wa kupitisha mkojo, uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa.
Matibabu: Ni pamoja na kufanyiwa uchunguzi wa mkojo au damu.
Unapotambuliwa daktari hupendekzeza dawa maalum ya kumeza, K**a umefanya mapenzi hivi karibuni basi yafaa mpenzi huyo aarifiwe ili naye atibiwe pia.
Kisonono (Gonorrhea)
Ugonjwa wa Kisonono (gonorrhea) husababishwa pia na bakteria waitwao kitalaamu Neisseria gonorrhea unapofanya mapenzi na mtu mwenye kisonono.
Ugonjwa huu unaweza kuaathiri viungo k**a vile Uke, Uume, sehemu ya haja kubwa na ya haja ndogo, Koo au Mdomo k**a ukifanya Mapenzi ya kunyonyana.
Ishara na dalili (Signs and symptoms).
Wanaume huwa na dalili k**a;
Uume kutoa ute wa njano au kijani.
Kupata maumivu wakati wa kukojoa (mkojo kuchoma).
Pia kuna uwezekano wa kuwashwa ama kutokwa na maji maji katika sehemu ya kupitishia haja kubwa. Ingawa hivyo baadhi ya watu hawaoni dalili zozote kabisa lakini bado wanaweza kuwaambukiza wanaofanya mapenzi nao.
Trichomonas Vaginalis – (TV)
Hiki nacho ni kijidudu cha bacteria, kidogo kinachoambukiza kupitia ukeni na kwenye mrija wa kupitishia mkojo.
Ugonjwa wa Trichomoniasis unasababishwa na vimelea vya jamii ya protozoa vinavyojulikana kitalaamu k**a Trichomonas va**nalis.
Ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitisha mkojo (urethra) na uke wa mwanamke (va**na).
Huathiri sana wanawake kuliko wanaume na wanawake wenye umri mkubwa wako katika hatari zaidi kuliko mabinti wadogo.
Hupatikana kwa njia ya kujamiana bila kutumia kinga na mtu aliyeathirika na Trichomoniasis.
Ishara na dalili (Signs and symptoms).
Dalili za Trichomoniasis huanza kuonekana kuanzia siku ya 4 mpaka ya 28 baada ya mtu kupata maambukizi, Wanaume huwa hawaonyeshi dalili zozote lakini baadhi wanaonyesha dalili k**a;
Kuwasha ndani ya uume,
Kutokwa na uchafu au majimaji kutoka kwenye uume.
Kuwasha au mkojo kuchoma wakati wa kukojoa au baada ya kutoa shahawa.
Dalili kwa mwanamke aliyeambukizwa ni;
Kutokwa na uchafu wa rangi ya njano/kijani ulio k**a mapovu huenda ukawa na harufu k**a ya samaki .
Harufu mbaya inayoambatana na kutokwa na uchafu,
Kuongezeka kwa uwingi wa uchafu wa ukeni.
Maumivu ya ukeni au sehemu za nje ya uke (v***a),
Kujisaidia haja ndogo mara nyingi zaidi,
Kuwashwa sehemu za siri.
Matibabu; Ugonjwa huu unaweza kutibiwa kwa urahisi, kwa madawa maalam ya kupambana na viini antibiotics.
Ili kuepuka kuambukizwa upya, na kusambaa zaidi kwa ugonjwa huu inabidi mpenzio pia naye atibiwe.
Mwanaume asipopata matibabu mapema huongeza hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI na huongeza hatari ya kupata saratani ya tezi dume.
Magonjwa mengine ya njia ya mkojo
Magonjwa mengine yanayoathiri njia ya mkojo husababishwa na bakteria na huathiri mfereji wa kupitisha mkojo (urethra).
Magonjwa hayo husambazwa kwa kujamiiana. Dalili kwa wanaume ni kutokwa na ute kwenye tundu la uume na huenda akahisi maumivu wakati wa kukojoa au akahisi maumivu na kuwashwa-washwa kwa pamoja.
Cystitis
Huu ni uvimbe mgumu, Huambukiza kupitia bacteria ambao huishi chini ya ngozi, eneo la sehemu za siri na hata kwenye utumbo mkubwa.
Ishara na dalili (Signs and symptoms).
Dalili kubwa ni Maumivu makali wakati wa kukojoa.
Kujisikia kutaka kwenda chooni mara kwa mara.
Maumivu yanaweza kuendelea kuwa makali kwa haraka sana.
Huwakumba zaidi wanawake hasa wakati wa hedhi na wakati wa hali fulani nyinginezo k**a vile kuwa na Ujauzito, au kuugua ugonjwa wa Kisukari.
Usipotibiwa kwa haraka unaweza kusambaa hadi kwenye figo na kusababisha madhara mabaya zaidi.
Matibabu: Kunywa maji kwa wingi au vinywaji majimaji k**a maji ya matunda (juisi hasa ile ya cranberry) Unapoona tu dalili za kwanza kwanza, juisi hiyo inaweza kusaidia sana. Hata hivyo ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi na dawa zinazokufaa.
Thrush
Huu ni ugonjwa wa kuvimba vimba ndani kwa ndani mwilini. Kwa kawaida husababishwa na 'fungus'- kukua kupita kiasi kwa kitu k**a hamira. Ugonjwa huu unaweza kusambazwa kwa njia ya ngono lakini pia unaweza kutokea kutokana na sababu nyingine, kwa mfano k**a kuvaa chupi, suruali iliyokubana zaidi, au k**a unaugua ugonjwa wa kisukari.
Ugonjwa huu unaweza kuwapata wanawake kwa wanaume.
Ishara na dalili (Signs and symptoms).
Dalili kubwa kwa wanawake ni;
Kupata maumivu na kujikuna kwenye mashavu ya upenyo wa Uke na sehemu ya kupitishia haja kubwa (mkunduni).
Kuhisi mfano wa kuanza vidonda katika eneo la sehemu za siri, Hali hiyo huambatana na kutokwa na majimaji mazito meupe kutoka ukeni yenye harufu k**a hamira, Sehemu hizo huenda zikawa nyekundu zaidi.
Wanaume;
Miwasho kwenye uume, hasa ncha ya uume (kichwa cha uume).
Kuhisi k**a karaha ya kupata vidonda.
Uume hutokwa na majimaji au ute mzito wa njano.
Matibabu: Pindi ukigunduliwa ugonjwa wa Thrust hutibika kwa urahisi. Daktari hupendekeza vidonge au krimu maalum ambazo zinapatikana kwa wingi, kwenye maduka ya madawa.
Muone daktari endapo;
Ikiwa unapata dalili isiyo ya kawaida ni busara kutafuta msaada wa kitabibu na siyo kusubiri mpaka hali inakuwa mbaya au kutumia dawa kiholela bila bila ushauri wa daktari.
Wanawake:
Maji maji au ute unaotoka kwenye uke ni hali ya kawaida, lakini wanawake wanapaswa kutafuta usaidizi wa kimatibabu wakigundua lolote kati ya yafuatayo;
Majimaji ya ukeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida na yenye rangi tofauti na wingi kuliko ilivyo kawaida.
Maumivu au kusikia k**a unachomeka au mwasho wakati wa kukojoa.
Maumivu na miwasho katika maeneo ya Uke.
Maumivu ya ukeni wakati wa kufanya ngono.
Vidonda na malengelenge katika eneo la Uke.
Wanaume:
Mwanaume anapaswa kwenda kutafuta ushauri wa daktari k**a ana dalili zifuatazo:
Majimaji kutoka uumeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida, au yakiwa mengi.
Kuhisi mwasho ndani ya uume, wakati na baada tu ya kwenda haja ndogo.
Vijidonda na sugu ama malengelenge juu au kwenye uume.
Vipele au uvimbe katika sehemu za siri.
Kumbuka, baadhi ya maambukizi huenda yasiwe na dalili. Hii haimaanishi kwamba huwezi kumwambukiza mpenzi wako, au kwamba hayawezi kukudhuru kiafya. K**a una wasi wasi, ni vyema kuchunguzwa na daktari haraka iwezekanavyo, ama katika kliniki.
Ikiwa umefanya mapenzi bila kutumia kinga na una wasiwasi huenda umeambukizwa, nenda ukafanyiwe uchunguzi na daktari.
Kwa mara nyingine tena, kumbuka maambukizo mengine k**a ya virusi vya ukimwi yanaweza kuwemo mwilini kimya kimya kwa muda bila dalili zozote kujitokeza.
Unaweza kuwa hutaona dalili yoyote kwanza, lakini haimaanishi kwamba huwezi kuwaambukiza wengine.
Athari (Risk factors)
Madhara ya Magonjwa haya kwa wanaume ni kuathiri korodani na kusababisha mwanamume kukosa uwezo wa kutengeneza mbegu za uzazi (manii/shahawa) au kuwa tasa na pia husababisha maambukizi kwenye tezi dume (prostatitis).
Kwa wanawake, husababisha maambukizi kwenye mirija ya uzazi, mfuko wa uzazi, na mayai ya uzazi, kwa hivyo kusababisha ugonjwa wa uvimbe katika fupanyonga (PID).
Pia huongeza uwezekano wa wanawake kupata mimba zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi (Ectopic pregnancies).
Mwanamke hupata maumivu sugu kwenye nyonga na ugonjwa wa mifupa (arthritis) aina ya Reiters syndrome. Vilevile, klamidia huweza kusababisha ugumba kwa mwanamke k**a hatapata tiba na kwa wanawake wajawazito, klamidia husababisha wajifungue kabla ya wakati wao.
Aidha, mtoto anaweza kuzaliwa na maambukizi kwenye masikio, sehemu za siri, macho na kwenye mapafu, yaani homa ya mapafu, na k**a mtoto hatapatiwa tiba ya haraka ya macho baada ya kuzaliwa basi anaweza kuwa kipofu.
Njia za kuzuia STIs (Prevention).
Njia sahihi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa ni kuacha, kuepuka kujamiiana au kufanya ngono zembe na sizizo salama.
Kwa wanawake wajawazito, ni vizuri kuhudhuria kliniki mapema wakati wa ujauzito na kupimwa vipimo mbalimbali ili kubaini ikiwa mama mjamzito ameambukizwa na ugonjwa wowote wa zinaa na kupatiwa matibabu mapema.
Kwa wale wenye maambukizi wanashauriwa kuchukua tahadhari ya kutowaambukiza wapenzi wao kwa kufanya ngono salama.
MUHIMU;
TUNAFANYA KAZI KUPITIA ONLINE, HIVYO UAMINIFU NI KIPAUMBELE CHETU KIKUBWA, HATUNA MAWAKALA POPOTE, ILA TUNATUMA POPOTE KWA UHAKIKA NA UAMINIFU MKUBWA.
Wasiliana nasi kwa namba 0769 247 626