afya Bora health

afya Bora health TULINDE AFYA

19/07/2024

*ZIJUWE SABABU ZINAZOPELEKEA MIMBA KUHARIBIKA ( MISCARRIAGE ) NA NAMNA YA KUJIEPUSHA NAZO"*

Miscarriage ni hali ya mama kupoteza ujauzito wake (kutoka) kabla ya wiki 20 kitaalamu Inaitwa Spontaneous abortion - Katika wanawake 10 wajawazito 2 kati yao wanaweza kupoteza ujauzito wao hivyo ndivyo tafiti nyingi zinavyoonyesha.

Wajawazito wengi mimba zao huaribika kipindi cha miezi 3 ya mwanzo

*SABABU ZINAZO PELEKEA MIMBA KUHARIBIKA*

➖Fetus au embroy anakuwa hana mfumo mzuri wa Ukuaji chromoses inakuwa haipo kwenye hali ya kawaida ni abdnomal hapo inaathiri mfumo mzima wa mimba na kupelekea kuharibika.

➖Magonjwa sugu-mama anapokuwa na magonjwa sugu k**a kisukari , Moyo au rheumatoid.

*➖Urinary Infection ( U.T.I )* Maambukizi Kwenye Njia ya Mkojo na Via Vya Uzazi K**a Vile Magonjwa ya Zinaa , K**a Kaswende n.k epuka Magongwa ya infections Yana Uwezo Mkubwa wa Kusababisha Mimba Kuharibika.

*➖Mapungufu kwenye uterus*
- Uterus ya mama inapokuwa na matatizo k**a uvimbe (fibroid) makovu au vidonda ni Sababu Nyingine inayoweza Kusababisha Kuharibika Kwa Mimba.

*➖Hormonal imbalance* Homoni za mama zinapokuwa hazipo kwenye uwiano ( balance) Pia Kuna Uwezekano Mkubwa Sana wa Kusababisha kuharibika kwa mimba.

*➖Uzito mkubwa (unene) na Uzito mdogo*
Unachangia mimba kuharibika na unaweza mfanya mama akapoteza maisha yake pia.

*➖Miscarriage zaidi ya mara 2*
Mama aliyepata miscarriage zaidi ya mara 2 anauwezo mkubwa wa kuharibika kwa mimba yake tena na tena Kila ashikapo.

*➖Kutoa mimba*: - Mwanamke anapotoa mimba mara kwa mara kizazi chake kinakuja shindwa kuhimili kubeba ile mimba kwa miezi 9 na kumfanya kila ashikapo ikifika miezi flani inatoka tu yenyewe sehemu za uzazi zinakuwa zimeshalegea.

*➖Matumizi ya Pombe*, Sigara , Bangi , Madawa ya kulevya vyote ni Moja Kati ya Vyanzo Vikuu Vya Mimba Kuharibika ( miscarriage).

*➖Ajali*-mama k**a amepata ajali akagonga maeneo ya tumbo au kupata mshtuko mkubwa basi ni rahisi mimba kuharibika.

*➖Caffein* - Mama anapotumia kahawa kwa Wingi , Soda aina Cocacola anaharatarisha Usalama wa Mimba na Kuwa na Uwezekano Mkubwa wakuharibu mimba

*➖Msongo( stress)*.

*➖Mimba za Utoto au Uzeeni* - Binti anaposhika mimba akiwa mdogo chini ya miaka 18 inahatari ya kuharimika sababu vizazi vyake havipo tayari kumudu kubeba mimba kwa miezi 9.

*Dalili ya mimba kuharibika*

🔻Kutokwa damu kwa wingi na mabonge.
🔻Kusikia maumivu makali chini ya kitovu Kwa Zaidi ya Saa ishirini na Nne .

▪️Mama mjamzito anaweza kuona dalili ya kutokwa damu akawahi hospital kuna vipimo anatakiwa Kufanyiwa cha Pelvic , Ultra sound na akasaidiea Kukaa Katika Hali yake njema.
▪️Uko Uwezekano wa kukutwa mimba haijaharibika vibaya , Kuna aina tofauti za miscarriage nyingine ni Lazima Zisaidiwe ili Kuhakikisha Imetoka Yote na Mama amebaki Salama na Ziko ambazo haziwezi Kusaidiwa huwa zinatoka moja kwa moja na nyingine zinaweza Okolewa na mimba ikabaki hai kuendelea Kukua mpaka miezi 9 , Cha muhimu ukiona hizo dalili awahi kituo cha afya.
▪️▪️Ukiona Hali K**a hiii wai hospitali cheki kipimo mapema
📞0788945354

06/07/2024

TATIZO LA UKE KUTOA HARUFU MBAYA LINALOWASUMBUA WANAWAKE WE GIVE
Kutokana na Hali hii ya wapo Wanawake wanaosumbuliwa na tatizo hili na Cha ajabu wameamua kuishi na changamoto na kupelekea kusemwa na kudhalilika mbele wa watu wanao date (pata Raha nao) na hupelekea kuwakimbia na kuona wenzie wao kuwatenga, zijue vyanzo vinavyo pelekea adi kupatwa na chango hiyoo ili uweze kuwa salama zaidi
🔶Sababu zinazosababisha uke kutoa harufu mbaya ni k**a zifuatazo
💠BACTERIAL VAGINOSIS
Kila uke wa mwanamke una bacteria ambao wapo asilia kwa ajili ya afya njema ya uke wako,Lakini k**a ikitokea hawa Bacteria wakazidi na kuwa wengi kupita kiasi ndani ya uke hadi uke wako kuto weza kuhimili ndio hapo hiki kitendo kinaitwa Bacterial Vaginosis.
🔶Mara nyingi Ukitaka kujua kua unasumbuliwa na Bacterial Vaginosis,utajikuta unapata Dalili zifuatazo
Uke kutoa maji maji mazito au mepesi yenye rangi ya njano au Brown yenye harufu mbaya
Maumivu kwenye maeneo ya nyonga
Hali ya kuwashwa ukeni
Maumivu ya kichwa
💠YEAST INFECTION
Katika Hali hii Mara nyingi uke ukumbwa na fungus candida albicans tofauti na bacteria vaginosis, fungus hawa Mara moja sana huwapata wanawake Katika maisha yao na nilazima.
🔶Mara nyingi ukitaka kujua unasumbuliwa na yeast infection utajikuta unapata dalili Zifuatazo
Uke wako ukawa unawashwa au usiwashwe
Kupata maumivu makali K**a vile waungua ukeni pindi unapopata haja ndogo
Uke kutoa maji maji mazito yenye rangi nyeupe k**a jibini

💠SEXUALLY TRANSMITTED DISEASES (STDs)
Kuna baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na kupeana Raha na Utamu bila Condom,k**a kaswende na kisonono k**a ukiyapata huwa yanasababisha Uke kutoa Harufu mbaya kwa sababu dalili zake zinahusiana na kutokwa na maji maji yenye harufu mbaya.
💠VAGINAL OR CERVICAL CANCER
Unapokuwa una kansa ya uke au kansa ya mlango wa kizazi ,kutokwa na maji maji yenye harufu mbaya ni sehemu ya dalili zake.Unapojiona kuwa una tatizo la uke kutoa harufu mbaya,ni heri na itakuwa busara ukienda hospitali,k**a ni kansa ya mlango wa kizazi itakuwa sio ngumu kuitibu k**a ukiwahi mapema.
💠POOR HYGIENE
Hii utokana na usafi wa mtu binafsi,Inawezekana pia tatizo la uke wako kunuka linasababishwa na uchafu. Unawezekana unaoga mara moja tu kwa siku au siku nyingine hata hauogi. Hauna mazoea ya kufua nguo zako za ndani na ikitokea siku umezifua basi hata hauzisugui zikawa safi.

ANGALIZO
Endapo utakua na tatizo la bacteria viginosis na yeast infection Aya ni matatizo ambayo yanaweza kutibika wai hospitalini mapema ili uweze kupata matibabu na uweze kupona mapema
🛑 Tatizo hili linatibika Wasiliana nami, ili uweze kupona mapema na kwa haraka.
Dr, AYOUB
📞0788945354

04/07/2024

Afya Bora ni Jambo la msingi kiafya, hufanya tuweze kufanikisha maendeleo yetu kiuchumi

Address

Mwanza

Telephone

+255788945354

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when afya Bora health posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to afya Bora health:

Share