Heritage herbal clinic-Hhc

Heritage herbal clinic-Hhc Watoaji wa huduma za afya kupitia mimia . tumebobea kwa Matibabu ya dawa za asilia yaani miti shamba.

🌿 Tambua Thamani Yako: Afya Njema Huanza na KujitambuaKila mtu duniani ana thamani ya kipekee. Lakini mara nyingi, maish...
22/12/2025

🌿 Tambua Thamani Yako: Afya Njema Huanza na Kujitambua

Kila mtu duniani ana thamani ya kipekee. Lakini mara nyingi, maisha ya haraka na changamoto za kila siku hutufanya tusahau jambo hili muhimu — wewe ni wa maana, na unastahili maisha yenye afya na furaha.

Kujitambua na kuelewa thamani yako ni hatua ya kwanza ya mafanikio ya kweli. Unapojua kuwa unastahili mema, unaanza kujitunza zaidi — kimwili, kiakili, na kiroho. Afya njema si bahati, bali ni matokeo ya upendo wa kweli kwa nafsi yako.

Njia moja ya kuonyesha upendo huo ni kwa kutunza mwili wako kwa njia ya asili. Mimea tiba imekuwa ikitumika kwa maelfu ya miaka kutuliza mwili, kuimarisha kinga, na kurudisha nguvu za asili. Dawa za mitishamba husaidia mwili wako kupata uwiano, huku zikiuimarisha bila madhara.

Hapa ndipo hekima ya tiba asilia inapoangaza — Hertage Herbals, chini ya uongozi wa Dkt. Bituro, imejikita katika kuleta suluhisho za kiafya zinazotokana na mimea halisi. Kupitia uzoefu wake wa kina katika tiba za mimea, tupigie kwa no 0757876596

07/12/2024

Sababu za upungufu wa damu mwilini
1.Upungufu wa madini ya chuma mwilini
2.Upungufu wa vitamini A na B-12 mwilini
3.Maradhi k**a HIV, UKIMWI, saratani, mardhi ya figo haya huweza kuleta upungufu wa damu
4.Mfumo wa kinga mwilini kuuwa na kuharibu seli hai nyekundu (autoimmune)
5.Uharibifu wa seli hai nyekundu kufanyika kwa haraka kuliko utengenezwaji.
6.Kuwa na maradhi ya sickle cell. Yawezekana ukawa mmoja kati yawabaosumbuka kwa magonjwa yanayotokana na mtindo wa maisha waweza kuwasiliana nasi kwa namba 0757876596 tunazo dawa bora kwa Madonda ya tumbo, figo, na mengine mengi

11/11/2024

RANGI ZA MATUNDA
Unaweza kujiuliza ni kwa nini matunda yana rangi mbalimbali? Hili swali Mwenyezi mungu aliyeumba kila kitu ndiye anajuwa saidi. Ila kwa ufupi utambuwe kuwa rangi katika matunda ni dalili ya ishara flani. Katika post hii tutaona baadhi ya rangi katika matunda. Mwisho wa post hii utaweza kutambua nini kimo katika tunda utakaloliona kwa kuangalia rang.

1.rangi nyekundu Rangi nyekundu kwenye matunda hutokana na nyembenchembe ziitwazo lycopene. Hizi ni antoxidant ambazo husaidia katika kulinda mwili dhidi ya sumu za vyakula. Sumu hizi mara nyingi huweza kuharibu seli ndani ya miili yetu. Pia sumu hizi husababisha mtu kuzeeka haraka. Chembechembe hizi pia husaidia katika kuzuia uharibifu wa seli mwilini. Huimarisha mfumo mzima wa kinga mwilini. Na pia husaidi akatika kulinda au kupunguza adhari za magonjwa ya moyo na saratani.matunda yenye rangi hii ni pamoja na tomato, matikiti, pilipili n.k

2.rangi ya njano. Rangi ya njano kwenye matunda husababishwa na chembechembe ziitwazo beta-carotene, hizi pia ni antoxidant. Chembechembe hizi husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini. Mwili huweza kubadili beta-carotene, kuwa vitamini A. Itambulike kuwa vitamini hivi ni muhimu sana katika afya ya mtu. Kupamabana mna maradhi mablimbali nna kuimarisha afya ya macho. Kupambana na wadudu wanaosababisha vidonda vya tumbo. Huimarisha afya ya ngizi na maeneo mengune yenye utando laini.miongoni mwa matunda yenye rangi hii ni viazi, karoti, maembe n.k

3.rangi ya kijani. Rangi ya kijani husaidia kutambuwa uwepe wa vitamini Ana C. K**a inavyotambulika mboga za majani zina rangi hii. Vitamini A na C huweza kupatikana kwa wingi kwenye rangi hii. Itambulike kuwa vitamini hivi ni muhimi katika kudhibiti mfumo mzima wa kinga mwilini. Upungufu wowote wa vitamini hivi viwili uanaweza kusababisha madhara makubwa mwilini.

4.rangi ya bluu na violet Rangi hii hutambulisha uwepo wa anthocyanin ambayo ni antioxidat. Itambulike kuwa antioxidant zina uwezo mkubwa wa kupambana na sumu mbalimbali ndani ya mwili. Sumu hizi zinasababishwa ba vyakula tunavyokula kwa kiasi kikubwa. Vyakula hivi vyenye rangi hii huwa vina vitamini C kwa kiasi kikubwa. Pia vyakula hivi vina kambakamba ambazo ni muhimu sana katika afya ya mtu.

Tupigie kwa namba 0757876596 kwa mawasiliana zaidi

08/11/2024

5.VIZAZI, FAMILIA NA KURIDHI (GENETICS)
Afya ya mtu inaweza kuathiriwa na kurithi kutoka kwa wazazi. Hapa mtu hana chaguo maana kurithi huku kumetokea toka tumboni kwa mama. Mtu anaweza kurithi maradhi k**a pumu, moyo, kisukari, siko seli na mengineyo.

02/11/2024

4.TABIA
Tabia za watu pia zinaeza kuwa ni sababu ya kupata maradhi na kuathiri afya. Watu wamekuwa wakikulia katika koo, familia na kabila mbalibali ambapo wanajifunza tabia tofautitofauti. Tabia hizi k**a hazitakuwa katika hali inayotakiwa zinaweaa kusababisga kupata maradhi

Nitoe mfano mzuri kuhusu maradhi ya fangasi sehemu za siri. Fangasi hawa wanafurahia sana mazigira yenye majimaji. Mara nyingi usafi wa nguo za ndani na mwili kwa ujumla hususan sehemu zile umaweza kuwa sababu ya kuendelea kuwalea wadudu hawa. Tabia ya kuvaa nguo mbichi hususani zile za ndni inaweza kuendelea kuwalea fangasi hawa.

Tabia ya kula mara kwa mara inaweza kusababisha kupata kitambi. Mtu akiwa anakula mara kwa mara bila ya kufanya mazoezi anaweza kupata tatizo la kuzidi kwa uzito. Tatizo hili linaweza kuathiri mwili kushindwa kuzalisha homoni za insulin kwa kiwango kinachotakiwa na hatimaye kupata kisukari.

Tabia ya kuchelewa kualal yaani kukosa muda mzuri wa kulala inaweza kuwa sababu ya kupata matatizo ya kiafya. Mwili unahitaji muda wa kutosha wa kulala ili uweze kurekebisha mwili ndani ya muda huo. Mwili unahitaji kupumzika pia.

Tabia ya kukaana misongo ya mawazo na kupenda kukasirika na kukaa na vinyongo. Hii ni hatari sana ka afya ya mtu kisaikolojia na kimwili pia. Misongo ya mawazo inaweza kuwa sababu nzuri ya kupata maradhi k**a vidonda ya tumbo. Maumivu ya kichwa na tumbo pia huweza kuletwa na misongo ya mawazo

Elisha Bituro 0757876596

02/11/2024

3.SHUGHULI ZA KILA SIKU
HAlikadhalika shughuli zetu za kila siku zinaweza kuwa sababu mojawapo ya kupata maradhi mablimbali za kutafutia riziki zinaweza kuwa sababu tosha ya kupata maradhi. Wataalamu wanaeleza maradhi kazaa ambayo yanaweza kuwa chanzo chake ni shughuli zetu za kila siku.

Vifaa vya kufanyia kazi k**a visipotumika ipasavyo kwa mfano kuvaa viatu maalumu na nguo maalumi kwa ambao wanafanya kazi viwanda vya kemikali, wanaweza kupata madhara. Wafanyaji kazi sehemu zenye mionzi hatari k**a x-ray wasipovaa mavazi maalumu kwa utaratibu husikwa wanaweza kuapata madhara.

Muda wa kufanya kazi usipizingatiwa pia madhara yanaweza kuapatikana. Kwa mfano sehemu zenye mionzi mikali k**a x-ray kuna muda maalumu wa kufanya kazi na ukipita anatakiwa aingie mtu mpya. Hivyo jkazi k**a hizi muda usipizingatiwa madhara ya kiafya yanaweza kutokea.

Halikadhalika teknolojia inayotumika kufanyika kazi k**a haitakuwa katika hali nzuri inaweza kusababisha madhara. Vifaa vya kisasa vinatakiwa vitumike zaidi kwa ajili ya usalama kuliko kuendelea na vile vya zamani vinavyohitaji nguvu nyingi na kufanya kazi mazingira ya hatari.

Hivyo shughuli zetu za kufanyia kazi zsipowekwa katika hali nzuri zinaweza kuwa ni sababu ya sisi kuapata madhara makubwa k**a kupiteza mali, kupoteza uhai au kupoteza viungo vya miili yetu. Somo hili tutaliona kwa undani zaidi kwnye kurasa zijazo.0757876596

Address

Nkwenda

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Heritage herbal clinic-Hhc posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share