
11/04/2025
*Uhusiano wa vyakula wanavyokula wanawake wengi na Vivimbe kwenye kizazi upoje?*ππππ₯π³
Vyakula vya kukaanga vyenye mafuta mengi ni chanzo kikubwa sana pia cha Vivimbe kwenye kizazi (fibroids). Juck food. Mfano: Clips, chips yai, na vitu vyote vyakukaangizwa ndani ya mafuta Kwa muda mrefu.
Mara nyingi vyakula hivi pamoja na mafuta, huzalisha mafuta machafu mwilini yanayoitwa Cholesterol, Na hii cholesterol ndiyo chanzo Cha malighafi ya Steroids ya kutengeneza Homoni mbalimbali mwilini ikiwemo Estrojeni. Matokeo yake ni kwamba mwanamke atanenepa bila kutarajia na kiwango kikizidi cha hii homoni tayari shida ya Uzazi inaanzia hapo hapo ikiwemo fibroids.
*Angalizo:* Uvimbe au vivimbe vinavyojitokeza ndani ya mji wa mimba sio kansa, ni uvimbe wa kawaida tu ambao unakua kwa kutegemea kichocheo cha estrojeni ambayo ni kichochezi cha Uzazi (homoni) ya k**e na ndio maana kuanzia kubalehe mpaka kukoma kwa hedhi ndio wako hatarini kupata aina hii ya vivimbe. Na mara nyingi uvimbe huu huwaga unaongezeka kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani vichocheo hivi huongezeka wakati huu kulinda makazi ya mtoto.
Ni watu waliofikia kikomo cha hedhi hawapati fibroids au kitaalam leomyoma.
*By Dr Victoria 065498254*