
19/07/2024
Hello Weight Watchers
Hivi ulishawahi kuwaza ni namna gani *UTI WA MGONGO NA MIFUPA YETU INAVYOELEMEWA NA UZITO* tuliokuwa nao?
Unajua moja ya kazi za mifupa ni kubeba nyama za misuli na zinginenzo, pia mifupa kazi yake ndio kukupa shape ya mwili wako.
Sasa tunakutana na changamoto nyingi sana ikiwa mwili wako umezidi uzito:-
📌 Lakini nimeshakutana na wamama wengi, na hapa nitaongelea wale waliotoka kujifungua wakilalamika sana kuhusu kuumwa kwa mgongo wa chini huku wakihusisha na sindani wakati za operation…😢😏 (_hili somo la kujitunza uzito kabla ya kujifungua na baada litafundishwa_)
📌Wakati mwingine, watu wengi tunalalamika sana *MAGOTI KUUMA, VISIGINO KUWAKA MOTO!*
Na mengine mengi mengi…
Haya kwa haraka haraka tunaenda kunywa _painkillers_ k**a vile panadols, diclofenac… kutuliza maumivu.
Ukweli ni kwamba *MIFUPA YETU ESPECIALLY ULE UTI WA MGONGO* umeziwa na UZITO MKUBWA SANA, hata k**a ni kilo 5 tu inaweza kuleta madhara makubwa sana, k**a kusagika kwa pingili na kadhalika. Embu fikiria uwe na FIMBO ambayo umetundika kilo 5 masaa 24 kwa siku na isimame, siku moja ile fimbo utaikuta imepinda. Ndio maana wengi sana wenye uzito mkubwa huishia kupata *MATEGE YA UKUBWANI AU KIBIONGO* yaani kutembea kwa kuinama. Si hivyo tu, wengi wetu wenye UZITO ZAIDI kwa sasa tuna matatizo ya *MAGOTI KUUMWA NA MIGUU KUPATA GANZI* Hizi changamoto zote zinatokana na kuzidiwa kwa mifupa na kubana hata mishipa ya fahamu kufikisha ujumbe au mishipa ya damu kupelekea oxygen na virutubisho vingine!
*USHAURI WA HARAKA*
Punguza UZITO HARAKA! Madhara ya kubaki na uzito kwa mifupa na uti wa mgongo ni makubwa kuliko tunavyodhani. Maumivu, kupinda kwa mwili, kusagika kwa mifupa nk yanaongezeka kila lisaa unalozidi kukaa na uzito huo. Kila dakika ipitayo ndio inavyozidi kuumiza mwili.
Pia zuia haraka matumizi ya DAWA ZA MAUMIVU maana nazo zina madhara makubwa sana kwenye miili yetu hasa kwenye FIGO NA INI.
Tuanze kujali leo UZITO wetu kuzuia changamoto za mifupa na viungo ...