Shayo health care

Shayo health care health education and advice

Grace Shayo:*TUNAWEZAJE KUWA PAMOJA KWENYE KUSHIRIKISHANA MAMBO MUHIMU YA USHAURI NA ELIMU JUU YA MASWALA YA  UZAZI, MAM...
09/08/2017

Grace Shayo:
*TUNAWEZAJE KUWA PAMOJA KWENYE KUSHIRIKISHANA MAMBO MUHIMU YA USHAURI NA ELIMU JUU YA MASWALA YA UZAZI, MAMA NA MTOTO BASI USISITE KUWA NAVYO HIVI CHINI:

1.Tunaweza jumuika pamoja Telegram;
https://t.me/joinchat/AAAAAA6vbJcLFx-Ya8huZg

2. Whatsapp group ;
Limeshajaa

3. Tunaweza pia kushirikishana mambo muhimu ya afya ushaur na elimu kupitia Application hii ;
https://www.androidcreator.com /app282615

4. Unaweza pia kuingia/kutembelea katika blog yangu ya
www.mtotoafya@blogspot.com" rel="ugc" target="_blank">www.mtotoafya@blogspot.com

UNAWEZA KUSHIKIKISHA NA WENGINE- Share kadri uwezavyo nitashukuru sana

By shayo grace

Email; gracedshayo@gmail.com .com

04/08/2017

JINSI YA KUREKEBISHA MZUNGUKO WA HEDHI

Jinsi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi
Tatizo la kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi huanza ghafla au polepole ambapo mwanzo mwanamke alikuwa akipata siku zake katika utaratibu unaoeleweka lakini mara haelewi au hajielewi namna mzunguko wake unavyoenda.
Kuvurugika kwa hedhi ni kitendo cha mwanamke kuanza kuona siku zake bila tarehe au mzunguko maalumu na matokeo yake ni kuwa mwanamke atashindwa kutimiza malengo yake kwa kutumia mzunguko huo sababu ni haueleweki.
Unaweza kutokewa ghafla tu unapata hedhi mahali usipotarajia jambo linakufanya ubaki na woga na huelewi nini cha kufanya kwani hukuwa umejiandaa kwa tukio hilo k**a matokeo ya siku zako kutokuwa mzunguko maalumu. Wakati mwingine unaweza kupitiliza mwezi hata miezi kadhaa bila kuona kabisa siku zako na hata ukipima ujauzito unakutwa huna ujauzito wala dalili huna.
Madhara ya kuvurugika kwa mzunguko ni pamoja na; kushindwa kupata ujauzito, maambukizi katika kizazi na kuziba kwa mirija ya uzazi.
Kwanini unahitaji mzunguko wa hedhi ulio sawa?

💥💥💥💥💥💥💥💥Faida za kuwa na mzunguko wa hedhi ulio sawa:

1⃣Utakusaidia kupata ujaouzito ulioupangilia
2⃣Utakuepusha kupata ujauzito ambao hukuupangilia
3⃣Utaweza kuamua jinsia ya mtoto unayemtaka

💥Nini husababisha kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi
Ni rahisi kugundua k**a mzunguko wako umevurugika ikiwa tu unauafahamu vizuri mzunguko wako ulio sahihi. Kufahamu mzunguko unahitaji uifahamu siku ambayo ulianza kuona damu hadi siku utakapoona tena katika mzunguko unaofuata. Karibu kila mwanamke huwa na mzunguko wake usiofanana na wa mwingine.
💥Tatizo linaweza kuanza kwa kurukaruka siku, mwanamke pia anaweza kupoteza siku yaani mwezi mwingine anaona na mwezi mwingine haoni, au anaingia mara mbili kwa mwezi au anaona damu ya hedhi kwa siku nyingi hata zaidi ya siku arobaini mfululizo. Damu yake inaweza kutokea kidogo kidogo kila siku au nyingi huku ikiambatana na mabongemabonge na maumivu pia. Maumivu haya ya wakati wa hedhi huenea chini ya tumbo mpaka miguuni na kiunoni.
💥💥💥💥💥💥💥💥Kuvurugika kwa hedhi kunaweza kutokea kutokana na sababu zifuatazo:
1⃣Mabadiliko ya mazingira ambayo hupelekea mfumo wa mwili hubadilika pia hasa mwanamke akitoka sehemu ya joto kwenda mikoa ya baridi au toka mikoa ya baridi kwenda mikoa ya joto.
2⃣Msongo wa mawazo (stress)
3⃣Hofu
4⃣Woga
5⃣Mabadiliko ya kisikolojia
6⃣Uvimbe kwenye kizazi
7⃣Matatizo kwenye mfumo wa homoni
8⃣Matatizo kwenye vifuko vya mayai
9⃣Mimba kuharibika
🔟.Maambukizi sugu ya kizazi pia ni mojawapo ya sababu.
1⃣1⃣Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ya mara kwa mara na kila ukipima unaambiwa ni ugonjwa wa U.T.I kumbe siyo yutiai
1⃣2⃣Kutokwa na uchafu ukeni
1⃣3⃣Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
💥Jinsi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi
Kabla ya yote unapopatwa na tatizo hili kwa muda mrefu ni vizuri ukaonana na daktari uweze kupata uchunguzi wa kutosha kubaini nini hasa inaweza kuwa ndiyo sababu hasa ya tatizo kwa upande wako
Pia hospital unaweza kupewa vidonge vya uzazi ili kurekebisha hedhi yako.
Ila pia waweza tumia vyakula Vifuatavyo kam njia mbadala

💥💥💥💥💥💥💥💥

Zifuatazo ni njia/chakula mbadala 6 unazoweza kuzitumia ukiwa nyumbani ili kurekebisha tatizo hili:

1. Papai
Papai ni moja ya chakula kizur sana katika kutibu tatizo la kuvurugika kwa hedhi. Ina viinilishe mhimu k**a carotene, chuma ( iron), Kalsiamu (calcium) na vitamini A na C ambavyo husaidia kulainisha na kunywea kirahisi kwa kuta za mji wa uzazi.
Siku 2 au 3 kabla ya kuanza kula papai kila siku nusu papai papai zima kutegemea na ukubwa wake au uwezo wako.
Kwa mtu mwelevu sababu ameshagundua papai laweza kumsaidia hivyo basi atalifanya papai kuwa sehemu ya chakula chake kila siku na si mpaka aumwe tu.
2. Mdalasini
Mdalasini unayo sifa ya kuondoa tatizo la damu kuganda sifa inayoweza kusaidia kuondoa tatizo la maumivu wakati wa hedhi.
Mdalasini ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (fiber), kalsiamu (calcium), chuma (iron) manganizi (manganese).
• Tengeneza chai ya tangawizi kwa kutumia kijiko kidogo cha mdalasini ya unga na maji kikombe kimoja (robo lita), ipua na uache ipowe kidogo, ongeza asali kijiko kikubwa kimoja ndani yake na unywe. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka mara tatu siku 2 au 3 kabla ya kuanza siku zako.
• Au changanya kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na kijiko kidogo kimoja cha asali katika glasi moja ya maji ya uvuguvugu na unywe kutwa mara 2 siku za mwanzoni unapoanza au kukaribia kuingia katika siku zako.
3. Tangawizi
Tangawizi ni dawa ya asili yenye maajabu katika kutibu tatizo la mvurugiko wa hedhi. Tangawizi hufanya kazi mhimu kabisa katika kushusha kiwango cha homoni inayosababisha maumivu ijulikanayo kwa kitaalamu k**a ‘prostaglandins’. Tangawizi husaidia pia katika kupigana na uchovu uletwao na mzunguko wa hedhi katika siku zile za mwanzo au siku 2 hivi kabla ya kuanza siku zako na huweza pia kufanya mzunguko usio sawa wa hedhi kuwa sawa
• Tengeneza chai ya tangawizi ukitumia tangawizi mbichi, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 wakati wa siku zako au siku yoyote tu k**a kinga. Kamulia ndimu kidogo ndani yake na utumie asali kupata radha badala ya sukari.
• Unaweza pia kuongeza tangawizi kwenye vyakula na mboga mboga nyingi unazopika kila siku.
4. KOTIMIRI (Parsley):
Tengeneza juisi ya kotimiri, viazi pori (Beet Root), karoti au matango. Tumia asali mbichi ukitengeneza juisi hii. Hii kotimiri inapatikana kirahisi Dar na Zanzibar ni mboga mboga inayotumika zaidi kwenye mahoteli ya kitalii. Mboga hii inacho kitu mhimu sana kijulikanacho k**a ‘Apiol’ amabcho kazi yake kuu ni kurekebisha na kuweka sawa homoni za k**e.
Changanya kwa ujazo sawa yaani k**a juisi ya kotimiri ni kikombe kimoja basi ya kiazi pori nayo kikombe kimoja kadharika kwa matango. Juisi hii ni dawa tosha ya maumivu wakati wa siku za hedhi, hurekebisha mzunguko wa hedhi na imethibitika kuwa bora kuliko dawa nyingi za kizungu.
Kunywa glasi moja ya juisi hii kutwa mara 2.
5. MREHANI
Mrehani au Basil kwa Kiingereza ni mmea mwingine mzuri sana katika kuondoa maumivu wakati wa hedhi na kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa ujumla. Mmea huu unatumika sana jikoni kwenye mahotel ya kitalii Dar na Zanzibar. Unao sifa kuu ya kuzuia au kuondoa maumivu mwilini.
• Ongeza kijiko kikubwa kimoja cha majani freshi ya mrehani yaliyokatwakatwa na kisu (chop) kwenye kikombe kimoja cha maji ya moto, funika vizuri na usubiri ipowe. Kunywa yote ikishapoa na ufanye zoezi hili kutwa mara 3 kwa wiki 3 mpaka 4 au mpaka tatizo lako limeisha.
• Au tengeneza juisi ya majani haya. Yatwange kwenye kinu au kwenye blenda ya umee kupata majimaji yake kisha chota vijiko vya chai viwili uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto na unywe yote. Fanya zoezi hili kutwa mara 3.
• Unaweza pia kuongeza majani freshi ya mrehani kwenye vyakula vingi unavyokula kila siku.
6. MAJI YA KUNYWA
Matatizo karibu yote mwilini chanzo chake ni mwili kutokuwa na maji ya kutosha. Maji ni uhai. Unachohitaji hapa ni kutokusubiri kiu. Kiu ni ishara ya mwili iliyochelewa kuhitaji maji.
Matatizo mengi ya kiafya tumeyaona kwa watu wasiopenda kunywa maji ya kutosha kila siku.
Jitahidi hata iweje iwe unaumwa au huumwi chochote unywe maji lita mbili mpaka tatu kila siku iendayo kwa Mungu na utaniletea mrejesho hapa hapa

03/08/2017

PID(PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI)
FAHAMU UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI)
PID ni kifupi cha Pelvic Inflammatory Disease ambayo ni maambukizi ya vijududu vya bakteria katika mfumo wa ndani wa uzazi wa mwanamke. Maambukizi yanaweza kuwa katika mji wa uzazi, mirija ya uzazi, ovari au shingo ya uzazi.
PID husababishwa na vijidudu vya bakteria kuingia kwenye mji wa mimba kupitia mlango wa shingo ya uzazi. Vijidudu hivi hutokana na magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa k**a kisonono au klamidia. Huingia kwenye mji wa uzazi na kisha kuweza kushambulia ovari,mirija au mji wa mimba wenyewe.
Dalili
P.I.D huleta dalili zifuatazo. Mgonjwa anaweza kupata zote au baadhi ya dalili hizi;
=>Maumivu ya kiuno
=>Kutokwa na uchafu ukeni
=>Maumivu wakati wa kufanya ngono
=>Kutokwa damu baada ya kufanya ngono
=>Maumivu chini ya kitovu baaada ya kufanya ngono
=>Maumivu wakati wa kukojoa
Mara nyingi dalili huwa sio kali na wakati mwingine zinaweza kutokea kwa kipindi cha muda mrefu. Wakati mwingine mwanamke anaweza kupatwa na dalili ghafla na kali hasa maumivu ya tumbo.
Vipimo
Vipimo hivi vinaweza kufanyika kujua k**a kuna ugonjwa wa PID.
=>Kipimo cha ultrasound
=>Kipimo cha magonjwa ya zinaa (VDRL)
=>Kuotesha uchafu wa kwenye uke (Cervical/vaginal swab for culture)
Matibabu
Mara nyingi tatizo hili hutibiwa kwa njia ya dawa za antibiotics kwa muda wa siku 14 ni muhimu kuzingatia matumizi na kukamilisha dozi ya dawa ili kuhakikisha umepona kabisa.
Madhara
PID isipotibiwa huleta madhara kwa mgonjwa hasa ikiwa ni hali ya ugumba na hata utasa.
Kujikinga
Kujikinga na PID, ni muhimu kujikinga na magonjwa ya zinaa kwa;
kuwa na mpenzi mmoja uliyepima nae afya na magonjwa ya zinaa.
kutumia kondomu kila mara unapofanya ngono.
kuacha tabia ya kuwa na wapenzi wengi.
Unaposhisi dalili za magonjwa ya zinaa, wahi hospitali kupata matibabu sahihi na hakikisha umepona.

30/07/2017

MAANDALIZI YA MAMA MJAMZITO KABLA YA KUJIFUNGUA

💥💥💥💥💥💥💥💥
Mama mjamzito anatakiwa kuanza kufanya maandalizi
muhimu yanayohitajika wakati wakujifungua, ni muhimu
kufanya maandalizi kabla ya kujifungua ili muda ukifika
mama mjamzito asije akakurupuka tu kukimbilia
hospitali bila kubeba vitu vya muhimu akiwa huko.
Vitu vya muhimu vya kujua na kuandaa kabla ya
kujifungua ni;
1. MAUDHURIO YA KLINIKI
Mama mjamzito na familia kwa ujumla wanatakiwa
wahakikishe kabla ya kujifungua mama awe
amehudhuria kliniki ya afya ya uzazi angalau mara nne,
mama baada ya kujitambua kuwa ni mjamzito anatakiwa
audhurie kliniki ya wajawazito kati Ya wiki 8-12 ya
ujauzito. mama ahudhurie kliniki katika kituo cha afya
ambacho kipo karibu nae.
KWANINI?
 Kufuatilia afya ya mama ikiambatana na
kuchunguza dalili za hatari ambazo zinaweza
kuhatarisha afya ya mama na mototo wakati
wa ujauzito
💫💫💫💫💫💫 Kutambua, kutibu na kuzuia matatizo ya
kiafya yanayoweza kuhatarisha maisha ya
mama na mtoto wakati na baada ya ujauzito
k**a vile malaria,upungufu wa damu
(anemia), HIV, magojwa ya zinaa na
maambukizi kwenye njia ya mkojo.
 Kufuatilia maendeleo ya ukuaji wa mtoto
 Huduma anazopaswa kupata wakati wa
mahudhurio ya kliniki
 sindano za kuzuia tetenasi walau
mara tatu,
 dawa za SP kwa ajili ya kuzuia
malaria walau mara tatu
 dawa za minyoo mara moja
 vidonge vya madini ya chuma kwa
ajili ya kuzuia upungufu wa damu
💥💥💥💥💥💥💥Kupitia mahudhurio ya kliniki mama
atafahamishwa yafuatayo
 Tarehe ya matarajio na njia ya
kujifungua na mahari pa
kujifungulia
 Dalili za hatari wakati wa ujauzito,
k**a vile kichwa kuuma, kutokwa
na damu au majimaji ukeni,
maumivu makali ya tumbo,
kutapika kupita kiasi, kuvimba
miguu, mikono na uso,kupatwa na
uchovu uliopitiliza hadi
anashindwa kuamka, kuhisi
kizunguzungu,
💥💥💥💥💥💥 MAANDALIO BINAFSI KABLA YA
KUJIFUNGUA.
 Kiuchumi, japokuwa huduma ya kujifungua ni
bure katika hospitali za serikali lakini ni muhimu
kufanya maandalizi ya kifedha kwa ajili ya
mambo mengine ambayo yanaweza jitokeza
katika kipindi cha kujifungua
 Usafiri, Mama mjamzito na familia yake
wanatakiwa waandae usafiri wa kumpeleka
mama mjamzito sehemu atakayojifungulia pia
kumrundisha nyumbani baada ya kujifungua.
 Mtu wa kumsindikiza siku ya kujifungua,
familia inatakiwa iandae mtu atakaye ambatana
na mama mjamzito hospitali na atakae baki
nyumbani na familia k**a ni familia ya baba na
mama tu.
 Mavazi, Mama mjamzito anatakiwa aandae
mavazi ya uzazi; hapa inamaanisha nguo za
kuvaa baada ya kujifungua pia nguo za
kumvalisha mtoto atakaekuwa amezaliwa; k**a
vile khanga na vitenge ,babyshow, soksi, kofia
pampers na whipers. na vitenge havitakiw
kuwa vipya ni bora kuchukua vilivyokwisha
valiwa na kufuliwa walau mara moja na vikiwa
safi
 Lishe bora, mama anatakiwa kupata lishe bora
kwa kipindi chote cha ujauzito na hata baada ya
kujifungua, mama anatakiwa kupata chakula bora
chenye virutubisho vyote muhimu mwili k**a
hususani vile vinavyo mzunguka bila kusahau
mboga mboga, matunda, nyama, maini,
maharagwe kwenye milo yake angalau mara
moja kwa wiki. Chakula ni muhimu katika
Nyanja tatu ambazo ni afya ya mama, afya ya
motto na kupunguza maudhi madogo madogo
wakati wa ujauzito
 Vifaa, andaa vifaa k**a mipira ya kuvaa
mikononi, wembe, Tembea navyo kwenye mkoba
popote uendapo maana hujui siku wala saa
itakapotokea dharura ili wasamaria wakusaidie,
Tembea na khanga hata mbili kwenye mkoba
wako kila uendapo. Note: kuanzia wiki ya 37
✨✨✨✨✨✨ MAMBO MUHIMU KUZINGATIA WAKATI WA UJAMZITO
 Mambo anayotakiwa kufanya
o Mazoezi mepesi k**a vile
kutembea
o Kupata muda wa kupumzika
wakati wa mchana pia usiku
o Mama apate mlo kamili
o Mama anatakiwa kuwa msafi wa
mwili na mavazi
o Kufuata maelekezo na ushauri
kutoka kwa wataalamu wa afya.
 Mambo ambayo mama mjamzito hatakiwi
kufanya
o Matumizi ya pombe na madawa
ya kulevywa
o Matumizi ya sigara, uvutaji wa
sigara unahusishwa na madhara
k**a kudumaa kwa ukuaji wa
motto angali tumboni, kuzaa
mtoto njiti, husababisha kifo cha mtoto mara baada ya
kujifungua, inaongeza
maambukizi mambukizi ya
mapafu na damu kuganda
kwenye mishipa ya damu.
o Mama hatakiwi kuvaa nguo
zinazobana na viatu vywenye
visigino virefu.
o Hatakiwi kutumiwa dawa
ambayo hajaandikiwa na
daktari
o Mama hatakiwi kusafiri mara
baada ya mimba kufikisha wiki
ya 32
o Asitumie chai wakati wa
chakula

20/10/2015

ZIJUE SABABU ZINAZOFANYA UGONJWA WA UTI
KUONGEZEKA KWA KASI KWA WANAWAKE SASA
TOFAUTI ZA ZAMANI
UTI kwa lugha ya kigeni huitwa URINARY TRACK
INFECTION(UTI) au kwa kiswahili tunasema ni
maambukizikwa njia ya mkojo,ugonjwa huu
husababishwa zaidi na bacteria ambao wanapatika
ndani ya sehem za siri za mwanamke bacteria
hawa wakiwa ndani ya uke hawana madhara
kabisa,lkn pindi uke unapopata mchubuko bacteria
hawa huanza kuathiri kibofu cha mkojo na mtu
kuanza kupata madhara.Wanawake wanapata UTI
kwa urahisi saana kuliko wanaume kwa sababu
urethra ya mwanamke ni fupi ambayo huruhusu
bacteria kuingia kwa urahisi tofauti na urethra ya
mwanaume.
VYANZO VYA UTI
1.Maji machafu,matumizi ya maji machafu wakati
wa kujisafisha huweza kuweka bacteria kwa urahisi
na mwanamke kupata UTI.
2.Vyoo kuwa vichafu,pia matumizi ya vyoo
ambavyo ni vichafu huweza kusababisha
mwanamke kupata UTI kwa sababu ndani ya choo
kunabacteria wengi amabao wanawezasababisha
UTI.
3.NGONO,kufanya ngono mara kwa mara ni tatizo
kubwa ambalo ndilo linafanya wanawake wengi
kupata UTI siku hizi kwani wakati wa ngono
msuguano huwa mkubwa ambao hufanya bacteria
kutoka kupitia maji maji ya ukeni na kuingia ktk
njia ya mkojo,
Mwanamke ambae anafanya ngono mara kwa mara
yuko kwenye hatari ya kupata UTI kuliko yule
ambae hafanyi ngono mara kwa mara.
4.Kuvaa nguo za mitumba bila kufua,matumizi ya
nguo za mtumba bila kufua husababisha kwa
urahisi mwanamke kupata UTI kwasababu ndani ya
nguo zile kunabacteria.
6.KEMIKALI hili ndo tatizo kubwa ambalo
linawaathiri wanawake wengi siku hizi kutumia
saana kemikali hasa kwenye vipodozi ambapo
kemikali hizi kwa kuwa ni sumu huenda hadi
kwenye kibofu na kuchubua kibofu hapo ndo balaa
huanzia.
7.Kubana mkojo kwa muda mrefu,pia kubanah
mkojo kwa muda mrefu kunasababisha UTI.
DALILI ZA UTI
1.Mwili kuchoka mara kwa mara
2.Homa ya mara kwa mara
3.Kichwa kuuma mara kwa mara
4.Kubanwa na mkojo halafu ukienda kukojoa
unakuta mkojo kidogo
5.Maumivu wakati wa kukojoa
6Kiuno kuuma.
USIHOFU UNAWEZA PATA KINGA YA U.T.I NA
USIUGUE MAISHA YAKO YOTE KWA KWA
MAWASILIANO

28/08/2015

MASHARTI KUMI YA KUZINGATIA
UWEZO KUPUNGUZA KITAMBI NA
UZITO MKUBWA BY DR MKUMBO
1-ULAJI
Ipo mifumo miwili ya kula. Chakula unachokula na
namna unavyokila.
Unavyokula.
-Kuna kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini,
vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku; au kula
milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili
kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya
na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa
mara chache. Tumbo lina musuli zinazofanya kazi
k**a mashine au mnyama. Gari likijaa sana
hupata taabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji
mdogo mdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa
siku ni bora maana mwili unachambua kila kitu
kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache
mikubwa unapalilia zaidi mafuta mwili.
(PENDEKEZO la kwa
nza. Asubuhi, kunywa maji kwanza, matunda,
kisha ndiyo chai na vitu vingine k**a mkate au
maandazi…)
-Wapo wanaodai kwamba wanakula matunda na
mboga.
Tatizo ni kwamba mipangilio yao huwa ya
makosa. Mathalan wengi hula matunda baada ya
chakula. Vimeng’enya chakula (enzymes)
tumboni hufanya kazi namna tofauti. Mathalan vile
vinavyonyambua matunda ni tofauti na
vinavyomeng’enya vitu vigumu zaidi k**a nyama
au wanga. Matunda hunyambuliwa haraka zaidi
kuliko vyakula vingine. Hivyo ni bora kula
matunda dakika10-20 kabla ya chakula. Ukila
baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe
(fermented food) inayoelea tu juu ya chakula na
kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka
ndani ya damu kupitia utumbo mdogo, uwengu,
moyo, ini, nk.
Tatizo jingine ni kupika sana mboga hadi
zikapoteza nguvu.
-Mseto wa vyakula pia ni muhimu. Kwa mfano
vyakula vyenye uchachu (“acid”) na vile
vinavyomumunyuka haraka (“alkaline”) havitakiwi
viliwe pamoja. Mfano ni matunda. Matunda
chachu k**a machungwa, mananasi na maembe
yatakiwa yawe pamoja; na yale laini zaidi: ndizi
mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk
Hali hiyo pia iko katika nyama. Nyama nyeupe
(ndege na samaki) tofauti na nyama nyekundu
(ng’ombe, kondoo, nk) ziliwe tofauti.
Chakula unachokula
Waafrika hatuna tabia ya kula mboga mboga
mbichi. Tunafuata ladha na mazoea kuliko
thamani.
Bara letu lina mboga na vyakula bora kuliko bara
lolote duniani lakini sisi tunakufa mapema na kwa
utapia mlo kuliko wale wanaotoka nchi kame.
Ulaya nzima imejazana mboga mboga
zinazoagizwa toka Afrika. Kenya na Tanzania
zinauza mboga za maharagwe mabichi (green
beans), matunda toka Afrika Kusini na Ivory
Coast; nk. Waafrika tunapenda kujaza matumbo.
Unene umekithiri hata wale walio matajiri
waliosoma bado wanakufa kwa kisukari shauri ya
kutokula mboga mbichi.
Ulaji wa mboga mbichi ni upi?
Ni mathalani ulaji wa salad. Tanzania tunaita
kachumbari. Lakini si lazima iwe kachumbari ya
nyanya, vitunguu na chumvi tu. Waweza
kuchanganya matango, nyanya kwa maparachichi;
au vitunguu saumu, giligilani na karote. Huu
mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukienda na
chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali,
wali, ndizi za kupika nk). Ulaji wa wanga asubuhi,
mchana na jioni kila siku huchangia sana katika
unene.
(PENDEKEZO LA 2. Ugali kwa samaki; mboga ya
majani ya matango kwa nyanya. Usiweke chumvi
kwenye chakula
2-UNYWAJI MAJI
Waafrika hatunywi maji, hasa wanawake.
Wanaokunywa maji zaidi ni wacheza michezo.
Wengi wetu hunywa zaidi soda (vinywaji baridi
k**a Cocacola, Pepsi, Mirinda ,Tangawizi na gesi
za kisasa k**a Red Bull) zilizojaa gesi inayoleta
vidonda tumboni; na chai. Kuliko maji. Na maji
haya hutakiwa dakika 10-20 kabla ya chakula au
nusu saa kuendelea baada ya chakula. Ukila
chakula huku unasakatia maji huimanisha mtu
una kiu. Ulaji chakula na unywaji maji ni vitu
viwili tofauti. Ila utawaona watu wanakula huku
wakibugia maji. Unapokula chakula huku unabugia
maji unapunguza nguvu za chakula, unajaza
tumbo maji na kuchelewesha mmeng’enyo wa
chakula (digestion).
Chakula kisipomeng’enywa vizuri kinaketi tu
tumboni. Matokeo wengi wetu tuna matumbo
makubwa. K**a hufanyi mazoezi lile tumbo
linakwenda pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa
watu wa makamo linaleta maradhi k**a kisukari,
kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbo, nk.
Kizungu huitwa “love handles.”…
3-SUALA LA UMENG’ENYAJI
Chakula huanza kumeng’enywa au kusagwa (kwa
lugha iliyozoeleka) mdomoni. Mate yako mdomoni
ni chanzo cha uchambuaji chakula. Unapobugia
chakula bila kutafuna sawasawa unasababisha
mambo mawili. Moja chakula kutochambuliwa
vizuri, pili chakula kwenda kukaa tu tumboni, au
k**a kikipita hakisaidii lolote mwilini. Utafunaji
wa taratibu husaidia umeng’enyaji. Chakula
kinapofika tumboni hukaa pale dakika ishirini.
Hapo huchanganywa na asidi (ya manjano iitwayo
Hydrochloric) inayokibadilisha tayari kupelekwa
utumbo mkubwa, kupitia kongosho. Kule uchafu
utapelekwa chini na rutuba kusafirishwa na
utumbo mdogo kuelekea katika uwengu, moyo.
Moyo utadunda chakula kilichoshageuzwa damu
kuelekea mwilini kufanya kazi na akiba
hubakishwa katika ini.
Sasa k**a usipotafuna vizuri, ukila huku
unakunywa sana maji au vinywaji vingine chakula
hakimeng’enywi vizuri. Ndiyo maana unawaona
watu wengine wanakula sana lakini hawana afya.
Wanaugua ovyo ovyo, wanatoka jasho ovyo,
wanajamba ovyo, wana matumbo makubwa,
wanavimbiwa, wanakaa siku nyingi bila kwenda
choo (inatakiwa mtu kwenda haja kubwa mara
moja au mbili kwa siku) nk.
4-ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA
Mafuta ni suala muhimu sana mwilini. Ila ulaji
wake shurti uwe wa mpangilio. Yaani unaowiana.
Lazima mtu uwe na wastani mzuri wa vyakula vya
nguvu, yaani “wanga” (ugali, ndizi, wali, viazi
mbalimbali, mikate, mahindi, nk), ujenzi yaani
“protini” (mboga na nyama), “madini” (mbegu
mbegu mbichi si za kukaanga sana na chumvi) na
“vitamini” (matunda, maziwa, mayai, nk).
Waafrika tunapenda nyama. Nyama ni muhimu
sana maana ina madini aina ya chuma (nyama
nyekundu) protini,nguvu na mafuta. Ila mafuta
yaliyoko katika nyama mara nyingi si mazuri
shauri hayatoki, huganda. Chukua nyama ya kuku
na samaki ambayo huwa na ngozi. Wengi wetu
hupenda sana kula ile ngozi ya wanyama hawa
kwa kuwa tamu. Lakini haya ni mafuta mabaya.
Mafuta ya samaki lakini ni mazuri. Samaki anayo
mafuta ya Omega-3 ambayo husaidia mwili na
kinga maradhi mwilini.
Tunapokula nyama choma au ya kukaanga, lazima
tule pia mboga za majani (mbichi) na si vizuri
kula nyama kila siku. K**a huwezi kukaa bila
nyama kila siku, fanya mazoezi ya mwili.
PENDEKEZO LA 3- Kula mbegu mbegu za
korosho, karanga au mlozi (ziwe mbichi badala ya
kukaanga na chumvi) kati kati ya siku. Haya ni
mafuta yenye rutuba mwilini kuliko nyama za
mafuta.
5-MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO
Mazoezi ni mfalme wa kupunguza unene.
Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi
ngumu za sulubu (wanachuruzikwa jasho) kwa
hiyo hayo ni mazoezi. Ila kazi na mazoezi ni vitu
viwili tofauti. Ingekuwa kufanya kazi ni mazoezi
basi kusingekuwa na wastani mfupi wa maisha
kwa maskini hasa sisi Waafrika.
Wengine watadai kwamba walipokuwa wadogo
shuleni walifanya mazoezi sasa wamekuwa watu
wazima (miaka 40 kuendelea) kwamba eti
mazoezi ni suala la ujana; kumbe kadri
unavyokuwa ki umri ndivyo kadri unavyotakiwa
kufanya mazoezi na kujitazama zaidi kiafya.
Watazame Wachina na Wajapani wanavyoishi
maisha marefu.
Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme
(mapafu na moyo kwenda kasi), viungo na mifupa
kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na
usafishaji wa damu. Mazoezi yanayosaidia haya ni
pamoja na kutembea kasi, kukimbia, kuogelea,
michezo mbalimbali ya riadha (k**a mpira wa
miguu, nyavu, kikapu, mikono, nk); michezo ya
kupigana na kujilinda yaani masho ati(karate,
kung fu, judo, capoeira, krav maga, jiu jitsu,
systema, kickboxing, thai boxing, kempo, kalari
payatu, aikido, nk) …
Ni muhimu mwanadamu ufanye mazoezi makali
ya viungo mara mbili tatu kwa juma. Si vizuri
kufanya kila siku kwani musuli na mishipa
inahitaji kupumzika na kukua.
K**a unapenda kuinua vyuma lazima uwe na
mwalimu wa kukuelekeza; na si vizuri kufanya kila
siku. Wastani wa mara mbili tatu kwa juma
inatosha kabisa.
6-UPO UFANYAJI MAZOEZI WA AINA MBILI
Mazoezi ya nguvu ya kuhema niliyotaja hapo juu
(cardio-vascular) na yale laini ya kujinyoosha
yaani ambayo hutumia zaidi nguvu za ndani na
pumzi. Haya ya pili ni k**a Yoga (India) , Tai Chi
Chuan (China) na aina mpya mazoezi iliyoanza
Majuu miaka ya karibuni yaani Pilates (hutamkwa
hivyo hivyo ilivyoandikwa Pilates). Haya laini
yanawafaa zaidi watu wazima na nchini China na
Japan mathalan utawakuta wazee wa miaka 80
hadi 90 bado wanayafanya. Husaidia moyo, damu
na akili.
Michezo na mazoezi ya mwili ni njia kuu ya
kupunguza unene, kurefusha maisha,
kuchangamsha ubongo, kupunguza ulevi, uvutaji
sigara, dawa za kulevya, tabia mbaya za uvivu,
ugomvi, nk. Mataifa yenye watu wanaofanya
mazoezi k**a Japan, Brazili, India, China nk
huwa na wachapa kazi wengi na wananchi
wanaoipenda jamii yao.
7-KULA SANA CHUMVI SI VIZURI
Ulaji chumvi mwingi hutokana na suala la ladha.
Kisayansi vyakula vyote vina chumvi asilia sema
tu tumezoea kuongezea madini hii iitwayo
Sodium. Sodium inachangia sana kufupisha
maisha. Huifanya mishipa ya damu ichoke; ni
k**a bomba lolote la maji ukilitazama baadaye
hugeuka rangi kutokana na yale maji kupita pale
kila siku.
Kwa wale tunaoishi nchi za joto na kutoka sana
jasho kula chumvi ni muhimu. Ila tatizo letu ni
kwamba hatunywi maji ya kutosha. Mtu ukiwa na
kiu unakunywa soda au kinywaji cha sukari;
inakuwa k**a unaendelea kuutesa mwili. Kwa
vipi? Mishipa inayopitisha damu mwilini badala ya
kusaidiwa kwa maji inawekewa kazi zaidi ya
kusafisha sukari na chumvi. Ndiyo maana vifo
vingi vinatokea mapema; wastani wetu wa maisha
haupiti miaka 50.
Utafiti uliofanywa chuo kikuu cha California,
Marekani mwanzoni mwa 2010, umethitibisha
kwamba vifo vingi duniani husababishwa na
maradhi ya moyo na saratani ambavyo hutokana
na uvutaji sigara, unene, ulevi na ulaji sana wa
chumvi na sukari. Tukipunguza ulaji wa chumvi
tunasaidia pia kupunguza maradhi ya moyo, utafiti
unasema.
8-TAFITI ZA VYUO KADHAA ULIMWNGUNI
KUHUSIANA NA AFYA
-Jarida la Kimarekani la sayansi lilieleza mwaka
jana kwamba utapunguza ugonjwa wa moyo
(ambao husababishwa na unene , wasiwasi na
purukshani) kwa asilia mia 42 k**a utakula
matunda na mboga za majani peke yake kila siku,
juu ya msosi wa kawaida.
(PENDEKEZO LA KULA- Na 4- Kula mlo wako.
Baada ya saa mbili au tatu, sakatia tunda au
matunda; baada ya mlo mwingine, kula sahani ya
mseto wa mboga mbichi k**a karote na
matango. Utaona tofauti ya afya, ngozi, wajihi,
kinyesi, usingizi, nk. Kidesturi tumezoea kunywa
chai au soda za sukari sukari na gesi kati kati
nya milo badala ya matunda na mboga mbichi za
majani).
-Utafiti uliofanywa na wanasayansi chuo kikuu
cha South Carolina mwanzo wa mwaka 2010
kuhusu faida za kuogelea.
Zoezi la kuogelea lina faida zaidi ya kukimbia au
kutembea kwa vile huchanganya mazoezi makali
na pumzi, kusaidia mapafu na moyo. Utafiti
ulithibitisha kuogelea hupunguza hatari za kifo
kwa asili mia hamsini.
-Utafiti wa jarida la chuo cha uganga Ulaya
umeeleza (desemba 2009) kwamba kulala nusu
saa kila mchana (“nap”) husaidia kupunguza
ugonjwa wa moyo kwa asilimia 37.
-Uchunguzi wa chuo cha michezo cha Hispania
mwanzoni mwa 2010 umethibitisha kwamba
ukikimbia mara tatu kwa juma (jogging)
unaongeza nyege mwilini kwa asili mia 75. Hasa
kwa watu wa makamo mnaoanza kupoteza nguvu
za urijali.
-Uchunguzi chuo kikuu cha Leeds, Uingereza
mwanzoni mwa 2010 umeonyesha unapotembea
kwa miguu, ukikwepa barabara kubwa zisisokuwa
na mioshi ya magari (pollution) unapunguza
matatizo ya maradhi ya hewa chafu k**a pumu,
mapafu na appendix.
-Uchunguzi wa chuo kikuu cha Texas mwaka
2010 umegundua kwamba kula tunda la divai
nyekundu mara kwa mara husaidia kupunguza
kupata ugonjwa wa kisukari.
-Hapo hapo tunaelezwa kwamba watu weusi na
bara la Asia wanakumbwa zaidi na ugonjwa wa
kisukari kutokana na vinywaji vya sukari sukari na
gesi (fizzy drinks). Ukinywa kiasi cha miligramu
300 za vinywaji hivi (Cocacola, Red Bull, Fanta
)
9-KUFUNGA
Neno kufunga linatambuliwa rasmi kuhusiana na
Waislamu (mwezi Ramadhani) au Wakristo (Lenti
nk). Ufungaji huo una masharti mengine ya kidini
tofauti na haya ya kiafya.
Mathalani wafungaji hawa hula chakula kingi
usiku; ukihesabu wanafunga wastani wa saa 12
tu. Kawaida ukitaka virusi na takataka nyingine
mwilini zitoweke, au viungo vipumzike wahitaji
saa 20 kuendelea.
Ufungaji ninaouongelea ni ufungaji wa kutokula
kabisa kwa saa 24, 36 hadi 48 kuendelea…
Ufungaji ni nini?
K**a mashine yeyote mwili wa mwanadamu
unahitaji kupumzika na kujisafisha. Hata tukiwa
tumelala bado viungo mbalimbali mwilini
vinafanya kazi. Kwa hiyo faida ya kwanza kabisa
ya kufunga ni kuupumzisha mwili k**a
mfanyakazi yeyote anapokwenda likizo.
Faida ya pili ya kufunga ni kusafisha mwili
kutokana na uchafu ambao haukutoka (kinyesi
hakitoi mabaki yote toka utumbo mkubwa), dawa
na takataka za mazingira tunayoyavutia hewa,
virusi au kuyanywa katika maji na vyakula
mbalimbali na pia uchafu wa hisia, yaani hasira,
huzuni, nk.
Kuna ufungaji wa aina mbalimbali.
1-Kufunga kwa kunywa maji tu, saa 24
kuendelea…
2-Kufunga kwa kutokunywa maji au kula
chochote, saa 24 kuendelea…
3-Kufunga kwa kula tu matunda au mboga
zilizopondwa k**a karote, matango nk, saa 24
kuendelea…
Ufungaji huu unatakiwa ufanywe kwa mpangilio.
Kitu muhimu si tu kufunga bali NAMNA
unavyofungua. Ukianza kula tena, unaanza
taratibu. Kawaida ni vizuri kuanza na maji,
kikombe au bilauri ya kwanza taratibu. Subiri tena
nusu saa, bilauri nyingine, halafu hadi ya tatu,
halafu ndiyo matunda yasiyo ya chachu, na
kadhalika. Kuanza kufungua kwa kunywa chai ya
maziwa, uji au vyakula vingine vya wanga
hakusadii sana mfungo huu.
Maana lengo lake ni kusafisha mwili.
PENDEKEZO LA 5- Kwa wenye imani za kidini.
Unaweza pia kufunga hivi ukawa pia unasali au
kuvaa mavazi yanayokufanya mtu wa amani.
Ukifanya hivi unajitakasa kimwili na kiroho. Si
lazima ungojee ile miezi ya kufunga na wengine.
10-USINGAJI
Usingaji au masaji ni njia nzuri sana ya
kupunguza unene. Ikiwa unaangalia namna
unavyokula, unafanya mazoezi na kusingwa mara
moja au mbili kwa mwezi unaupalilia mwili vizuri.
Nini faida ya usingaji? Kusinga husaidia ngozi,
mishipa ya damu na sura nzima ya mwili na
taswira yako mwanadamu. Wengi wetu
tunaposikia neno kusinga tunafikiria usingaji wa
mapenzi. Hivi ni vitu viwili tofauti kwani usingaji
wa mapenzi unaimanisha mahusiano ya kihisia.
Kifupi mwanadamu unatakiwa uwe unautunza na
kuungalia mwili wako k**a nyumba au hekalu
lako. Wengi wetu tunaoga, tunajipaka marashi,
tunasuka, tunanyoa nywele au ndevu; lakini miili
yetu kiundani inaoza taratibu…
Kwa maswali ya kiafya chakula k**a tiba
unaweza kunitumia sms kupitia no 0754509936

Address

Njombe

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Shayo health care posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram