04/01/2024
Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 04.01.2024
Wan-Bissaka alijiunga na United kutoka Crystal Palace msimu wa joto wa 2019
Manchester United inapanga kuanza mazungumzo juu ya mkataba mpya na beki wa Uingereza, Aaron Wan-Bissaka mwenye umri wa miaka 26 mwishoni mwa msimu huu. (Mail)
Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 31, anakaribia kuongezewa mkataba mpya katika klabu ya Liverpool licha ya kutakiwa na Saudi Pro League. (Football Transfers na Anfield Watch)
Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF) umefufua nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City na Ubelgiji, Kevin de Bruyne, mwenye umri wa miaka 32. (Rudy Galetti)
Borussia Dortmund wanataka kumsajili beki wa kushoto wa Chelsea, Ian Maatsen, 21, kwa mkopo au kwa mkataba wa kudumu. (Telegraph)
Dortmund wanataka winga wa Manchester United, Muingereza, Jadon Sancho, 23, ajiunge na timu hiyo kwa mkopo katika kambi yao ya mazoezi ya Marbella wiki ijayo. (Sky Sports)
Manchester United wana nia ya kumfanya winga wa Crystal Palace Michael Olise, 22, kuwa mmoja wa wachezaji wa kwanza kusajiliwa huko Old Trafford. (Standard)
Crystal Palace wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uingereza, Eddie Nketiah lakini Arsenal hawatamuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 mwezi Januari - ikiwa hawatapata mbadala wake. (Ben Jacobs)
Meneja wa Girona, Michel Sanchez ameibuka k**a mbadala wa meneja wa Newcastle United Eddie Howe. (Marca)
Klabu ya Ligue 1 ya Ufaransa, Lyon inataka kumsajili winga wa West Ham na Algeria, Said Benrahma, huku Wolves na Fulham pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Footmercato)